Tamko kuhusu Chenge lasubiri Sekretarieti ya Maadili

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Tamko kuhusu Chenge lasubiri Sekretarieti ya Maadili
Gloria Tesha
Daily News; Saturday,February 21, 2009 @19:00

Sektarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inatarajia kutoa tamko kuhusu mwenendo wa maadili ya Andrew Chenge kama mtumishi wa umma, kutokana na madai kuwa anamiliki akaunti nje ya nchi yenye thamani ya Sh bilioni moja.

Kamishna wa Sektretarieti hiyo, Jaji Stephen Ihema, aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam, kwamba wanasubiri uchunguzi unaoendelea dhidi yake ukamilike ndipo watoe kauli kulingana na tamko lake la mali anazomiliki kama alivyowasilisha katika chombo hicho. “Sisi tuna matamko yake kama kiongozi wa umma; hatuwezi kuyasemea sasa hivi, ngoja uchunguzi unaofanywa sasa ukamilike,” alisema Jaji Ihema wakati akijibu maswali ya waandishi hao.

Jaji Ihema alikuwa akizungumza baada ya uzinduzi wa ofisi ya Mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi Dar es Salaam, akijibu maswali yao kuhusu nini msimamo wa chombo hicho cha maadili kwa kiongozi huyo kutokana na kashfa dhidi yake.

Chenge, ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, anatuhumiwa kuhusika katika rushwa ya dola za Marekani milioni 12 zilizolipwa na kampuni ya BAE System iliyoiuzia rada Tanzania. Anatuhumiwa kula rushwa kutoka kwa Shailesh Vithlani ambaye pia anatuhumiwa kuwa kinara katika ununuzi wa rada hiyo, jambo lililosababisha ajiuzulu uwaziri wa Miundombinu, mwaka jana.
 
sisi tunachotaka Chege kuchukuliwa hatua n kufikishwa mahakamani haya matamko mbona walishatamka sana.
 
Pamoja na hilo tamko kutobadilisha kitu, huu ni wakati muafaka wa kubadili taratibu na kanuni za mali za viongozi ili ziwe more transparecy kwa kutangazwa mali anazomiliki wakati akiigia kwenye uongozi na mrejesho wa mali anazomiliki wakati wa kumaliza kipindi chake na the difference ndizo mali alizochuma kama kiongozi.
Ni transparecy pekee ndio inaweza kuibua mali za siri, viwanja, hisa na acount za benki za mamilioni zinazomilikiwa na nasaba za viongozi hao(wengine watoto wadogo) ambazo kamwe haziwezi kuorodheshwa Tume ya Maadili.
Hayo ya Chenge ni madogo tuu tena yameweza kuibuliwa na Waingereza, kuna wakina Chenge wengi wenye vijisenti kibao kwenye mabenk safe heavens ya Uswisi na hakuna namna ya kuwagundua bila trasnsparency kwa jamii nzima.
 
Chenge kwa hatua aliyofikia tayari alitakiwa awe amekwisha wekwa pembeni katika kila sehemu ,alitakiwa asiwe kwenye madaraka au cheo kutoka sehemu yeyote ile iwe serikalini au kwenye Chama ,vilevile Raisi alitakiwa amuwajibishe na kumuezua katika nafasi zote za uongozi bila ya kungojea mahakama au majaji ,ile kumiliki tu bilioni moja na kuhusishwa na rushwa ya Rada tayari Raisi angekwisha kumwita Ikulu na kumuwajibisha ,lakini Rais nae anasubiri uchunguzi,Raisi ambae alitakiwa ajue moja kwa moja kuwa jamaa hakuwasilisha mali zake,jamaa alihusika kwenye rada na mambo mengine ,rais ana uwezo wa kuyajua hayo bila ya kupitia uchunguzi ,maana hili la mtu kutaja mali zake ni jambo ambalo limeshapita ,kumbukumbu zipo, alichokuwa nacho raisi huyu ni uswahiba tu kwa ufupi Mkpa na biashara huyu na uswahiba. Serikali hii haifai kabisa kuongoza nchi ni lazima ijiuzulu tu ,japo hawataki lakini kwa wanavyoendesha nchi si viongozi wanaowajibika kwa wananchi wao badi tupo pale pale kwenye masilahi binafsi.
 
Uchunguzi gani tena, mie nilifikiri uchunguzi ulikamilika tangu April 2008. Yaani Tanzania hii kweli inaendeshwa kienyeji sana. Uchunguzi ulishakamilika, kilichobaki ni Chenge kusogezwa pale Kisutu. Watanzania hawahitaji hayo matamko, wanahitaji ACTIONS. Matamko mnatakiwa mpeane huko kwenye vikao vyenu vya SISIEMU na si kuwaadaa WATANZANIA. Hatuna muda na matamko bali tunataka kuona sheria inachukuwa mkondo wake.
 
Hii tume ya maadili haiko huru kabisa katika maamuzi yake. Eti inasubiri uchunguzi ukamilike ndiyo na wao watoe kauli yao!!!! Kwa maana nyingine wao wapo tu hawana kazi yoyote ile hawana uhuru wowote wa kutoa kauli yao mpaka wasubiri chombo kingine kiwafanyie kazi na wao wakafanye ukasuku wa kuimba na kuyarudia yale yaliyofanywa na chombo kingine. Hii tume ya maadili inastahili kufutwa maana haina kazi yoyote ile bali inafuja fedha za serikali tu. Pamoja na kuwa na tume hiyo ya maadili ya uongozi sasa hivi maadili ya viongozi wa serikali yameanguka vibaya sana kuliko wakati mwingine wowote ule tangu tupate uhuru lakini hatuwasikii hata siku moja wakisema lolote au kufanya lolote lile kuhusu kukosekana kwa maadili ya viongozi. Tume ya maadili ivunjwe maana imeshindwa kufanya kazi yake ili kuhalalisha kuwepo kwake.
 
Stori nyiiiingi usiku unakuwa mkubwa....na wakambane nanihino huko keko ili atuambie fweza wamezichotaje...
 
Hii tume ya maadili haiko huru kabisa katika maamuzi yake. Eti inasubiri uchunguzi ukamilike ndiyo na wao watoe kauli yao!!!! Kwa maana nyingine wao wapo tu hawana kazi yoyote ile hawana uhuru wowote wa kutoa kauli yao mpaka wasubiri chombo kingine kiwafanyie kazi na wao wakafanye ukasuku wa kuimba na kuyarudia yale yaliyofanywa na chombo kingine. Hii tume ya maadili inastahili kufutwa maana haina kazi yoyote ile bali inafuja fedha za serikali tu. Pamoja na kuwa na tume hiyo ya maadili ya uongozi sasa hivi maadili ya viongozi wa serikali yameanguka vibaya sana kuliko wakati mwingine wowote ule tangu tupate uhuru lakini hatuwasikii hata siku moja wakisema lolote au kufanya lolote lile kuhusu kukosekana kwa maadili ya viongozi. Tume ya maadili ivunjwe maana imeshindwa kufanya kazi yake ili kuhalalisha kuwepo kwake.

Watakuambia hawana meno. Lol.
 
Chenge kwa hatua aliyofikia tayari alitakiwa awe amekwisha wekwa pembeni katika kila sehemu ,alitakiwa asiwe kwenye madaraka au cheo kutoka sehemu yeyote ile iwe serikalini au kwenye Chama ,vilevile Raisi alitakiwa amuwajibishe na kumuezua katika nafasi zote za uongozi bila ya kungojea mahakama au majaji ,ile kumiliki tu bilioni moja na kuhusishwa na rushwa ya Rada tayari Raisi angekwisha kumwita Ikulu na kumuwajibisha ,lakini Rais nae anasubiri uchunguzi,Raisi ambae alitakiwa ajue moja kwa moja kuwa jamaa hakuwasilisha mali zake,jamaa alihusika kwenye rada na mambo mengine ,rais ana uwezo wa kuyajua hayo bila ya kupitia uchunguzi ,maana hili la mtu kutaja mali zake ni jambo ambalo limeshapita ,kumbukumbu zipo, alichokuwa nacho raisi huyu ni uswahiba tu kwa ufupi Mkpa na biashara huyu na uswahiba. Serikali hii haifai kabisa kuongoza nchi ni lazima ijiuzulu tu ,japo hawataki lakini kwa wanavyoendesha nchi si viongozi wanaowajibika kwa wananchi wao badi tupo pale pale kwenye masilahi binafsi.
Mwiba, Kitine anajua anachomaanisha nashangaa kwanini Chiligati amekanusha! CCM ya sasa inajiendesha kienyeji haijawahi kutokea. Hili linadhihirishwa na hatua ya UVCCM kumweka pembeni Francis ili kupisha uchunguzi wa ukiukwaji wa hatua.

Kama UVCCM imemsimamisha Francis kwa kigezo cha kupisha uchunguzi na CC (ya chama hichohicho) ikaendelea kuwatetea Chenge, Lowassa, Rostam, et al., ni dalili tosha kwamba CCM inaendeshwa kienyeji. Hili haliitaji uchambuzi maana ni sawa na kusema kama A=B na B=C, basi 'automatically' A=C.
 
Msije mkashangaa kwamba katika hiyo tume ya maadili Chenge naye ni mjumbe.
 
Back
Top Bottom