sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Alichokifanya Kafulila sioni kama ni kosa,kama alikwisha sema na umma mzima ukasikia na spika akafumba macho bila kutaka kusoma na kutaka uthibitisho toka kwa Mh.Kafulila mlitaka yeye fanye nini zaidi ya kuwalikisha fikra na mawazo yake.
Pili bunge hii limekuwa la kulindana pasi na sababu za msingi.Tumeona aliyekuwa mbunge wa Arusha bwana Godbless Lema alivyouliza hatua gani kwa kutumia kanuni za bunge zitachukuliwa kama mbunge atathibitika amelidanganya bunge.Maamuzi ya kukurupuka badala ya kujibu swali la msingi lilipelekea spika wa bunge kumtaka atoe maelezo kimaandishi,maandishi yametolewa kama alivyoagiza lakini hakuna hat stahiki alizochukuliwa mpaka mahakama inatengua matokeo yake ya ubunge.
Mawazo yako mh.Kafulila yanafaa kufanyiwa kazi ikithibitika kanunu na sheria zinazoliongoza bunge zichukuwe mkondo wake.Esma kweli daima fitina kwako iwe mwiko kwa maslahi ya taifa.

Siungi mkono tamko la Ndugu Kafulila.
Siungi mkono kwa sababu nafahamu ,pamoja na matatizo yetu ya kimfumo na kitaasisi ,bado tunaamini katika utawala wa sheria ambao ni moja ya misingi na viashiria vya dhana ya demokrasia.
Hadi hapo mahakama itakapotamka vinginevyo ,mbunge mtuhumiwa asitendewe kama mtu aliyepatikana na hatia.Kwa sasa bado ni mtuhumiwa tu.
Vinginevyo,kwa siasa zetu za ajabu ,zinazoratibiwa na CCM & washirika wake,tunaweza kupoteza wabunge wetu wengine mahiri kama tukikubaliana na hoja iliyoletwa.Eti mtu avuliwe ubunge kwa kutuhumiwa tu!Hata mahakama hazifikii hukumu bila kuzingatia na kupima ushahidi.
Hata hivyo,ni juu ya mbunge anayetuhumiwa kutafakari na kufuata kile dhamira yake inamuelekeza.
Kama kweli anafahamu ametenda kosa husika,hana sababu yoyote ya kusubiri hukumu ya mahakama kuweza kufanya uamuzi.Alipaswa awe amkwisha kujiuzulu nafasi yake tangu jana alipokamatwa.
Nataka kueleweka wazi kuwa matazamo wa kisheria (legality) usiwekwe katika fungu moja na mtazamo wa kimaadili (morality) ingawa dhana hizi mbili,aghalabu, huhusiana katika mazingira mahususi.Hoja hii inaimarishwa na ukweli kuwa mtuhumiwa anaweza kuwa alitenda kosa kabisa ,dhamira yake ikimshuhudia,lakini hatimaye, mwenendoo & hukumu /ushahidi wa kimahakama ukaaamua kutomtia hatiani.
Ni kwa kuzingatia ukweli huu, bado Ndugu Kafulila anaendelea na majukumu yake ya kibunge,licha ya kuwa na kesi mahakamani na chama chake kuhusiana na uanachama wake.Vinginevyo,asingetoa tamko lake kama mjumbe wa kamati ya bunge, bali kama mwanachi anayewajibika!