Tamko: CCM yawajibu Lowassa na Zitto pia yakana kushiriki kwenye kuivuruga CUF

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Ikiwa imepita siku mbili tangu aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kueleza tathimni ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli, ambapo alidai kuwa, katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi huo, kumekuwepo na ukiukwaji wa misingi ya demokrasia na utumishi wa umma kuwa kaa la moto.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimevunja ukimya na kumjibu kwa kusema kuwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita alikuwa wa kwanza kukiuka misingi ya demokrasia. Kuhusu utumishi wa umma kuwa kaa la moto, imemjibu kuwa wanao lalamika hivyo ni wale wanaotumiwa kuficha mafisadi na wakwepa kodi.

Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka amewaambia waandishi wa habari kuwa Lowassa hastahili kuituhumu serikali ya Rais Magufuli kuwa inakiuka misingi ya demokrasia.

“Demokrasia ya kweli lazima ianze ndani ya chama, ni demokrasia ipi iliyotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea kuvigharamia kwa kuamua kumteua mgombea mtunguo ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania?,” amehoji.

Ole Sendeka ameongeza kuwa “Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kulidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia.”

Amesema CCM haigopeshwi na matamko ya Lowassa anayotoa katika vyombo vya habari kwa kuwa havitaiathiri na kwamba imemamua kumjibu kwa madai kuwa anapotosha umma kwa kueleza mambo yasiyo na ukweli.

Ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutochukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko.

“Wanasayansi wa masuala ya siasa waiangalie demokrasia ya CHADEMA na UKAWA inavyofanya kazi maana ni kihoja, watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge viti maalumu. Kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA,” amesema.

Pia Sendeka amemtaka kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo kutoichukia serikali ya Rais Magufuli kwa kuwa inatekeleza yale aliyokuwa anayapigania.

“Chuki ya Zitto ya kuendelea kunyooshea kidole serikali ya CCM haina tija, sababu inatekeleza yote aliyokuwa akiyapigania,” amesema.

Katika hatua nyingine, Sendeka amedai kuwa CCM haijashiriki kukihujumu chama cha Wananchi (CUF) kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa kuwa kinawachonganisha viongozi wa chama hicho ili kigawanyike.

“Hatuna haja ya kuhangaika na CUF na wapanga siasa za uongozi CHADEMA, hatujashiriki kukivuruga na hatuna muda huo,” amesema.

=======

Ndugu wanahabari,

Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taairifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zinazolenga kukejeri, kudhihaki, kukatisha tama, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Seikali zake katika kuleta maendeleo kwa Watanzania

Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti mawili ya nje ambazo hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha na kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania

Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na kuichafua taswira ya nchi yetu.

Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua kujivua uzalendo na kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi yetu kwa maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia kujua nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni watanzania. Je ni tama ya madaraka tu au mengine?. Hakuna anayepinga ukosoaji bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema

Ndugu wanahabari,

Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita tathimini ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa octoba 25,2015

Katika taairifa yake, alidai kuwa alileta msisimko mpya katika siasa za Tanzania, kwamba ameshirikiana na wenzake kuionyesha nchi yetu maana ya demokrasia na kukosoa juhudi za serikali na wateule wa Rais.

Demokrasia kimsingi ni dhana inayohusisha ushiriki na kuheshimu mawazo ya wengi katika kufikia uamuzi. Ikiwa maana halisi ni hii, tunajiuliza ni ipi demokrasia aliyoionyesha Lowassa ambayo leo anajisifu kuwa nayo?

- Tulishuhudia akiwa mgombea Urais wa chama ambacho hakijui, hakushiriki kukijenga wala kutoa mchango wowote unaompa hadhi ya kupeperusha bendela huku katiba na kanuni ya chama hicho ikivunjwa. Kidemokrasia anayepewa fursa ya kupeperusha bendela ya chama chochote makini duniani ni kiongozi au mwanachama aliyethibitika kwa imani na matendo, kuzielewa, kuzitekeleza, kuzitetea falsafa, itikadi na malengo ya msingi ya chamahicho. Mgombea ni taswira halisi na alama muhimu inayoakisi dhamira ya chama husika machoni kwa wananchi.

