Tamko la Rostam Aziz dhidi ya Reginald Mengi na yatokanayo. Amuita fisadi Nyangumi

Status
Not open for further replies.

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Mbunge wa Igunga na Mweka hazina wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, hatimaye amejibu rasmi madai mazito yaliyotolewa na Reginald Mengi kuhusu "mafisadi papa". Tamko hilo rasmi linapatikana katika ukurasa wa 6 wa gazeti la 'The Citizen' la leo Alhamisi, tarehe 30 Aprili 2009. Wakati tunamsubiri nakala yake tupate dondoo hii kutoka kwenye hitimisho la tamko hilo:

"I am therefore calling upon Mr. Mengi to either surrender whatever evidence he has to support his wild accusations and to appoint the appropriate legal bodies or state organs to act accordingly. Alternatively he is it to apologize to me personally within 48 hours, failing all of which, I reserve the right to exercise any appropriate actions in order to expose his wrongdoings"

Wakati huo huo gazeti hilo linaripoti kuwa mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji, yeye ameshachukua hatua ya kufungua kesi dhidi ya Reginald Mengi ambapo anadai fidia. Maswali ya msingi ya kujiuliza ni : Je, katika mpambano huu ile methali ya "wapiganapo tembo nyasi huumia" itatimia au nyasi ndio zitapata fursa ya kustawi zaidi? Je, mpambano huu utaishia kuwa mchezo wa kuigiza au utazitimizia hizo nyasi methali ya "avumaye baharini papa kumbe wengi wapo"?

TAMKO LAKE HILI HAPA:

MAELEZO YA MHESHIMIWA ROSTAM AZIZ KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI, JUMAPILI, 03 MEI, 2009

Ndugu zangu waandishi wa habari,

Naomba nianze kwa kuwashukuru nyote kwa kupokea mwaliko wangu wa kuwaita katika mkutano huu na pia kwa kuja kwenu hapa kunisikiliza. Nataka niwahakikishie kuwa nathamini sana heshima hiyo mliyonipa.

Nimeitisha mkutano huu kufuatia tuhuma nzito, ingawa ni lazima niseme pia ni za kipuuzi, zilizotolewa na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Abraham Mengi, dhidi yangu na wafanyabiashara wengine wanne akituhusisha na kile alichokiita “mafisadi papa“, alizozitoa wakati akilihutubia Taifa kupitia kituo chake binafsi cha televisheni cha ITV tarehe 23 Aprili, 2009.

Mara baada ya kutoa matamshi yake, nilihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari vilivyonitaka nitoe maoni yangu. Niliwaambia kuwa sitaki kujibizana na mzee mwenye umri mkubwa unaozidi hata wa baba yangu. Hata hivyo, baada ya kupata nafasi ya kuangalia mkanda mzima wa maelezo yake, na kuona athari mbaya ya uzushi, chuki na sumu iliyomo, nimeona kuna haja ya Watanzania kuufahamu ukweli hasa ulivyo.

Naelewa kwamba tayari Serikali na vyombo vyake vimeshatoa kauli za kumuonya Mengi kuhusu kauli alizozitoa. Waziri wa Nchi anayeshughulikia Utawala Bora, Mheshimiwa Sofia Simba, amemtahadharisha Mengi kwamba kitendo chake cha kutumia vibaya vyombo vyake vya habari kuwachafua washindani wake wa kibiashara hakikubaliki.

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa George Mkuchika, amesema Wizara yake inafanya uchunguzi wa matamshi ya Mengi kwa kuupitia mkanda wenye maelezo yake na ikibainika amevunja sheria atachukuliwa hatua.

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, amemuonya dhidi ya kuwahukumu watu ambao kesi zao bado zinaendelea Mahakamani. Na Jeshi la Polisi nalo limeeleza kumshangaa kwake Mengi kutokana na siyo tu kutowasilisha ushahidi wa shutuma zake kwa vyombo vinavyohusika lakini pia kumueleza Mengi kuwa hana jipya alilosema zaidi ya kurejea mambo yaliyokwisha fanyiwa au yanayoendelea kufanyiwa kazi na vyombo vinavyohusika. Pamoja na kuheshimu na kuthamini maelezo hayo ambayo yamemuumbua Mengi lakini bado nahisi binafsi nina wajibu wa kutoa maelezo ya kina kuhusu kiherehere hiki cha Mengi.

Kwanza, nataka niweke wazi kwamba tuhuma zote zilizotolewa na Mengi dhidi yangu ni za uongo na ni upuuzi mtupu. Tuhuma hizo ni mwendelezo wa wimbo ule ule ambao amekuwa akiuimba kwa muda mrefu sasa na tayari nilikwishazitolea kauli huko nyuma. Nilipofanya mkutano na waandishi wa habari kama huu mwaka jana, nilisema wazi kwamba sihusiki na tuhuma zote zinazoelekezwa kwangu na nikatoa changamoto kwamba iwapo wale wanaotoa na kusambaza uzushi huo wana ushahidi wa wale wanayoyasema, basi kwa sababu nchi yetu inafuata utawala wa sheria, walipaswa wapeleke ushahidi wao katika vyombo vinavyohusika ili sheria ichukue mkondo wake. Hakuna aliyefanya hivyo.

Hata baada ya Mengi kurudia tuhuma hizo wiki iliopita, nilimpa taarifa kupitia vyombo vya habari niliyoitoa tarehe 29 Aprili, 2009, nikimtaka ndani ya siku mbili (2) awe amewasilisha kwenye vyombo vya sheria vinavyohusika ushahidi wa tuhuma zake dhidi yangu kwamba mimi ni fisadi na kwamba mimi ni muuaji ninayepanga mauaji dhidi yake na watu wengine aliowaita “watu waliojitolea kupambana na ufisadi”. Kama akishindwa kufanya hivyo, basi aniombe radhi hadharani. Na nilimwambia wazi kuwa asipofanya mojawapo kati ya hayo, nitakuwa na haki ya kumuanika ili Watanzania waelewe tabia na hulka ya mtu huyu. Hakufanya chochote kati ya hayo. Na hawezi kufanya hivyo kwa sababu anaelewa kuwa alichokisema ni uzushi alioutunga mwenyewe. Ni kutokana na kushindwa kwake kuwasilisha ushahidi huo ndiyo maana nimeona sasa nifanye mkutano huu ili kuweka kumbukumbu sahihi.

Nimetafakari kwa kina athari zinazoweza kulifika Taifa letu ikiwa mwenendo wa watu kama Mengi kujipa haki ya kuchafua wale anaowaona ni washindani au wapinzani wake utaachiwa uendelee, na hasa kutokana na sumu mbaya iliyomo katika maelezo anayoyatoa na malengo aliyoyakusudia kwa kutoa maelezo hayo. Nimeona sitakuwa natenda haki kwangu, kwa familia yangu, kwa wapiga kura wangu wa Igunga, kwa Chama changu cha CCM, na kwa Watanzania wenzangu kwa ujumla iwapo nitakaa kimya.

Kuendelea kwangu kukaa kimya kunaweza kukapelekea Watanzania wakaziamini propaganda chafu za Mengi zenye dhamira potofu na ovu kwa nchi yetu. Kwa hivyo, kama mzazi na kama mwanafamilia kwa upande mmoja, na pia kama Mbunge, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambazo zote ni nafasi za kuchaguliwa nilizopewa kutokana na kuaminiwa na wale walionichagua kwa kura nyingi, nina wajibu wa kukemea uchafu na uovu unaotaka kupandikizwa na Mengi ambaye watu wanajiuliza amepata wapi uhalali wa kujifanya msemaji wa Watanzania wakati hawajawahi kumchagua katika nafasi yoyote na hivyo hana ridhaa yao.

Taifa letu limepita katika vipindi vingi vya majaribio makubwa lakini limebaki kuwa taifa imara na la kupigiwa mfano katika Bara la Afrika. Tanzania ni nchi ambayo bado wananchi wake wanapambana kuyaondoa matatizo makubwa ya umasikini, ujinga na maradhi lakini inasifika duniani kote kwa umoja na mshikamano wa watu wake, na amani na utulivu walioujenga. Haya yamefikiwa kutokana na misingi madhubuti iliyojengwa na waasisi wa Taifa hili.

Leo hii anapokuja mtu kama Mengi ambaye kutokana na tamaa, uroho, wivu, chuki, fitina, ubaguzi na ubinafsi uliovuka mipaka alio nao na kujipa jukumu la kuivunja misingi hii, sidhani itakuwa ni haki kuendelea kukaa kimya na kumwacha afanikishe malengo yake hayo. Hatuwezi kukaa kimya maana kufanya hivyo kutakuja kuligharimu vibaya sana Taifa letu.

Historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao.


Ameanzisha ugomvi na watu wa kada mbali mbali kuanzia Maaskofu hadi kikundi cha wachekeshaji cha Ze Comedy. Huyo ndiye Reginald Abraham Mengi.


Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.


Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.


Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.


Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.


Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.


Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.


Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.


Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.


Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.


Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Na orodha hii inaendelea na inaendelea.


Sasa ameanzisha ugomvi na mimi, baada ya kuona kwamba mimi nimekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, anataka pia kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.


Huyu ndiye Reginald Abraham Mengi.

Tena kwa jinsi alivyo mtu wa visasi na chuki, akishajiingiza katika ugomvi na watu, huhakikisha kuwa habari za watu hao hazitangazwi wala kuandikwa katika vyombo vyake vya habari. Kama ni kutangazwa au kuandikwa basi huwa ni kwa kuwashambulia binafsi na kuwachafulia majina tu.

Hivi ni kwa nini tuendelee kumvumilia mtu kama huyu? Kwa nini anapokuwa na matatizo yake binafsi na wale anaowaona wabaya wake kibiashara au pengine hata kisiasa aiingize nchi nzima na wananchi wote?

Nimeamua kuitisha mkutano huu ili kuwaeleza, na kupitia kwenu kuwaelewesha Watanzania, wamjue Reginald Abraham Mengi katika sura yake halisi na dhamira zake chafu na ovu, na kumtambua kwamba mtu huyu ni nyangumi wa ufisadi katika nchi hii. Nimeamua kuwaondolea Watanzania ngozi yake ya kondoo aliyojivika ili waweze kuiona sura yake halisi ya mbwa mwitu anayojaribu kuificha. Nafanya hivi ili kulinusuru Taifa lisije likatumbukia kule Mengi anakotaka kulipeleka.

Wanasaikolojia wanasema mtu anapotuhumu wengine kuwa na tabia fulani, mara nyingi huwa yeye ndiye mwenye tabia hizo. Hiyo ndiyo hali halisi inayoonekana kwa Mengi kutokana na yale aliyoyasema katika mkutano wake na waandishi wa habari.


Ukweli wa mambo unathibitisha kwamba ni yeye ndiye mwenye kuhusika na yote hayo aliyotutuhumu sisi kuwa nayo. Hapa nitatoa mifano michache tu ya ufisadi mkubwa sana wa mtu huyu.


