Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

Viongozi Dhaifu wa serikali ya CCM waki nukuu madai ya Madaktari husema tu yale ya Posho.
Madai ya hali mbaya na mazingira mabovu ya Hospitali zetu wanashindwa kuyasema kwa vile ndimi zao husinyaa kwa udhaifu.
Kwa sababu viongozi wetu dhaifu wanajua kwamba Mtanzania avearage hajitafutii ukweli bali husubiri mtu mwingine ahangaike kumtafutie, kitu ambacho ni udhaifu. Hutumia mwana huo kueleza sehemu ndogo tu ya madai ya Madaktari katika vyombo vya habari na kuirudia tena na tena na tena ili wale wanaosubiri kutafuniwa kumezeshwa chochote kinachotoka katika Main stream Media.

Madai kuhusu Mazingira duni ya hospitali zetu.
Hospitali kunyimwa mafungu yake.
Majibu ya kunya wanayopewa na warasimu wa serikali pale wakitaka kufuatilia mambo ndiyo mambo ya msingi katika mgomo huu.
Udhaifu wa waziri mkuu Rais na wabunge wa CCM ni sababu tosha ya kuogopa kuyasema haya atika vyombo vvya habari.
Wakibanwa utasikia, hilo ni jipya katika madai.

Ili ku score point nyingi kisiasa Waziri mkuu Rais na wazembe wenzao wengine wamekuwa wakilia lia kwamba madai ya msingi ya madaktari ni posho.

Mgonjwa akifa kwa sababu handling ilikuwa mbaya anayela umiwa ni Daktari aliye mtibu si katibu wa Wizara aliye iba fungu la Hospitali na kumjengea nyumba hawala yake au kusomesha kijana wake UK. Lawama wanazopata madakatari kwamba ni wazembe siku zote hazihusishi udhaifu wa serikali na wizi wa mafungu, ununuzi wa vifaa vibovu na ukosefu wa good maintanance ya vifaa vilivyopo.

Wagonjwa wanao kufa kwa cross contamination inayotokana na ukosefu wa maji safi na Gloves ni kwa maelfu kila mwaka. Lawama zote za vifo hivi kutoka katika familia ni kwa madaktari tu.

Kama hakuna maji bombani Daktari anatakiwa kufanya nini?
Kama meza na makabati yameoza daktari anatakiwa kufanya nini?
Kama hakuna gauze daktari anatakiwa kufanya nini?
Kama vyoo vimefurika kwa sabu sewage system imezeeka daktari anatakiwa kufanya nini?
Kama hakuna vifaa vya kudekia na kusterize sakafu dakatari anatakiwa kufanya nini?
Kama hakuna dawa za kutuliza maumivu makali dakatari anatakiwa kufanya nini?
Kama hakuna gauze,nyembe, bandage, thermometer, x ray na gari la wagonjwa daktari antakiwa kufanya nini??

Wengi wanaona mahali alipo lazwa Dr Ulimboka wanadhani hiyo ndo Muhimbili ambayo kila mlala hoi ana access.
hapo ni MOI ambako ni pochi tu ndo inaongea. Huna pochi dont even think abaout it, comeooon this is Tanzania!

As a National we are not serious at all.

Mbona katika madai ya madaktari kinacho tamkwa sana ni posho mbalimbali na mishahara?Kama kweli wanaumia kuon watanzania wakisongamana hospitalini mbona sasa wana waacha wana kufa bila kuonyesha jitihada za kuokoa maisha wagonjwa hao?Hu ni uzalendo au ubinafsi mbele?
 
Sidhani kama ni bora kwa wao kuendelea kufanya kazi katika hali ngumu kama hiyo basi tu kwa kuwa wagonjwa watakufa, maana wakiacha kugoma madai yao hayatafanyiwa kazi kamwe, na kama tunavyojua serikali yetu lazima uimwagie maji ya baridi ndio itaamka la sivyo hola!!
 
Common, lets come to our senses...vita vya panzi furaha ya kunguru. Ubabe sio dawa ya matatizo popote pale duniani.

Huo sio ubabe na nshangaa watu wanavyosema madaktari ni wababe kwa kugoma, la hasha, wanadai madai ya msingi ambayo pasipo kusimama imara hayatafanyiwa kazi, na wewe unalifahamu hilo kabisa maana unaijuia serikali yako ilivyo
 
TZ naona kila mtu amekuwa msanii na mwanasiasa, hili tamko la madaktari wanajifanya wanagoma kutetea wagonjwa wakati kikubwa wanadai pesa.
Madaktari hawa hawa ndo wamesababisha vifo au ulemavu wa kudumu kwa mamia ya waTZ kwa uzembe wao au kutojali kwao harafu leo wanaleta picha kuonyesha wako na wananchi, wengine ndo wezi wa dawa hospitalini.
Hii ni mchemko tu, ngojeni ndo mtajua madai yenu na jeuri yenu si chochote.

Kijana madaktari HAWAJIFANYI wamegoma ila WAMEGOMA, there is a difference and you or anyone can do nothing about it. Serikali inatakiwa kujua jinsi ya ku-prioritise mambo na mojawapo ni kujali hospitali zetu kuliko kitu kingine, so WAKE UP!!!!
 
KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012

Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.

Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.

Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.

Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka ,

Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja

Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.

Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.

Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.

Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!

Imetolewa na
Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

huu ni ujumbe kutoka kwa Dr ulimboka stephen kutoka ICU!!!!
View attachment 57669

Iweje polisi kuichunguza Usalama wa Taifa?!
 
Tamko limekosewa hawajaweka yale madai yao ya msingi ya shilingi milioni 3 , wamejifanya this time wapo upande wa wananchi wakati wananchi wakifika hapo Muhimbili hawatibiwi. Mtu anayelala chini kakosa kitanda ndio anastahili aachwe afe kwakuwa serikali haijaleta kitanda?
 
KAMA NI KWELI HAYO MADAKTARI WANAYOSEMA, Majadiliano ya Dhati ndicho kilichoagizwa na mahakama; mbona wameng'ang'ania kugoma na kukiuka amri ya chombo cha Sheria.

Tusiweke Watanzania REHANI na Maisha yao. Tumuogope MUNGU; Turudi kazini na kutafuta suluhu kwa MAJADILIANO kama ilivyoagizwa na mahakama

KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012

Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.

Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.

Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.

Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka ,

Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja

Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.

Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.

Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.

Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!

Imetolewa na
Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

huu ni ujumbe kutoka kwa Dr ulimboka stephen kutoka ICU!!!!
View attachment 57669
 
Wazushi tu nyinyi ..nyinyi mnadai fedha sasa mnakuja na uboreshaji wa afya .tumewachoka sasa msifikiri sisi wananchi tuko pamoja nanyi wauaji wakubwa ambao mumeweka fedha mbele... tumewachoka kama mmeshindwa kufanya kazi serikali nende mkaazishe zahanati zenu..... hongera serikali asiyetaka kazi fukuzeni tu tujue moja hatuna hawa binadamu wapenda fedha badala ya utu kwanza. mana madai yenu ya msingi mumetekelezewa lakini bado tu sijui mnawatakia nini watz... mengine mumeambiwa yatatekelezwa huko mbeleni kama uwezo ukiwepo lakini bado tu..ni haki kusema anajambo lenu nyuma

Aisee ubongo wako ni mdogo sana hata sijui unaishije nao, umeshawahi kwenda hospitali ukaandikiwa vipimo, ukaenda kwenye xray-mbovu, ct scan-mbovu, ultra sound-mbovu, etc ukaambiwa uje baada ya mwezi utakuta vimetengamaa na wewe unaumwa karibia ya kufa. Acha kubwabwaja ovyo kama vile unajua unachokiongea, wanaofanya kazi mahospitalini wanayaona hayo so SHUT UP. Au kwa sababu wewe una hela utaenda private hospitals na kupata matibabu, vipi kuhusu hao wagonjwa wasio na hela ambao madaktari kazi yao ni kuwarudisha kila siku nyumbani na ugonjwa wao kwa sababu hakuna vipimo vya kuwapima? Mtu umesoma udaktari miaka na miaka matokeo yake unashindwa kuwatibu wagonjwa wako kwa kuwa hakuna vifaa na dawa, whats the point? Si ni bora basi wakafunga hizo hospitali tujue moja? Wanaowaua wagonjwa sio madaktari ni serikali maana hata kama madaktari watarudi kazini leo, bado wagonjwa wengi wataendelea kufa kwa sababu ya huduma duni zilizopo kwenye hospitali zetu...
 
Wapo madaktari wengi ambao wamesomeshwa na serikali mwisho wake wamekimbilia nchi nyingine kufanya kazi na serikali haijawalazimisha warudi hapa. Na hawa wagomaji kama demand yao kubwa ni afadhali waende huko wanapotakiwa maana hapa kwetu hata wakifika ofisini hawatupatii matibabu hadi tuwape cha juu.
 
Viti maalimu CCM nini?

Mimi najali sana hatma ya TAIFA letu sio mambo ya itikadi, si hilo tu vile vile naona mambo beyond my noses.

Bahati nzuri umeweka quotation yako ambayo ina-nullify kila kitu kama sikosei, it goes "Simple life is healthier than egoism" How do you mean my fellow countryman, if I may ASK?
 
Viti maalimu CCM nini?

kwa kweli huyu ni viti maalumu chama dhaifu... kama anawaonea huruma namna hiyo wagonjwa ... aitishe maandamano tazania nzima ya kuwashurtisha serikali wasekilize matakwa ya ma dr. ili madr wao wawe wanaendelea nakazi... sio yeye anakaa kimya tu... nakuongea kokokooo.... walimu wakitaka waongezewe mshahara watagoma wanafunzi?? wagonjwa wenyewe wako tayari ili kwa kufa kwao watoto na vijukuu waje watibiwe kwa mapenzi ...,
 
Mbona katika madai ya madaktari kinacho tamkwa sana ni posho mbalimbali na mishahara?Kama kweli wanaumia kuon watanzania wakisongamana hospitalini mbona sasa wana waacha wana kufa bila kuonyesha jitihada za kuokoa maisha wagonjwa hao?Hu ni uzalendo au ubinafsi mbele?
Waacheni wafe kwa manufaa ya wengi na kizazi kijacho. Unajua ni wa ngapi wanakufa kwa kukosa vifaa vya kuwatibia. Madakitari wanaona wa ngapi wakifa kwa kukosa matibabu yakinifu kutokana na uduni au ukosefu wa vitendea kazi? Tusiongee tu kwa kuwa sis tuna kadi za kutibiwa mahospital makubwa na kwa garama zozote. Acheni siasa watu wanakufa kwa kukosa ambulance, dawa tena panado, unaambiwa kanunue nje. Panado!! Doctors nawaombea kwa Mungu wangu na katika yeye mtashinda. Anayekufa kwa ajiri ya wengine ni fahari kwa kwake na manufaa ya wengi. Natamani kuugua ili nife wakati huu na Mungu wangu ataniona shujaa
 
wavivu wa kufikir ndio wanaoshabikia mgomo wa madactari, binafsi siwaungi mkono hasa hao wa muhimbili baadhi yao ni wauwaji wakubwa wapo kipesa zaidi, sitosahu siku moja nilipoenda kujifungua muhimbili mwaka 2010 mwezi february. Nikiwa nagugumia maumivu docta mmoja jina ninalo akaanza kunitukana eti kwa nini nilienda usiku hospitali na kunitaka nimpe hela ya tax, nikamwambia asubiri. Nilitukana sana na kuandikiwa nijifungue kwa kisu bila kujua sababu nilipelewa thieter huku nalia. Baada ya hapo nikaanza kudaiwa hela ya tax na kwa kuwa sikuwa na pesa kwa wakati ule nilimpa elfu kumi, wee alinitukana nilishamsamehe ila sitomsahau maishani mwangu. Naomba tu madaktari na serikali mmalize migogoro na kutuhudumia bila migomo weken uzalendo mbele.
MaBaraka, yule daktari mmoja alikukwaza usiku ule ndio amekufanya uwe na bitterness kiasi hicho? si ungemshitaki kwa utawala wa hiyo hospitali?
Isengukuwa hayo maneno kwenye mstari wa mwisho wa comment yako, ningelikuwa na shida kuamini kuwa mtoto uliyempata usiku ule amekuwa baraka kwako.
Asante kwa kujifunza kusahau baada ya kusamehe
 
I will always stand for my personal views:

Lakni pia naungana na bwana FIDIVIN hapo juu. Demand kubwa ya ndugu zetu doctors ni pesa (salary and allowances), but pia tukumbuke kuwa suala la vitendea kazi na mazingira bora kwa wagonjwa limekuja baadae hasa baada ya kuona kuwa wananchi wengi walisita ku-support kugoma kwao ambao hasa kulilenga maslahi yao zaidi (the maximum figure ni apx Milioni 13 kwa wale Seniors)

Hata nisingependa kuzungumzia ni watu wangapi wameathirika na huu mgomo hasa kupoteza maisha, wengi wao ni wale maskini kabisa wasio na uwezo wa kupata tiba ktk Hospitali binafsi.

Kwaiyo binafsi nayaafiki madai yao kwa kiwango flani, lakini kama the Govt failed to meet 100% of their demand basi ni vyema tukaawaangalia hawa wananchi wanaokufa pia. Hata imeweza kufika angalao 50% ya kile wanachokitaka basi wangekaa chini ku-negociate kupeana muda mwingine hata miaka miwili mingine ili serikali kufikia 100% of their demand.

Lakini sioni sawa kutoa kisingizio cha kudai vitendea kazi na maboresho ya mazingira kwa wagonjwa.... wakati watanzania wanazidi kufa.... haya mazingira na vitendea kazi duni tulikuwa navyo siku zote lakini angalao wagonjwa walikuwa wanapata ahueni ya tiba kwa hivyo hiyo, yes ni kweli tunahitaji vitendea kazi na mazingira bora, hatutaki wagojnwa walale chini... lakini maana yake tunazidi kumwadhibu huyo mgonjwa kwa kufa kabisa kwani hata hiyo huduma ya awali ameikosa kabisa sasa.

Pia, inashangaza sana kuona watu wengi wanashabikia na kuthubutu kusema "bora madaktari wagome" jamani mnaosema hivyo mnawakumbuka wale bibi zenu, babu zenu na wengine wengi walioko huko mikoani na vijijini kweli ambako pengine hakuna mbadala.

I do not support huu mgomo, natamani everything should be settled on the table, lakini ndugu zetu doctors -- you should think about humanity in wide.
 
mbona katika madai ya madaktari kinacho tamkwa sana ni posho mbalimbali na mishahara?kama kweli wanaumia kuon watanzania wakisongamana hospitalini mbona sasa wana waacha wana kufa bila kuonyesha jitihada za kuokoa maisha wagonjwa hao?hu ni uzalendo au ubinafsi mbele?

je hufahamu kwamba inapasa wachache wafe kwa ajili ya wengi? Umeshalazwa hospitali wewe?
 
Mbona katika madai ya madaktari kinacho tamkwa sana ni posho mbalimbali na mishahara?Kama kweli wanaumia kuon watanzania wakisongamana hospitalini mbona sasa wana waacha wana kufa bila kuonyesha jitihada za kuokoa maisha wagonjwa hao?Hu ni uzalendo au ubinafsi mbele?
.
Wtanzania wamezoea kudanganywa kwa muda mrefu ingawa wadanganyaji huja kwa sura na mitindo tofauti..lakini kwa ujumla wao ni Hao hao....Wanachokipigania madaktari ni vijisenti tu wala sio kwamba wanahuruma sana kwa wananchi wanaopaswa kuwatibu...km wangekuwa na huruma hiyo wasingewaacha wagonjwa wakifia hospitalini eti kwa madai ya kudai mashine za x-ray kwa mfano! Badala ya kutibu sasa wamekuwa wauaji km majambazi wengine..na baada ya kadhia hii jamii itabaki na kovu moja muhimu ya kutokuwa na imani na madaktari hususan hawa wa 'dot.com'. kwani ni rahisi kughilibiwa kwa pesa hata na wapuuzi ambao wanafahamika kazi zao ni 'kuchumia tumbo' kwani kwao maoni sahihi ni wanayoyatoa wao, na si ya wengine.
 
wewe ndiyo unatakiwa ulete alichosema. Mimi nimesema alisema madaktari wanapewa pesa na wanasiasa ili inekane hii nchi haitawaliki. wewe kama unalingine uje hapa acha kukurupuka zomba

Hapana hakusema "wanasiasa" alisema "vikundi". Rekebisha kauli yako.
 
Mbona katika madai ya madaktari kinacho tamkwa sana ni posho mbalimbali na mishahara?Kama kweli wanaumia kuon watanzania wakisongamana hospitalini mbona sasa wana waacha wana kufa bila kuonyesha jitihada za kuokoa maisha wagonjwa hao?Hu ni uzalendo au ubinafsi mbele?
. Hengo kumbuka waliokufa kwa kukosa huduma bora wanazozitetea ni wengi sana, maana kuna waliofia hopsitalini kwa sababu tu hakukua na sindano au nyuzi za kushonea kidonda kisiendelee kutoa damu. Serikali ifanye hima iwasikilize madaktari Pinda unachelewa nini ulisema kinachofuata madaktari wanakijua na mkuu akakusaliti, Tunza heshima yako hujafisadi kama wenzako hao wenzako account zao Uswisi ni nono wewe Utarudi mpanda na huko utakamatwa kama kuku kwa kusababisha shida kwa wa TZ wote. Ushauri wa bure.
 
Huo sio ubabe na nshangaa watu wanavyosema madaktari ni wababe kwa kugoma, la hasha, wanadai madai ya msingi ambayo pasipo kusimama imara hayatafanyiwa kazi, na wewe unalifahamu hilo kabisa maana unaijuia serikali yako ilivyo

Najua kabisa nani anafanya ubabe ndo maana nashauri kurudi mezani.Wale wazee wote ni kina baba haambiliki...hata usemaje hawsikilizi. Wanasema yale wanayotaka kusema
 
David Abeid bado anaishi? inakuaje kama kweli kuna peoples power how long shall they kiil our prophets while we stand aside and look? hivi tunaakili sisi, lazima wanza kudondoshwa mmoja baada ya mwingine kuanzia leo,

Umesomeka mkuu wangu,tuache maneno ni muda wa vitendo sasa!
 
Back
Top Bottom