Tambwe Hiza ndani ya 'Tuongee Asubuhi' StarTv kipindi kinaendelea...

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wakuu,
Kipindi cha tuongee asubuhi cha StarTv kinaendelea muda huu. Mada ni Je, haiwezekani kuwa na siasa bila vurugu?

Bw. Tambwe Hiza ni miongoni mwa wazungumzaji.
 
Tambwe Hiza: tatizo la vurugu kwenye siasa ni wanasiasa kutaka madaraka na kutoheshimu katiba na sheria za nchi. Mfano ni wa hivi karibu. Kwa mujibu wa kanuni za bunge, chadema inastahili kuunda kambi ya upinzani. Ni haki yao. Lakini vyama vingine vya upinzani vimeanza kuleta chokochoko.
 
Tambwe: kwanza ni ugeni wa demokrasia. Wakati wa utoto wetu haikuwa rahisi kumsema rais. Lakini leo watu wameruhusiwa kumkosoa rais. Tatizo ni watu kutumia uhuru kupita kiasi. Kwa hiyo demokrasia ni suala geni.

Wengine wakisikia kiongozi fulani wa ccm kasema jambo fulani hadharani basi inakuwa ni tatizo lakini ndiyo uhuru huo. Ndiyo demokrasia hiyo. Jambo la msingi ni kuheshimu taratibu za kuongea au kutoa maoni.

Nasikia watu wanasema mitaani kwamba ccm inakataliwa sana. Hiyo siyo kweli. Mbona kwenye uchanguzi ccm ina viti vingi vya wawakilishi.
 
Anaitwa Lisasi Mwaulanga. Anasema yeye ni mwanachama wa ccm, balozi wa amani. Anawalaumu viongozi waandamizi wa ccm wanaopinga hadharani mpango wa shule za kata wakati nao walishiriki kwenye vikao vya chama vilivyotoa maamuzi ya mpango hu.
 
Sorry anaitwa Risasi siyo Lisasi.

anasema amefurahishwa na sera ya chadema ya kuuza mfuko wa saruji kwa sh. 5,000 anasema kama ndivyo basi trei moja ya mayai itakuwa sh. 250. Anasema hiyo sera imemfurahisha sana kiasi cha kuwasiliana na waziri wa viwanda na biashara kuona namna ya kumkaribisha Dr. Slaa na timu yake ya wachumi waeleze namna ya kuitekeleza kwa manufaa ya umma.
 
Tambwe hiza: ndani ya ccm kuna uvumilivu wa hali ya juu. Ni chama chenye uzoefu mkubwa. Kwa hiyo wakati wa majadiliano wa suala lolote reference inakuwa uwanja mpana. Tofauti na vyama vipya vya upinzani ambavyo vimejaa vijana zaidi.
 
Huku Jimbo la Segerea hakuna umeme siku ya pili, hatuwezi kuangalia tivii!! Sijui ni hili litapeli Makongoro liliochakachua kura zetu au ni Dowans rafiki yake!!
 
Wakuu kwa upande wa StarTV Kituo cha Ilemela yupo Mpiganaji mmoja sijui anaitwa nani na cheo chake ni kipi. Kama kawaida ya wapiganaji, yupo ndani ya kombati.
 
Mtangazaji amemuuliza Tambwe Hiza kwamba anaionaje ccm ya leo ikilinganishwa na ccm ya zamani. Hiza anasema ccm inapoekekea kusherehekea miaka 34 inajivunia uimara wake na imani kubwa kutoka kwa watanzania. Anasema chama kimeendelea kuwa imara wakati wote na bado kina nafasi nzuri ya kuendelea kuiongoza nchi yetu.
 
Yule mkaribishwa kwenye tuongee asubuhi ya star tv kituo cha Dar [Bahati mbaya sikumnasa jina] kanihamasisha kuhoji vigezo vinavyotumika kuchagua Mabalozi wa amani. Mambo yalonitatiza ni haya:-

Jamaa kaponda Sera ya CHADEMA akisema cement haiwezi kuuzwa TSHS 5000/- kwa madai kuwa kama cement itauzwa 5000 then tray ya mayai itauzwa shilingi 250/=. kwa nini hasemi sababu za serikali kuzuia uagizaji wa cement kama hilo punguzo haliwezekani? Kwa sasa serikali imekataa katakata kuagiza cement nje ya nchi si kwamba inataka kulinda viwanda vya ndani, la hasha!! hao viongozi wanavuna kutoka viwanda vya cement kama wanavyovuna TANESCO kwa hivyo wanachelea mavuno yao kushuka. Kuthibitisha hilo angalia CEMENT ikiagizwa nje ya nchi. Inapolipiwa kodi na logistics zote, mfuko waweza kuuzwa TSH 7000 hadi 9000. Je, ikitengenezwa ndani itashindikana vipi kuuzwa 5000/-?

Kama ni kulinda viwanda kwanini viwanda vya nguo vyenye kuajili watu wengi kwa mpigo havikulindwa kwa mtindo huo? vivyo hivyo viwanda vya Baiskeli na vingine vingi!

Pia jamaa akasema wapinzani waache kutumia muda mwingi kupinga chama tawala badala yake wahamasishe watanzania kufanya utalii wa ndani. Tena kaenda mbali zaidi kwa kudhihaki wanywa bia kwamba, kwa nini unywe heineken ya TSH 3000 badala ya kwenda serengeti kutoa 1500 ukaangalia simba na swala!! Huyu jamaa nahisi kalewa hizo sifa za UBALOZI WA AMANI hadi anashindwa kuchambua mambo. HEBU tujiulize kwa nini Mtanzania akatoe 1500/- ambayo itatumiwa na mtoto wa Kigogo au kimada wake kwenda Ulaya kununua CHUPI au PEDI ambayo pia inapatikana mlimani City?

WANA JF WHY
? Angekuwa ni balozi wa kweli, angekemea ubadhilifu wa kutisha unaofanywa na hao CCM waliojihalalishia nchi hii kuwa mali yao binafsi!! NINASHAWISHIKA KUSEMA JAMAA ANAFANYA UBALOZI WA PROPAGANDA ZA UPOTOSHAJI!!
 
Back
Top Bottom