Tamko la Ikulu juu ya Richmond

"Walikubali, na USD 225 milioni zilitumika kukodisha mitambo ya Kampuni za Aggreko, Alstom na Richmond"

Aggreko: 40MW
Alstom: 50MW
Richmond:100mw
$225 million:

Kama walikuwa na hizo pesa kwa nini wasingenunua mitambo yao mipya, kipindi hicho gharama ya 100MW ilikuwa $50 million mpaka kuwashwa. kwa hesabu ya haraka haraka tungepata 450MW inakuwa mali ya serikali siyo kukodisha na tungekuwa nayo kwa miaka 40-50. badala ya kukodisha kwa miaka 3 kwa gharama hiyo hiyo tena 190mw tu.

Kweli JK hawezi kukataa kwa hili kwamba hausiki,

Leo hii mtambo wa 100mw ni $60million, lakini Dr Idrisa wametoa tender kwa gharama ya $120 million kwa mtambo wa 100mw. na hapa watatumia kampuni ambayo haizalishi hii mitambo kama noor oil ya matapeli wa kihindi na waharabu ambayo ni mjomba wake ni Richmond
kwanza kuna suala la simple arithmetic, kununua na kukodisha lipi lilikuwa suluhisho lilo bora kwa taifa? yaani tunataka kuelezwa kwa kiongozi wetu alishindwa kuona hilo? bila kwenda ndani zaidi ya hayo mambo ya kamati ya majadiliano etc etc
 
This is stupid & wrong move

sasa msemaji wa ikulu ni nani? Luhanjo, salva au wale ma mediocres wengine?

Ikulu imekuwa kama chaka la incompetents...yaani media wanaset Agenda halafu wao wanafuata

hiii issue as far as i know uchunguzi haujakamilika nau liko mikononi mwa vyombo vya sheria sasa whats this kujibizana na media...sometimes i dont understand those ******...tangu juzi naona wanatoa statements kila kukicha

why pick a fight wanajua clearly they cant win? Just wehn tunataka kujua kwa nini miradi ya Milleium Challenge Account ina delay wao wanataka kufufua mambo ambayo yatawatoa from main agenda ya kuwahudumia wananchi

sasa sijui nani kawaambia kuwa its better kujibizana kuhusu mambo haya..ukweli ni kuwa wakishatoa statement next week nzima wataandamwa mpaka mwiki mbili...sasa wakishatoa hii whats next? watajibu na Meremeta ? then baada ya hiyo watajibu na kwa nini kamati ya mauaji ya Mwembechai haijaundwa mpaka leo?

hawa jamaa wanatia kinyaa sana

I guess the only person than can save JK's presidency ni Mama Salma maana husikii wao kujibizana na media..huu ni mtego na i am not sure they will get themselves out of it
[esa za millenium bado kuna technicalities (Rushwa kubwa kubwa ambazo hazija Shughulikiwa)
 
watanzania wakipata uhuru wa kuongea, wanautumia vibaya. Siyo uungwana hata kidogo kumuita rais wetu 'idiot'. Kamwe siwezi kukubaliana na utovu huu wa nidhamu uliokithiri. Rais ni 'head of state' ndiyo 'baba' yetu. Sasa wewe unaweza ukamuita baba yako mzazi 'idiot'? HAPANA, tusifikishwe huko. Kinachotakiwa katika 'blog' hii ni hoja zenye mantiki kwa faida ya nchi yetu na siyo matusi yasiyo na tija.

Ni kweli JK ana mapungufu, kwani yeye ni binadamu kama sisi. Lakini pamoja na mapungufu hayo JK 'has this country at heart". Hana utajiri, ni 'mlalahoi' mwenzetu; hana makuu. JK ni mchukia rushwa na ufisadi, hana uroho wa kujilimbikizia mali. Amefananafana na Mwalimu Nyerere kwa upande wa tabia na kuipenda nchi yake na watu wake.

Lakini ni kweli tamko hilo la IKulu kuhusu Richmond lina kasoro. Hakukuwa na sababu ya kutoa tamko hilo. Maelezo hayo yangeweza kutolewa katika namna nyingine lakini siyo kutolewa na IKULU. Kwa maoni yangu kuna kasoro na mapungufu mengi kuhusiana na baadhi ya watendaji wa IKULU. Tukumbuke IKULU ni 'taasisi' nyeti. Inapaswa iwe na watu makini na waadilifu. Sina hakika sana kama kweli baadhi ya watu ndani ya IKULU ni makini na waadilifu kwa kiwango cha kutotiliwa shaka. Sina hakika na hili, kama kweli baadhi wanaipenda nchi na ni watendaji wazuri.

Suala hili la Richmond lisipofanyiwa kazi kwa umakini linaweza likaigawa nchi yetu. Mjadala ndani ya Bunge kwa hakika haukuwa mzuri kwa umoja wetu. Nina hofu ya kitakachotokea mjadala huu ukianza tena na kuendelea zaidi.
 
watanzania wakipata uhuru wa kuongea, wanautumia vibaya. Siyo uungwana hata kidogo kumuita rais wetu 'idiot'. Kamwe siwezi kukubaliana na utovu huu wa nidhamu uliokithiri. Rais ni 'head of state' ndiyo 'baba' yetu. Sasa wewe ....

Baba yako sio wangu.
 
.[Snip]...............Kwa nini safari hii asiende tena Bungeni na kulifanya tena mahakama na atoe “hukumu” dhidi yake mwenyewe na watu wake kwamba hawahusiki na Richmond na kwa hiyo “case closed?”

Huyu Luhanjo naye! Hivi bado hajastaafu tu! Au ni ule mtindo uliozuka wa kuongeza mikataba pamoja na madaraka juu!

Now I can see performance failures at the helm of the government. No memory, No performance, No outputs, even No understanding of the nation’s problems.

Kila wakati hawa jamaa ni kutaka kuoyesha kwamba hakuna kosa la makusudi, ila kuna uzembe au kutojua (ignorance).

Kwa maelezo hayo, Rais alifahamu matatizo ya Richmond kabla ya mtu mwingine serikalini. Sawa! Mbona hakushangaa Hosea alipotoa ripoti iliyoonyesha kwamba hakuna tatizo ktk Richmond?

Hawa ni wasanii walioshindwa hata kuonyesha sanaa yao.
 
[esa za millenium bado kuna technicalities (Rushwa kubwa kubwa ambazo hazija Shughulikiwa)

Hebu Uliza pesa za World Bank kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi ziko wapi?

Si unaona jinsi World Bank inavyowashika mikono hata wanashindwa na akina Mwandosya wanaanza kulalama Bungeni.

Natabiri: South-East Asia pesa za Milenia zitaleta faida lakini hutaona kitu cha mana hapa kwetu.
 
Jitahidini tu. Richmond, Meremeta, Kiwira,.....vinaweza kusaidia kuipasua CCM na hivyo tukapata mwelekeo na hatma MPYA kabisa ya UONGOZI wa NCHI yetu. Tukapata KATIBA mpya, Tume ya Uchaguzi mpya, VIONGOZI wapya na TAIFA jipya la TANZANIA.
Njia zingine zote kuiondoa CCM madarakani zimeshindikana.
 
Huyu Luhanjo naye! Hivi bado hajastaafu tu! Au ni ule mtindo uliozuka wa kuongeza mikataba pamoja na madaraka juu!

Now I can see performance failures at the helm of the government. No memory, No performance, No outputs, even No understanding of the nation’s problems.

Kila wakati hawa jamaa ni kutaka kuoyesha kwamba hakuna kosa la makusudi, ila kuna uzembe au kutojua (ignorance).

Kwa maelezo hayo, Rais alifahamu matatizo ya Richmond kabla ya mtu mwingine serikalini. Sawa! Mbona hakushangaa Hosea alipotoa ripoti iliyoonyesha kwamba hakuna tatizo ktk Richmond?

Hawa ni wasanii walioshindwa hata kuonyesha sanaa yao.

Mchunguzi!
You are absolutely right huyu Luhanjo ni mchovu wala hayuko smart kama yule ndugu yake aliyekwenda Geneva!

Kama mambo yalikuwa technically sound mbona mtambo wa kwanza wa Richmond nasikia haukuwahi kuzalisha hata Megawati moja na haukuingiza kwenye Grid ya Taifa.

Hivi Luhanjo anajua madhara ya kuzembea kwenye jambo nyeti kama kuzalisha umeme. Na hatimaye kulisababishia taifa hasara ya Tshs. 153m/= kwa siku na huyu mpuuzi anazungumzia mamlaka za nidhamu ! Mbona alipoteza muda kufanya uchunguzi mwingine juu ya ule wa Mwakyembe. Mlichotakiwa ni kuchukua adminstrative measures na kuwaondoa wote kwenye hizo nafasi na kuweka wachapa kazi wengine kwani akina Mrindoko wakifa taifa halitakwenda mbona Gray Mgonja kastaafu na bado hazina inapeta wacheni upuuzi na nkulindana pambaf!!

Nadhani huyu Luhanjo hajaenda shule proper. Kama hakuna rushwa nini kiliwasukuma kumpatia Richmond pesa bila kuwa na Perfomance Bond. Wote waliohusika kuanzia pale nishati, Hazina kwa akina Gray Mgonja, na Tanesco wote walikula rushwa na haijawahi kutokea mtu akapokea rushwa ikadhibitika kama mchana na usiku ila its only the daylight inatosha kuashiria uwepo wa rushwa.

Mkataba wa Richmond kuridhiwa na DOWANS ilifanyika baada ya matatizo ya umeme kwisha ile ni rushwa per se !! Kama Jakaya Mrisho Kikwete na wapumbavu wake hilo hawkuliona then inatia kinyaa!!

Kama Kikwete hatawadabisha watu wa TANESCO;HAZINA;OFISI YA MWNASHERIA MKUU;na TAKUKURU pamoja na kuwafuta uanachama wa CCM akina Lowasa, Msabaha, Karamagi na akina Mwanyika basi arudi Bungeni na kuwaomba RADHI wabunge na amrudishie Lowasa Uwaziri mkuu kama makatibu wakuu wa Hazina na Nishati walizembea why take the Prime Minister to task!!

Aisee Luhanjo kule kanisani usiende tena kuna siku wakristo wenzako watakupiga mawe kama una mawazo mgando kiasi hicho na ukafikiri tutakubali mbona hukudhubutu kukubali kuulizwa maswali na hao waandishi uchwara uliowaita!!
 
Hivi wabunge walivyochachamaa walimtaja yeye kuhusika moja kwa moja? Au huyu Luhanjo anajibu vyombo vya habari. Nisaidieni wakuu. Maana naona ni kama mfa maji anatapatapa.
 
Mkataba wa Richmond kuridhiwa na DOWANS ilifanyika baada ya matatizo ya umeme kwisha ile ni rushwa per se !! Kama Jakaya Mrisho Kikwete na wapumbavu wake hilo hawkuliona then inatia kinyaa!!

Kama Kikwete hatawadabisha watu wa TANESCO;HAZINA;OFISI YA MWNASHERIA MKUU;na TAKUKURU pamoja na kuwafuta uanachama wa CCM akina Lowasa, Msabaha, Karamagi na akina Mwanyika basi arudi Bungeni na kuwaomba RADHI wabunge na amrudishie Lowasa Uwaziri mkuu kama makatibu wakuu wa Hazina na Nishati walizembea why take the Prime Minister to task!!

Aisee Luhanjo kule kanisani usiende tena kuna siku wakristo wenzako watakupiga mawe kama una mawazo mgando kiasi hicho na ukafikiri tutakubali mbona hukudhubutu kukubali kuulizwa maswali na hao waandishi uchwara uliowaita!!

Jamani, hili suala la Richmond ni baya kwa nchi yetu. Kwa kutoa taarifa yake IKULU wanaweza wakachochea moto. Kwa hakika IKULU hawakutakiwa kutoa 'statement' ile. 'Timing' yake haikuwa nzuri. Narudia kama nilivyosema awali kuwa maelezo yangetolewa kwa namna nyingine kabisa. Watendaji wa IKULU wawe makini sana na masuala nyeti kama haya. Wasiingizwe mtegoni kirahisirahisi tu. Hoja ya Luhanjo (kwamba Kama kweli kungekuwa na mkono wake wa upendeleo kwa Kampuni ya Richmond kupata tenda, iweje tena yeye ndiye akatae kampuni hiyo isilipwe fedha za kianzio mpaka kuifanya ishindwe kazi? Ndiyo maana tunasema maneno hayo hayana msingi, yanasemwa na watu ambao ama hawaujui ukweli au wameamua kutokusema kweli kwa makusudi kwa sababu wanazozijua wao. Tunatoa ufafanuzi huu kuwafanya Watanzania waelewe ukweli wa mambo) haina nguvu na . inaweza kuleta mjadala usio na maana. IKULU wasiingizwe mtegoni kirahisi hivyo.
 
Nadhani tunaogopa KUIYUMBISHA NCHI. JK anajua kila kitu kuhusu Richmond tangu mwanzo. Ipo siku EL atasema.
 
watanzania wakipata uhuru wa kuongea, wanautumia vibaya. Siyo uungwana hata kidogo kumuita rais wetu 'idiot'. Kamwe siwezi kukubaliana na utovu huu wa nidhamu uliokithiri. Rais ni 'head of state' ndiyo 'baba' yetu. Sasa wewe unaweza ukamuita baba yako mzazi 'idiot'? HAPANA, tusifikishwe huko. Kinachotakiwa katika 'blog' hii ni hoja zenye mantiki kwa faida ya nchi yetu na siyo matusi yasiyo na tija.. ukitaka kujua kwanini Wacha kamuita 'Idiot'.. jaribu kumfungia Paka chumbani halafu uanze kumpiga..

Ni kweli JK ana mapungufu, kwani yeye ni binadamu kama sisi. Lakini pamoja na mapungufu hayo JK 'has this country at heart". Hana utajiri, ni 'mlalahoi' mwenzetu; hana makuu. JK ni mchukia rushwa na ufisadi, hana uroho wa kujilimbikizia mali. Amefananafana na Mwalimu Nyerere kwa upande wa tabia na kuipenda nchi yake na watu wake...
Lazima atuonyeshe kwa vitendo na siyo huu uoga anao tuonyesha...na nina hakika JK anajua kila kitu kuhusu Richmond ila anawaongopa au anawaone huruma maana wengi na maswahiba na makada wa chukua cha Mapema..Ang'ekuwa mwalimu using'ejua wananyea wapi debe hao mafisadi lkn kwa mwalimu huyu kama unavyotaka kumfananisha mafisadi yamemzidi..

Lakini ni kweli tamko hilo la IKulu kuhusu Richmond lina kasoro. Hakukuwa na sababu ya kutoa tamko hilo. Maelezo hayo yangeweza kutolewa katika namna nyingine lakini siyo kutolewa na IKULU. Kwa maoni yangu kuna kasoro na mapungufu mengi kuhusiana na baadhi ya watendaji wa IKULU. Tukumbuke IKULU ni 'taasisi' nyeti. Inapaswa iwe na watu makini na waadilifu. Sina hakika sana kama kweli baadhi ya watu ndani ya IKULU ni makini na waadilifu kwa kiwango cha kutotiliwa shaka. Sina hakika na hili, kama kweli baadhi wanaipenda nchi na ni watendaji wazuri.
Nani wakulaumiwa au nani kawaweka pale IKULU kwani hakuna watanzania wengine wanao fit kwenye hizo nyazifa..

Suala hili la Richmond lisipofanyiwa kazi kwa umakini linaweza likaigawa nchi yetu. Mjadala ndani ya Bunge kwa hakika haukuwa mzuri kwa umoja wetu. Nina hofu ya kitakachotokea mjadala huu ukianza tena na kuendelea zaidi.

Yeye ndiyo atakuwa amesababisha yote hayo unayoyadhani...na siyo Richmond tu kuna meremeta pia..
 
Rais alikataa Kampuni ya Richmond isipewe malipo ya awali (down payment) ya USD 10 milioni na kutaka ukweli kuhusu uaminifu na ukamilifu (integrity) wa kampuni hiyo ujulikane. Kwani ni kazi ya Rais wa nchi kuamua "downpayment" ilipwe au isilipwe....je kwenye Wartsila na Aggreko mbona hakujihusisha kwenye mambo ya malipo kama kwenye Richmond?
Kama baada ya yeye kuamuru uchunguzi ufanyike juu ya Richmond, lakini haukufanyika ...na baadae ikagundulika kuwa Richmond ilikuwa Feki, aliwafanya nini wale watu aliowaagiza awali wachunguze Richmond isije ikawa ya Kitapeli?
Je baada ya kugundua kwamba wizara ya nishati na madini kujihusisha na kuiingilia Tanesco ilikuwa ni kinyume cha sheria ya manunuzi, alifanya nini?

Kwa vile haya maswali yote yanamshinda jk kujibu....kuna kila ishara kwamba yeye ndiye alikuwa kinara wa Richmond
 
Lazima kuna kitu huko kinakuja na kitalipuka tu. Wala huitaji elimu ya form IV kujua kuwa maamuzi ya kipuuzi ya Richmond hayajachangiwa na mkulu.... ni busara, haki na heshima akiwajibika.
 
Yaani this thing is simple na nashangaa kwanini wanatumia nguvu nyingi na kuita wahariri,kupoteza muda na kutusumbua tu.

Ndiyo Jk hausiki nani anahusika sasa,kwanini wasimtaje jina?na kama walipuuzia maagizo ya Mkulu walichukuliwa hatua gani?

Navyojua Rais ana uwezo wa kutengua uteuzi wa mtu yeyote,alifanya aliutenguza uteuzi wa balali(usanii flani).Hata hili linawezekana kabisa na afanye sana.

Hili suala la RDC ni siasa za maji taka ambazo wamezipiika wao wenyewe.tatizo ni uwaziri mkuu na hawana lolote.Tokea six alipokosa U-PM basi imekuwa vuru vuru mechi tu..

sasa watamalizana wao kwa wao na mie naona tuangalie 2010..tunampa nani Nchi,Je tunaamua kumsuport Mkwere au tunaunganisha nguvu na kuchagua Chaguo La Mungu.
 
Back
Top Bottom