Tamko la Jipya UDOMASA, Mkutano utaendelea kesho

Colgate

Member
Dec 30, 2010
16
1
*UDOMASA*

University of Dodoma Academic Staff Association

University of Dodoma, Chimwaga Complex, P.O. Box 259,Udom,
Cell +255 755210310 +255 755210310
+ 255 786 336690 + 255 786336690
Email: udomasa2011@gmail.com

*MAENDELEO YA MKUTANO WA WAHADHIRI CHUO KIKUU CHA DODOMA*

Mkutano endelevu wa wadhahiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma utaendelea siku
ya Alhamis, tarehe 13 Januari, 2011 ili kuendelea kusubiri majibu kutoka
kwa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Lakini tunasikitika kuwa kumekuwa na upotoshwaji wa matatizo ya msingi
ya yanayotukabili. Menejimenti ya UDOM imeripotiwa na vyombo vya habari
imekuwa na mazungumzo na wahadhiri. Tunapenda kuweka wazi kuwa tangu
tuanze mikutano yetu endelevu hatujafanya mazungumzo yoyote na
menejimenti ya Chuo.

Aidha, menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma imekuwa ikitoa taarifa za
uongo juu ya madai ya wahadhiri. Kwa mfano, menejimenti ya chuo
imeripotiwa ikidai kuwa mishahara iliyoletwa chuoni hapa na Hazina
imekosewa. Wahadhiri wamesikitishwa sana na taarifa hizi za uongo.

Tunapenda kuweka wazi kuwa mishahara mipya iliyoletwa chuoni ni sawa na
ngazi ya mishahara iliyolipwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kwa mfano /Tutorial Assistant/ (PUTS 12), kwenye vyuo vyote viwili
imekuwa Tsh 1,248,070/=, lakini UDOM imekatwa. Wahadhiri wamebaini
nyaraka za ndani ya chuo Kikuu cha Dodoma zikionyesha kuwa mishahara
mipya imeletwa na kimsingi hazina makosa yoyote kwa wanataaluma.
Tunasikitika kuwa tatizo hili la udanganyifu linalofanywa na menejimenti
ya chuo litazidisha mgogoro huu badala ya kuelekea katika utatuzi.

Wakati huo huo menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma, kupitia kwa Makamu
Mkuu wake Profesa Idrisa Kikula, imeripotiwa ikidai kuwa wahadhiri
wamekosa uelewa na madai yao si ya msingi. Wadhahiri wanasikitishwa na
kauli hizi ambazo zinatolewa na menejimenti. Tunapenda kuweka wazi kuwa
kauli hizi za menejimenti zina lengo la kukwepa uwajibikaji. Tunapenda
kusisitiza kuwa Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Idrisa Kikula aiombe radhi
jumuiya hii ya wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Imeripotiwa na menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma kuwa viongozi wa
wahadhiri walioenda Hazina hawakutoa taarifa sahihi kwa wahadhiri
wenzao. Tunapenda kuweka wazi kuwa viongozi wa wahadhiri wamekwenda
Hazina mara mbili na kujiridhisha kuwa mishahara mipya ililipwa kwa Chuo
Kikuu cha Dodoma mwezi Novemba na Desemba mwaka jana. Viongozi wa
wahadhiri wametoa taarifa sahihi sana kwa wahadhiri wenzao, na hii ni
baada ya kufanya mchakato wa ufuatiliaji, Hazina, Utumishi na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Mbali na kufuatilia tulikwishaandika barua
kuwajulisha juu ya hili.

Mbali na juhudi mbalimbali tunazofanya kuhakikisha tunapata haki zetu,
ikiwamo kumsubiri Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
tumeazimia jana, 11 January 2011 kuanza kufanya mchakato wa kuwafungulia
kesi ya kugushi /(Fraud)/ salary slip, wizi wa mishahara na riba ya
fedha zetu zilizochelewa.

Aidha, kauli ya Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Idrisa Kikula, kuwa
wahadhiri wana agenda ya siri si sahihi. Tunapenda kuweka wazi kuwa
madai yetu ni ya msingi sana na pia ni stahiki za msingi za kisheria.
Makamu Mkuu wa Chuo ajibu hoja na si kueneza propaganda zisizo na msingi
wowote.

Mwisho, tunashukuru vyombo vya habari kwa kutusikiliza na kutupa nafasi
ili kuweza kutoa habari za ukweli kwa jamii.

Imetolewa na Ofisi ya Katibu – UDOMASA

12/1/2011

..........................

*Peter, Kokeli*

*NAIBU KATIBU*

*UDOMASA*

Source JIACHIE
 
Vyema. Moto ule ule. Actions only,no more talking! Kikula na wenzake m**i yanawagonga. Moto wa UDOMASA si wa kuzimwa na propaganda uchwara. This time lazima mkaozee jela,mana lazima mfikishwe mahakamani.
 
to be honest, sina hamu kabisa na mambo ya UDOM, they are too munch into politics kuanzia pre-election hadi leo
 
hongereni kwa kukataa kuendeshwa kama chuo kikuu cha kata. Naona vijana wenu wamewafungulia njia ya namna ya kudai haki.
 
Hiv hawa viongoz wanatupeleka wap? Kwa nin,inauma sana halafu mbona uongoz wa chuo haujib hoja unaishia tu kuwatishia wahadhir! Hawatachelewa kusema kuna mkono wa CDM.wapen hak zao wafanye kaz.
 
Kikula anazidi kutia petroli kwenye moto anawaona wahadhiri kama watoto wasiojua kudai haki zao. Hao ni watu wazima na akili zao wanajua wanachokifanya madai yote ni ya msingi na yana vithibitisho vya kutosha sasa wao wasubiri watakapopandishwa kisutu ya dodoma ndipo watakapotambua kwamba vijana hawatanii wamedhamiria kudai haki zao.
 
Mkutano endelevu wa wadhahiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma utaendelea siku ya Alhamis, tarehe 13 Januari, 2011 ili kuendelea kusubiri majibu kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mbona mnakwepa kumuita Dr? ...you recently controversially awarded this gentleman a UDOM honorary degree. Hatukusikia protest - si kutoka kwa academic staff wala kwa wanafunzi (ikimaanisha mliridhia).
 
Mbona mnakwepa kumuita Dr? ...you recently controversially awarded this gentleman a UDOM honorary degree. Hatukusikia protest - si kutoka kwa academic staff wala kwa wanafunzi (ikimaanisha mliridhia).

crap,akili yako ka ya makamba
 
Kumbe Prof Shaabani Mlacha alikua akitoa tu taarifa za kudanganya umma wa Tanzania huku akijua ya kwamba yote aliyokua akiyasema ni ya uongu mtupu??
 
Protest against honorary degree!!?? Bushit. Kwan digrii ya heshima inamuongezea kitu gan had watu protest! Isitoshe alishapata kutoka nnje, sijui umesikia wapi watu wanaandamana kupinga digrii ya heshima ambayo haina tija. Kweli akili yako na ya makamba/chatanda zinafanana.
 
:A S-fire1:

Nilikuwa nasubiri kwa Hamu nione leo itakuwaje- nafarijika kuwa ndugu zangu hamjaishiwa nguvu- TUKO PAMOJA
na nna wapongeza kwa juhudi zengu Inshallah Mungu awalipe mara elfu zaidi!

Aluta Continua
 
sasa comment za nini kama huna hamu, kaa kimya.
i never know you are moderator... btw, why reading it if it wasnt relevant for you

wanasema kushauri mtu kukaa kimya kwa kupiga kelele ni sawa na mtu anayejisaidia vichakani.... clueless
 
Back
Top Bottom