Tamko la Lissu kuhusiana na sakata la kesi ya Arusha; Mbowe naye alonga

Taarifa ya vikao vya bunge inajulikana kwa kila mtu isipokuwa Judge Magessa wa Arusha. Sasa amkamate Mbowe aone!

Dola haitishwi ww, na huna uwezo wa kubishana na dola . Mbona hapo kabla aliisha kamatwa, ulifanya nn sasa kumtoa ili hali alilazwa sakafuni na kipigo juu
 
Crap
Hajajibu chochote hapo zaidi ya porojo nyingi zisizo na mashiko kabisa. Mdhamini wake mbona nae hakufika ? Mbowe hana kinga hiyo na akamatwe kwa kuidharau mahakama. Yeye avunje sheria eti ni kiongozi wa kambi kivuli ya upinzani. Mkae mkielewa kivuli, maana yake si halisi, hivyo yeye ni kiongozi wa kambi isiyo halisi hana nguvu.
UNAHITAJI NURU WEWE Japokua upo kwenye Mwanga
 
Hapa ndio siku zote ninapoingia kiwewe na wanasheria au wana taaluma mbalimbali huko Tanzania. Kwani wanaonekana wanakuwa wazuri sana wanapokuwa nje ya siasa lakini wakiingia kwenye siasa tu basi na taaluma zao zinapotea.

Sasa hapa namshangaa sana mwanasheria mahiri Tindu Lissu. Amesahau kabisa kujua kuwa Kuna mihimili mitatu nayo ni Serikali, Mahakama na Bunge na kila kimoja kina kanuni zake.

Kinachoweza kuviunganisha hivi ni TAARIFA na si vinginevyo. Kwa mujibu wa hapa Mbowe ana makosa ya Kudharau mahakama kwani Hakimu Hana taarifa ya vikao vyake vya Bunge. Ilimpasa MBOWE atoe taarifa ya maandishi kwa hakimu kuwa nina shughuli za Kibunge basi mambo yangeisha na hapa sasa mila na desturi zinakuwa applied.

hakimu hawezi soma kutoka kwenye magazeti au kusikia radioni kuwa Mbowe anahudhuria Bunge.

Naomba Lissu na wabunge wenzako muangalie sheria na sio kuleta dharau dhidi ya mihimili mingine ya doula.

Kama umefutailia hili swaga vizuri, utaona kuwa hakimu alipewa tayari taarifa ya maandishi kuhusiana na wabunge kuwa na udhuru kwa shughuli za kibunge, akakataa. Kwa hiyo alitumiwa barua kwa maandishi.

Pili Tundu Lissu anajaribu kuelezea sheria za nchi zinavyofanyakazi, akimaanisha sheria mama. Hizi sheria zinahusu mihili yote mitatu, na ukumbuke hajasema kuwa Mbowe hakamatiki ila ni kupitia kwa Spika halafu spika atoe ruhusa, wakati wa kazi. na vile vile lazima spika akiombwa akakikubali anamwambia Mbunge na mbunge anakwenda sehemu husika, hakuna swala la kukimbizana na Mbunge na kudhalilishana. Muda wa kuwaelimisha Magamba umefika tunakwenda nao sambamba mwaka huu. Wakiamka wananchi wote wajanja.
 
Chadema nanyi mna mzinzi wenu Saanane,hata kenyewe kangesema hivyo tu.kamemtia Mimba Rebecca Tusizwe wa Ubalozi wa South Africa nchini,kaiteni hapa kajisafishe.Ibilisi

Hiyo ya mimba ya mtu tena mfanya kazi ubalozini ni ujiko na sifa kubwa isitoshe ni heshima maana kajenga undugu!sema lingine
 
Hapa ndio siku zote ninapoingia kiwewe na wanasheria au wana taaluma mbalimbali huko Tanzania. Kwani wanaonekana wanakuwa wazuri sana wanapokuwa nje ya siasa lakini wakiingia kwenye siasa tu basi na taaluma zao zinapotea.

Sasa hapa namshangaa sana mwanasheria mahiri Tindu Lissu. Amesahau kabisa kujua kuwa DOULA ina mihimili mitatu nayo ni Serikali, Mahakama na Bunge na kila kimoja kina kanuni zake.

Kinachoweza kuviunganisha hivi ni TAARIFA na si vinginevyo. Kwa mujibu wa hapa Mbowe ana makosa ya Kudharau mahakama ambao ni muhimili unaojitegemea kabisa kwani Hakimu Hana taarifa ya vikao vyake vya Bunge. Ilimpasa MBOWE atoe taarifa ya maandishi kwa hakimu kuwa nina shughuli za Kibunge basi mambo yangeisha na hapa sasa mila na desturi zinakuwa applied.

Hakimu hawezi soma kutoka kwenye magazeti au kusikia radioni kuwa Mbowe anahudhuria Bunge.

Vile vile Polisi ni sehemu ya muhimili wa Serikali. Sioni kwa nini wanachanganya mada hapo. Polisi wanakazi kubwa ya kuhakikisha sheria zinafuatwa. Na mtuhumiwa akifikishwa mahakamani basi pale atakuwa chini ya kanuni za mahakama mpaka atakapopata hukumu yake.

Naomba Lissu na wabunge wenzako muangalie sheria na sio kuleta dharau dhidi ya mihimili mingine ya doula.

ilitakiwa achukue kibali kwa spika wa bunge ndipo aendelee na taratibu zingine
 
Crap
Hajajibu chochote hapo zaidi ya porojo nyingi zisizo na mashiko kabisa. Mdhamini wake mbona nae hakufika ? Mbowe hana kinga hiyo na akamatwe kwa kuidharau mahakama. Yeye avunje sheria eti ni kiongozi wa kambi kivuli ya upinzani. Mkae mkielewa kivuli, maana yake si halisi, hivyo yeye ni kiongozi wa kambi isiyo halisi hana nguvu.

AkIkamatwa Mbowe basi JK na Mkapa nao washikwe kwa kudharau mahakama katika kesi ya Prof Mahalu
 
mh! huyu hakimu akifuata maadili ya kazi yake hataaibika hv mpaka sasa anaelekea kushindwa kuindesha kesi hii kutokana na kukurupuka kwake mara kwa mara inaonesha wazi hatambui mipaka ya mihimili 3 ya serikali anaaibisha taaluma ya uanasheria tz

Lazima waChadema mujuwe kuwa hakimu haongozwi na taarifa za magazeti au radioni. Labda niwaulize JE Mh MBOWE aliiarifu mahakama kwa maneno au maandishi kuwa yeye anahudhuria vikao vya Bunge? kama hakufanya hivyo anafikiri hakimu atajuaje kuwa yupo kwenye vikao au ndio anaidharau mahakama kwa kuwa yeye ni kiongozi wa upinzani Bungeni?
 
Hiyo Photoshop trick uliyotumia ndio inayokuzuzua ila kiukweli unamzimia Dk wa Ukweli

Hi picha kaweka kama avata yake baada ya kuitohoa ili aweze kuipotosha umma,hakika your great foolish
 
Hapa ndio siku zote ninapoingia kiwewe na wanasheria au wana taaluma mbalimbali huko Tanzania. Kwani wanaonekana wanakuwa wazuri sana wanapokuwa nje ya siasa lakini wakiingia kwenye siasa tu basi na taaluma zao zinapotea.

Sasa hapa namshangaa sana mwanasheria mahiri Tindu Lissu. Amesahau kabisa kujua kuwa (DOULA) ina mihimili mitatu nayo ni Serikali, Mahakama na Bunge na kila kimoja kina kanuni zake.

Kinachoweza kuviunganisha hivi ni TAARIFA na si vinginevyo. Kwa mujibu wa hapa Mbowe ana makosa ya Kudharau mahakama ambao ni muhimili unaojitegemea kabisa kwani Hakimu Hana taarifa ya vikao vyake vya Bunge. Ilimpasa MBOWE atoe taarifa ya maandishi kwa hakimu kuwa nina shughuli za Kibunge basi mambo yangeisha na hapa sasa mila na desturi zinakuwa applied.

Hakimu hawezi soma kutoka kwenye magazeti au kusikia radioni kuwa Mbowe anahudhuria Bunge.

Vile vile Polisi ni sehemu ya muhimili wa Serikali. Sioni kwa nini wanachanganya mada hapo. Polisi wanakazi kubwa ya kuhakikisha sheria zinafuatwa. Na mtuhumiwa akifikishwa mahakamani basi pale atakuwa chini ya kanuni za mahakama mpaka atakapopata hukumu yake.

Naomba Lissu na wabunge wenzako muangalie sheria na sio kuleta dharau dhidi ya mihimili mingine ya doula.

Kwenye blue hapo mbona unaongea lugha za kigaidi?
halafu inawezekana wewe unatafutwa na CIA
tuachie nchi yetu,
 
Wakuu habari!!

Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe leo wamezungumza na vyombo vya habari kwenye Ofisi za Kambi ya Upinzani DSM kuhusiana na amri ya mahakama kutaka kumkamata Kamanda Mbowe.

Jisomeeni wenyewe!!

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Simu Na. 026 2322761-5
Fax Na. (255) 026 2324218
E-Mail: mbowe2008@gmail.com

(Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa
Kiongozi wa Upinzani)

OFISI YA BUNGE

S.L.P. 941 DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

AMRI YA KUMKAMATA KIONGOZI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI YAINGILIA UHURU WA BUNGE, YAHATARISHA DEMOKRASIA!!!
Dar es Salaam, Juni 3, 2011:

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imepokea kwa mshtuko, masikitiko na mshangao mkubwa taarifa za Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha kutoa amri ya kumkamata Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe. Mheshimiwa Mbowe pamoja na Wabunge, viongozi na wanachama kadhaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanakabiliwa na mashtaka kadhaa yanayotokana na maandamano tarehe 5 Januari 2011 katika Jiji la Arusha yaliyopelekea Jeshi la Polisi kuua wananchi watatu na kujeruhi wengine wengi. Taarifa zinaonyesha kwamba amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Charles Magessa, siku ya Ijumaa ya tarehe 27 Mei 2011 na kurudiwa tena jana, yaani tarehe 2 Juni 2011.

Mheshimiwa Mbowe hakuhudhuria mahakamani katika tarehe zote mbili kwa vile amekuwa akihudhuria vikao vya Kamati mbali mbali za Bunge vilivyoanza tarehe 23 Mei 2011 na ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotazamiwa kuanza tarehe 7 Juni hadi tarehe 7 Septemba 2011. Kama Mbunge na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Mbowe ni mjumbe wa Kamati mbali mbali za Bunge kama vile Kamati ya Uongozi, Kamati ya Kanuni za Bunge na Kamati ya Fedha na Uchumi. Aidha, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni mjumbe katika Tume ya Utumishi wa Bunge na ndiye msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na amri ya kumkamata Mheshimiwa Mbowe kwa vile inakiuka moja kwa moja sheria, mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, haki na mamlaka ya Bunge na ambazo ndio msingi mkuu wa demokrasia yetu ya kibunge. Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua na kulinda "uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge." Uhuru huu wa kikatiba umetiliwa mkazo katika vifungu vya 5, 6 na 11 vya Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge ya mwaka 1988 vinavyokataza Mbunge kukamatwa au kupewa amri ya kuhudhuria mahakamani wakati akiwa ndani ya eneo la Bunge au wakati Bunge limekutana bila kuwepo kwa kibali cha Spika.

Maneno ‘eneo la Bunge' limetafsiriwa na kifungu cha 2 cha Sheria hiyo kumaanisha "ukumbi ambao hutumiwa kwa vikao vya Bunge, pamoja na ofisi, vyumba, vibambaza (lobbies), maeneo ya wageni (galleries), courtyards, bustani na maeneo mengine yaliyowekwa kwa ajili ya matumizi au malazi ya wajumbe, maafisa au wageni wa Bunge pamoja na njia zinazounganisha maeneo hayo na maeneo mengine yanayoweza kutangazwa na Spika kuwa ndani ya maeneo ya Bunge." Kwa maana hiyo, Mbunge anapokuwa anahudhuria vikao vya Bunge au Kamati zake au anapokuwa mahali pengine popote kwa kuitikia wito wa kuhudhuria vikao hivyo vya Bunge hawezi akakamatwa ili kutekeleza amri ya Mahakama au ya chombo kingine chochote nje ya Bunge.