Reginald Abraham Mengi, nyangumi wa ufisadi, alianza kuifisidi nchi kwa kushiriki katika vitendo vya ufisadi vilivyochangia kuifilisi iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ambayo ni mali ya Watanzania na hatimaye kupelekea kubinafsishwa kwake kwa bei poa. Akitumia kampuni yake ya Anche Mwedu Limited (AML), alichukua mkopo mwanzoni mwa miaka ya 80 wa mabilioni ya shilingi ambayo amegoma kuyalipa hadi leo na kulazimisha suala hilo kufikishwa Mahakamani.


Mkopo wa kwanza ulikuwa kupitia Akaunti Nam. 6543000020 (uliotolewa kupitia Overdraft Agreements) ambao ulifikia jumla ya shilingi 3,255,429,100.75 ambao hadi Januari 1996 ulifikisha riba ya shilingi 1,737,862,471.75.


Mkopo wa pili chini ya kampuni hiyo hiyo (kupitia Loan Agreements) ulikuwa ni kupitia Akaunti Nam. 10430000008 ambao ulihusu jumla ya shilingi 386,746,631.06 hadi kufikia Januari 1996.

Mkopo wa tatu ulihusu Akaunti Nam. 654300584 (kupitia utaratibu wa Government Guarantee) ulikuwa wa jumla ya shilingi 1,803,137,210 hadi kufikia Januari 1996.


Na wa mwisho kupitia utaratibu wa heading interest on jotter/suspense account ulikuwa wa jumla ya shilingi 417,689,254.10 hadi kufikia Januari 1996.


Jumla ya fedha zote za NBC ambazo akidaiwa Mengi kupitia kampuni yake ya Anche Mwedu Limited (AML) hadi kufikia Januari 1996 zilikuwa ni 5,863,002,196.45. Fedha hizi hadi kufikia sasa 2009 pamoja na hesabu ya riba zinafikia takriban bilioni 28.



Hivi ndivyo Mengi alivyochangia kuifilisi NBC, benki ya wananchi masikini wa Tanzania. Fedha hizi zilizochukuliwa na Mengi, shilingi bilioni 28, zinaweza kujenga shule za sekondari 100 ambazo zingeweza kuwanufaisha watoto wa kimasikini wa Tanzania.


Ukiacha ya NBC, Mengi huyu anayetaka aonekane ni msafi kiasi cha kujipa uthubutu wa kuwatukana watu wengine kuwa ni mafisadi, alichukua fedha nyingi kupitia msaada wa nchi wafadhili wa “Commodity Import Support” ambazo hakuzilipa hadi leo.


Hizi ni fedha zilizotolewa kwa njia ya mkopo ili kuwasaidia wafanyabishara kuweza kuagiza bidhaa na zinaporejeshwa ziwasaidie wananchi kwa kuendeleza miradi ya maendeleo hapa nchini kama vile ujenzi wa shule na zahanati. Wafanyabishara wengi tulikopa lakini tumelipa na tunaendelea kulipa. Mengi anayedai ana uchungu na Watanzania anawaongezea umasikini kwa kuchota fedha hizo na baadaye kuruka na kukataa kuzilipa hadi leo. Kati ya fedha hizo ambazo Mengi alichukua ni kama ifuatavyo:


- Norway CIS 1988/89 IPP – Anche Mwedu- NOK (M) 6.00

- Norway CIS 1989/90 - IPP – Anche Mwedu - NOK (M) 4.00

- EEC CIS 1988/89 - Bonite Bottlers - EEU (M) 0.5199


- Japan CIS 1991/92 - Bonite Bottlers -JY (M) 160.000


-Japan CIS 1991/92 - Medicare - JY (M) 115.000


-Canada CIS 1988/89 - Anche Mwedu - C$ (M) 0.5


- Italy CIS 1988/89 - Anche Mwedu - LIRA (M) 1,774.50


- Japan CIS NPG–9-1997 - Anche Mwedu- JY (M) 20,000,000


- Japan CIS NPG–5-1994 - Bonite Bottlers - JY (M) 160,000,000


Fedha hizi zilizo katika sarafu tofauti za kigeni zikibadilishwa kwa shilingi za Tanzania pamoja na riba kwa miaka yote tokea zilipochukuliwa zinafikia mabilioni ya shilingi. Na hizi ni sehemu tu ya fedha zote alizochukua ambazo kumbukumbu zake tumeweza kuzipata baada ya kumbukumbu nyengine kupotea katika mazingira ya utatanishi. Badala ya kurejesha fedha hizi alizozikwapua robo karne iliyopita, Mengi alizitumia kujitajirisha.


Kuonyesha jinsi alivyobobea katika ufisadi, Mengi alikula njama na kushirikiana na afisa mmoja wa Hazina kutengeneza barua ya eti kuthibitisha kwamba alishalipa fedha hizo huku akijua kuwa hakulipa chochote. Pakifanyika ukaguzi huru hata leo hii itathibitika kwamba hakulipa fedha hizo na iwapo anakanusha haya, namtaka akubali kufanyika ukaguzi huo huru. Mtu yeyote wa kawaida angeshangaa Mengi amepata wapi utajiri alio nao katika kipindi kifupi namna hii lakini vielelezo hivi vinatoa majibu ya uhakika.


Tukiacha ufisadi huo, Mengi kwa kutumia nafasi yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji yenye wajumbe watatu (3) tu ya kampuni ya NICO ambayo ni kampuni iliyoanzishwa kusaidia Watanzania kuwekeza katika biashara na viwanda, amefanya ufisadi mkubwa kwa kukiuka maadili ya kibishara pale alipoitumbukiza kampuni hiyo katika kununua hisa kwenye kiwanda cha Interchem Pharma Ltd kinachomilikiwa na familia ya Mengi, wakati akijua kwamba kiwanda hicho kilikuwa njiani kufilisika.


Huku akijua hali mbaya ya kiwanda hicho alitumia nafasi yake kuziteketeza Shilingi bilioni 2.558 fedha za Watanzania masikini wasiopungua 22,000 wenye hisa katika NICO kwa kuifanya inunue asilimia 51 ya hisa (majority shareholding). Kiwanda hicho sasa kimewekwa kwenye orodha ya kufilisiwa baada ya kushindwa kujiendesha chini ya mwaka mmoja tokea Mengi kuizamisha NICO.


Mfanyabishara wa kawaida tu anayeheshimu maadili hawezi kufanya utapeli kama huu kwa kampuni ya wananchi masikini aliyopewa dhamana ya kusimamia uwekezaji wake.


Akiwa mhasibu na mfanyabiashara alijua kuwa kiwanda hicho kinakufa lakini alitumia hila na ujanja wa kusuka mipango yote ya kuiingiza NICO katika hasara ili kunusuru kampuni ya familia yake. Ukweli huu unabainishwa katika kitabu cha Prospectus cha NICO cha Oktoba 2007. Kama amebaki na chembe ya aibu, Mengi anapaswa arejeshe fedha hizi za wanahisa wa NICO.


Ufisadi mwengine wa dhahiri uliofanywa na Mengi ni pale alipoingia ubia na Serikali katika umiliki na uendeshaji wa kiwanda cha TANPACK Industries Ltd. Bila ya kumjulisha mbia mwenzake yaani Serikali, Mengi kisiri siri alitumia dhamana ya TANPACK kwenda kukopa shilingi milioni 600 kutoka benki ya NBC na kuzitumia kwa njia anazozijua yeye. Benki hiyo ilipochachamaa kutaka ilipwe fedha zake, Mengi alitaka TANPACK ilipe lakini Serikali, ikiwa mbia, ilikataa kulitambua deni hilo ambalo haikulijua. Matokeo ya ufisadi huo wa Mengi, TANPACK ikafilisiwa na kufa.


Huyo ndiyo Reginald Abraham Mengi, nyangumi wa ufisadi, katika sura yake halisi. Anawahujumu maskini huku akijidai kwamba anawaonea huruma. Mtu muadilifu hawezi kusema anawatakia wananchi masikini mema huku anafanya maovu kama haya yanayovuruga misingi ya kusaidia masikini hao hao.


Lakini mbali na hayo, ngoja niwachekeshe kwa kuwaeleza jinsi mtu huyu alivyokubuhu katika kujenga chuki na fitina kwa kujifanya mtetezi wa wale anaowaita “wazawa“, huku akiwa na lengo la kujinufaisha binafsi kwa kutumia mgongo wa chuki na fitina hizo anazopandikiza.


Mwaka 1994, alitoa kauli zake zenye sumu ya ubaguzi pale alipodai kwamba sehemu kubwa ya maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam inakaliwa na Watanzania wenye asili ya Kiasia na kwamba “wazawa“ hawapo katika maeneo hayo. Aliyekuwa Rais wakati huo, Mzee Ali Hassan Mwinyi, akamuagiza Waziri aliyekuwa akishughulikia masuala ya ardhi, Mheshimiwa Edward Lowassa, kumpatia Mengi eneo kubwa la ardhi katikati ya jiji karibu na ilipo International House. Lakini mara tu alipopewa eneo hilo akaliuza kwa Fida Hussein, mfanyabishara Mtanzania mwenye asili ya Kiasia. Huyo ndiye Reginald Abraham Mengi, nyangumi wa ufisadi.



Biashara pia ina maadili yake na mwenendo wa mfanyabiashara na biashara zake unaweza kuonyesha ni kwa kiasi gani anafuata au hana maadili. Mambo kadhaa ninayoyafafanua hapa chini yanatoa mwongozo wa kumjua vyema Mengi:


Inafahamika kwamba utajiri wote wa Mengi ameupata katika kipindi cha kama miaka minane, kuanzia 1984 hadi 1992. Watanzania wanapaswa wajiulize amewezaje kuwa tajiri ghafla katika kipindi hicho kifupi? Lakini hata baada ya kuupata utajiri huo, sasa biashara zake zinasuasua na zimeanguka. Amewezaje kuvurugikiwa kiasi hicho? Kwa mtu yeyote anayeelewa misingi ya biashara atafahamu kwamba Mengi hana uwezo wa kuendesha biashara.


Utajiri wake ulitokana na kukwapua fedha kupitia mipango ya ujanja ujanja na kutolipa madeni. Haya yalifanyika huku kumbukumbu zake zikipotea katika mazingira ya ajabu ya majengo kuungua na nyaraka kupotea. Alijifaidisha kwa fedha hizo na sasa zimemalizika. Amebaki kulia wivu na kuonyesha chuki kwa njia ya kutaka kuwakomoa wale anaowaona wamefanikiwa katika uendeshaji wa biashara. Asichokielewa ni kwamba baadhi yetu hatukuamka tu na utajiri bali tumetokana na familia zenye rekodi ya kujishughulisha na bishara tokea mwaka 1852 huko Tabora.


Dalili nyengine ya ufisadi wa Mengi ni rekodi yake ya kuua kampuni zake. Ni vyema ikaeleweka kuwa mfanyabiashara makini na anayezimudu biashara zake hawezi kuua kampuni.


Mfanyabiashara huua kampuni kwa ama lengo la kukwepa kodi, au kukwepa kulipa madeni, au ameshindwa kibiashara na hivyo hawezi kuiendesha tena kampuni yake. Katika kipindi chake kifupi cha kujishughulisha na biashara, Mengi ameshaua kampuni nyingi.


Baadhi tu ya kampuni alizoziua ni pamoja na Tanzania Kalamu Industries Ltd., Anche Mwedu Ltd., TANPACK Tissue Industries Ltd., Chemical Industries Ltd., Bodycare Ltd., na Medicare Ltd. Hebu tujiulize ni kwa nini Mengi anaua kampuni zake halafu anatafuta mchawi kwa wale waliofanikiwa? Bila shaka ameziua kampuni hizo kwa lengo la kukwepa kulipa kodi na kulipa madeni, mambo ambayo ni ufisadi mkubwa. Binafsi sina mchezo wa namna hiyo.


Mfanyabiashara mzalendo pia hupimwa kwa utashi wake wa kulipa kodi na kutoa ajira za uhakika kwa wananchi wenzake. Kama unawatakia heri na ni mtetezi wa wananchi masikini kama Mengi anavyotaka aonekanwe basi utatoa ajira za kudumu na za uhakika, na utalipa kodi ambayo malengo yake ni kuiwezesha Serikali kuhudumia masikini hao kwa kuwapatia matibabu na madawa katika hospitali, watoto wao kupata elimu bora na yenye manufaa, kujengewa miundombinu na hata kupatiwa chakula ikibidi pale nchi inapokumbwa na ukame au njaa.


Kama unawadhulumu wananchi masikini kwa kutowapa ajira za kudumu na badala yake kuwaajiri kama vibarua wa siku na kama hulipi kodi unawezaje kusema unawasaidia wananchi wanyonge? Mengi anafahamika kwa kutimua wafanyakazi kila mara na kutowalipa haki zao na pia kukwepa kodi huku akidai kwamba kampuni zake siku zote zinapata hasara.


Huu ni udanganyifu kwa sababu kama kampuni hizo zinapata hasara haya mamilioni ya fedha anazodai kuzitoa kama michango anazipata wapi? Katika kuendeleza udanganyifu wake na kujaribu kuchezea akili za Watanzania, Mengi amekuwa anakwepa kodi ambazo zingeweza kutumiwa kusaidia kuwaondoshea matatizo wananchi walio wengi na badala yake amekuja na mtindo wa kualika walemavu wachache na kuwapa chakula na kisha kuvitumia vyombo vyake vya habari kwa staili ya Kim Jong Il, Kiongozi wa Korea Kaskazini, ya kusifiwa na kutukuzwa kwa kuandikiwa habari, kutolewa picha na kuchapishiwa makala maalum kila siku za kumpamba.


Amekuwa akiwakaanga wananchi masikini wa Tanzania kwa mafuta yao wenyewe. Binafsi ninajivunia rekodi yangu kwamba kampuni zinazomilikiwa na familia yangu zimetoa ajira za uhakika kwa wafanyakazi takriban 6,000 na pia zinalipa kodi inayostahiki Serikalini. Ninaona fahari kusema kwamba kampuni zetu zinatambulika hata na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba zinaongoza katika ulipaji wa kodi hapa nchini. Hiki ndiyo kipimo cha uzalendo kwa nchi na siyo ule wa kutafuta kuonewa huruma kwa kuwazushia maovu watu kupitia vyombo vya habari ulivyovianzisha kukutukuza wewe na kuwachafua wengine.


Mbali ya hayo, Reginald Mengi huyu huyu ambaye amenituhumu mimi na wengine kuwa tuna akaunti za fedha nje ya nchi ambako ndiko tunakoweka fedha zetu na akadai huo si uzalendo, yeye mwenyewe ana akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi. Nampa changamoto akanushe kwamba hana akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi.


Mengi huyu huyu pia anatutuhumu sisi kutumia fedha zetu kuanzisha magazeti ya kumchafua yeye na eti “wale wanaomsaidia Rais Jakaya Kikwete kupambana na ufisadi“. Anayasema haya wakati yeye anaongoza kwa kuanzisha magazeti, tena mengine yakionekana wazi wazi kwamba yameanzishwa kupambana na watu fulani fulani ambao ni mahasimu wake kibiashara au kisiasa. Tayari ameanzisha magazeti ya The Guardian, This Day, Nipashe, Kulikoni, Sema Usikike, Taifa Letu, Alasiri, Lete Raha, Kasheshe, Acha Umbeya na mengine mengi anayoyafadhili kwa mlango wa nyuma. Hivi yeye amepata wapi fedha za kuanzisha magazeti haya yote?


Kwa muda mrefu nilikuwa nikihisi kuwa Mengi ndiye aliye nyuma ya kampeni zote chafu za kutuchafua baadhi yetu. Siku zote amekuwa akikanusha hilo kwangu lakini sasa amejianika na kujidhihirisha wazi kuwa ndiye kinara wa mbinu hizo chafu.


Wakati fulani mwaka jana, akiwa hewani umbali wa futi 35,000 kutoka usawa wa bahari, aliwaambia watu aliokuwa nao kwamba Jumatano inayofuata “tutammaliza Rostam katika MWANAHALISI”. Nilipopata habari hizo nilimpigia simu na yeye alikanusha vikali kuwa hakutamka maneno hayo. Nilimuamini lakini ilipofika Jumatano, kweli MWANAHALISI lilikuja na habari ya kunichafua kama alivyokuwa ameahidi Mengi.


Katika kipindi cha takriban mwaka mmoja uliopita, nilipata taarifa kwamba ni Mengi ndiye aliyekuwa akiendesha na kusimamia kampeni ya kunisakama kwa kupika na kusambaza habari zote chafu zilizolenga kunichafua. Nilipoonana naye kumueleza juu ya taarifa hizo, siyo tu aliruka sana bali pia aliapa kwa jina la mama, mke na mtoto wake kwamba hahusiki kabisa na kampeni hizo na kwamba hata yeye anakerwa nazo. Kujitokeza kwake wiki iliopita na tuhuma chafu dhidi yangu zisizo na ushahidi wowote sasa kumeweka kila kitu hadharani kwamba yeye ndiye kinara wa uchafuzi huu wenye lengo la kuleta chuki na mifarakano katika nchi.


Najua atakanusha haya kwa sababu yeye ni mwepesi wa kulalamika kuwa anaonewa huku akidhani amepewa haki na Mungu ya kuonea wengine.


Kwa upande mwengine, tabia na mwenendo wake havishangazi sana. Anaonekana kuchanganyikiwa. Hatua ya mzee wa zaidi ya miaka 70 anapofikia kuwaita wengine wauaji pasipo kutoa ushahidi wowote na pia kurejea madai ya kutaka kuuliwa au kudhuriwa mara kwa mara ni dalili ya kuchanganyikiwa. He is a paranoid old man!


Ni vyema Watanzania wakafahamu kwamba kila anapokabiliwa na matatizo au anapotenda maovu, kimbilio lake la haraka la kujifichia limekuwa ni kusaka huruma kwa wananchi kwa kutaka aonekane ni sehemu yao na kwamba anaonewa kwa kuwatetea wao. Ukweli ni kwamba amekuwa akifanya hivyo ili kutafuta hifadhi na kinga akijua ana madhambi mengi.


Kwa ufupi, Reginald Abraham Mengi ndiye kinara wa fitina zilizoivuruga nchi na hata kujaribu kuvuruga mipango ya Serikali ya kuwatumikia wananchi na kutekeleza ahadi zake. Halafu mtu huyu anapata ujasiri wa kudai eti anamuunga mkono Rais Jakaya Kikwete. Ameingiza vurugu kila mahala alipotia pua yake. Nchi imekuwa haiendi. Kila kukicha, shughuli imekuwa ni porojo zake na malumbano tu yanayotumia muda mwingi ambao ungeweza kutumika kuendeleza nchi na wananchi wake.


Niseme kwamba tofauti na yeye ambaye ameishia kutoa porojo zake bila ya kutoa ushahidi wowote na kufikisha hoja na ushahidi wake kwa vyombo vya sheria vinavyohusika, mimi nawagawia hapa baadhi tu ya ushahidi wa ufisadi wa Mengi ambao pia nakusudia kuuwasilisha pamoja na maelezo haya kwa vyombo hivyo ili wamchunguze Mengi na kuchukua hatua zipasazo. Kwa upande mwengine, nimewaagiza wanasheria wangu kuzifanyia kazi tuhuma za uzushi alizozitoa na kuchukua hatua za kisheria zinazofaa dhidi yake.


Nimalizie kwa kusema Reginald Abaraham Mengi hana mamlaka wala nguvu ya kimaadili (moral authority) ya kuwanyooshea vidole wengine kwa kuwaita mafisadi wala ya kujifanya ni shujaa wa kupambana na ufisadi. Sote tunakubali kwamba kuendesha vita dhidi ya ufisadi ni lazima lakini wale wanaopambana ni lazima vile vile wawe watu safi. Ukweli wa maelezo haya unaonyesha wazi kuwa Mengi hana sifa hiyo bali ni nyangumi wa ufisadi anayejaribu kuficha ufisadi wake kwa kuchafua watu wengine. Watanzania si wajinga kama anavyodhani yeye. Wanaelewa mchele ni upi na pumba ni zipi.


Nawashukuru kwa kunisikiliza.

Ahsanteni sana.

i372_Rostam.jpg




 
Last edited by a moderator:
. Alternatively he is it to apologize to me personally within 48 hours, failing all of which, I reserve the right to exercise any appropriate actions in order to expose his wrongdoings

Appropriate Actions according to who? MAFIOSO
 
Mmh something doesn't click, '...any appropriate actions in order to expose his wrongdoings...' Kwa hiyo malengo siyo kusafishiwa jina bali yanaenda mbele zaidi kuibua na yeye yale yote ayajuayo kuhusu mzee Mengi! Hapa naona ni biashara ya ntaje nkutaje (umemwaga mboga nami namwaga ugali).

I wish Mzee Mengi awe na bulungutu la ushahidi, aumwage..hapo ndio movie itakuwa worth kutazamika....
 
Kwanza wamechelewa kupeleka hata huko mahakamani, mbona Mengi mpiganaji aliwambia wapeleke siku ileile!!! Wanatafuta njia ya kujiosha lakini waangalie mtu mzima hawezi kusema kitu hovyohovyo tu, anajua anachosema na wasije wakaoga maji machafu bila kutegemea!!
 
kwa nini huyu bwana ni muoga sana kuongea hadharani? si bungeni au mbele ya waandishi wa habari....aliongea mara moja tu ile ya mtikila kwa vile alikuwa na ushahidi!!!!!
 
Nilichokibaini kwa upande mwingine ni kuwa, kama ukisoma katikati ya mistari hiyo statement ya RA, anamtukana Mengi matusi mabaya sana
 
Naona magazeti mengi ya leo yana hilo tamko la Rostam kwenda kwa Mengi....kichwa chake kwa kiswahili chasema:

"POROJO ZA MENGI"

Mmmmhhhhhhh! Naongeza stock yangu ya ze laga.
 
Jana asubui nilifanikiwa kuona interview TBC1 ya Waziri Sophia Simba kuhusu sakata la Mengi na wale aliowaita mafisadi papa. Mambo aliongelea kama waziri ndio msimamo wa serikali. Binafsi naona msimamo huo wa serikali una kasoro.

1) Kama serikali ilitaka kutoa tamko ingemtafuta waziri ambaye ni "eloquent" wa kuweza kuzungumzia swala nyeti kama hili la ufisadi. With due respect kwa Mheshimiwa Simba alijigonga gonga kuhusu maswali aliyokuwa anaulizwa. Majibu yake hayakuwa "factual" enough na hivyo kuoneka anapwaya! Kwa mfano mdogo, Marin Hassan alimuuliza dhana ya kutengenisha baishara na siasa na yeye akajibu kwamba katika wale watuhumiwa watano hakuna mwana siasa hata mmoja! Duinia nzima inajua kwamba Mhe. Rostam Aziz ni mbunge wa Igunga na mjumbe wa kamati Kuu ya CCM na alikuwa Mweka Hazina wa CCM. Juzi Mama Simba amenukuliwa kwenye gazeti akisema kwamba Kamati ya Maadili ya Viongozi haipaswi kujishugulisha pesa za viongozi zilizoko nje ya nchi! My foot!! Maoni yangu ni kwamba serikali ikiachia watu kama waziri Simba kuelezea msimamo wake katika mambo nyeti kama hili tunaweza tukaishia kama swala la Zitto Kabwe na Buzwagi. That issue was mishandled by the government at a high political cost.

2) Historia inatukumbusha kwamba mwaka juzi wakati swala la EPA lilipoibuka kwenye mtandao na Dr. Slaa kulileta Bungeni, Waziri Meghji (akiwa waziri-Fedha) na Spika walimbeza (skepticism) wakisema hakuna ushaidi na hayo ni mambo ya mitandao. Waingereza wanasema " It came to pass". Leo hii kesi za EPA zinanguruma mahakamani na waziri Meghji sio waziri tena!

3) Katika nchi yetu sio mara ya kwanza kutaja wazi wazi majina ya watuhumiwa wa ufisadi. Septemba 2007 Dr. Slaa na wenzake walitaja majina kumi ya watuhumiwa wa ufisadi pale MwembeYanga, Temeke. Baadhi yao walicharuka na kutishia kwenda mahakamani kwa kuchafuliwa na wengine wakasema hakuna ushaidi. Mpaka leo hakuna hata kesi moja ilifunguliwa mahakamani kwa "uzushi" huu! Leo hii Mhe. Lowassa, Karamagi na Chenge wako nje ya Baraza la Mawaziri kwa tuhuma kama walizosema kina Dr, Slaa. Mhe, Mramba, Yona na Mgonja wako mahakamani kwa tuhuma kama hizo. Rais mstaaafu Ben Mkapa halali usingiz mzurii kwa kutuhumiwa na umma kwa kutumia madaraka vibaya. Kinachoshangaza wakati wote huu sijaona serikali ikitoa msimamo wake mkali (kama Mama Simba) kuhusu watuhumiwa wa Dr. Slaa. Kulikoni sasa waziri anakuja mbogo kwa kutajwa mafisadi watano tu? Labda kwa kuwa limeongezeka neno " papa"? Mbona serikali haijatoa tamko kuhusu kutuhumiwa Rais mstaafu?

4) Mhe. Rostam Aziz amekuwa akitajwa tajwa katika haya mambo ya ovyo. It is not by coincedence, I believe. Alitajwa Mwenbeyanga, anatajwa katika wizi wa EPA, alitajwa na Tume ya Mwakyembe kuhusu Richmond na Dowans na sasa anatuhumiwa na Mengi kuwa ni fisadi "papa" . Huyu ni sawa na "Yuda Iscariot" kwa kuisaliti CCM hapaswi kula meza moja na viongozi wetu labda kama nao ni "birds of the same feathers"? Kwa nini asitolewe kamati kuu CCM hadi hatakapojitakasa? Bila hivyo maswali yataulizwa tu. Wakubwa wapende wasipende.

5) Tanil Somaiya amefadhili uchaguzi wa juzi wa UV-CCM kwa "mchango" wa shs. 400 milioni. Je waziri Simba hakuona kwamba kwa utetezi wake kwa hawa watuhumiwa kunaweza kukatafusiriwa kwamba serikali ya CCM inalipa fadhila? Je wananchi wakisema CCM imetekwa na matajiri kuna wakubisha?

6) Mama Simba anasema Mengi kama ana ushahidi aupeleke kwenye vyombo husika hususan TAKUKURU. Tunauliza TAKUKURU ipi? Hii inayoongozwa na Hosea? Kuna azimio la Bunge kuhusu kiongozi huyu kwa kuboronga uchunguzi wa ufisadi Richmond. Mengi kama mtu mwelevu hawezi kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere. Na hata wananchi hawana imani na Polisi katika mambo haya. Kama imani ingekuwepo serikali hii isengeitisha kura za maoni kutafuta wauaji wa Maalbino. Watu wangewataja watuhumiwa kwa jeshi la polisi na Polisi wangeisha maliza tatizo hili. Iko wapi ile orodha ya wauza unga aliyotuaaidi Mhe. Mwapachu akiwa waziri wa Usalama wa Taifa?

7) Sio mara ya kwanza wala haitakuwa ya mwisho kwa Mengi kuzozana hadharani na wafanya biashara wenzake. Walikwaruzana na Yusuf Manji mpaka wakafikishana mahakamani. Mengi alizozana na Rostam kuhusu Rostam kuzindua album katika kanisa moja la Kiluteri mpaka (tunaambiwa) mchungaji akachukuliwa hatua. Hakuna jipya na sisi hatuoni kwa nini serikali inaigilia mzozo huu. Kuna sheria zinazohusu kafsha na kama waliotajwa na Mengi wanafikiri wameonewa Mengi kwa kauli yake atafurahi kukutana nao. Manji ameshatinga mahakani ni Rostam aende huko. Why is the minister poking her nose in the affairs that do not concern her? Ana kihele hele. Kwa hili yeye ndie KACHEMSHA na aambiwe hivyo.

8) Swala la Ubaguzi wa rangi halina mashiko. Hatuwezi kuogopa kutajana na kusutana eti tutaambiwa ni wabaguzi. Kama Wahaya kumi ni wezi wa mali ya Umma nawatajwe. Mbona wachaga wanasemwa kwa kujazana TRA kwa misingi ya Ukabila na hawajalalama? Lipumba na wenzake walikuwa wapi wakati Salum Mohamed Salum akibaguliwa wazi wazi wakati wa mchakato wa Urais ndani ya CCM 2005 na hakuna aliyenyosha kidole? Rostam should not hide behind racism veil to justify his misdeeds.

Nimalizie kwa kutoa mfano wa Biblia. Yesu alipowasema sana mafarisayo, mazudakayo na wakuu wa dini ya kiyahudi walipanga njama ya kumuua. Na katika kuhalilisha kifo chake Kuhani Mkuu wa wakati ule jina lake Keyafa aliwashauri kwamba " inabidi mtu mmoja afe kwa ajili ya wengi". Baadhi ya magazeti yamesema Mengi kwa kufanya alichofanya anajitoa mhanga. Inawezekana lile neno likatimia. Hatuwezi kuendelea na uoza huu katika nchi yetu. Tanzania bila Ufisadi inawezekana.
 
Hii inafurahisha sana, huyu jamaa anaposema ana reserve right ya kutaja maovu ya Mengi anataka kutufikishia ujumbe gani? Huku ndo kupiga mbizi ukiwa umeshika kwenye kingo. Teheee!!!!
 
Kauli ya Rostam baada ya press conference ya Mengi ilikuwa kwamba kiumri, Mengi ni sawa na mzazi wa Rostam, hivyo isingekuwa busara kujibizana naye. Ni washauri gani waliombadilisha huyu hadi kutoa tamko hilo?
 
Hii inafurahisha sana, huyu jamaa anaposema ana reserve right ya kutaja maovu ya Mengi anataka kutufikishia ujumbe gani? Huku ndo kupiga mbizi ukiwa umeshika kwenye kingo. Teheee!!!!

Kweli hii kali; Sijui hizo rights alipata wapi hakimiliki yake inawezekana hata cosota kawekeza na kuchukua haki zote

Truely, his statements seems to be cautious and it looks like he is already scared

Duh!!!
 
Kauli ya Rostam baada ya press conference ya Mengi ilikuwa kwamba kiumri, Mengi ni sawa na mzazi wa Rostam, hivyo isingekuwa busara kujibizana naye. Ni washauri gani waliombadilisha huyu hadi kutoa tamko hilo?

Ndugu yangu haya mambo ya umri tuyaweke pembeni. Tanzania tumekaa miaka mingi tukifikiria umri mkubwa ndio busara na njia ya kukomboa nchi and what we got from those old people ni baraha tupu.

Simtetei RA ila anahaki ya kujitetea bila kuangalia umri, umri is nothing coming to ufisadi au biashara. Ila huyu RA ajiangalie asitegemee watanzania tutanunua huu utetezi usio na miguu wala mikono.
 
Rostam nae anachemka. Anasema kama Mengi ana ushahidi basi Mengi ateue chombo cha kisheria au cha serikali kichukue hatua zinazotakiwa. Mengi kawa Director of Public Prosecution? duuu

Halafu Rostam anasema mtu anae toa opinion kwa kesi ambayo iko mahakamani basi hiyo kisheria ni contempt of court. Rostam anahitaji msaada wa wakili, awali ya yote, kama kaandika mwenyewe hivi vitu.

Ila Mengi ane alichemka kurudia rudia wimbo wa Manji na Patel, na Mithun Chakraborty na Shashi Kapoor... anauimba toka the 1990s.
 
Last edited:
Mbunge wa Igunga na Mweka hazina wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, hatimaye amejibu rasmi madai mazito yaliyotolewa na Reginald Mengi kuhusu "mafisadi papa". Tamko hilo rasmi linapatikana katika ukurasa wa 6 wa gazeti la 'The Citizen' la leo Alhamisi, tarehe 30 Aprili 2009. Wakati tunamsubiri nakala yake tupate dondoo hii kutoka kwenye hitimisho la tamko hilo:

"I am therefore calling upon Mr. Mengi to either surrender whatever evidence he has to support his wild accusations and to appoint the appropriate legal bodies or state organs to act accordingly. Alternatively he is it to apologize to me personally within 48 hours, failing all of which, I reserve the right to exercise any appropriate actions in order to expose his wrongdoings"
LOL
Bwa ha-ha-ha-ha-hah, Bwa ha-ha-ha-ha-hah!


Mbavu sina!

attachment.php
 

Attachments

  • mbavu sina.PNG
    mbavu sina.PNG
    4.4 KB · Views: 1,076
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom