Tamko la Ikulu juu ya Richmond

MM heshima yako mkuu, hata mimi nadhani mwisho wa yote kutakuwa na showdown kati ya Jakaya na Sita na ishara hizo zimeanza kuonekan kwa Executive kuanza kujipanga! Kama unavyojua kama mgogoro kati ya Executive na Legislature utatakiwa utatuliwe na Judiciary kama itafikia hapo, basi Jakaya atamshinda Sita hands down; kwani ndio maana amekazana kuwateuwa majaji wa High court haraka haraka na lukuki; na ukichunguza hao anaowateuwa ni wa aina gani utajua ni wale wale ambao hawawezi kumuangusha. Sio High court tu bali hata court of Appeal kuna majaji ambao ni wa CCM [ ndio maana hata ile kesi ya independent candidates haipewi uzito unaostahili] Nilikuwa na imani na Judiciary when Samatta was at the helm!!
 
Katika kuweka record sawa.. Karamagi hakuhusika na kuingia kwa Richmond. Aliyekuwa waziri wa nishati wakati huo alikuwa Msabah na aliachishwa ngazi kwa scandal ya Richmond.
Kama sikosei Karamagi tunamkuta ktk swala zito la mkataba wa Buzwagi, kitu ambacho sielewi ni kwa sababu gani aliachishwa Uwaziri ikiwa mradi huo huo bado umekamatwa na Barricks kwa mpini wa mkataba ule ule feki uliotiwa sahihi mjini London Hotelini..
 
Wajameni inawezekana Phillemon Luhanjo akadhani sisi wazawa hatuelewi ili hali yeye kumbe ndiye asiyeeleweka.

JK atakuwa anahusika kwa namna moja au nyingine kwa kuwa:

Maneno aliyokuwa akiniambia mama yangu wakati akiniadhibu yalikuwa haya "kuharibika kwako kitabia aibu yangu mama yako mtaani, ni jukumu langu kuhakikisha huharibikiwi ili nitunze heshima yangu mtaani"

Mkuu wa kaya alikosa busara kulifahamu hilo kwa hiyo hata kama hahusiki hawezi kui-justfy
 
Ndugu yangu kama mtu ni IDIOT lazima watu waseme...hata kama ni mkuu wa nchi lakini mambo anayofanya yanatufanya sisi watanzania tuliompigia kura kuhoji utashi wake, unavyojaribu kumfananisha JK na Mwalimu unakosea sana manake mwalimu alikuwa hakumbatii mafisadi, na wala alikuwa hawapi watu nafasi nyeti kutokana na ushkaji au shinikizo la mafisadi kama afanyavyo JK kwa shinikizo la RA na watu wake....kwahiyo ondoa hiyo statement yako ya kumfananisha mwalimi na JK
 
Soma kwa makini hii Taarifa ya Mhe. Pinda kuhusu suala la Richmond utabaini jinsi gani Serikali inavyojikanganya na kujaribu kutapatapa kupotosha ukweli ili kulinda wale waliohusika moja kwa moja na ufisadi huu. Haiyamkiniki kwa Mhe. Rais akatoa matamko ambayo mahudhui yake yamejaa hadaa tupu. Hivi hana uchungu na fedha za watanzania zinazopotea kulipa gharama za utekelezaji wa mikataba hewa pamoja na kulipia watendaji wake wabovu ambao wamelifikisha Taifa hapa tulipo na bado wanaendekea kututia matatizoni akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali yake?

http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/PM_Richmond.pdfhttp://Taarifa ya Waziri Mkuu kuhusu Richmond aliyoitoa leo Bungeni
 
Soma kwa makini hii Taarifa ya Mhe. Pinda kuhusu suala la Richmond utabaini jinsi gani Serikali inavyojikanganya na kujaribu kutapatapa kupotosha ukweli ili kulinda wale waliohusika moja kwa moja na ufisadi huu. Haiyamkiniki kwa Mhe. Rais akatoa matamko ambayo mahudhui yake yamejaa hadaa tupu. Hivi hana uchungu na fedha za watanzania zinazopotea kulipa gharama za utekelezaji wa mikataba hewa pamoja na kulipia watendaji wake wabovu ambao wamelifikisha Taifa hapa tulipo na bado wanaendekea kututia matatizoni akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali yake?

http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/PM_Richmond.pdfhttp://www.parliament.go.tz/bunge/docs/PM_Richmond.pdfhttp://www.parliament.go.tz/bunge/docs/PM_Richmond.pdf

Nashukuru kwa kutuletea tukumbushie za siku zilizopita: Ila kuna kitu kinachosumbua hapa. Riport ya richmond president alipewa? Je ilisemaje na president aliamua nini?

Je Richmnd waliiambia serikali kama mdau mkuu kuwa tunaiuza tenda?

Wizara ya nishati na madini kwanini walisaini mkataba bila ya kumhusisha preident? au hizi baraka za mkataba alizitoa president. Basi kama baraka zilitolewa na presida then mzigo wa kwake na analijua fika uozo wote.

Heri ya ya mimi mfa maji.
 
And yet we are still forced to believe by fans and cronies of JK that he's the one, the real one kututoa hapa kutupeleka kuleeeee!
 
Nashukuru kwa kutuletea tukumbushie za siku zilizopita: Ila kuna kitu kinachosumbua hapa. Riport ya richmond president alipewa? Je ilisemaje na president aliamua nini?

Je Richmnd waliiambia serikali kama mdau mkuu kuwa tunaiuza tenda?

Wizara ya nishati na madini kwanini walisaini mkataba bila ya kumhusisha preident? au hizi baraka za mkataba alizitoa president. Basi kama baraka zilitolewa na presida then mzigo wa kwake na analijua fika uozo wote.

Heri ya ya mimi mfa maji.

Mkuu ripoti ya Richmond ilikuwa commissioned na Bunge na impliedly kuwa endorsed na Serikali kupitia majibu ya Waziri mkuu wakati huo Eddoo na baadae Pinda kwa kujikanyaga zaidi. Aliyesaini mkataba ni Tanesco kwa shinikizo la serikali ambayo iliamua kutwaa zabuni ya umeme wa dharura kinyume cha taratibu zilizowekwa chini ya sheria ya Manunuzi ya Umma (Public Procurement Act 2004).serikali iliunda kamati kwenda kutafuta wazabuni kienyeji na wakakutana na wajanja RA na wenzake na kushawishi zabuni itolewe kwa Richmond kampuni hewa!
 
for me ikulu is the holy place like a church or mosque ila ninachojua hata ndani ya nyunba hizi za ibada kuna kinyaaa... namwomba the only ONE atuwekee watu makini ambao wataendana na holiness ya ikulu....hodiii wanajamiiF
 
Kikwete alipata urais kwa bahati...hakujiandaa kuwa Rais,...alipewa support kubwa na RA na EL na kwa kua hakujiandaa EL alimfunika kiutendaji...yes...El kwa muda mfupi alipokua PM kafanya mengi huku mfalme JK akichubua vitambaa vya makochi ofisini kwa kua kiutendaji EL alisimama vyema..Kwa msaada mkubwa RA aliompa kukalia hicho kiti alimwacha ale katika shamba la bibi bila kikomo,na kweli alijipanga vyema! Ndo maana naamini kama uchumi wa nchi ni watu basi walioshikilia uchumi huo ndio wenye nchi..RA ndiye mwenye nchi! Kikwete haoni mbali kwa kua being mkuu wa dola ni zaidi ya kila kitu kwake! Kwa mambo yanavyoenda hovyo hovyo alistahili kusimama na kusema yatosha sasa...ukimya wake ndio unafanya tuone wepesi wake ama uchache wa hisa kiutawala! Tanzania Bila JK inawezekana, RA ameshavuna vya kutosha, EL ni ajali tu kisiasa! Time will tell!
 
Unajua hawa wakina luhanjo wanafikiri kuwa bado wa tz ni wale wa miaka ya sabini ! Watized wa sasa hawadanganyiki na niwafuatiliaji wa mambo kuliko anavyofikiri. Asituletee siasa za chama hapa
wameshikwa pabaya
 
Ili kutaka kulielewa zaidi suala hili la Richmond, ni kwanini leo hii ndio taarifa zinakuja rasmi kuwa wataalam waliofanya tathmini walikosea? Hii taarifa ingetolewa mapema labda hapangekuwa na mashaka mengi kiasi hiki.
 
sidhani kama tuna cha kuamini when it comes to viongozi wetu, tafiti zetu, na ujinga mwingine unaopangwa ofisini kwa rostam na kusikika ikulu.Rostam sijamsikia tena kuhusu Loliondo..
 
Kwa ufupi, karamagi alionewa, tenda atoe mwingine na mkataba a-sign mwingine muwajibikaji mwingine?!
Katika kuweka record sawa.. Karamagi hakuhusika na kuingia kwa Richmond. Aliyekuwa waziri wa nishati wakati huo alikuwa Msabah na aliachishwa ngazi kwa scandal ya Richmond.
Kama sikosei Karamagi tunamkuta ktk swala zito la mkataba wa Buzwagi, kitu ambacho sielewi ni kwa sababu gani aliachishwa Uwaziri ikiwa mradi huo huo bado umekamatwa na Barricks kwa mpini wa mkataba ule ule feki uliotiwa sahihi mjini London Hotelini..
 
Nyimbo ile ile, waimbaji wengi. Nani mwengien atakuja kumwaga mistari yake, ni suala la kusubiri.
 
wee bwana Luhanjo hatutaki siasa mambo yako wazi tunachotaka hatua ndio zichukuliwe sio siasa, hapa hatukuelewi.
 
Back
Top Bottom