Tamko la Serikali: Mgomo wa Madaktari

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,325
2,498
Heshima mbele wana jamvi

Ni zaidi ya saa 24 sasa tangu mgomo wa madaktari uanze.

Je, ni kweli serikali imeshatoa tamko au taarifa rasmi juu ya mgomo au bado. Na kama bado inasubiria nini. Au ndio uleule ugonjwa aliosema ndugu yetu mwingine ambaye naye yuko Ujerumani kwa ajili ya ‘check up’ ya macho!? …yaani “Kutokuwa na Maamuzi”.

Nimemuona jana Mh. Waziri Mkuu akiongea pale Ikulu lakini ilivyokuwa ni kama alikuwa anaongea kama Ngugu ‘Mizengo Pinda’ na sio ‘Waziri Mkuu’. Nasema hivyo kwa maana iaelekea waandishi walimvamia na ndio akasema alivyosema kwa hiyo sidhani kama hiyo inaweza kuwa taarifa rasmi.
bado napitia pitia vyanzo vya habari na sioni tamko la Serikali
hivi waziri na naibu wake si wajiuzulu tu wenyewe maana mgomo huu ni kwa ajili yao!!
mpaka sasa kikwete yuko kimya
 
Nchi iko kwenye autodrive. Jk amejificha labda kafunga mungu ashuke. Alilia sana urais sasa afanye tuone. Wale wanaoutaka waone mfano wa kujipeleka huku una kichwa cha nazi
 
Tuingieni barabarani thts 'e only sln madktari wamefanya wanachoweza kupigania maslahi na matatizo yanayoizongo taaluma yao,kazi 2mebki nayo sisi raia kudai huduma za kiafya na wa kumdai huduma hzi hakuna mwngne bali serikali tujipange wa tz hakuna wakutukomboa bali sisi wenyewe..nakupenda tz.
 
Mgomo huu ahuwezi kuisha mpaka waziri na naibu wake wachomoke na wenyewe wamegoma kutoka,wakoradhi wananchi wafe wenyewe waendelee kubaki madalakani.hii ndiyo TZ.
 
Hapo ndio tuijue serikali isiyokuwa na Maamuzi kabisa, whether yawe sahihi ama si sahihi , ni kwamba haina maamuzi kabisa.
 
Wanatoa taarifa kuhusu mikoa na wilaya mpya ambazo wakazi wao wanakufa kwa kukosa huduma bora za afya.
 
Urais ni kazi ngumu siyo ya kuamuliwa tuu na wanamtandao na kuikimbilia ilihali mtu unajifahamu kichwa chako Nazi
 
Wanangoja madaktari kutoka misri, cuba na china waje kuokoa jahazi! tuendelee kungoja si wanasema wamejipanga?
 
Mtanzania leo amekuwa hana thamani anaachwa afe kisa ni Mponda na Nkya ebu muogopeni mungu.
Uwaziri ni mpito tuu na hamkuzaliwa ili muje kuwa mawaziri.
Usikute JK anataka fumua baraza lote ili asionekane ametii amri ya madr
 
Wako bize wanapanga mikoa mipya na wilaya mpya nani awe mkuu wa mko na wilaya kwani shangazi bado hajapata cheo, mjomba, kakabinamu, dadabinamu, mwanaasha naye ukuu wa wilaya ss akimaliza vyooooote hivyo ndipo aje kwenye suala lenu la madaktari na hapo inategema kama hajawa na kajisafari maana pasaka inakaribia shoping hatujafanya bado so endeleeni kusubiri tu tutakuja na majibu mazuri!!
 
Heshima mbele wana jamvi

Ni zaidi ya saa 24 sasa tangu mgomo wa madaktari uanze.

Je, ni kweli serikali imeshatoa tamko au taarifa rasmi juu ya mgomo au bado. Na kama bado inasubiria nini. Au ndio uleule ugonjwa aliosema ndugu yetu mwingine ambaye naye yuko Ujerumani kwa ajili ya ‘check up' ya macho!? …yaani "Kutokuwa na Maamuzi".

Nimemuona jana Mh. Waziri Mkuu akiongea pale Ikulu lakini ilivyokuwa ni kama alikuwa anaongea kama Ngugu ‘Mizengo Pinda' na sio ‘Waziri Mkuu'. Nasema hivyo kwa maana iaelekea waandishi walimvamia na ndio akasema alivyosema kwa hiyo sidhani kama hiyo inaweza kuwa taarifa rasmi.

Hii nchi ina viongozi ambao hawawezi kufanya maamzi, na haya unayoyaona ni matokeo ya kukosa utashi wa uwajibikaji..
 
Wazee wetu walipigana kumuondoa mkoloni na kuiletea nchi yetu Uhuru, sisi watanzania wa leo tunalalamika tuuu, sasa ni wakati wa kuikomboa nchi yetu kutoka katika mikono ya maghaidi CCM na serikali yake, watanzania tuungane tuiondoe serikali hii dhalimu madarakani sasa hivi kwani haitusaidii kitu licha ya kutuacha tufe, Madaktari wamekataa kulalamika wameonesha njia na wanaharakati wamewaunga mkono, sasa ni zamu yetu sisi wananchi kufanya uamuzi mzito wa MAPINDUZI, silaha yetu ni UMOJA. TUACHE KULALAMIKA tuamuke tuikomboe nchi yetu ili watoto wetu waje wafaidi tunu za taifa letu. TUCHUKUE HATUA SASA NA TUFANYE MAPINDUZI. WAKATI WA UKOMBOZI NDIO SASA.
 
Nchi iko kwenye autodrive. Jk amejificha labda kafunga mungu ashuke. Alilia sana urais sasa afanye tuone. Wale wanaoutaka waone mfano wa kujipeleka huku una kichwa cha nazi

kwa sababu Kiwete hatukani mabepari , hawachukii wayahudi,hana habari na kujiingiza katika migogoro ya nchi jirani wala kujifanya anajua kutatua migogoro yao, hajifanyi kuwa najua kuwakamia wamarekani na waingereza umoja wa mataifa, ndio maana unamtukana. uzuri wake wewe hutaujua na wala huujui kamwe. anaglia sana anavyojitahidi kutatua unemployment rate halafu uone ni nani kama yeye! kuwa na kuiamini injili!
 
wako bize wanapanga mikoa mipya na wilaya mpya nani awe mkuu wa mko na wilaya kwani shangazi bado hajapata cheo, mjomba, kakabinamu, dadabinamu, mwanaasha naye ukuu wa wilaya ss akimaliza vyooooote hivyo ndipo aje kwenye suala lenu la madaktari na hapo inategema kama hajawa na kajisafari maana pasaka inakaribia shoping hatujafanya bado so endeleeni kusubiri tu tutakuja na majibu mazuri!!

hayo mambo ya kupanga mikoa na wilaya mpya sipendi. Ni kuongeza gharama tu kwa nchi na kugawana madaraka kwa vibaraka wao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom