Tamko la Ikulu juu ya Richmond

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
2607%5B1%5D%5B1%5D.jpg


TAARIFA KUHUSU SUALA LA KAMPUNI YA RICHMOND

Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na maneno na vijembe ati kuwa kuna mkono wa Rais Jakaya Kikwete katika kutoa tenda ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopata Kampuni ya Richmond. Kiini cha maneno hayo ni kauli za baadhi ya wanasiasa zilizopazwa sauti na baadhi ya vyombo vya habari.

Tunapenda kusema, tena kwa msisitizo, kuwa maneno hayo si ya kweli na hayana msingi wowote. Rais hajahusika na uamuzi wa tenda hiyo kupewa kampuni ya Richmond kama vile ambavyo hakuhusika na kupewa tenda kwa kampuni za Aggreko na Alstom.

Kama mtakavyokumbuka wakati ule kampuni hizo tatu ndizo zilizopewa tenda ya kuzalisha umeme wa dharura. Kampuni ya Aggreko ilipewa tenda ya kuzalisha umeme wa megawati 40 na Richmond kuzalisha megawati 105.6 pale Ubungo kwa kutumia gesi asilia. Kampuni ya Alstom ilipewa tenda ya kuzalisha megawati 40 za umeme pale Mwanza kwa kutumia mafuta ya dizeli.

Katika uamuzi wa kupewa tenda kampuni hizo, Rais hakujihusisha, hakuhusishwa na wala hapakuwepo na sababu ya kuhusishwa au kujihusisha . Hiyo siyo kazi ya Rais. Hiyo ilikuwa ni kazi ya TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini na ndiyo walioifanya. Hayo ndiyo matakwa ya Sheria ya Manunuzi ya Umma na ndivyo ilivyofanyika.

Katika shughuli nzima ya uteuzi kulikuwa na Kamati mbili za kushughulikia upatikanaji wa makampuni ya kutoa huduma ya mitambo ya kukodi ya kuzalisha umeme wa dharura. Ya kwanza ilikuwa Kamati ya Watalaamu kutoka TANESCO, Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini iliyokuwa na jukumu la kutathmini wazabuni wote waliojitokeza kuomba na kupendekeza wanaofaa kufikiriwa kupewa kazi hiyo. Kamati ya Pili ilikuwa ni ile ya Serikali ya Majadiliano (Government Negotiating Team) iliyokuwa na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, TANESCO, Benki Kuu na Shirikisho la wenye Viwanda kuwakilisha sekta binafsi. Kamati hii ilikuwa na jukumu la kufanya majadiliano na wale waliopendekezwa na Timu ya Wataalamu na hatimaye kupendekeza anayefaa kupewa.

Kamati ya Majadiliano ilipomaliza kazi yake ilikabidhi taarifa yake Wizarani kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ndugu Arthur Mwakapugi ambaye naye akaikabidhi kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Ibrahim Msabaha kwa uamuzi. Kama tulivyokwishasema mamlaka ya uamuzi yalikuwa chini yao. Hakuna wakati wowote katika mchakato wa kuamua kampuni ipi ipewe tenda alipofikishiwa Rais kwa uamuzi wake wala kutakiwa kutoa maoni.

Mambo aliyofanya Rais

Katika suala zima la kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme, Rais alihusika katika mambo manne. Kwanza, katika kuamua TANESCO itumie mitambo ya kukodi kuzalisha umeme na Serikali igharamie ukodishaji huo. Suala hilo lilikuwa lazima liamuliwe na yeye kwa sababu lilikuwa linahitaji Serikali kugharamia ukodishaji. Kama si hivyo lisingefikishwa kwake kwani ni jambo ambalo lingekuwa juu ya TANESCO kuamua kukodisha na kulipia. Gharama hizo hazikuwa zimepangwa katika bajeti ya serikali hivyo ilikuwa ni lazima kupata idhini ya Rais ya kutafuta hizo pesa na kuzitumia kwa ajili hiyo.

