Tamko la Chama Cha Walimu(CWT)

Waalimu ha2wezi goma kwasababu kwanza wengine tumegushi vyeti, pili karibu wote ha2na servings bank, wakikata mshahara habari imeisha, kwa hiyo lazma tuwe waoga
 
Kufuatia hukumu iliyotolewa hapo jana na mahakama ya kazi ya kuwataka walimu kurejea kazini na kuwaamuru viongozi wa CWT kutangazia Umma kuwa mgomo umekwisha, Chama kimesema kitatoa tamko leo saa 4:00 asubuhi. Tamko hilo litaeleza kama chama kimeridhika na hukumu au wanakata rufaa. Taarifa hiyo haijaweka wazi kama walimu warejee kazini ama laa. Mtoa taarifa amewataka walimu kufuatilia vyombo vya habari saa 4 asubuhi. Nawaomba wadau mtakaopa updates mtuwekee humu. Karibuni.

Walimu ndio tuliowafundisha hao wanaojiita watawala na majaji leo wanadhani watatuzidi akili?

hakuna haja ya kuongea sana hata CWT wakitangaza mgomo umeisha Wasubili watayaona matokeo yake.. Mgomo huu utaisha kwenye vyombo vya habari Lakini katika nafsi zetu na makazini HAUTAISHA KWA MDA MREFU
 
walimu wa iringa baadhi waligoma kugoma wakidai kwanza waelezwe mapato ya cwt,na pia kuwashtumu viongozi kutaka umaarufu kupitia kwao
 
kwani cwt haiwezi toa notice ya saa 48 siku za kazi?wafanye taratibu halali za mgomo!pia wamuulize kikwete yeye na familia ya watoto 7 anaweza ishi kwa sh 240000 kwa mwezi?
 
walimu wa iringa baadhi waligoma kugoma wakidai kwanza waelezwe mapato ya cwt,na pia kuwashtumu viongozi kutaka umaarufu kupitia kwao

Mkuu wakiyaju au wasipoyajua hayo mapato ya cwt, kimahesabu na kwa ufahamu wako itaboresha kwa asilimia ngapi mshahara wa mwalimu?
 
kuanzia leo Hesabu darasani watakoma na kwa vile mi ni mtaaluma! wategemee kufaurisha -ve shuleni kwangu na 0% kwa masomo nayofundisha
 
Poleni sana Wajenzi wa Taifa la amani yaani Tz walimu ambao kazi yenu hatuna budi kujivunia kwani kazi yenu ni muhimu sana kuwaaandaa wtz hadi wengine wakawa Marais, Mawaziri , wabunge, marubani nk, kitu kimoja naomba niwakumbushe miaka mingi mmekuwa mkitoa elimu kwetu lakini mmesahau ya kwamba serikali yenu ya CCm daima haijali watu wake wanaishi maisha gani? kipato wanachokipata kinakidhi haja? bahati mbaya ninyi kama walimu hamjaliona hilo japo kazi yenu ni kufundisha. Baadhi ya walimu wamekuwa wasaidizi wakubwa wa chama tawala kuendelea kukaa kwenye uongozi bila kujali kama kinatimiza wajibu wake kwa waliowaweka madarakani baadhi ya walimu wakipata vijiposho kidogo kuandikisha wapiga kura, sensa, nk wanashindwa kukikosoa chama na makosa yake mfano wa kupiga kura walimu mnakisaidia sana chama tawala na serikali yake matokeo yake ndiyo haya walimu mnapodai mshahara japo ufikimme shilingi laki mbili 2 mnasahau kuna wenzenu hata laki moja hawajaifikia Je Uwiano wa maisha upo wapi ? hiyo ndiyo serikali ya CCM Chapendeza nawasihihi muachane na mgomo huu muwafundishe watoto wetu kusudi nao wakawafundishe wazazi wao jinsi ya kuiondoa serikali ya CCM kwenye uongozi serikali ambayo hajali hata kidogo watu wake wanakula nini kipindi kilichobaki ni kifupi sana 2015 poleni sana msije mkapigwa virungu,na mabomu ya kutoa machozi mkapoteza Ajira zenu ushauri wa bure. Mujwahuzia
 
Kufuatia hukumu iliyotolewa hapo jana na mahakama ya kazi ya kuwataka walimu kurejea kazini na kuwaamuru viongozi wa CWT kutangazia Umma kuwa mgomo umekwisha, Chama kimesema kitatoa tamko leo saa 4:00 asubuhi. Tamko hilo litaeleza kama chama kimeridhika na hukumu au wanakata rufaa. Taarifa hiyo haijaweka wazi kama walimu warejee kazini ama laa. Mtoa taarifa amewataka walimu kufuatilia vyombo vya habari saa 4 asubuhi. Nawaomba wadau mtakaopa updates mtuwekee humu. Karibuni.
j CWT imeshindwa. Kunahitajika umakini wa hali ya juu kuandaa mgomo wa nchi nzima wa kundi kubwa kama la walimu. Unatoaje notisi ya saa 48 ukijua jumamosi na jmapili siyo siku ya kazi. Madai not realistic.
 
Viongozi hawana hasara, watoto wao wanasoma international school ambako walimu wanalipwa vizuri. Maskin wanaotegemea st Kayumba imekula kwetu.
 
Nimechoka sana, kila siku matatizo hayaishi,migomo kila kukicha,madaktari,walimu,wanafunzi vyuo vikuu mpaka kwa wananchi wa kawaida.Hakika nchi hii ingekuwa daladala ningeshuka nipande inayokuja nyuma.
 
Mukoba asilaumiwe, ni vigumu sana kuwagomesha walimu. Tena safari hii naona wamejitahidi sana. Walimu ndiyo wanatakiwa kubadili mindset yao na kufanya kitu cha uhakika. Tatizo siyo cwt, tatizo kubwa ni walimu wenyewe
 
Kufuatia hukumu iliyotolewa hapo jana na mahakama ya kazi ya kuwataka walimu kurejea kazini na kuwaamuru viongozi wa CWT kutangazia Umma kuwa mgomo umekwisha, Chama kimesema kitatoa tamko leo saa 4:00 asubuhi. Tamko hilo litaeleza kama chama kimeridhika na hukumu au wanakata rufaa. Taarifa hiyo haijaweka wazi kama walimu warejee kazini ama laa. Mtoa taarifa amewataka walimu kufuatilia vyombo vya habari saa 4 asubuhi. Nawaomba wadau mtakaopa updates mtuwekee humu. Karibuni.
Taarifa zilizotangazwa ni kwamba CWT imekubaliana na uamuzi wa mahakama na kwamba wamekubali kusitisha mgomo na kurejea kazini kama kwaida. Taarifa kamili saa 2.00 jioni source. tbc1
 
wewe ndio mnafiki mkubwa kwa kujitahidi kupandikiza chuki kwa wananchi.cwt inakula pesa za walim kwa kuwakata mishahara yao kila mwezi tena wengine bila ridhaa yao.huo nao ni ufisadi mkubwa.

acha uzushi ww kimeo, kama huna stori kaa kimya
 
waalimu ni wanafiki sana,wanaudhi sana wanapotumiwa kuiba na kuchakachua kura na kushiriki kikamilifu kuiweka CCM madarakani kwa miaka mingi.kinachowapata kinawastahili ili wajifunze kuwa magamba ni janga la kitaifa.hivi hawakujua tabia za magamba:wizi/ufisadi,uzinzi,uuwaji,ushirikina,unafiki,ubinafsi,dhuluma,ulafi na dhambi nyingi zifananazo na hizo na chama kama hicho hakifai kukaa ikulu manake IKULU NI MAHALA PA TAKATIFU NIKIMNUKUU MWL.J.K.NYERERE.Dawa ni kuwaondoa magamba madarakani kinyume cha hapo tutazidi kuibiwa,kunyanyaswa,kudhalilishwa,kupuuzwa,kuuawa na uchumi wa nchi kuzidi kudidimia,hawa walimu wanatakiwa wawe na utambuzi manake hata kama mtu hujui kusoma hata picha huioni
 
huyu jamaa bwana tamuchungu bado ni kipofu na kiziwi pia manake maovu ya CCM hayaoni wala kusikia,huu ni ulevi wa maji ya bendera
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom