Tambwe Hizza amshambulia Mwanakijiji

.

Muosha uoshwa.

Mwana kijiji amekuwa akiwashambulia sana wana jf kwa majina tofauti humu ndani.

wacha na yeye achafuliwe.

Naona mkuu umevamia kiwanja ambacho si chako umekurupuka humjui MJJ ni nani loser wa ze utamu utawajua tu.
 
kama tunahitaji nchi hizi za kiafrika ziendelee lazma tujifunze kumteua/kumchagua/kumpendekeza kiongozi asie na masihara, mwenye kuonyesha uwezo si kwa kuongea au kuongelewa bali kwa kutenda na kuonekana.mkali na mtamani maendeleo. sasa leo mwanakijiji anaongelea mambo muhimu na dhabiti kwa nchi duh kashaanza kushambuliwa.tatizo tunaangalia maslahi binafsi na si ya nchi,umaarufu binafsi,kuwa tajiri binafsi.kwa njia hii nani atakuja kuwazia ya nchi?nasema tena inabidi tupate mtu mwenye kauditekta ka maendeleo na kuona mbele 100yrs, si kila mtu akikaa anawazia 2010,that is poor vision, na inaonyesha ni namna gani nchi ilivyodororeshwa kimawaZo na hawa viongozi wetu.too much concerned na uchaguzi kuliko maendeleo.tufike mahali tuwe na deep analyisis za viongozi tunaowachagua, na kumwomba mola atupe hekima na busara za kutambua kiongozi bora na si bora kiongozi.
 
Dubya yuko fiti, Obama naye yuko fiti si unaona mara kwa mara anashoot hoops na marines. Bongo ukiwa na mtumbo kama fuko la rambo si ndio unaonekana una mapesa.

Kwa hili mtatukana wengi hata hapa JF maana wengi matumbo kama fuko la rambo kwi kwi kwi!!!

Suala la afya tunazembea kama tunavyozembea suala la elimu. Watu wanafikiri kujaza matumbo ndio afya kama ambavyo wanafikiri kuwa na Ph.D hata kama ni fake ndio elimu.
 
huyo tamwe hizza ni nani mpaka amponde M.M. Mwanakijiji, mtu mwenye degree ya taifa la tz, nimesema hivi kwamaana anaijua nchi yake in out na maduidud yote wanayofanya hao vilaza wa tz (viongozi wetu), ni nadhan huyo hiza sijui tambwe ni kibaraka tu wa Chama Cha Mafisadi Tanzania (CCMT) na mwenzake Makamba, kisa kusifia tu mafisadi bila hata kujali masilahi ya walalahoiwatanzania na wala hana uchungu na nchi yetu. mi hawa waCCMT wananiuzi sana.
 
Dogo Tundu;

Tulia tukwambie wakubwa wako. Mambo sikuzote hayapo kama unavyoyaona!

Asante

FP
 
Mwanakijiji, Hana haja ya kujibu. Tambwe sio size yake. Akatafute mengine ya kusema.
 
Babu niko fit. 205lbs ambayo kwa kilo ni kama kilo 90 na kitu kama sijakosea. Ila ni all muscle. Hakuna minyama ya uzembe hapa.

hahahah!nakuaminia.mimi nina kama 94 sasa.ni mtu wa gym sana na kikapu pia nimecheza sana wakati nasoma o-level!i'm a super tall,na misuli kibao.anyways pamoja sana kaka!mimi nimeshapasha na awadh-tamimo bondia huyu,pamoja na japhet kaseba kwenye centre fulani hapa dar!

tutaongea basi!............
__________________

Nyani/Geoff mnatisha. I wont pick quarrel with you. Join na zile martial arts tunazoziona DSTv hapa. Mnaweza mkawa champs.
 
Last edited:
Huyu Tambwe Hiza ni moja ya maadui wakubwa wa ustawi wa nchi, Nilipata kusikiliza sehemu ya mahojiano hayo kwa sehemu kubwa yeye alikuwa anatetea mafisadi na akina Hosea na Mwanyika. Ukusikiliza mahojiano hayo inaonesha dhahiri kuna watu wanamtumia ili alopoke upuuzi, mtu mwenye akili timamu hata kama ni mwapropaganda wa chama kwa hali ya ufisadi ulivyo na mafisadi wanajulikana wazi hawezi kusimama kwenye public na kusema kuwa hawa mafisadi wanatuhumiwa ni wa kufikirika.
Mwanakijiji hongera na kaza buti cheche zako zinawachoma akina Tambwe na timu yake ya mafisadi. Ombi mwaga waraka wa cheche kujua mbinu wanazotumia kuiba kura ili mwakani tutakakuwa tunachagua tujue jinsi ya kuwadhibiti ili wasichue ushindi kwa wizi kama Biharamulo, Busanda etc.
 