Kufuatana na mila na desturi za kibunge za Jumuia ya Madola ambazo nchi yetu imezikubali na inatakiwa kuzifuata, kinga ya Wabunge dhidi ya kukamatwa inakuwa na nguvu wakati wa mkutano wa Bunge pamoja na ‘muda muafaka na wa kutosha' kabla na baada ya mkutano wa Bunge. Kwa mujibu wa Erskine May, mwandishi maarufu wa mila na desturi za mabunge ya Jumuia ya Madola, "muda muafaka na wa kutosha umechukuliwa kwa ujumla kuwa ni siku arobaini kabla na baada ya mkutano wa Bunge." Kwa mantiki hiyo, wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha inatoa amri dhidi yake, Mheshimiwa Mbowe alikuwa analindwa na kinga ya Bunge. Aidha, Mheshimiwa Mbowe ataendelea kulindwa na kinga hiyo kwa kipindi chote cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na ‘muda muafaka na wa kutosha' - kama unavyotambuliwa katika mila na desturi za Mabunge ya Jumuia ya Madola - utakapokwisha baada ya Mkutano huo!

Kwa upande mwingine, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshangazwa na unafiki na ubaguzi wa wazi unaoonyeshwa na Jeshi la Polisi juu ya Wabunge wa vyama vya upinzani. Hii ni kwa sababu wakati Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata Wabunge wa Upinzani bila kuomba kibali chochote cha Spika kama inavyotakiwa na Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge - kama ilivyotokea kwa Wabunge wa CHADEMA Waheshimiwa Mbowe, Godbless Lema (Arusha Mjini), Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Joseph Selasini (Rombo), Meshack Opulukwa (Meatu), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Esther Matiko (Viti Maalum, CHADEMA) na Magdalena Sakaya (Viti Maalum, CUF), wabunge wa CCM – na ambao wanakabiliwa na tuhuma za makosa makubwa zaidi – wamekuwa wanaombewa kibali cha Spika kabla ya kukamatwa. Kwa hili, tuna ushahidi wa barua ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mwanza SP B.M. Wakulyamba kwa Katibu wa Bunge ya kumwomba Mheshimiwa Titus Mlengeya Kamani (Busega, CCM) ili akahojiwe na Jeshi la Polisi kuhusu kuhusika kwake na njama za kutaka kumwuua aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Busega Dk. Raphael Masunga Chegeni. Barua hiyo ya tarehe 31 Mei 2011 ilinakiliwa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, Makao Makuu ya Polisi DCI Robert Manumba. Hakuna Mbunge hata mmoja wa CHADEMA au chama kingine cha upinzani ambaye – kwa taarifa zetu – amewahi kuombewa kibali cha kukamatwa na Polisi kama inavyoonekana kwa Wabunge wa CCM. Hii inadhirihisha upendeleo wa wazi wa Jeshi la Polisi kwa Wabunge wa CCM

Kwa sababu hizo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haitarajii, na itapinga kwa nguvu zake zote, kitendo chochote cha kumtishia au kumkamata Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kwa kipindi chote ambacho ana kinga ya Bunge kama inavyotambuliwa na Katiba na sheria zetu pamoja na mila na desturi za kibunge ambazo tumechagua kuzifuata kwa hiari yetu wenyewe. Aidha, tunatarajia Mahakama pamoja na vyombo vingine vyote vilivyoanzishwa na vinavyofanya kazi zake kwa mujibu wa sheria za nchi yetu vitatumia busara ili kuiepusha nchi yetu na fedheha ya kuonekana inakamata Wabunge wake wakati wakiwa wanatekeleza wajibu wao wa kibunge!

------------------------------------
Tundu A.M. Lissu (MB.)
Mnadhimu Mkuu
KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

Aluta Continua
Kutoka Ofisi ndogo za Bunge

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Jamani siku hizi bunge halina domain za kutoa email kwa wabunge? Mbowe, how can you use your personal email for office purpose?
 
Lazima waChadema mujuwe kuwa hakimu haongozwi na taarifa za magazeti au radioni. Labda niwaulize JE Mh MBOWE aliiarifu mahakama kwa maneno au maandishi kuwa yeye anahudhuria vikao vya Bunge? kama hakufanya hivyo anafikiri hakimu atajuaje kuwa yupo kwenye vikao au ndio anaidharau mahakama kwa kuwa yeye ni kiongozi wa upinzani Bungeni?

Kama umefutailia hili swaga vizuri, utaona kuwa hakimu alipewa tayari taarifa ya maandishi kuhusiana na wabunge kuwa na udhuru kwa shughuli za kibunge, akakataa. Kwa hiyo alitumiwa barua kwa maandishi.

Pili Tundu Lissu anajaribu kuelezea sheria za nchi zinavyofanyakazi, akimaanisha sheria mama. Hizi sheria zinahusu mihili yote mitatu, na ukumbuke hajasema kuwa Mbowe hakamatiki ila ni kupitia kwa Spika halafu spika atoe ruhusa, wakati wa kazi. na vile vile lazima spika akiombwa akakikubali anamwambia Mbunge na mbunge anakwenda sehemu husika, hakuna swala la kukimbizana na Mbunge na kudhalilishana. Muda wa kuwaelimisha Magamba umefika tunakwenda nao sambamba mwaka huu. Wakiamka wananchi wote wajanja.

Nadhami hujasoma hii post nimeinukuu kwa ajili yako
 
Lazima waChadema mujuwe kuwa hakimu haongozwi na taarifa za magazeti au radioni. Labda niwaulize JE Mh MBOWE aliiarifu mahakama kwa maneno au maandishi kuwa yeye anahudhuria vikao vya Bunge? kama hakufanya hivyo anafikiri hakimu atajuaje kuwa yupo kwenye vikao au ndio anaidharau mahakama kwa kuwa yeye ni kiongozi wa upinzani Bungeni?

Alitoa taarifa Hakimu akakataa, wewe tushauri ulitaka Mh Mbowe afanye nini?
 
Wakuu habari!!

Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe leo wamezungumza na vyombo vya habari kwenye Ofisi za Kambi ya Upinzani DSM kuhusiana na amri ya mahakama kutaka kumkamata Kamanda Mbowe.

Jisomeeni wenyewe!!

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Simu Na. 026 2322761-5
Fax Na. (255) 026 2324218
E-Mail: mbowe2008@gmail.com

(Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa
Kiongozi wa Upinzani)

OFISI YA BUNGE

S.L.P. 941 DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

AMRI YA KUMKAMATA KIONGOZI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI YAINGILIA UHURU WA BUNGE, YAHATARISHA DEMOKRASIA!!!
Dar es Salaam, Juni 3, 2011:

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imepokea kwa mshtuko, masikitiko na mshangao mkubwa taarifa za Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha kutoa amri ya kumkamata Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe. Mheshimiwa Mbowe pamoja na Wabunge, viongozi na wanachama kadhaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanakabiliwa na mashtaka kadhaa yanayotokana na maandamano tarehe 5 Januari 2011 katika Jiji la Arusha yaliyopelekea Jeshi la Polisi kuua wananchi watatu na kujeruhi wengine wengi. Taarifa zinaonyesha kwamba amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Charles Magessa, siku ya Ijumaa ya tarehe 27 Mei 2011 na kurudiwa tena jana, yaani tarehe 2 Juni 2011.

Mheshimiwa Mbowe hakuhudhuria mahakamani katika tarehe zote mbili kwa vile amekuwa akihudhuria vikao vya Kamati mbali mbali za Bunge vilivyoanza tarehe 23 Mei 2011 na ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotazamiwa kuanza tarehe 7 Juni hadi tarehe 7 Septemba 2011. Kama Mbunge na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Mbowe ni mjumbe wa Kamati mbali mbali za Bunge kama vile Kamati ya Uongozi, Kamati ya Kanuni za Bunge na Kamati ya Fedha na Uchumi. Aidha, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni mjumbe katika Tume ya Utumishi wa Bunge na ndiye msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na amri ya kumkamata Mheshimiwa Mbowe kwa vile inakiuka moja kwa moja sheria, mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, haki na mamlaka ya Bunge na ambazo ndio msingi mkuu wa demokrasia yetu ya kibunge. Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua na kulinda “uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.” Uhuru huu wa kikatiba umetiliwa mkazo katika vifungu vya 5, 6 na 11 vya Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge ya mwaka 1988 vinavyokataza Mbunge kukamatwa au kupewa amri ya kuhudhuria mahakamani wakati akiwa ndani ya eneo la Bunge au wakati Bunge limekutana bila kuwepo kwa kibali cha Spika.

Maneno ‘eneo la Bunge’ limetafsiriwa na kifungu cha 2 cha Sheria hiyo kumaanisha “ukumbi ambao hutumiwa kwa vikao vya Bunge, pamoja na ofisi, vyumba, vibambaza (lobbies), maeneo ya wageni (galleries), courtyards, bustani na maeneo mengine yaliyowekwa kwa ajili ya matumizi au malazi ya wajumbe, maafisa au wageni wa Bunge pamoja na njia zinazounganisha maeneo hayo na maeneo mengine yanayoweza kutangazwa na Spika kuwa ndani ya maeneo ya Bunge.” Kwa maana hiyo, Mbunge anapokuwa anahudhuria vikao vya Bunge au Kamati zake au anapokuwa mahali pengine popote kwa kuitikia wito wa kuhudhuria vikao hivyo vya Bunge hawezi akakamatwa ili kutekeleza amri ya Mahakama au ya chombo kingine chochote nje ya Bunge.

Kufuatana na mila na desturi za kibunge za Jumuia ya Madola ambazo nchi yetu imezikubali na inatakiwa kuzifuata, kinga ya Wabunge dhidi ya kukamatwa inakuwa na nguvu wakati wa mkutano wa Bunge pamoja na ‘muda muafaka na wa kutosha’ kabla na baada ya mkutano wa Bunge. Kwa mujibu wa Erskine May, mwandishi maarufu wa mila na desturi za mabunge ya Jumuia ya Madola, “muda muafaka na wa kutosha umechukuliwa kwa ujumla kuwa ni siku arobaini kabla na baada ya mkutano wa Bunge.” Kwa mantiki hiyo, wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha inatoa amri dhidi yake, Mheshimiwa Mbowe alikuwa analindwa na kinga ya Bunge. Aidha, Mheshimiwa Mbowe ataendelea kulindwa na kinga hiyo kwa kipindi chote cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na ‘muda muafaka na wa kutosha’ - kama unavyotambuliwa katika mila na desturi za Mabunge ya Jumuia ya Madola - utakapokwisha baada ya Mkutano huo!

Kwa upande mwingine, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshangazwa na unafiki na ubaguzi wa wazi unaoonyeshwa na Jeshi la Polisi juu ya Wabunge wa vyama vya upinzani. Hii ni kwa sababu wakati Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata Wabunge wa Upinzani bila kuomba kibali chochote cha Spika kama inavyotakiwa na Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge - kama ilivyotokea kwa Wabunge wa CHADEMA Waheshimiwa Mbowe, Godbless Lema (Arusha Mjini), Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Joseph Selasini (Rombo), Meshack Opulukwa (Meatu), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Esther Matiko (Viti Maalum, CHADEMA) na Magdalena Sakaya (Viti Maalum, CUF), wabunge wa CCM – na ambao wanakabiliwa na tuhuma za makosa makubwa zaidi – wamekuwa wanaombewa kibali cha Spika kabla ya kukamatwa. Kwa hili, tuna ushahidi wa barua ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mwanza SP B.M. Wakulyamba kwa Katibu wa Bunge ya kumwomba Mheshimiwa Titus Mlengeya Kamani (Busega, CCM) ili akahojiwe na Jeshi la Polisi kuhusu kuhusika kwake na njama za kutaka kumwuua aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Busega Dk. Raphael Masunga Chegeni. Barua hiyo ya tarehe 31 Mei 2011 ilinakiliwa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, Makao Makuu ya Polisi DCI Robert Manumba. Hakuna Mbunge hata mmoja wa CHADEMA au chama kingine cha upinzani ambaye – kwa taarifa zetu – amewahi kuombewa kibali cha kukamatwa na Polisi kama inavyoonekana kwa Wabunge wa CCM. Hii inadhirihisha upendeleo wa wazi wa Jeshi la Polisi kwa Wabunge wa CCM

Kwa sababu hizo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haitarajii, na itapinga kwa nguvu zake zote, kitendo chochote cha kumtishia au kumkamata Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kwa kipindi chote ambacho ana kinga ya Bunge kama inavyotambuliwa na Katiba na sheria zetu pamoja na mila na desturi za kibunge ambazo tumechagua kuzifuata kwa hiari yetu wenyewe. Aidha, tunatarajia Mahakama pamoja na vyombo vingine vyote vilivyoanzishwa na vinavyofanya kazi zake kwa mujibu wa sheria za nchi yetu vitatumia busara ili kuiepusha nchi yetu na fedheha ya kuonekana inakamata Wabunge wake wakati wakiwa wanatekeleza wajibu wao wa kibunge!

------------------------------------
Tundu A.M. Lissu (MB.)
Mnadhimu Mkuu
KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

Aluta Continua
Kutoka Ofisi ndogo za Bunge

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
Ahsante saana Mhs Mbunge Bi Regia Mtema kwa kutujulisha hilo, nadhani wengi tulikuwa vipofu. Kumbe sheria za bunge letu zipo, ila watu wameamua kuzikanyaga tu kama ilivyo destuli ya utawala huu wa maghamba!!!!!!!!!!! Mbunge ana heshima zake Bwn ya nini anyanyaswe????????? Spika Anna Makinda yuko wapi kutetea wabunge wake, au wapinzani hawamuhusu?????????
 
ilitakiwa achukue kibali kwa spika wa bunge ndipo aendelee na taratibu zingine

Nafikiri hapa unachanganya mambo. Kwenye Kesi Mbowe alitakiwa kutoa Taarifa kuwa hakimu kwa maandishi kuwa anahudhuria vikao vya Bunge.

Sasa Polisi wanapotaka kumkamata wanatakiwa wapate kibali kwa Spika. Lakini kwa kosa lake la kutakiwa akamatwe kwa Amri ya mahakama hapa hakuna kibali anatakiwa akamatwe na kuwekwa rumande mpaka siku shauri lake litakapo tajwa
 
Akamatwe kama amri inavyotaka, hakuna aibu yoyote hapo ! yeye ni kiongozi wa kambi feki bungeni hana hadhi ya kutokamatwa ( kivuli = feki )

Sio kosa lako ni yale magamba yaliobaki hayajui kinachondelea duniani! :A S 39:
 
Mbowe hayuko juu ya Sheria, lazima sheria za nchi zifuatwe!. kama alikuwa na majukumu ya kikazi za kibunge, ni lazima angetuma mwakilishi(mdhamini) wake hapo mahakamani. Sheria iheshimiwe, hatuwezi kuendesha nchi kikanjnja na personality
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Taarifa ya vikao vya bunge inajulikana kwa kila mtu isipokuwa Judge Magessa wa Arusha. Sasa amkamate Mbowe aone!
FJM, hana hadhi ya kuwa Judge huyo jamaa. Ni Hakimu mkazi tuu, na nina mashaka kama Degree yake iko sawa. Ukiwapa u Judge watu kama hawa kila siku hata kesi ya madai wao wananyonga tuu.
 
Back
Top Bottom