Pili, Rais alihusika katika kuzungumza na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuwaomba wakubali sehemu ya pesa waliyopanga kuipa Tanzania kama msaada kutokana na mpango wa msamaha wa madeni itumike kugharamia ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme. Walikubali, na USD 225 milioni zilitumika kukodisha mitambo ya Kampuni za Aggreko, Alstom na Richmond (ambayo baadae ikawa Dowans) na matumizi mengine ya dharura za umeme. Matumizi hayo mengine yalijumuisha pia ununuzi wa mitambo ya aina ya Watsilla ya kuzalisha megawati 100 za umeme pale Ubungo kwa kutumia gesi asilia. Mitambo hiyo imeshanunuliwa, kufungwa na tayari inazalisha umeme.

Tatu, Rais alihusika katika vikao vya Baraza la Mawaziri vilivyojadili matatizo ya upungufu mkubwa wa umeme nchini na kuamua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo. Moja ya hatua zilizoamuliwa kuchukuliwa, ni hii ya kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme. Katika vikao hivyo vya Baraza la Mawaziri alitoa maelekezo ya mambo ya kuzingatiwa katika zoezi zima la kupata makampuni au watu watakaotoa huduma hiyo. Hususan, Rais alisisitiza kuwa pamoja na udharura uliokuwepo Kanuni na Sheria ya Ununuzi wa Umma zizingatiwe.

Nne, Rais alikataa Kampuni ya Richmond isipewe malipo ya awali (down payment) ya USD 10 milioni na kutaka ukweli kuhusu uaminifu na ukamilifu (integrity) wa kampuni hiyo ujulikane. Rais alikataa maombi yaliyopelekwa kwake na Wizara ya Nishati na Madini ya kumuomba aagize Wizara ya Fedha, iilipe kampuni hiyo fedha hizo. Rais aliagiza Wizara ya Fedha ibaki na msimamo wake na kuitaka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO wafanye mambo mawili. Kwanza, wafanye utafiti zaidi kujua undani wa Kampuni ya Richmond. Isije kuwa ni kampuni bandia wakapewa fedha wakatokomea nazo na mitambo isipatikane na hukuna namna ya kuipata kampuni wala wahusika wake. Pili aliagiza wawatake viongozi wa Kampuni ya Richmond kwanza walete mitambo, ikishafika, ndipo walipwe. Maagizo hayo ya Rais yalizingatiwa na Kampuni ya Richmond ikapewa sharti hilo. Lakini, ikashindwa kulitekeleza na kuishia kuingia mkataba na Kampuni ya Dowans iliyokuja kuleta hiyo mitambo badala yake.

Hivyo ndivyo alivyohusika Rais katika suala zima la ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme kutoka kwa makampuni ya Aggreko, Alstom na Richmond. Kama kweli kungekuwa na mkono wake wa upendeleo kwa Kampuni ya Richmond kupata tenda, iweje tena yeye ndiye akatae kampuni hiyo isilipwe fedha za kianzio mpaka kuifanya ishindwe kazi? Ndiyo maana tunasema maneno hayo hayana msingi, yanasemwa na watu ambao ama hawaujui ukweli au wameamua kutokusema kweli kwa makusudi kwa sababu wanazozijua wao. Tunatoa ufafanuzi huu kuwafanya Watanzania waelewe ukweli wa mambo.

Watumishi wa Umma
Kuhusu watumishi wa Umma waliohusika na uchambuzi wa zabuni, majadiliano na uamuzi, napenda kuwahakikishia kuwa, Serikali imelishughulikia jambo hili na sasa linafikia ukingoni. Mamlaka za nidhamu zimeangalia mambo mawili: tuhuma za rushwa na uzembe. Tuhuma za rushwa hazijathibitika mpaka sasa na tuko tayari kuchunguza zaidi. Lakini tuhuma ya uzembe imethibitika kwa ukweli kwamba Kampuni ya Richmond haikufanyiwa uchunguzi wa kina kuijua kampuni hiyo kwa undani kabla ya kuipa tenda. Due diligence haikufanywa. Kwa sababu ya makosa hayo mamlaka za nidhamu husika kwa watumishi hao zitawachukulia hatua zipasazo kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi.

Wenzetu hawa waliridhika tu na maelezo ya mwakilishi wa Kampuni ya Richmond aliyetosheleza masuala ya kuwa na mitambo ya kuweza kuzalisha megawati 105.6, mitambo ambayo itafaa kwa mfumo wetu wa umeme, itapatikana kwa wakati na umeme kuuzwa kwa bei nafuu. Ni kweli kwamba kampuni hiyo iliwashinda wazabuni wote kuhusu masharti hayo lakini walisahau msemo wa wahenga kuwa “si kila king’aacho ni dhahabu.” Naamini wangefanya uchunguzi wa kina kuhusu kampuni ya Richmond wangegundua kuwa ni ya bandia na haikuwa na uwezo wa kifedha wa kutekeleza zabuni ile. Kwa sababu ya upungufu huo hatua zipasazo za kinidhamu zitachukuliwa kwa kila mmoja kwa kiwango chake cha kuhusika.Yaani kwa uzito wa kosa lake. Kazi hiyo imeanza na inaendelea kufanyika.

***** Mwisho ******

…………………………………….
Imetolewa 01 Agosti, 2009 PHILLEMON LUHANJO
IKULU, KATIBU MKUU KIONGOZI
DAR ES SALAAM.
 
Last edited by a moderator:
This is stupid & wrong move

sasa msemaji wa ikulu ni nani? Luhanjo, salva au wale ma mediocres wengine?


Ikulu imekuwa kama chaka la incompetents...yaani media wanaset Agenda halafu wao wanafuata

hiii issue as far as i know uchunguzi haujakamilika nau liko mikononi mwa vyombo vya sheria sasa whats this kujibizana na media...sometimes i dont understand those ******...tangu juzi naona wanatoa statements kila kukicha

why pick a fight wanajua clearly they cant win? Just wehn tunataka kujua kwa nini miradi ya Milleium Challenge Account ina delay wao wanataka kufufua mambo ambayo yatawatoa from main agenda ya kuwahudumia wananchi

sasa sijui nani kawaambia kuwa its better kujibizana kuhusu mambo haya..ukweli ni kuwa wakishatoa statement next week nzima wataandamwa mpaka mwiki mbili...sasa wakishatoa hii whats next? watajibu na Meremeta ? then baada ya hiyo watajibu na kwa nini kamati ya mauaji ya Mwembechai haijaundwa mpaka leo?

hawa jamaa wanatia kinyaa sana

I guess the only person than can save JK's presidency ni Mama Salma maana husikii wao kujibizana na media..huu ni mtego na i am not sure they will get themselves out of it
 
Tamko hili litakuwa ni jipya tofauti na juzi sijui jana ambalo Luhanjo amefafanua ? Mbona wanaongeza kasi ya matamko what is happening with these guys ndugu wananchi ?
 
Kuna nini kipya kwenye hiyo taarifa? Mbona kila kitu tunajua, naona tusubiri hatua atakazochukua rais. Waliohusika wanajulikana na ni wazi kuwa kulikuwa na wizi,usanii na bunge letu lilitoa pendekezo. Tuambiwe mapendekezo ya bunge yatatekelezwa lini.
 
You know what Kikwete anahusika na Ufisadi wote unaotokea Tanzania kuanzia urais wake alivyoupata hadi kufika hapa kwenye hazina zote za ufisadi, Meremeta, EPA, Richmonduli and everything. Sasa baada ya kuona Watanzania walipa kodi wanamuona yeye ndiye Fisadi papa nambari moja ananza kutapatapa. Aliambiwa tangu alifu Salva sio Mtanzania akabisha sasa angalia yatakayotokea, aliambiwa usimpe EL uwaziri mkuu akabisha. Tena akaonywa vikali achana na RA na Chenge akabisha akaambiwa huyu Mramba pia ni tapeli akabisha na uwaziri akampa. Tena hata yule muuaji aliyeteketeza watoto na shirika lake la NSSF bado anachekacheka naye tu.

Sijaona rais idiot kama huyu, hata mzee rukhsa pamoja na mapungufu yake hakuweza kutunza mizoga. Amejaza vichaa wanaoangalia matumbo yao kila kona.
 
Jamani, hebu tukumbushane iwapo nitakuwa nimekosea. Taarifa hiyo ya Ikulu ni taarifa ya kwanza kabisa ya Ikulu (yaani ya JK) kuhusu Richmond, Right?

Comment ya karibu sana na hilo toka kwa JK lilikuja wiki chache baada ya EL kuanguka, pale Jk aliwaambia wazee wa CCm wa Dar kuwa ilikuwa ni ajali ya siasa. Hakugusia kabisa Richmond kwa undani wake. Sikumbuki iwapo Ikulu ilisema chochote kuhusu richmond, hata hayo yaliyosemwa katika taarifa ya jana ya Luhanjo Ikulu haikuwahi kuyasema hapo nyuma.

Ingeyasema huko nyuma, angalau JK angepata kauhalali ka-kusema: 'nilishazungumzia hili: kwamba Richmond ilikuwa ya kitapeli tu.'

Sasa anabwata nini? Kwa kuwa maji yanaanza kufika shingoni? Kama alilikoroga, si bora alinywe tu?

Na uko wapi ule 'ujasiri' wake aliouonyesha mwaka jana Bungeni (tarehe kama hizi) pale alipoligeuza Bunge kuwa mahakama yake na kujipachika u-CID, u-prosecutor na ujaji alipotoa hukumu dhidi ya wezi wa EPA?

Hatujasikia tena mkazo wa hukumu hasa kwa wale "waliorudisha' hela na pia kutueleza nani alirudisha ngapi.

Au anataka tuamini kuwa mamilioni "yaliyorudishwa" yalishanunuliwa mbolea na wakulima mikoa kadha wameshafaidika, na kwa hiyo "file closed?"

Kwa nini safari hii asiende tena Bungeni na kulifanya tena mahakama na atoe "hukumu" dhidi yake mwenyewe na watu wake kwamba hawahusiki na Richmond na kwa hiyo "case closed?"
 
Last edited:
You know what Kikwete anahusika na Ufisadi wote unaotokea Tanzania kuanzia urais wake alivyoupata hadi kufika hapa kwenye hazina zote za ufisadi, Meremeta, EPA, Richmonduli and everything. Sasa baada ya kuona Watanzania walipa kodi wanamuona yeye ndiye Fisadi papa nambari moja ananza kutapatapa. Aliambiwa tangu alifu Salva sio Mtanzania akabisha sasa angalia yatakayotokea, aliambiwa usimpe EL uwaziri mkuu akabisha. Tena akaonywa vikali achana na RA na Chenge akabisha akaambiwa huyu Mramba pia ni tapeli akabisha na uwaziri akampa. Tena hata yule muuaji aliyeteketeza watoto na shirika lake la NSSF bado anachekacheka naye tu.

Sijaona rais idiot kama huyu, hata mzee rukhsa pamoja na mapungufu yake hakuweza kutunza mizoga. Amejaza vichaa wanaoangalia matumbo yao kila kona.


Hiyo kali zaidi kidogo mkulu, huogopi mods? Lakini najua hasira zako, kwani nami huwa najitahidi sana kuzuia ku-vent my venom kuhusu uendeshaji mambo wa huyu Bwana ambaye alifikiria Urais ni starehe au kitu cha mchezo.

Hata msemaji madhubuti hana na ndiyo maana kila mmoja anasema vyake kwa niaba ya ikulu, wengine wakiwemo watu wa RA.
 
Jamani, hebu tukumbushane iwapo nitakuwa nimekosea. Taarifa hiyo ya Ikulu ni taarifa ya kwanza kabisa ya Ikulu (yaani ya JK) kuhusu Richmond, Right?
No si ya kwanza. two days kabla hawajatoa hii, walitoa nyingine inayosema Kikwete hakuhusika kwa namna yoyote na suala la Richmond. na kabla ya hiyo walishawahi kutoa nyingine wakisema hivyo hivyo. Hiyo ya juzi waliitoa wakikanusha habari ya kwenye Tanzania daima. Hii hapa:


DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.






TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Richmond haina mkono wa Rais Kikwete

LEO, Jumatano, Julai 29, 2009 Gazeti la Tanzania Daima limechapisha habari yenye kichwa cha habari kisemacho: “Richmond ina mkono wa JK”.

Kichwa hicho cha habari kinapotosha ukweli na hali halisi ya mchakato wa suala zima la Richmond, hatua zilizochukuliwa, na yote yaliyotokana na suala hilo tokea lilipojitokeza Februari, mwaka jana, 2008.

Madhumuni ya kichwa hicho cha habari ni kuupotosha umma, na kudhamiria kumdhalilisha na kumpaka tope Rais kwa kusema uongo ulio dhahiri dhidi ya kiongozi huyo.

Tuhuma za kumhusisha Rais Kikwete hazina msingi wowote na kwa kweli ni hisia za Gazeti lenyewe tu kwa sababu ambazo linazijua lenyewe.

Ni tuhuma zisizokuwa na nafasi katika uandishi wa habari wa heshima na wenye kuongozwa na ukweli, weledi na haki.

Tumepata kusema huko nyuma, na tunapenda kusisitiza kwa mara nyingine kuwa Rais hana mkono katika Richmond na hata Ripoti ya Bunge iliyotolewa kufuatia uchunguzi katika suala hilo la Richmond, haikumhusisha Rais Kikwete.

Kama tulivyokwishakutamka huko nyuma, tunathamini kazi ya waandishi wa habari pamoja na ile ya vyombo vya habari kwa ujumla wake.

Dhamira hiyo inatokana na imani ya Serikali juu ya mchango mkubwa wa waandishi na vyombo vya habari katika mwenendo mzina wa taifa letu – iwe ni katika masuala ya usalama, ama amani, ama utulivu, ama uchumi na au maendeleo ya jamii.

Upotoshaji kama ulivyodhamiriwa na Gazeti la Tanzania Daima haulengi katika kudumisha imani hiyo ya Serikali. Linachofanikiwa kufanya gazeti hili ni kuchapisha kauli ya kashfa na kejeli dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Nchi, yenye lengo la kumdhalilisha.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

29 Julai, 2009
 
Tatu, Rais alihusika katika vikao vya Baraza la Mawaziri vilivyojadili matatizo ya upungufu mkubwa wa umeme nchini na kuamua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo. Moja ya hatua zilizoamuliwa kuchukuliwa, ni hii ya kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme. Katika vikao hivyo vya Baraza la Mawaziri alitoa maelekezo ya mambo ya kuzingatiwa katika zoezi zima la kupata makampuni au watu watakaotoa huduma hiyo. Hususan, Rais alisisitiza kuwa pamoja na udharura uliokuwepo Kanuni na Sheria ya Ununuzi wa Umma zizingatiwe.
hayo yanayoitwa maelekezo ndiyo yanayotiliwa shaka
 
"Walikubali, na USD 225 milioni zilitumika kukodisha mitambo ya Kampuni za Aggreko, Alstom na Richmond"

Aggreko: 40MW
Alstom: 50MW
Richmond:100mw
$225 million:

Kama walikuwa na hizo pesa kwa nini wasingenunua mitambo yao mipya, kipindi hicho gharama ya 100MW ilikuwa $50 million mpaka kuwashwa. kwa hesabu ya haraka haraka tungepata 450MW inakuwa mali ya serikali siyo kukodisha na tungekuwa nayo kwa miaka 40-50. badala ya kukodisha kwa miaka 3 kwa gharama hiyo hiyo tena 190mw tu.

Kweli JK hawezi kukataa kwa hili kwamba hausiki,

Leo hii mtambo wa 100mw ni $60million, lakini Dr Idrisa wametoa tender kwa gharama ya $120 million kwa mtambo wa 100mw. na hapa watatumia kampuni ambayo haizalishi hii mitambo kama noor oil ya matapeli wa kihindi na waharabu ambayo ni mjomba wake ni Richmond

 
Wana JF,
Hebu tukumbusheni ule ujumbe ambao Kikwete alimpa Msabaha kabla ya mambo ya Richmond kuripuka. Hiyo ni ishara tosha kwamba alijua what was happening.
 
naomba nijibiwe,na nijibiwe kwa ufasaha tafadhali...hivi tatizo ni kikwete ama ni washauri wa Kikwete???
 
FILAMU YA RICHMOND inaendelea, leo tumeona starling mpya akionyesha ujuzi wake, bado kama matoleo matatu kutoka hili la Katibu mkuu kiongozi, masikini mzee yule, wamtwika zigo ambalo hata Waziri mkuu limeshinda.
 
Back
Top Bottom