- Demokrasia ya kweli lazima ianzie ndani ya chama, ni demokrasia ipi inayotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea, kuvigharamia na walivyovitumikia kwa kuamua kumteua mgombea “MTUNGUO” (ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania). Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kilidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia

- CHADEMA watuambia njia iliyotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu. Ni demokrasia gani inayotoa fursa kwa baadhi tu ya viongozi kuteua wabunge ambao wanakiwakilisha chama chote. Ambapo kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA walikosa watu wanaowafahamu na kuamua kuwateua wanawake maswahiba wao ndani ya CCM. Msingi wa kawaida wa kupata wabunge wa viti maalumu ukiacha kura za maoni, kigezo kingine muhimu ni mchango wa mgombea / mwanachamahuyo katika kukijenga na kukitumikia chama chake. Yaliyotokea kwa CHADEMA kwenye wabunge wake wa viti maalumu ni mapya kwenye ulimwengu wa demokrasia. Inahitaji wataalamu wa sayansi ya siasa kufanya utafiti wa aina hii mpya ya demokrasia

Tulidhani baada ya mwaka mmoja kupita, wenzetu hawa wangelikuwa wamejifanyia tathimini, kujikosoa, kujisahihisha, na hata kufanya uungwana wa kuwaomba radhi wanachama wao kwa uvunjifu mkubwa wa misingi ya demokrasia, katiba na kanuni za vyama vyao

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutokuchukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko, yasiwe ni nyimbo za kuburudisha au kutoa matumaini hewaq kwa wanachama na wananchi. Kanuni mojawapo ya demokrasia ndani ya vyama ni lazima ionekane katika muundo wake na katika utekelezaji wa muundo huo

Umefika wakati vyama vya siasa vinapaswa kujifunza kuuza sera ili kujenga na sio kusubiri matukio kwa ajili ya kupata huruma ya wananchi. Tunasubiri kushuhudia na kusikia demokrasia demokrasia itakavyoendeshwa katika uchaguzi wa ndani wa vyama hivyo ambapo kuna taarifa mmoja wa vigogo amefanikiwa kupata kiasi cha dola milioni 15 zitakazomsaidia kupanga safu yake ya uongozi

Katika kutimiza mpango huo, tayari yapo mawasiliano ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi wakitoka Zanzibar na sehemu zingine za nchi kuja Dar es Salaaam, na imeonekana dhahiri mazungumzo yao kutowashirikisha viongozi wenzao waandamizi kwani yanalenga kafanikisha mpango huo.

Mheshimiwa Rais Dk John Pombe Magufuli, ameendelea kufanya juhudi kubwa katika kujenga nchi kwa kuimarisha utendaji na nidhamu ya utumishi serikalini, kukusanya mapato na kusimamia matumizi sahihi ya fedha, kupambana na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na kusimamia haki, usawa na wajibu kwa raia. Mwenzetu anayaona haya kuwa ni kuufanya utumishi wa umma kaa la moto.

Juhudi hizi na nyinginezo ikiwemo ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, afya na kununua vitanda vya wazazi, kutoa elimu burekuanzia shule ya msingi mpaka sekondari na nyinginezo hazipaswi kukatishwa tama kwa maslahi ya wachache ni vyema kuziunga mkono kwa maslahi ya taifa letu

Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Rais Dk. Magufuli madarakani, CCM inawaomba wananchi kuendelea kummunga mkono katika dhamira yake safi yakuwaondolea kero, kuboresha huduma za jamii na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na;-

CHRISTOPHER OLE SENDEKA

MJUMBE WA NEC NA MSEMAJI WA CCM

28/10/2016
 
Kumbe CCM wanafurahia maisha yanavyozidi kuwa magumu wadogo zetu kukosa mikopo tetemeko la Kagera njaa Karagwe na sehemu nyingine zenye shida Eee mungu tunusuru na hili dudu Baba wa mbingu Twakuomba utusikilize wanaotoa matamko ya ajabu baba wape ububu au upofu baba twakuomba midomo yao ipeleke upanda baba twakuomba Amina

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni hadithi ambayo huwezi kuamini kuwa inaweza kuandaliwa na watu wenye weledi. Hakuna hata hoja moja iliyojibiwa katika zile walizozitaja.

