Tamko la serikali kuhusu mauaji Tarime?

Kauli hii hapa chini ni uongo mtupu!


jmkikweteJakaya Kikwete



Mambo ya msingi yanayotuunganisha ni ubinadamu wetu na uraia wetu wa Tanzania.Kila mmoja wetu anazo haki sawa na mwingine.

7 hours ago

Twitter
 
Hivi CDM suala la Meya Arusha limewashinda kabisa? Pamoja na watu wa tatu kufariki naona na madiwani wenu kususa naona mmeshindwa na kukubali yaishe! Eti maandamano ya mikoa ya kusini unaleta swaga ya kuwambia tunataka uchaguzi wa meya arusha urudiwe,watu wa mbeya,ruvuma na umeya Arusha hakuna uhusiano kabisa! Sasa mlitaka mlete ujinga wenu tarime!? Serikali itoe tamko la nini sasa? Kuhusu hao wavamizi wa mgodi? Chadema maiti za watu sio dili ya kupata umaarufu wa kisiasa! Wajinga wakubwa mnafikiri kwa kutumia magoti

Pointless
 
Hivi Ocampo ameenda likizo?????????
Haya ni makosa ya uhalifu wa kibinadam lakini serikali yetu imefumba macho na masikio Eee Mungu uturehemie makosa yetu kwani bado watz hatujaamka tupo kwenye lindi la usingizi.
 
Chadema inakua karibu baada ya kuona watu wamekufa ndio timu yote ikahamia Tarime safari hii hadi Babu yenu Bepari Edwin Mtei alienda Tarime kuandaa maandamano! Mmezimwa vizuri sana Kimyaaa hakuna maandamno kama mlivyo taka! Chama kinaenda kwa matukio! CDM Hopeless kabisa!
The opposite of this is true for CCM. Hata kama tatizo ni kubwa kiasi gani haiwezi kuwa karibu na wanaoteseka, na hata kinara wake asitegemewe kuwa anaweza kanyaga Tarime? Kufanya nini waliokufa walistahili. Yeye alishahudhuria maziko ya Sheikh Yahya inatosha. CCM hawawezi kuandamana kupinga unyanyasaji wa aina yoyote, wao huandamana kupongeza hatua mbali mbali za serkali. Chama chenu hakijui kabisa yanayoendelea kwa mwananchi wa kawaida, matukio pekee yanayokigusa ni sherehe za kitaifa. Hongera
 
Keep it up jeshi la polisi will see you soon ....

Keep it up kikwete na massawe we will see you jail soon ...

Keep it up january na nape we will see you jail soon ...

Heshima za dhati kwa wafiwa na wajane na ndugu wote. Hii ndio uchungu na damu za sacrifices za democracy hakuna yeyote yupo immune na uuaji wa ccm, hata mkitaka kuwasha bunduki Tanzania nzima "we will not surrenderssssssss"
 
Polisi wadaiwa kuchoma 'majeneza’ ya Chadema



SAKATA la mauaji ya wananchi wanne katika mgodi wa Nyamongo uliopo Tarime, mkoani Mara umechukua sura mpya baada ya ndugu wawili wa marehemu kudai kuwa polisi waliwapiga na kuwalazimisha kuyachoma majeneza waliyonunuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ajili ya mazishi.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa ndugu hao walipigwa ili wayachome majeneza hayo na kuyatumia yale yaliyonunuliwa na kukabidhiwa kwao na polisi.Mkono Bhoke ambaye ni kaka wa marehemu Chawali Bhoke, alisema tukio hilo lilitokea juzi baada ya kusimamishwa na askari polisi wakiwa njiani na majeneza hayo kuwahi mazishi.

Katika mkasa huo, Mkono alisema polisi wakiwa na bunduki, waliwalazimisha wanandugu hao kuyamwagia petroli majeneza hayo mawili na kuyateketeza kwa moto.Kama hiyo haitoshi, Mkono alidai polisi hao waliwapiga na kuwaweka mahabusu kwa muda jambo lililowafanya washindwe kuhudhuria mazishi ya ndugu zao.

Mkono aliongeza kuwa alikutwa na mkasa huo akiwa na ndugu wa marehemu Mwikabwe Mwita, mkazi wa Kijiji cha Kitunguruma."Kutokana na kadhia hiyo, ilibidi wanandugu kutumia majeneza ya polisi kuzika marehemu wao," alisema Mkono.

Hata hivyo, habari zingine zimeeleza kuwa wakati ndugu hao wakilazimishwa kutumia majeneza ya polisi kuwazika ndugu zao, ndugu wa marehemu Chacha Ngoka wa Kijiji cha Kewenja na Emmanuel Magige walizikwa kwa kutumia majeneza ya Chadema.Kwa mujibu wa habari hizo, ndugu hao jana walikuwa kwenye mikakakti ya namna ya kuwarejeshea polisi majeneza hayo, huku wakijua kwamba wenzao walikumbwa na kipigo.

RPC Boaz asema
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz alipoulizwa kuhusu matukio hayo, alisema haamini kama polisi wanaweza kufanya jambo hilo, ila akaahidi kufuatilia kwa karibu kujua kilichotokea

"Sikuwapo kazini, ila pia siamini kama polisi wamefanya hivyo. Nitafuatilia kwa karibu nijue kilichotokea," alisema
Taarifa zilizozagaa mjini Tarime zinaeleza kwamba polisi walitibua kwa makusudi mpango wa Chadema wa kufanya mkutano wa pamoja na ndugu wa marehemu siku ya mazishi kabla ya taratibu za maziko.

Juzi, wanachama kadhaa wa Chadema, Tundu Lisu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki na wenzake saba walifikishwa mahakamani kwa shtaka la uchochezi.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Matena Mwikwabe alidai kuwa wananchi wamekosa imani na Serikali ya CCM kutokana mfululizo wa matukio tangu ndugu zao walipouawa.Diwani wa Kata ya Kibasuka, Suleimani Moya (CCM), alikiri kufika kwenye msiba wa Emmanuel Magige na kueleza kuwa hali kwa wapiga kura wake siyo nzuri na kuvilalamikia vyombo vya dola.

“Mimi ni diwani wa CCM, lakini kwenye ukweli nalazimika kuusema. Vifo vya watu hawa lazima halmashauri tutoe tamko, maana wanaokufa niwapiga kura wetu, kisha zinatolewa lugha zisizo nzuri,”alilalamika.

Katika hali ya kutafuta suluhu kati ya wananchi, mgodi na polisi, kesho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wassira amepanga kukutana na viongozi wa vijiji vya Kewanja, Nyangoto, Matongo, Genkuru, Nyamwaga, Nyakunguru na Kerende.

Baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo walilithibitishia gazeti hili lakini wakasisistiza haki za wananchi lazima zipatikane.
Baadhi ya wakazi wa hapa wanaeleza kuwa tukio hilo limejenga uhasama baina ya wananchi na polisi ambao ni watu wanaopaswa kuhakikisha kuwapo kwa ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Tamko la CUF
Katika hatua nyingine, Elizabeth Ernest anaripoti kuwa CUF imemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu kutokana na Jeshi la Polisi kuua raia mgodini.

Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba alisema hayo jana alipokuwa akisoma maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la chama hicho. Alisema chama kinamtaka waziri huyo ajiuzulu kwa kushindwa kusimamia ukiukwaji wa haki za binadamu kunakofanywa na jeshi hilo.

"Baraza linalaani vitendo hivyo ambavyo huripotiwa mara kwa mara kama ilivyotokea hivi karibuni katika mgodi wa North Mara. Kutokana na hali hiyo, CUF inamtaka waziri mhusika ambaye ndiye mwenye dhamana ajiuzuru kwa hili la Nyamongo," alisema Prof Lipumba.


Chanzo: Mwananchi

Eti uliuliza suali hapo juu? Sijui labda unajilazimisha katika jambo fulani!
 
Wazee Tarime watoa masharti kwa Jeshi la Polisi


Na George Marato


28th May 2011



Sakata la mauaji ya watu watano kwa kupigwa risasi na polisi wanaolinda mgodi wa dhahabu wa North Mara, limechukua sura mpya baada ya wazee wa mila wa kabila la kikurya kutoa masharti kwa askari wa Jeshi la Polisi.

Taarifa zilizopatikana juzi jioni wilayani Tarime, zilieleza kuwa baada ya kufanyika mazishi ya watu wawili wanaotoka vijiji vinavyozunguka mgodi huo,wazee wa mila walikutana na kutoa sharti moja kubwa kwa Jeshi la Polisi la kuwakamata na kuwafikisha mahakamani askari wote wanaotajwa kufanya mauji hayo.


Walisema endapo litashindwa kufanya hivyo katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa, wazee hao wanalitaka Jeshi hilo kuwarejesha kambini askari wake kutoka uraiani na kuwapiga marufuku wananchi wa wilaya hiyo kuwapangisha nyumba askari yeyote.


"
Kweli baada ya kumaliza kuzima yule kijana Emanuel Magige pale Nyakunguru, tulikwenda tukaa na wenzetu kutoka koo mbalimbali za kabila la kikurya tukatoa maazimio hayo,"alisema mmoja wa wazee wa kijiji cha Nyakunguru ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini.

"
Tulisema kwasababu polisi wameua watu wetu na wamechukua maiti za vijana wetu na kuzitupa ovyo barabarani na maporini tena usiku kinyume na mila za kikurya tunalitaka Jeshi hilo kuwakamata wote waliohusika kufanya unyama huo la sivyo wajiandae kuhamisha askari wake kutoka huku uraiani pia hatutawapangisha nyumba zetu,"alisisitiza.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mzee huyo wa umri kati ya miaka 80 hadi 85,alisema hakuna sababu ya uamuzi wa wazee hao kupelekwa kwa maandishi kwa uongozi wa Jeshi la Polisi kwasababu wamewaua watoto wao na kinachotakiwa ni kuchukua hatua kwa wahusika.


"
Sisi hatuwezi kuwapelekea maadishi hatuna sababu ya kuwabembeleza,tunataka haki itendeke kwa wahusika kufikishwa katika vyombo vya sheria wakishindwa kufanya hivyo kwa mwezi mzima maazimio yetu yataonekana wazi wazi,"aliongeza

Alisema pia wanakusudia kususia ulinzi shirikishi iwapo madai yao ya kuwafikisha wahusika mahakamani hayatafanyiwa kazi.

Akizungumzia madai hayo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Tarime na Rorya Constantine Massawe, alisema ingawa ofisi yake haijapa taarifa hizo lakini alisema tayari Jeshi lilishatoa taarifa kwa wafiwa kuwa suala hilo linachunguzwa.

"
Hatuwezi kukamata watu tu na kupeleka mahakani ndio maana nasema hata hao wazee tulishawaambia jambo hili tunalichunguza na baada ya uchunguzi tutajua cha kufanya ili haki iweze kutendeka,"alisema Kamanda Massawe.

Aliwaomba wazee hao kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo kwani amani iliyopo hivi sasa wilayani Tarime imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuwepo kwa askari polisi.


"
Wakiwafukuza askari katika nyumba zao sawa na sisi tutafunga virago turudi makwetu lakini watambue amani hii sasa ni juhudi za askari hawa pia kuwepo kwa askari hao kumeleta manufaa makubwa,"alisema kamanda huyo.
Mei 16 mwaka huu majira ya asbuhi watu watano waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kudaiwa kutaka kuvamia mgodi wa dhahabu wa north mara uliopo eneo la nyamongo.

Waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi hivi karibuni kuwa ni pamoja na Chacha Mwita(25)Chacha Ngoka(25)Chawali Bhoke(26)Mwikwabe Marwa(35) na Emanuel Magige(27) ambapo mmoja kati yao mkazi wa wilaya ya Serengeti na wengine wakazi wa wilaya ya Tarime.


CHANZO: NIPASHE
 
Hawa jamaa wanaosema wanalinda raia na mali zao hata wao wamechoka,lakini bado wanabanwa na ile kauli mbiu ya mheshimu na mlinde mkubwa kadira uwezavyo, mapinduzi ya kweli yanaletwa na wananchi, Polisi wao ni vibaraka wa JK gOVERNMENT,

Nuhu tufungulie safina: twaangamia na magamba
 
Kanisa laingilia kati mauaji ya North Mara

Na George Marato


30th May 2011

Wiki chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum Tarime na Rorya, kutuhumiwa kuwaua kwa risasi raia watano na kujeruhi wengine kadhaa wakidaiwa kutaka kuvamia mgodi wa North Mara, Kanisa la Anglikana Doyosisi ya Tarime limeitaka serikali kuacha kuingiza siasa katika kutafutia ufumbuzi wa mgogoro huo.

Kanisa hilo limesema mgogoro huo wa muda mrefu kati ya wawekezaji na wananchi wanaozunguka mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold, umechangiwa na serikali kushindwa kuchukua hatua za haraka za kuwapatia haki ya msingi wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE nyumbani kwake juzi mjini Tarime, Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Tarime, Dk Mwita Akiri, alisema lazima serikali ibebe lawama kuhusu mgogoro huo na roho za watu zinazopotea kila wakati kwa kushindwa kuchukua hatua za kuwatengea eneo mbadala la uchimbaji wananchi hao.

"Ndio tunakubali sera ya uwekezaji ya serikali na ndio imefanya kuwapo kwa hawa wenzetu wageni katika eneo la Nyamongo na ni faida kwa taifa kwa kupata kodi lakini tunajiuliza serikali inatambua wazi wananchi wa pale miaka yote mashamba yao ni uchimbaji sasa ilitegemea imewanyang'anya maeneo na kuwapa wageni na baada ya hapo nini kifuate kama si kuruhusu uvamizi huo,"alisema na kuongeza.
"Huwezi kumaliza tatizo kwa kuongeza ulinzi wa askari polisi na kufanya matumizi makubwa ya nguvu za dola katika eneo hilo cha msingi hapa serikali imechelewa tu kuchukua hatua za kumaliza mgogoro huu..utaleta majeshi yote lakini ipo siku utakuja kujuta kwani ni hatari kuimba amani wakati vijana hawana ajira na watu wana njaa,"alisema askofu huyo.

Kiongozi huyo wa dini aliwashutumu baadhi ya viongozi wa serikali kwa kutokuwa wa kweli kwa mamlaka wanazowakilisha kuhusu hali ilivyo katika eneo hilo, badala yake wamekuwa wakitoa taarifa za kupika na za uongo ili kuwapendezesha wawekezaji kwa maslahi binafsi.
"Rais akija hapa Tarime anaelezwa mazuri tu ya mwekezaji na jinsi anavyolipa kodi serikalini lakini haambiwi ukweli shida wanazopata wananchi wa eneo hilo na baada ya hapo wanamchukua kiongozi wa nchi bila kumpeleka kwa wananchi wanamwingiza mgodini kisha anaondoka je hapa unatarajia nini,"alihoji kingozi huyo.

Alisema hatua iliyofikia sasa ni lazima serikali ikatambua wazi mgogoro huo ni janga la kitaifa na si la Tarime pekee na endapo itashindwa kuchukua hatua za haraka kumaliza suala hilo kuna hatari eneo hilo likakosa amani, kuongezeka kwa chuki hasa kutokana na ongezeko la watu wanaozidi kupoteza maisha kwa kupigwa risasi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi kanda hiyo maalum Constantine Masawe, waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi hivi karibuni kuwa ni Chacha Mwita(25)Chacha Ngoka(25)Chawali Bhoke(26)Mwikwabe Marwa(35) na Emanuel Magige(27) ambapo mmoja kati yao mkazi wa wilaya ya Serengeti na wengine wakazi wa wilaya ya Tarime.

CHANZO: NIPASHE
 
Hawa jamaa wanaosema wanalinda raia na mali zao hata wao wamechoka,lakini bado wanabanwa na ile kauli mbiu ya mheshimu na mlinde mkubwa kadira uwezavyo, mapinduzi ya kweli yanaletwa na wananchi, Polisi wao ni vibaraka wa JK gOVERNMENT,

Nuhu tufungulie safina: twaangamia na magamba

Fuateni sheria, na mkumbuke kuwa kuna dola pia !
 
Back
Top Bottom