Tamko la DEOGRATIUS KISANDU mgombea uenyekiti BAVICHA

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
kisandu.jpg

DEOGRATIUS KISANDU

MGOMBEA UENYEKITI BARAZA LA VIJANA CHADEMA,

Mimi Deogratius kisandu ninawania nafasi ya mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mei 28, 2011.

Nimesukumwa kugombea nafasi hiyo kutokana na uwezo nilionao katika uongozi, ikiwa ni pamoja na uzoefu, kwakuwa nimewahi kushika nyazifa mbalimbali na kuzimudu vilivyo ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na jamii kwa ujumla.

Niliwahi kuwa mwalimu wa taaluma katika shule ya sekondari ya sister Irene iliyopo wilaya ya kahama na Mwamala sekondari iliyopo wilaya ya Nzega.

Mimi nimeamua kugombea nafasi ya uenyekiti kwa sababu ninaiweza kutokana na kujihusisha na uongozi katika chama nikiwa Kaimu katibu wa wilaya ya Lushoto na nafasi nyingine za ngazi ya chini ambazo nimewahi kuzishika awali.

Natambua uwepo na uhitaji wa watanzania katika rasilimali tulizonazo katika Taifa letu. Mimi nitawaongoza vijana wenzangu kutumia upembuzi yakinifu, kutokomeza nidhamu ya uwoga, unafiki na kupigania haki za wanyonge wa Taifa hili,ili kuwapo ukombozi wa pili wa Tanzania yetu. Ukombozi huu utaletwa na sisi vijana.

Mahitaji ya vijana ndio wajibu wangu wa kwanza kwa ukombozi wa pili wa Taifa letu.

Natambua sisi vijana ndio chachu ya mabadiliko katika Taifa lolote Duniani kutokana na nguvu, ubunifu na wingi wetu, hivyo nitawaleta vijana pamoja kwa ushirikiano wa pamoja.

Nilizaliwa juni 28, 1983 kahama, Shinyanga. Nilianza masomo ya Elimu ya msingi shule ya msingi kahama kati ya mwaka 1990-1996. Elimu ya sekondari 'O' level nimesoma katika sekondari ya Kishimba mwaka1999-2002 na Tabora Boys kati ya mwaka 2003 na 2005 kwa masomo ya 'A' level'

Mwaka 2007 nilihudhuria mafunzo ya "Crash program" katika chuo cha ualimu Tabora kwa ajili yakufundisha shule za sekondari.

Kwasasa nipo mwaka wa pili wa masomo katika chuo kikuu kishiriki cha Tumaini(SEKUCO) kilichopo Lushoto nachukua masomo ya Shahada ya kwanza katika Elimu maalum,Siasa na Utawala.

Mwaka 2010 niligombea ubunge jimbo la Lushoto kwa tiketi ya Chadema na kuwa mshindi wa pili,huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Henry Shekifu.

Aidha, kwasasa ni mwenyekiti wa Chadema Students Organization(CHASO), umoja ulioanzishwa mwaka 2009 kwa ajili ya kuwauunganisha wanafunzi wote wa elimu ya juu, kati na sekondari nchini kote.

Lengo langu ni kuwajenga vijana kuwa viongozi bora wa baadae pia kuwa na itikadi moja ya vijana nchi nzima ili wawe tayari kushika nyazifa mbalimbali za kulitumikia Taifa kila watakiwapo kufanya hivyo.

Nikiwa mwenyekiti wa CHASO nimeeneza harakati zangu katika chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM), Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Chuo kikuu cha Tumaini tawi la Lushoto,Chuo kikuu cha Arusha, Chuo kikuu cha Makumira na shule mbalimbali za sekondari ambako yamefunguliwa matawi.

Kauli mbiu yangu ya kuwahamasisha vijana wenzagu ni "VIJANA TUFUNGE MIKANDA KWA UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU" nikiwataka vijana wenzangu wasirudi nyuma katika harakati za kupigania haki zetu na Taifa kwa ujumla, ili kuwa na Taifa linalojali Usawa na Ajira katika nafasi mbalimbali.

