Tamko la CHADEMA kuhusu Mafuriko lililotolewa na Dr. Slaa leo

dr early warning sysetem inaunganishwa kwenye nchi za sadec na iko hatua nzuri hilo hulijui au ili mradi tamko

Kwanza ni SADC!!

Anyway, hata kama itaunganishwa na ya SADC unafikiri individual Member States hazitakuwa nazo. Au unafikiri SADC watapataje hizo info??
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Kuna mchangiaji mmoja amesema JK anashindwa aanze lipi aishie wapi maana wakati akitafakari suala la katiba la Kadhi linamsubiri huku Jairo akimngoja mlangoni, ni juzi tu amekwenda mbugani kutafakuri hayo mnamsumbua tena na mafuriko hapo bado zile ahadi 69 hajateleza hata moja na muda dio huo unamyoyomea. Pole rais wangu, JK senior alikwambia wewe hujakomaa ukalia sana leo umebakiza takribani miaka miwili hatujaona unachofanya zaidi ya porojo za magazetini.
 
Ama kweli rais wako. Alikuwa wapi na hilo wazo kabla maafa hayajatokea? he is simply an opportunist.

Soma walaka vizuri siyo. Walaka unasema hivyo vipengere vipo kwenye irani ya uchaguzi wa CDM. Kama huamini labda waombe wana CDM wadhibitishe hayo!!! Tatizo lenu hamkubali kukosolewa!!
 
Nimesoma Tamko la Chadema hakuna cha maana zaidi ya kukosoa...cha kujiuliza Chadema wamechangia nini kwa waathirika wa mafuriko? Au ni porojo tu? Tuliona kule Japan walichangangia dola 2000..

Hapa nyumbani mmewasaidia nini au ndio ilo Tamko?

muulize pinda wa kulialia fungu la maafa liko wapi? mbona tulisomewa na mkulo dom mnamo julai na 11?
 
Nimesoma Tamko la Chadema hakuna cha maana zaidi ya kukosoa...cha kujiuliza Chadema wamechangia nini kwa waathirika wa mafuriko? Au ni porojo tu? Tuliona kule Japan walichangangia dola 2000..

Hapa nyumbani mmewasaidia nini au ndio ilo Tamko?

natamani watu kama wewe wote mzolewe na maji,maana hamna faida ndani ya jamii.
Chadema ama Dr Slaa hawana mamlaka ya hali ya hewa,ingekuwa ni msimamizi wa mamlaka hiyo,ingetoa taadhari kabla ya madhara kwa msisitizo na kuwapa warning a day befre.
Pili chadema haina kitengo cha maafa kwa taifa ingekuwa hivyo wangefanya matende zaidi.rafiki siku zote mnalalamika kuwa chadema kazi yao kukosoa bila kutoa alternative,leo wameeleza njia au ni nini serkali ilipaswa na inatakiwa kufanya nayo mnalalamika what do you need?
Ndiyo maana kila mtu anayetafuta nafasi ni vema akapitia usaili kupima uwezo wake wa ufahamu katika kutatua matatizo ndani ya eneo lake la kazi.
 
Safi sana Dr. Slaa... ila toeni na chopa ikaokoe wahanga maana serikali hii legelege kutwa kulala... yani waziri mkuu anamsubiri rais aseme...mkuu wa jeshi nae hajiongizi mpaka rais hata kutoa chopa ili iokoe ama kuweka daraja la dharura wanajeshi wamelala,... wazee wa intelejensia ndio kabasa hawana hata vifaaa... kazi kweli kweli... kumbe hii issue ilikuwepo kwenye ilani ya chadema .. sasa magamba kwenye ilani yao kulikuwa na nini? katiba hakuna walikuwa na nini?

Wazee wa Intelijinsia wanaweza kurispond rapidly kukiwa na maandamano ya CDM au wanachuo wa Udsm au wamachinga wa Mwanjelwa. Lakini kwenye majanga mmmh! hawana time
 
Mtasema yote lakini mimi sintosahau utendaji wa huyu jamaa alikuwa anakwenda mwenyewe na kutoa maelekezo kwenye tukio si kuhutubia watu kwenye TV.

1.JPG

You are right, but kwenda pekee haitoshi... prevention is better than cure

MTM
 
natamani watu kama wewe wote mzolewe na maji,maana hamna faida ndani ya jamii.
Chadema ama Dr Slaa hawana mamlaka ya hali ya hewa,ingekuwa ni msimamizi wa mamlaka hiyo,ingetoa taadhari kabla ya madhara kwa msisitizo na kuwapa warning a day befre.
Pili chadema haina kitengo cha maafa kwa taifa ingekuwa hivyo wangefanya matende zaidi.rafiki siku zote mnalalamika kuwa chadema kazi yao kukosoa bila kutoa alternative,leo wameeleza njia au ni nini serkali ilipaswa na inatakiwa kufanya nayo mnalalamika what do you need?
Ndiyo maana kila mtu anayetafuta nafasi ni vema akapitia usaili kupima uwezo wake wa ufahamu katika kutatua matatizo ndani ya eneo lake la kazi.

Shemeji usiwe na roho mbaya kuniombea mabaya! Vipi lakini Kakamanda ketu ka Bavicha kanaendeleaje?
 
natamani watu kama wewe wote mzolewe na maji,maana hamna faida ndani ya jamii.
Chadema ama Dr Slaa hawana mamlaka ya hali ya hewa,ingekuwa ni msimamizi wa mamlaka hiyo,ingetoa taadhari kabla ya madhara kwa msisitizo na kuwapa warning a day befre.
Pili chadema haina kitengo cha maafa kwa taifa ingekuwa hivyo wangefanya matende zaidi.rafiki siku zote mnalalamika kuwa chadema kazi yao kukosoa bila kutoa alternative,leo wameeleza njia au ni nini serkali ilipaswa na inatakiwa kufanya nayo mnalalamika what do you need?
Ndiyo maana kila mtu anayetafuta nafasi ni vema akapitia usaili kupima uwezo wake wa ufahamu katika kutatua matatizo ndani ya eneo lake la kazi.
Dada yangu Jose achana nae huyo si kuwa haelewi ila ni kati ya walamba makombo sisi humu JF tumeshajifunza kuishi na hivyo virusi kwa matumaini.
 
Ifike mahali sasa watawala waone umuhimu pia wa kusambaza huduma za kiserikali kwenye mikoa mingine.....maana mpaka yatokee mabalaa kama haya ya mafuriko ndio watu wanatafakari jinsi mji wa dar ulivyo hovyo.......alafu mbaya zaidi ni kwamba shughuli zooote za utawala wa nchi.....yaani mawizara na taasisi zoote nyeti eti ziko dar.....watawala wameshindwa kabisa baada ya miaka 50 angalau kusambaza hizi huduma nchi nzima......mpaka pale mji utakapodondoka jumla (collapse) siku moja ndipo vichwa vya watawala vitaamka.....we angalia tu juzi vidaraja kadhaa vimeshindwa kupitika....watu wameshindwa kuingia mjini makazini........yaani shughuli za kuendesha nchi ziliingia matatani.....kwasababu kila kitu nchini kiko kwenye kasehemu tu kadogo ka mji ambao nao ni feki......it takes disasters in tz yaani ili watu waamke,wafikiri na wachukue maamuzi.......what a country eh!!
 
Dada yangu Jose achana nae huyo si kuwa haelewi ila ni kati ya walamba makombo sisi humu JF tumeshajifunza kuishi na hivyo virusi kwa matumaini.

Kumbe Dr Slaa ni shemeji yako! Haki yako kumtetea bwana shemeji...kumbe na wewe unakula makombo ya shemeji...leo ndio nimejua aise!!
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAAM ZA RAMBIRAMBI NA POLE KWA WANAFAMILIA NA WANANCHI KUHUSIANA NA JANGA LA MAFURIKO YALIYOKUMBA JIJI LA DAR ES SALAAM, MBEYA NA DODOMA .

Usiku wa kuamkia tarehe 20.12.2011 Maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, Mbeya na Dodoma yamekumbwa na maafa makubwa ya mafuriko ambayo yamesababishwa na mvua kubwa ambazo zimeendelea kunyesha mfululizo katika maeneo hayo.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kutoa pole za dhati kwa wanafamilia na wananchi wote ambao wamekumbwa na janga hili kubwa , kwani limesababisha maafa makubwa sana ya vifo, kupoteza mali na miundombinu mbalimbali kuharibiwa vibaya kwenye maeneo husika. Tunapenda kuwahakikishia wananchi hawa kuwa tutakuwa nao pamoja katika kipindi hiki kigumu katika maisha yao kutokana na madhara waliyopata yaliyosababishwa na maafa haya.

Kutokana na janga hili limetukumbusha jambo moja kuwa kama Taifa hatujajiandaa kikamilifu kuweza kukabiliana na majanga kama haya pindi yanapotokea na hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeonyesha dhahiri kuwa havijaandaliwa kimfumo na kinyenzo katika kuweza kukabiliana na majanga kama haya na huu ni udhaifu mkubwa sana kwa taifa lenye miaka 50 baada ya uhuru wake .

Mathalani mpaka sasa hatujaona jitihada zozote ambazo zimechukuliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa katika kuonyesha juhudi za kukabiliana na janga hili kubwa kwa taifa letu,hii inaonyesha wazi kuwa kitengo hiki hakijaandaliwa kuweza kukabiliana na maafa kama ambavyo majukumu yake yanavyopaswa kuwa . Na hii ni hatari kwani kama chombo cha kukabiliana na maafa hakiwezi kufanya hivyo kwa wakati ni kuendelea kuwaacha wananchi waendelee kupata madhara makubwa zaidi. Na haswa ikizingatiwa kuwa idara ya hali ya hewa ilishatahadharisha kuhusiana na mvua hizi.

CHADEMA tunapenda kuikumbusha serikali kuhusiana na ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambayo ilieleza wazi kuhusiana na kukosekana kwa mifumo thabiti ya kujulisha umma kuhusiana na majanga mbalimbali katika miji yetu (Early Warning Systems) kama ambavyo ipo katika nchi nyingi , mfumo huu ni muhimu sana katika kuweza kuufanya umma uwe na elimu ya jinsi ya kuweza kujikinga na majanga haya kwa lengo la kupunguza madhara yasiwe makubwa kama ambavyo taifa hivi sasa linashuhudia.

CHADEMA inapendekeza hatua zifuatazo ziweze kuchukuliwa haraka na serikali ili kuweza kukabiliana na majanga/maafa mbalimbali hapa nchini yanapojitokeza;

I) Kuandaa mfumo wa awali wa kutahadharisha umma juu ya ujio wa majanga (Early Warning Systems) kwa kutumia vyombo na nyenzo mbalimbali ili kuepusha madhara makubwa kwa watu na mali zao.

II) Kutunga sheria mpya ya ujenzi na kuweka viwango vya ujenzi viwe vyenye hadhi ya kimataifa na haswa ujenzi wa kuta mbalimbali na majengo marefu na kuhakikisha kuwa ujenzi holela haujitokezi kwenye miji na majiji yetu hapa nchini.

III) Kuhakikisha kuwa kwenye miji yote mikubwa mtandao wa mabomba ya maji ya dharura unawekwa ili kuweza kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.

IV) Serikali ijiandae mara moja kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama vile kuhara ,kipindupindu na mengineyo ambayo yatajitokeza kutokana na mafuriko haya kuharibu miundombinu ya kusambaza maji, makazi ya watu n.k.

V) Kitengo cha maafa kiwe na vifaa wakati wote , na haswa vifaa kwa ajili ya uokoaji na wawe na utaratibu wa kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuweza kutumia vifaa hivyo kuweza kujiokoa na sio kuacha hali iwe kama ambavyo imejionyesha Dar Es Salaam jana baada ya baadhi ya majaketi okozi kufikishwa kwa wahanga na kushindwa kuyatumia kikamilifu.

VI) Serikali itoe elimu ya jinsi ya kujikinga na magonjwa ya milipuko kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko haya ili kuepusha wananchi wengi kukumbwa na magonjwa hayo pindi yakijitokeza.

Mwisho tunapenda kuendelea kutoa pole kwa wanafamilia wote na wananchi kwa ujumla kutokana na madhara makubwa waliyoyapata , Mungu awajaze nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Tamko hili limetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu CHADEMA .

……………….

DR. Willbroad P. Slaa.

Katibu Mkuu –CHADEMA.

22/12/2011.

Dr. W.Slaa salaam!
Nadhani ili linaweza kuwa tamko la kwanza na zuri na la kufunga mwaka la chadema

siku zote tumepingana swala la kulaumu na kutotoa suluhisho...hapa umefanya, umenena siyo kama mpinzani bali kama mtanzania anayeipenda nchi yake! iwe kwa mengi mengineyo..onyesheni mnaweza na mnajua!!

then chadema ikiwa hivi...mtatuvuta , pepepepe nyingi huwa zinawaweka na nyie muonekane ni wale wale! hii statement inawaweka juu zaidi ya CCM na serikali yake kwa asilimia zaidi ya mia tisa!

moyo wangu saafii!!
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAAM ZA RAMBIRAMBI NA POLE KWA WANAFAMILIA NA WANANCHI KUHUSIANA NA JANGA LA MAFURIKO YALIYOKUMBA JIJI LA DAR ES SALAAM, MBEYA NA DODOMA .

V) Kitengo cha maafa kiwe na vifaa wakati wote , na haswa vifaa kwa ajili ya uokoaji na wawe na utaratibu wa kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuweza kutumia vifaa hivyo kuweza kujiokoa na sio kuacha hali iwe kama ambavyo imejionyesha Dar Es Salaam jana baada ya baadhi ya majaketi okozi kufikishwa kwa wahanga na kushindwa kuyatumia kikamilifu.

Tamko hili limetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu CHADEMA .

……………….

DR. Willbroad P. Slaa.

Katibu Mkuu –CHADEMA.

22/12/2011.

Heshima kwako ndugu Slaa. Hakika umenena vyema na kutoa nini kifanyike badala ya kulalama tu! Natumaini serikali itazingatia chama kiliyoyapendekeza.

Katika hilo hapo juu (pamoja na masuala mengine uliyoyasema kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga), ni jambo la msingi sana. Hapo umeongelea juu ya drills (ambazo zinaweza kua evacuation drills, response drills, relief drills etc.); mara nyingi tumekua tukiona evacution drills zikifanywa kwenye majengo ya mabenki hapa nchini. Lakini aina hizi za drills hazifanyiki kwa wananchi kiujumla katika lengo la kuwaelimisha. Najua ni vigumu kufanya drills kwa watu milioni 40; lakini angalau kunaweza kua na shows (visual shows) ambazo zingekua zinaonyesha namna ya kujiandaa, kukabiliana na kufanya pale maafa yanapotokea. Kwenye luninga zetu kuna vipindi vingi ambavyo havina manufaa kwa jamii (mfano tamthilia zinaonyesha maisha ya watu wa nchi nyingine), vipindi kama hivyo vingeweza kuwa replaced na drill shows.
 
Nimesoma Tamko la Chadema hakuna cha maana zaidi ya kukosoa...cha kujiuliza Chadema wamechangia nini kwa waathirika wa mafuriko? Au ni porojo tu? Tuliona kule Japan walichangangia dola 2000..

Hapa nyumbani mmewasaidia nini au ndio ilo Tamko?

hela zilizopangwa kwa ajiri ya mafuriko hazijaonekana lakini pia Mnyika hukumuona? Na sisi wengine tulikuwa tukisaidi kwaniaba ya CDM
 
Padre na dk wangu Slaa.pole kwa majukum.umepotlea wapi mbona siku ile kwenye kahawa na juice pale umekula kona? pili tamko hili siamini kama ni lako mana hujaeka sahihi yako,naona kama ni magumash tu haya.suala lingine padre,ile HELKOPTA uliyokuwa una chanja nayo mbuga kule IGUNGA IKO WAPI LEO WAKATI WANA DAR WATESEKA NA MAFURIKO?tamko lako HALIENDANI NA UHALISIA, NI KIINI MACHO TU HIKI.nilitegemea helkopta ile ya igunga iongozwe na Mnyika na Halima Mdee chini ya uratibu wako kuokoa maisha ya watu matokeo yake unatuletea SOUND.

Kejeli zako hazina maana bali zinaonyesha usivyo makini katika masuala makuu. Kwani Dk. Slaa ndiye mkuu wa kitengo cha maafa? Kikwete ameweka mfumo gani wa kukabiliana na maafa? Hakuna. Pinda yuko wapi wakati yeye ndiye mkuu wa kitengo hicho kwa ujumla? Helikopta za Warugaruga wetu, eti si za uokoaji ni za kutanua. Wewe badala ya kuwabana wale ambao wamejipa madaraka ya kuwatawala na kuwaringia Watanzania unaanza kuwabeza wale wanawakosoa na kuwapa mawazo mapya. Kazi yako wewe ni ya kupindua hoja.

Mtu mdogo ovyo!
 
Watu wanatumia pesa nyingi sana kukusanya watu kwa ajili ya mikutano, lakini kutumia hizo pesa kwa ajili ya kuwasaidia watu wahame haraka au kuwatangazia basi kuwa kuna hatari inakuja hakuna. We have to change, and the changes start now.

By government, us or whom?
 
Padre na dk wangu Slaa.pole kwa majukum.umepotlea wapi mbona siku ile kwenye kahawa na juice pale umekula kona? pili tamko hili siamini kama ni lako mana hujaeka sahihi yako,naona kama ni magumash tu haya.suala lingine padre,ile HELKOPTA uliyokuwa una chanja nayo mbuga kule IGUNGA IKO WAPI LEO WAKATI WANA DAR WATESEKA NA MAFURIKO?tamko lako HALIENDANI NA UHALISIA, NI KIINI MACHO TU HIKI.nilitegemea helkopta ile ya igunga iongozwe na Mnyika na Halima Mdee chini ya uratibu wako kuokoa maisha ya watu matokeo yake unatuletea SOUND.

Mkuu kwa ninavyojua helcopter ilikuwa ya kukodi kenya sijui ulitaka akakodi ije ikaokoe, na mpaka taratibu zote zilifuatwe sijui ingekuja kumwokoa nani maana maafa yangekuwa ndo yanaishia. Sjui kwanini Jk hajaitumia hiyo aloruka nayo leo kuangalia uaribifu uliotokea badala ya kuokoa kwanza
 
Nimesoma Tamko la Chadema hakuna cha maana zaidi ya kukosoa...cha kujiuliza Chadema wamechangia nini kwa waathirika wa mafuriko? Au ni porojo tu? Tuliona kule Japan walichangangia dola 2000..

Hapa nyumbani mmewasaidia nini au ndio ilo Tamko?
Teh teh!
Japan walikufa watu wengi kidogo hapa kwetu idadi hiyo bado watato(CDM) lakini subiri utasikia wamechangia kiasi gani.
Pia mapendekezo ya taarifa hii yangefanyiwa kazi tungeweza kuokoa majanga mengine yasijitokeze au kupunguza madhara ya hayo majanga.
 
Back
Top Bottom