Serikali hii imethibitika kugandamiza demokrasia. Kwa maelezo ya Olesendeka inaonekana kuwa serikali kugandamiza demokrasia ni sahihi kabisa kwa sababu na vyama vya siasa vinagandamiza demokrasia.

Hoja nyingine muhimu ni ugumu wa maisha ambao raia wanapitia. Jibu la Olesendeka ni kuwa huo ugumu wa maisha haupo kwa sababu serikali imenunua ndege.

Lazima uwe na upungufu mkubwa sana kuamini kwamba haya ndiyo majibu ya hoja zilizotolewa. Hawa ndiyo wanaoiba, wakifikishwa mahakamani, utetezi wao ni kwamba wizi wao siyo kosa kwa sababu wengi wanaiba!!!!
 
Humu JF kuna watu takiribani miaka 8 tokea Lowassa aachie uwaziri mkuu walikuwa Lowassa haters na ant JK kwa hali yoyote,walipondwa na kusimangwa,hakuna zuri hata mmoja.Na kwa namna mmoja au nyingine zilikuwepo sababu zilizopelekea watu wakatamka hivyo.
Sasa baadhi ya watu wale wale ghafla wanamtukuza Lowassa na kwa JK.hadi JK kasema msimlishe maneno.
Isije ikawa sisi kwa sisi wananchi tumeshindwa kujitambua,kumnukuu Mwalimu Nyerere sio muarobaini,labda makomredi tumedanganywa kwa hila.
 
Natarajia msemaji wa chama kinachotawala kwenda kwenye vyombo vya habari kuelezea utekelezaji wa sera za chama chake, mafanikio na matarajio ya wananchi kwa mambo yajayo. Chama kinachotawala hakina majukumu sawa na vyama vya upinzani, chenyewe kina dhamana kubwa kwa wananchi. Lakini kwa kukosa umakini, tunaona hapa kainuka mzee mzima kwa hasira kwenda kufoka dhidi ya vyama vya upinzani. Amekisema zaidi Chadema kwa sababu ambazo wote tunazifahamu. Watanzania wa sasa si wale wa miaka ya 1990. Wanajua sana mchele na pumba katika yote yanayosemwa. Ni kupoteza muda kujaribu kufanya damage control.
 
Hawa ccm wanatuona watanzania hatujitambui,wengi tunawaelewa maovu yao,kwanza press ya kitoto sana kuzungumzia individual lowasa na zito,badala wazungumzie mambo ya msingi yanayowagusa watz kama madawa,hali ya uchumi unamshambulia mtu,wana akili ndogo,ccm nawafananisha na shetani.
 
Taarifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyotolewa na msemaji Ndg Christopher Ole Sendeka kwa vyombo vya habari, leo tarehe 28/10/2016 Lumumba, Dar es salaam.
View attachment 425621
View attachment 425624View attachment 425625

Form Six FFF Div 0 haikuwa ya bahati mbaya bali ni halali kwa uhakika.

Nani asiyejua taratibu, kanuni na demokrasia vilivyo kiukwa ndani ya CCM wakati wa kumpata mgombea urais???????
Ni kiongozi gani wa CCM anayepatikana bila rushwa hadi kuihalalisha kwa kuibatiza jina la TAKRIMA. Nani asiyejua kuwa mwenye nacho ndiye kiongozi ndani ya chama tawala???????

Ni aibu kubwa kwa level ya chama tawala tena cha siku nyingi kuitisha press kwa ajili ya kumsema mtu mmoja tena ambaye hana madaraka yeyote ya kiutawala katika nchi hiii.

Zamani press kama hii ikiitishwa na chama tawala nchi inasimama inasubiri kusikia habari nzito zinazohusu mstakabali wa maendeleo na mwelekeo wa nchi na si malumbano dhidi ya mtu mmoja. Kama chama tawala kinapashwa kuwa na mengi ya kuadress kwa wananchi kuliko mahusiano yake na Lowasa.
 
Asante sana kwa taarifa ila Ole Sendeka hakuna kitu. Hili ndio tamko gani? !.

Rais Magufuli amepiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa nchi nzima kwa hoja kuwa uchaguzi umekwisha na sasa ni wakati wa kuchapa kazi.

Chama cha Mapinduzi kinatuletea Press Conference na kuzungumzia madudu ya mchakato wa uchaguzi wa Chadema! . Wa nazungumzia watu badala ya kuzungumzia utekelezaji wa ilani.

Nape, January, Mwingulu kisaidieni Chama, kitaaibika!, Ole Sendeka kwenye kuongea ni majanga tuu. Bado najiuliza, hivi Comred Kinana aliupitisha utumbo huu Sendeka aliyoongea? .

Pasco
 
Aghriiiiiii! Nini hii! Ccm tena wanahubiri demokrssia? Ni.lini walishakuwa na demokrasia hadi wawe na moral authority ya kuwaelekeza wengine? Hivi ni lini ccm walisharuhusu demokrssia katika kumteua mgombea wao? Ni.lini ccm wameruhudu demokradsia katika kumchagua mwenyekiti?
Hivi ccm of all the political parties ndicho cha kufundisha watu demokrasia? Aghriiii give me a break!
 
Ajira lini?.......

Nini hatima ya wadogo zetu chuoni??.....

Wapi pesa ya maafa kagera?......

Hayo ndiyo mlitakiwa kuyabainisha kwenye taarifa yenu kwa kuishauri serikali !!......

Lowassa anausika vipi kwenye kukwapua pesa za maafa Bukoba,kuzuia Ajira, au kuwanyima wanafunzi pesa za kwenda masomoni?..........
 
Kweli upinzani wa sasa ni wa vioja kwelikweli...!!!
Mbona hamjibu hoja kuwa Lowassa hakufuata mifumo ya democracia alipohamia chadema ? Kama alivyoeleza ole sendeka kama ni kweli ama sio kweli ?
Mbona hamkanushi kuwa baadhi yenu mmepata ubunge wa viti maalumu kwa kutoa papuchi..!!
Mnashangaa kuwa ole Sendeka anamjibu Lowassa mlitaka amjibu nani ? Kwani alietoa tathmini ya uongozi wa Magufuri kwenye vyombo vya habari ni nani.?
Mmepoteza dira sana Chadema kama kuna mtu anawasapoti atakuwa ama mwizi, au fisadi,ama mchora michongo tu wa town ! Au anavuta bangi kama baadhi ya wabunge wenu,! Au atakuwa akili yake mbovu .
 
Alichosema leo Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka mbele ya vyombo vya habari.

Watanzania wamecomment hivi..

1. Hivi mbona mnakuwa mnamhofia sana Mzee Edward Ngoyai Lowassa? Hii mnaonesha kwamba hamjiamini na hata huo urais mnajidhihirisha kwamba mlijipa kwa nguvu tu na sio kuchaguliwa na wananchi.

Maana tangu uchaguzi umepita ni mwaka sasa lakini mnaacha kukaa na kutafuta mbinu za kitu gani kifanyike ili uchumi wetu ukue nyi ndio kwanza mnafanya ujinga na kuongea vitu na kuwafaaminisha wananchi kwamba Mzee Lowassa hafai kuongoza nchi kwa kuogopa uchaguzi ukifanyika mwaka 2020 mtaanguka tu kwa madudu yanayofanyika.

Tayari mmeshaangukia pua sio kwenye elimu, afya na hata huduma za kijamii ni sifuri mnatapatapa tu. Mumeshamaliza zenu kaeni pembeni nchi imewashinda.

2.Na kama hamwogopi Lowassa ruhusuni mikutano ndio mtajua anakubalika au hakubaliki. Lowassa mmoja kutwa mnamuwaza ivo inaonyesha ni jinsi gani anawatesa. Fanyeni kazi kwa vitendo wakati wa maneno umeisha, tukutane 2020 ndio mtamtambua Mhe Lowassa ni nani..

3. Ukimsikiliza kwa makini mzee huyu, hawezi kutofautisha dini na siasa, huo ni mfano wa kijinga. Pia kwenye katiba ya chama chochote hazisemi eti ukifikisha umri wa miaka kadhaa kama mwanachama ndio unaweza kugombea. Ila tukumbuke, hebu CCM mjiulize tangu mnamsema Lowassa yeye hajawajibu kitu anaendelea kufanya harakati zake na nijuavyo mimi ukiona mjinga anaongea ujinga huwezi kumjibu kama wewe una busara. Hivyo waaache tu hakuna kipya toka huko.

4. Tatizo CCM mnaimba kama malaika mnacheza kama mashetani. Kama mnaamini katiba ya CHADEMA ilikiukwa kwanini hamkumwekea pingamizi ili mpite kiuwepesi au ndiyo mnazidi kutuaminisha kuwa Lowassa bado anawatesa kimawazo. Na nyie wenyewe mlisema mna imani na Lowassa tena bila kulazimishwa. Ifike mahali CCM mpunguze unafki watu tunataka tuone selikali ya viwanda.

5. Yaani mbona hamna kazi za kufanya CCM mnazidi kumpa kiki mzee Lowassa kwanini? Kwanini hawaishi mdomoni? Hofu inawatanda kwa kuwa mnajua if akichukua nchi atafanya more than expected.

Mungu mbariki Lowassa, uzidi kumpa afya njema.

6. Kuna watu kila wakilala na kuamka wanamuwaza Edward Ngoyai Lowassa tu! bila SHAKA ule uchaguzi uliopita BAADA ya huyu jamaa kuangusha kule kwenye jimbo lake kutokana na nguvu ya EDO ashakuwa ADDICTED anahitaji MAOMBI.

7. Lowassa mmoja anawanyima usingizi pamoja na dola kuwa chini yenu... Katika wakati ambao chama chakavu kimepata msemaji wa ovyo basi ni miaka hii!! Wananchi wamemnyima kura jimboni leo hii ni msemaji wa chama taifa.

8. Badala ya kuongelea mambo ya chama chake yeye ndio kwanza anaingia upande wa pili, kwanza mmewazulumu watu wa Kagera misaada iliyotoka hadi leo hakuna kinachoendelea wezi wakubwa nyinyi CCM.

9. Hao Eddo na maalif seif wangekuwa wanaleta fyoko sijui ingekuaje? Maana wako kimya wanafanya mambo yao kidiplomasia lkn kila siku CCM midomo juu. Kweli diplomasia inashnda mizinga na Vifaru.

10. Twaweza hamkosea, kati ya wale na huyu mzee yupo. Nyumba yako imekushinda unazungumzia ya Jirani. Hii ni janja yakuzulumu UMEYA Kinondoni na Ubungo.

Hapa kazi tu!

CY8rLPCWsAAvvK0.jpg
 
Kuweni tu wakweli, Hii Chadema inawasumbua sana kwa sababu hamjui kufanya siasa za kisayansi. Kura nyingi inazopata chadema zinatoka kwenye chama chenu. Vyama vya upinzani vinapata nguvu kwa sababu ya udhaifu mkubwa sana wa chama chenu, but you seem to not learn the lesson. Matokeo ya hali hii ndiyo haya tunayoyaona sasa, mnapaniki na mmeanza kufanya siasa za ghiriba na matumizi ya nguvu kubwa dhidi ya vyama pinzani. Je mmefanya utafiti wa kutosha kwamba mbinu hizi zitawavusha?? Kwa sababu zisipofanikiwa, ule msemo wa "usiyempenda kaja" hautaepukika siku si nyingi... just watch that space.
 
Ikiwa imepita siku mbili tangu aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kueleza tathimni ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli, ambapo alidai kuwa, katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi huo, kumekuwepo na ukiukwaji wa misingi ya demokrasia na utumishi wa umma kuwa kaa la moto.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimevunja ukimya na kumjibu kwa kusema kuwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita alikuwa wa kwanza kukiuka misingi ya demokrasia. Kuhusu utumishi wa umma kuwa kaa la moto, imemjibu kuwa wanao lalamika hivyo ni wale wanaotumiwa kuficha mafisadi na wakwepa kodi.

Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka amewaambia waandishi wa habari kuwa Lowassa hastahili kuituhumu serikali ya Rais Magufuli kuwa inakiuka misingi ya demokrasia.

“Demokrasia ya kweli lazima ianze ndani ya chama, ni demokrasia ipi iliyotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea kuvigharamia kwa kuamua kumteua mgombea mtunguo ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania?,” amehoji.

Ole Sendeka ameongeza kuwa “Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kulidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia.”

Amesema CCM haigopeshwi na matamko ya Lowassa anayotoa katika vyombo vya habari kwa kuwa havitaiathiri na kwamba imemamua kumjibu kwa madai kuwa anapotosha umma kwa kueleza mambo yasiyo na ukweli.

Ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutochukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko.

“Wanasayansi wa masuala ya siasa waiangalie demokrasia ya CHADEMA na UKAWA inavyofanya kazi maana ni kihoja, watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge viti maalumu. Kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA,” amesema.

Pia Sendeka amemtaka kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo kutoichukia serikali ya Rais Magufuli kwa kuwa inatekeleza yale aliyokuwa anayapigania.

“Chuki ya Zitto ya kuendelea kunyooshea kidole serikali ya CCM haina tija, sababu inatekeleza yote aliyokuwa akiyapigania,” amesema.

Katika hatua nyingine, Sendeka amedai kuwa CCM haijashiriki kukihujumu chama cha Wananchi (CUF) kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa kuwa kinawachonganisha viongozi wa chama hicho ili kigawanyike.

“Hatuna haja ya kuhangaika na CUF na wapanga siasa za uongozi CHADEMA, hatujashiriki kukivuruga na hatuna muda huo,” amesema.

=======

Ndugu wanahabari,

Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taairifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zinazolenga kukejeri, kudhihaki, kukatisha tama, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Seikali zake katika kuleta maendeleo kwa Watanzania

Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti mawili ya nje ambazo hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha na kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania

Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na kuichafua taswira ya nchi yetu.

Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua kujivua uzalendo na kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi yetu kwa maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia kujua nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni watanzania. Je ni tama ya madaraka tu au mengine?. Hakuna anayepinga ukosoaji bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema

Ndugu wanahabari,

Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita tathimini ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa octoba 25,2015

Katika taairifa yake, alidai kuwa alileta msisimko mpya katika siasa za Tanzania, kwamba ameshirikiana na wenzake kuionyesha nchi yetu maana ya demokrasia na kukosoa juhudi za serikali na wateule wa Rais.

Demokrasia kimsingi ni dhana inayohusisha ushiriki na kuheshimu mawazo ya wengi katika kufikia uamuzi. Ikiwa maana halisi ni hii, tunajiuliza ni ipi demokrasia aliyoionyesha Lowassa ambayo leo anajisifu kuwa nayo?

- Tulishuhudia akiwa mgombea Urais wa chama ambacho hakijui, hakushiriki kukijenga wala kutoa mchango wowote unaompa hadhi ya kupeperusha bendela huku katiba na kanuni ya chama hicho ikivunjwa. Kidemokrasia anayepewa fursa ya kupeperusha bendela ya chama chochote makini duniani ni kiongozi au mwanachama aliyethibitika kwa imani na matendo, kuzielewa, kuzitekeleza, kuzitetea falsafa, itikadi na malengo ya msingi ya chamahicho. Mgombea ni taswira halisi na alama muhimu inayoakisi dhamira ya chama husika machoni kwa wananchi.

- Demokrasia ya kweli lazima ianzie ndani ya chama, ni demokrasia ipi inayotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea, kuvigharamia na walivyovitumikia kwa kuamua kumteua mgombea “MTUNGUO” (ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania). Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kilidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia

- CHADEMA watuambia njia iliyotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu. Ni demokrasia gani inayotoa fursa kwa baadhi tu ya viongozi kuteua wabunge ambao wanakiwakilisha chama chote. Ambapo kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA walikosa watu wanaowafahamu na kuamua kuwateua wanawake maswahiba wao ndani ya CCM. Msingi wa kawaida wa kupata wabunge wa viti maalumu ukiacha kura za maoni, kigezo kingine muhimu ni mchango wa mgombea / mwanachamahuyo katika kukijenga na kukitumikia chama chake. Yaliyotokea kwa CHADEMA kwenye wabunge wake wa viti maalumu ni mapya kwenye ulimwengu wa demokrasia. Inahitaji wataalamu wa sayansi ya siasa kufanya utafiti wa aina hii mpya ya demokrasia

Tulidhani baada ya mwaka mmoja kupita, wenzetu hawa wangelikuwa wamejifanyia tathimini, kujikosoa, kujisahihisha, na hata kufanya uungwana wa kuwaomba radhi wanachama wao kwa uvunjifu mkubwa wa misingi ya demokrasia, katiba na kanuni za vyama vyao

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutokuchukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko, yasiwe ni nyimbo za kuburudisha au kutoa matumaini hewaq kwa wanachama na wananchi. Kanuni mojawapo ya demokrasia ndani ya vyama ni lazima ionekane katika muundo wake na katika utekelezaji wa muundo huo

Umefika wakati vyama vya siasa vinapaswa kujifunza kuuza sera ili kujenga na sio kusubiri matukio kwa ajili ya kupata huruma ya wananchi. Tunasubiri kushuhudia na kusikia demokrasia demokrasia itakavyoendeshwa katika uchaguzi wa ndani wa vyama hivyo ambapo kuna taarifa mmoja wa vigogo amefanikiwa kupata kiasi cha dola milioni 15 zitakazomsaidia kupanga safu yake ya uongozi

Katika kutimiza mpango huo, tayari yapo mawasiliano ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi wakitoka Zanzibar na sehemu zingine za nchi kuja Dar es Salaaam, na imeonekana dhahiri mazungumzo yao kutowashirikisha viongozi wenzao waandamizi kwani yanalenga kafanikisha mpango huo.

Mheshimiwa Rais Dk John Pombe Magufuli, ameendelea kufanya juhudi kubwa katika kujenga nchi kwa kuimarisha utendaji na nidhamu ya utumishi serikalini, kukusanya mapato na kusimamia matumizi sahihi ya fedha, kupambana na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na kusimamia haki, usawa na wajibu kwa raia. Mwenzetu anayaona haya kuwa ni kuufanya utumishi wa umma kaa la moto.

Juhudi hizi na nyinginezo ikiwemo ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, afya na kununua vitanda vya wazazi, kutoa elimu burekuanzia shule ya msingi mpaka sekondari na nyinginezo hazipaswi kukatishwa tama kwa maslahi ya wachache ni vyema kuziunga mkono kwa maslahi ya taifa letu

Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Rais Dk. Magufuli madarakani, CCM inawaomba wananchi kuendelea kummunga mkono katika dhamira yake safi yakuwaondolea kero, kuboresha huduma za jamii na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na;-

CHRISTOPHER OLE SENDEKA

MJUMBE WA NEC NA MSEMAJI WA CCM

28/10/2016

Olesendeka kumbuka ccm ndio chama kinachoongoza dola, sasa unapokuja kujibu mipasho kwenye maswala yanayogusa taifa huo ni utoto. Hakuna mwananchi atakaye kuelewa kwa majibu ya kitoto..hivi umesahau kwamba wananchi wa Kagera wanamaumivu makali ya majanga yaliyowapata ya tetemeko na njaa inayoendelea? Misaada itagawika lini?
CCM walishajua kinga yao ni polisi na vyombo vya dola basi hawana wasisi laiti kungekuwa uchaguzi huru Tanzania mngeshanyooka
 
Chama badala ya kuwa mama au mlezi wa serikali, kinageuka kuwa mtoto.
Hatua hii ni mbaya sana, maana km wapinzani wameshindwa kututetea basi hata chama tawala si msaada tena kuonya mwanae akivurundaa.

Tuishi kwa sababu hatuna namna. Matatizo ni jadi yetu.
 
Yan huyu Msemaji wa CCM kazi yake ni kujibu tu kila lisemwalo na Lowassa, sawa na yule msemaji wa Ikulu ambaye kazi yake ni kutangaza tu teuzi, tenguzi na kufutwa kwa sherehe mbalimbali za kitaifa, zaidi ya hapo hawana la kusema wala kutenda.

Halaf ikiwa Lowassa hakijui CHADEMA, Magufuli anakijua FISIEMU? Mwenyekiti ambaye hajui Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Magazeti ya Chama huteuliwa na kikao anachokiongoza yeye mwenyewe si jipu tu hilo?
 
Back
Top Bottom