Tamko la serikali kuhusu mauaji Tarime?

Damu ya Watanzania,ndugu na Rafiki zetu iliyomwagika Nyamongo itazirutubisha mbegu za mti utakaochipua na kuleta HAKI na TANZANIA MPYA yenye kuyajali MASLAHI ya wananchi wake,Taifa lenye kusimamia kwa umakini MIKATABA yote ya uchimbaji wa MADINI,Ili kila Mtanzania anufaike na MALIASILI ya TANZANIA.Mungu akawafanyie wepesi ndugu wa wafiwa katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Thanks for your note, I hope he/she understands it.

Kwa hiyo wewe watu kupoteza maisha sio tukio? Hivi unajua maana ya hope wewe? Hope is the belief in a positive outcome related to events and circumstances in one's life...its the hope that CHADEMA has for TANZANIANS
 
Hivi CDM suala la Meya Arusha limewashinda kabisa? Pamoja na watu wa tatu kufariki naona na madiwani wenu kususa naona mmeshindwa na kukubali yaishe! Eti maandamano ya mikoa ya kusini unaleta swaga ya kuwambia tunataka uchaguzi wa meya arusha urudiwe,watu wa mbeya,ruvuma na umeya Arusha hakuna uhusiano kabisa! Sasa mlitaka mlete ujinga wenu tarime!? Serikali itoe tamko la nini sasa? Kuhusu hao wavamizi wa mgodi? Chadema maiti za watu sio dili ya kupata umaarufu wa kisiasa! Wajinga wakubwa mnafikiri kwa kutumia magoti


Haya ndio mawazo yanayochelewesha ukombozi wa mtanzania. Kwa kweli, CHADEMA tunatakiwa tuongee bidii kuelimisha watu kama wewe kabla ya mabadiliko ya kiutawala.
 
Hizi ID za matukio hiziii! Zilikuwepo za uchaguzi mkuu,.....zikaja za kuvuana magamba, na sasa za Nyamongo. Somebody somewhere busy dancing to CDM tunes.
Hivi CDM suala la Meya Arusha limewashinda kabisa? Pamoja na watu wa tatu kufariki naona na madiwani wenu kususa naona mmeshindwa na kukubali yaishe! Eti maandamano ya mikoa ya kusini unaleta swaga ya kuwambia tunataka uchaguzi wa meya arusha urudiwe,watu wa mbeya,ruvuma na umeya Arusha hakuna uhusiano kabisa! Sasa mlitaka mlete ujinga wenu tarime!? Serikali itoe tamko la nini sasa? Kuhusu hao wavamizi wa mgodi? Chadema maiti za watu sio dili ya kupata umaarufu wa kisiasa! Wajinga wakubwa mnafikiri kwa kutumia magoti
 
Dingiswayo, serikali inaona,inaamini na inalichukulia suala la mauaji ya Tarime kama mauaji mengine tu ya vibaka na majambazi mitaani. Yote hayo huwa hayatolewi matamko. Tofauti ya hili ni kwamba polisi walitoa rambirambi na wakanunua masanduku na pia walitamani sana wakazike wenyewe. Nadhani ni kutokana na taarifa fulani za kiinteligensia kutoka makao makuu.
Tumefahamishwa na vyombo vya habari kuwa hawakuwa wavamizi wa mgodi na serikali (polisi) ikatoa coffins na pesa za mazishi kwa wafiwa. (Leo nimesoma mahali kuwa polisi walilazimisha wazikwe kwa kutumia coffins hizo za polisi). Itakuwaje unabadili hapa na kutufanya kuwa walikuwa ni wavamizi wa mgodi? Hata hivyo, serikali haioni kwamba kuna haja ya kutoa tamko hapa, maana jambo hili limeongelewa sana hata kuvuka mipaka ya nchi na kuwa ni polisi walifanya mauaji hayo kwa wananchi? Kuna leo na kesho, angalia jana Mladic kakamatwa na si punde atafikishwa the Hague. Viongozi hawaoni hatari hiyo? Mwisho, mimi sio mwanachama wa Chadema, ni Mtanzania wa kawaida ambaye amestushwa na vitendo vinavyotokea. Nahisi sio mimi peke yangu.
 
Habari za kinafik.

We! wakati watu wazima wanazungumza uwe unakaa kimya, hasa wanaume wanapoongea mambo mazito kama hayo. Kumbuka jamii yako hata haikuruhusu wewe kufanya maziko. Hivyo usisahau wewe ni wa kike.
 
Dingiswayo, serikali inaona,inaamini na inalichukulia suala la mauaji ya Tarime kama mauaji mengine tu ya vibaka na majambazi mitaani. Yote hayo huwa hayatolewi matamko. Tofauti ya hili ni kwamba polisi walitoa rambirambi na wakanunua masanduku na pia walitamani sana wakazike wenyewe. Nadhani ni kutokana na taarifa fulani za kiinteligensia kutoka makao makuu.

Kwa kitendo hicho sasa, ndio maana serikali inatakiwa kutoa tamko rasmi. Kama marehemu wangekuwa ni vibaka na wavamizi wasingetoa rambirambi na kununua masanduku.
 
Kaimbe taarabu wewe usitake kujifanya una akiri ya kufundisha watu hapa JF,kawafundishe viongozi wako wa Chadema

Na wewe kawafundishe waliokutuma huku,unamshambulia mwenzio ili kupoteza maana wakati yeye anatetea haki?JF hakuna wauaji Kama wewe unaeyashangilia
 
Kwa hiyo wewe watu kupoteza maisha sio tukio? Hivi unajua maana ya hope wewe? Hope is the belief in a positive outcome related to events and circumstances in one's life...its the hope that CHADEMA has for TANZANIANS

iyo lugha kwa mzaramo si sawa na tusi? Mtu anajiita mlango wa kati unategemea nini?
 
Niliweka post moja hapa ikaondolewa haraka haraka yenye kichwa cha habari kwamba: Mauaji Tarime yamefanywa na serikali, kwa hoja ifuatayo. Askari wa kawaida hawezi kwenda kufanya mauaji hayo ila kwa agizo la mkubwa wake wa juu. Hali kadhalika mkuu wake wa juu huagizwa kutokana na mlolongo wa viongozi waandamizi hadi kwa Jemadari Mkuu wa Majeshi nchini ambaye ni rais.
Ukimya wa viongozi waandamizi wa juu kunzia Rais Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya ndani Vuai kutotoa tamko lo lote juu ya mauaji hayo na papo hapo kuwabambikiza kesi viongozi wa Chadema waliokwenda kuwasaidia waathiriwa ni ushahidi tosha.

Leo wanaanza kuwasakama waandishi wa kimataifa kutopeleka taswira za tukio nje ili wasichafuke kwa kumshika mwandishi wa kimarekani huko kwenye matukio. Naona wanavyobabaika kuficha matukio lakini too late, kila kitu kimeshavuja hakuna pakushika kila mtu unateleza sasa.
 
Mbunge Tundu Lisu waliyembambikiza kesi huko Tarime anatambuliwa Kimataifa juu ya uteteaji wa haki za raia, ni wiki chache tu ametoka kupata tuzo huko nchini Marekani, na haya yanatokea na ninahakika habari hizo zinawashangaza wanaharakati wa haki za binadamu po pote duniani.
 
jenezaa.jpg
Hii ndiyo serikali ya CCM ambayo inajigamba kwamba inafuata utawala wa kisheria na ipo makini sana kama Waziri Mkuu wake alipoliambia Bunge January huko Dodoma.
 
Chadema inakua karibu baada ya kuona watu wamekufa ndio timu yote ikahamia Tarime safari hii hadi Babu yenu Bepari Edwin Mtei alienda Tarime kuandaa maandamano! Mmezimwa vizuri sana Kimyaaa hakuna maandamno kama mlivyo taka! Chama kinaenda kwa matukio! CDM Hopeless kabisa!

Siku zote Mkuki mtamu kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, ingekuwa katika hao waliofariki kuna ndugu yako wa karibu sidhani kama ungeandika uliyoyaandika. Serikali yoyote duniani ambayo haiheshimu wala kujali uhai wa raia wake basi Serikali hiyo haistahili kabisa kuwepo madarakani.
 
Ni Muungwana tu ndie huomba radhi na kukubali kuwajibika kwa makosa yake au yalioyendwa na anaowaongoza, kwa CCM nakumbuka muungwana wa mwisho at least alikuwa niu Mzee Mwinyi, aliomba radhi baada ya mauaji ya vikongwe shinyanga! kwa serikali ya CCm ya sasa ya mafisadi na wezi hakuna muungwana anayeona haja ya kutoa tamko. Hii hutokea kwa serikali iliyokosa kibali cha kutawala machoni na kwenye mioyo ya wananchi wake, so ndugu yangu Dingiswayo don't expect anything like that kutoka kwa "kilaza JK"!
 
John marwa kumbuka hata kama hawa waliouawa sio ndugu zako ila jua kuwa ni damu ya mtanzania ndo imemwagika kwa ajili ya kulinda mwekezaji nakushauri leo hii nenda kokote kule ujitambulishe kuwa umetoka Tanzania kitu cha kwanza kuulizwa ni vipi hao raia wa tanzania wameuawa na polisi na kisha polisi kutakaka kutoa rambirambi na kulazimisha watu kuzika kabla ya uchunguzi wa kina kufanyika
Pia ni kweli kuwa huenda hakuna hata ndugu yako aliyeuawa lakini kumbuka kama leo halijakukuta hili la Tarime basi tia maji huenda kesho likakukuta la dar ama kokote tanzania sasa nitaona kama utalia ama utaendelea kuandika ujinga wako humu kwa Great Thinkers Jf
 
Back
Top Bottom