Nothing new to me! Tambwe anaweza kuwa member hapa JF na akawa mmoja wapo ya wale ambao kila akisemacho MKJJ wanakipinga....so kumpatia attention ya namna hii is like kumpa attention NL or NN or Mkandara etc wanapompinga MKJJ of which we normally do not do!

Huko kutapatapa kwa Tambwe kwanza kunaimarket sana JF na pia kunamwongezea umaarufu MKJJ na kijarida cha cheche kwani wale walimsikia Tambwe akimponda MKJJ na Cheche na hawajawahi msikia before wataanza kufuatilia makala zake pamoja na Cheche zake of which will be helping him zaidi kuliko kumdestroy!

Thanks Tambwe kwa kufanya free marketing ya Cheche!....next time toeni nakala nyingi....wasomaji watakuwa wameongezeka!
 
MJJ usijibu kitu, toa nakala za kutosha kwenye kijarida cha cheche kiwachome na wale wakatoliki watoe waraka wao uwachome kama msumari.
 
Tambwe ni looser mmoja hivi nyie mnamuona kakamilika kiakili huyo?
 
Tambwe ni looser mmoja hivi nyie mnamuona kakamilika kiakili huyo?

Wala hastahili kujadiliwa hapa jamvini kwa kuwa hana credibility yoyote.Nafikiri ni bora sana kujadiliana mambo yatakayoboresha Taifa letu kuliko kutumia muda wetu kumjadili mtu asiye na mwelekeo.Mimi hata akiongea kwenye TBC1 kwa hali ilivyo sasa hakuna mtu asuyejua ufisadi ni nini na mafisadi ni kina nani.Hili ni suala la muda tuu na wataumbuka kweli kweli.
 
.

Muosha uoshwa.

Mwana kijiji amekuwa akiwashambulia sana wana jf kwa majina tofauti humu ndani.

wacha na yeye achafuliwe.


Mwanakijiji hawezi kuchafuliwa na mtu pumbavu kama Tambwe hiza. Huyu ni mropokaji na ajue kuwa vyeti vyake feki alivyo navyo atashitakiwa tu muda ukifika.

Kitu cha ajabu ni kuona CCM wanakumbatia watu wenye vyeti vya kughushi, je nchi wataiendeleza kwa elimu feki???
 
Nilidhani Hizza angekuwa memba humu JF. Invisible mwalike bwana! Ninyi hamna kawaida ya kualika watu hadi tujilete wenyewe? Mwanakijiji angalia kama unaweza kumpa nafasi ya kumhoji kama ulivyofanya kwa wanasiasa wengine. Muwahi kabla hajaondoka CCM!!
 
Nakuomba Mzee Mwanakijiji usikate tamaa kwa haya maneno ya kijinga ya hiza. Mjinga hiza anasema jarida la cheche za fikra lina hatarisha amani, je, watu waliokufa kutokana na sumu kule North Mara, hiyo ni kujenga amani??

Je, mapigano ya tarime ambayo ni mradi wa CCM ndo kujenga amani?
Je, watu walidhulumiwa kule buzwagi na wengine wazikwa wakiwa hai kahama ndo kujenga amni?

Mwanakijiji, wewe endelea kutusaidia kufichua uozo na kuuweka hadharani kwa njia hii tutafika. Nasi hapa bongo tunajitahidi lakini hatuna pa kupumlia make mafisadi wamejaaevery corner.
 
Siasa kweli mchezo mchafu. Mnakumbuka alipokuwa CUF na madongo aliyokuwa anipiga CCM, leo yote yamekuwa lulu kwake, na kweli amebadilika hata taswira, AMENONA.
 
Siasa kweli mchezo mchafu. Mnakumbuka alipokuwa CUF na madongo aliyokuwa anipiga CCM, leo yote yamekuwa lulu kwake, na kweli amebadilika hata taswira, AMENONA.
.......pia mimi nadhani NJAA NI MBAYA SANA,INAUZA UHURU WA TAMBWE HIZZA
 
Back
Top Bottom