Tambwe hiza ndani ya radio one live

segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,789
729
Anaongelea mambo ya matusi na kupakana matope kwenye kampeni,msikilizeni ana hoja za msingi
 
Namsikia hapa anasema awali Richmond walikuwa the "lowest bidder". Sina hakika kama anajua tofauti ya hilo neno na the "lowest evaluated bidder"
 
Tambwe:
Badala ya kuleta megawati 220 alileta 100. (eti anaona hapa haoni ufisadi)
mbona anachanganya mada?
hana hoja huyu mpuuzi
 
Antony Komu- CDM
  • Anamshangaa Tambwe hasa akimkumbuka alikotoka
  • Anajua watanzania wanakumbuka aliyosema huko nyuma
  • Udhaifu wa CCM lazima uzungumzwe ili kuwe na justification
  • CDM ni chama cha mlengo wa kati
  • Vyama vya upinzani vina sera tofauti kabisa na CCM (Sera ya majimbo) sababu zipo
 
Kiherehere kilimfanya afe kifo cha kisiasa huyo. Hata wengine tulishamsahau kwenye midani ya siasa za tz. Simtofautishi na mtu mmoja aliyegombea ubunge miaka fulani aliyekuwa anaitwa KIHIYO.
 
Anasema vyama vya upinzani havina sera,kila siku ni mambo yale yale ya kuongelea richmond.Na anasema richmond haikuwa ni tatizo kwa sababu serikali ilichukua kampuni ambayo ilikuwa na alternative nzuri ya kutengeneza umeme wa bei rahsi yaani sh 9 badala ya sh 40 kwa kampuni nyingine.Kwa hiyo yeye haoni ufisadi kwenye suala la richmondi
 
Anthony Temu:
Tambwe alikuwepo NCCR, akaenda CUF, na leo yupo CCM. kitendo cha kusema chadema hawana sera namshangaa sana.
Ili kuwe na justification lazima tutumie udhaifu wa ccm.
CHADEMA ni chama chenye mrengo wa kati.
CHADEMA tuna sera tofauti na ccm
Ili nchi hii iweze kufikia malengo sisi tunasema tuwe na sera za majimbo
Kwa mfano kule Arumeru tulizungumzia sera ya maji, ccm wameshindwa, lakini sisi tumechukua jimbo leo hii kuna watu wanatumia maji, tumechimba visima kule watu wanatumia maji
Tumezungumzia sera ya Ardhi Arumeru, ndiyo maana tumepewa kura na wananchi
Ili kukabiliana na mazingira haya, watu wanatakiwa waandaliwe kielimu ili waweze kushindana katika ulimwengu wa utandawazi
 
ANTHONY KOMU:
Nashindwa kumwelewa Tambwe sijui anataka CHADEMA wawe na sera za namna gani
 
Aongelee ya mawaziri wanaotakiwa kung'oka leo na aachane na mavi ya kale. Au ndio kusema pale alikolalia ndio kaamkia leo. Nape alimpaki huyu kutokana na kila issue sisiem kuipropagate. Leo hii wamemkumbuka kwenye kabati alilofungiwa? Ama kweli gamba limebanwa mbavu. Wanaonaje kama wakimpa cheo cha Millya?
.
 
tambwe hiza kwangu me namchukulia kama limbukeni wa siasa asiye na namna nyingne ya kupata kipato isipokuwa kuburuza mtumbo wake kwa magamba ili apate kuishi,that y nimeandika jina lake kwa herufi ndogo kuweka mcctizo kuwa ni mtu mdogo sana kma ccmizi kwenye siasa za bongo na makamanda wa CDM,Atajisalimisha tu.
 
Namsikia hapa anasema awali Richmond walikuwa the "lowest bidder". Sina hakika kama anajua tofauti ya hilo neno na the "lowest evaluated bidder"

Ni kweli watu wengi na hata wasomi hawaelewi tofauti kati ya term hizo mbili kwenye mchakato wa ununuzi kwa njia ya zabuni.
 
Kwanza bosi gani kawalika Radio one,atakuwa ni kilaza kama tambwe mwenyewe.whom'z tambwe nowdayz,kafa kisiasa.
 
(b) Njia kuu za uchumi ni chini ya wakulima na wafanya
kazi:

Namna ya pekee ya kujenga na kudumisha ujamaa ni
kuthibitisha kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu
zinatawaliwa na kumilikiwa na Wakulima na Wafanyakazi

wenyewe kwa kutumia vyombo vya Serikali yao na Vyama
vyao vya Ushirika. Pia ni lazima kuthibitisha kuwa Chama
kinachotawala ni Chama cha wakulima na wafanyakazi.


Njia kuu za Uchumi ni: kama vile ardhi, misitu, madini,
maji, mafuta na nguvu za umeme; njia za habari, njia za
usafirishaji; mabenki, na bima; biashara na nchi za kigeni na
biashara za jumla; viwanda vya chuma, mashini, silaha, magari,
simenti, mboleo; nguo, na kiwanda cho chote kikubwa
ambacho kinategemewa na sehemu kubwa ya watu katika
kupata riziki zao au kinachotegemewa na viwanda vingine;
mashamba makubwa na hasa yale yanayotoa mazao ya lazima
katika viwanda vikubwa. SEHEMU YA PILI

SIASA YA UJAMAA

(a) Hakuna Unyonyaji:

Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi: haina
ubepari wala ukabaila
. Haina tabaka mbii za watu: tabaka ya
chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya
watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa
kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi
hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi
aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali
hayapitani mno.

Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi
kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao
ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao,
kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya
kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe.

Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanya kazi, lakini sin
chi ya Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na
vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza
ikapanuka na kuenea.


Haya ni mambo ya CCM?


Falsafa ya Chama

  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

Haya ni ya CDM

Yapi yanatekelezeka? Nani asiye na sera?
 
Tambwe Hiza msambaa hana adabu yule, samahani wasambaa kwani naongelea baadhi ya wasambaa wanaorubuniwa na chama tawala wakasahau maslahi ya wasambaa wenzao.
Tukimuuliza huyo Tambwe pale kwao Mazinde CCM imefanya nini toka miaka hiooooo na mpaka leo hii hata maji bomba yenye uhakika hawana wakati Mazinde iko bondeni na maji yote kutoka milima ya Usambara yanapitia Mazinde.
Mvua zikinyesha Mazinde hawana maji masafi bali kunywa matope.
Wakati wa jua wananchi wamekua kama ngamia.

Msambaa mwingine anaitwa Makamba
Ukiuliza huko anakotoka amefanya nini hatakupa jibu.
Kinachoonekana ni binti yake kununua jumba la kifahari kwa pesa za ufisadi.
Kiukweli msambaa aliyekua na akili nakujali wasambaa alikua Shekilango lakini hawa wasasa ni vibaraka wa mafisadi.

Samahani kama nimewakwaza baadhi ya wasambaa ambao sio vibaraka wa mafisadi.
 
Back
Top Bottom