Nataka kuijenga BAVICHA mpya yenye tija kwa vijana wote wa kitanzania ili kila mmoja anufaike na uwepo wa baraza la vijana.Kuvunja makundi na kuleta umoja wenye tija na nia moja ya kujenga BAVICHA na chama kwenda kushika dola 2015.hivyo 2015 ni mwaka wa CHADEMA.

KWA USHAURI 0655 025 609.
Deogratius Kisandu
 
kuna kitu humu jf, jana kulikuwa na taarifa heading inanhusu zito then ndani mambo ya uchaguzi cdm. so wt this?
 
Wewe hufai kuwa kiongozi maana ni muongo. Kwani ukiweka heading inayoendana na content watu hawatasoma post yako? Ningekuwa mpiga kura ningeku-disqualify kwa hili-maana hujiamini na sio muadilifu. Huu ni wakati wa kujenga chama, sio kuwania uongozi hata kwa mbinu haramu...
 
Uongo hujidhihirisha mapemaaaaaaaaaaaaaa......
sorry Bw Deo Kisandu kama ningekuwa one of the voters nisingekupa kura yangu..........wewe ni muongo....umekwisha...
Tubu kabla mambo hayajakuendea kombo..
 
hii si mala ya kwanza kutokea.unakuta mtu habari inatofautiana heading na kilchomo ndani.hii mod inabidi aifanyie kazi.watu wote wa cdm wanajiamini so sidhani kama mtu anaweza kumtumia shibuda.
 
kuna kitu humu jf, jana kulikuwa na taarifa heading inanhusu zito then ndani mambo ya uchaguzi cdm. so wt this?

Wewe hufai kuwa kiongozi maana ni muongo. Kwani ukiweka heading inayoendana na content watu hawatasoma post yako? Ningekuwa mpiga kura ningeku-disqualify kwa hili-maana hujiamini na sio muadilifu. Huu ni wakati wa kujenga chama, sio kuwania uongozi hata kwa mbinu haramu...

Uongo hujidhihirisha mapemaaaaaaaaaaaaaa......
sorry Bw Deo Kisandu kama ningekuwa one of the voters nisingekupa kura yangu..........wewe ni muongo....umekwisha...
Tubu kabla mambo hayajakuendea kombo..

Wakuu, msiwe wepesi sana kutoa hukumu kwa huyo Deo japo simfahamu.

Ninachokiona hapa huyu sio Deo Kisandu wala sio mpambe wake bali ni adui yake mwenye lengo mahsusi la kumuharibia aonekane ni mtu wa hovyo.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Wakuu, msiwe wepesi sana kutoa hukumu kwa huyo Deo japo simfahamu.

Ninachokiona hapa huyu sio Deo Kisandu wala sio mpambe wake bali ni adui yake mwenye lengo mahsusi la kumuharibia aonekane ni mtu wa hovyo.

Mwambie ajitokeze atolee ufafanuzi kuhusu hizo headings na maelezo yanamhusu yeye. Akikaa kimya watu watajua ni yeye au wapambe wake.
 
inamaana hizo comment hujaziona hapo juu hata utueleze kwa nini imetokea hivi? wake up bwana.
 
Mwambie ajitokeze atolee ufafanuzi kuhusu hizo headings na maelezo yanamhusu yeye. Akikaa kimya watu watajua ni yeye au wapambe wake.
........................
Wakuu, msiwe wepesi sana kutoa hukumu kwa huyo Deojapo simfahamu.

Ninachokiona hapa huyu sio Deo Kisandu wala sio mpambe wake bali ni adui yake mwenye lengo mahsusi la kumuharibia aonekane ni mtu wa hovyo.
 
Una akili sana Butola!:A S thumbs_up:
Wakuu, msiwe wepesi sana kutoa hukumu kwa huyo Deo japo simfahamu.

Ninachokiona hapa huyu sio Deo Kisandu wala sio mpambe wake bali ni adui yake mwenye lengo mahsusi la kumuharibia aonekane ni mtu wa hovyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom