Tambaza Taifa Kubwa!!

Ni kweli, A-Level Azania walikuwa vibonde. Lakini O-Level ni vizuri umekubali Tambaza walikuwa wanateswa.

Kulikuwa na pointi saba Azania kila mwaka, Abdil Rashid, Frank Minja, Omary Mtiga... just being objective

kweli wewe wa jana....
 
Yani mmekaa mnaanza kusifia ule ugangwe wa kipuuzi wa kufanya fujo? Duh!! kweli waafrika ndivyo tulivyo.
 
Duh! yaani mmenikumbusha mbali sana nakumbuka generation yetu ya akina Shetani, Big Papa, Paul Rusimbi, Ramadhani Said, Taki Mussa, Fella Ramson Kuti, Joseph Lusungu, Mmasa Msuya na wengine wengi. Enzi hizo head Master alikuwa Kalumuna alikuwa na fimbo zake za mwanzi anazifungia kwenye kabati leke. Ukipigwa 1 lazima ukoowe.
 
Yani mmekaa mnaanza kusifia ule ugangwe wa kipuuzi wa kufanya fujo? Duh!! kweli waafrika ndivyo tulivyo.

wee hebu tupishe hapa! we're talkin bout stuffs done when we were teenagers...too ashamed au hukupitia hiyo stage?? kama wewe ulipokuwa form two ulikuwa na miaka 22 tayari, huo mzigo usitake kututwisha sisi. kama wewe shule yenu was a bunch of mommy's boy woosies then u can talk about that too, kama mlikuwa mnafungwa bib na kunyweshwa maziwa mkiwa form three basi wewe ongelea hilo, labda kuna wengine wapo wanaoshare experience kama hiyo. if you're too shy to recount ya stuffs on this thread, feel free to start a new one. Btw, if you don't mind, shule gani vile tena ulisoma secondary?!

Tambaza ilikuwa na best teachers na wanafunzi wake walikuwa top performers. Hili halina ubishi. Kuna mwalimu gani tena mwingine alikuwa top Dar na Bongo kwa geography ukiachilia mama Msuya? Nitajie....!! Practicle gani nyingine ya chemistry na biology Bongo ilikuwa top class ukiondoa iliyofanyika kwenye laboratories za Tambaza? (Physics sawa, hatukujaliwa sana, some of us had to go kwa mwalimu Mkichwe pale Jangwani). But as Tambaza stands, kila leo tulikuwa tunaona wanafunzi kutoka Shabaan Roberts, Aghakhan Mzizima, watoto kutoka boarding schools kila walipofunga walikuwa lazima wajiandikishe tuition pale. n.k.. wakimiminika kwenye corridors za ATC, what another encounter could better elaborate the academic performance of Tambaza??!
 
SteveD
Kuna mwalimu anaitwa Kweka, unamjua na bado yupo Tambaza?nilihudhuria twishen zake!
Halafu, bora kuliwekwa ukuta kati yenu(Tambaza) na Muhimbili primary mana mlikuwa wachokozi na uwanja wetu wa basketbal/netbal/futbal.
 
GT kasoma wapi? anasema yeye mtoto wa mjini shule zoote za town hayumo....IST miaka yoote niliosoma pale sikuwahi kuona shekhe yeyote

Mara ya kwanza niliposoma comments zake nilifikiri ni mtu wa Kinondoni Muslim, lakini kila nilipoendelea yawezakana kabisa mazee yule alisoma ile shule ya Almuntanzir pale Upanga... sijui kama spelling nimepatia. Ni shule fulani hivi wanafunzi wake walikuwa hawawezi kukatisha barabara pale UN road bila msaada kutoka kwa traffic police kutoka Salander bridge. Wanafunzi wa kike walikuwa wanavaa full cover, dizaini dizaini zile mtu unaweza kukutana nazo ukiwa Kabul.

KadaMpinzani naye nahisi alisoma shule hiyo... ngoja aje hapa a-substantiate... lol
 
SteveD
Kuna mwalimu anaitwa Kweka, unamjua na bado yupo Tambaza?nilihudhuria twishen zake!
Halafu, bora kuliwekwa ukuta kati yenu(Tambaza) na Muhimbili primary mana mlikuwa wachokozi na uwanja wetu wa basketbal/netbal/futbal.

Duuh...:) kuna mwalimu mmoja pale Muhimbile P.Sch. alikuwa mashuhuri sana kwa elimu, ni mwanaume, naomba unikumbushie jina pls...

Zile shule zilitakiwa ziwe pamoja... shared pitches and everything. Hata majengo yake yanafanana!! Wakina John Kisomo iliwabidi watumie viwanja vile Belinda... lasivyo Vijana Basketball club isingekuwa na stars kama wale enzi zile.... lol. viwanja tulitakiwa ku-share vile my dear.
 
Kama shule yenye wanafunzi iliyokuwa ikiongoza kwa wanafunzi wenye nicknames ni ile. Mimi niliingia nikapewa jina langu la utani .Kulikuwa na majina mengi kama vile mzuka, Kanaruza, Sauti ya bomba, Fuvu, Vimto, No Mbungi n.k Saambukile...Tambaza.. Ukisoma ile shule mkitembea mnakuwa kama watoto wa baba mmoja na mama mmoja ukichokoza ugomvi wanakusaidia mpaka ugomvi unaisha halafu baadae unasemwa. Hao ni Tambaza sijawahi kuona shule kama hiyo maishani mwangu na haitakaa ije irudi . Mwinyi aliifuta baada ya fujo za Azania. Ila na yeye aliweka Bifu kwa sababu nakumbuka watoto wa Tambaza waliingia Ikulu na Bango la kumponda wakati wa Mgomo wa Chuo Kikuu ambapo kulikuwa na maandamano ya wanafunzi wote wa DAR kulaani mgomo huo. Nakumbuka tuliitwa wote Ikulu tukaandikwa majina yetu kisha jumatatu tukahojiwa tena lakini iliisha kinamna. Tambaza noma!
 
Dar, kuna mwalimu mmoja pale Muhimbile P.Sch. alikuwa mashuhuri sana kwa elimu, ni mwanaume, naomba unikumbushie jina pls...

Zile shule zilitakiwa ziwe pamoja... shared pitches and everything. Hata majengo yake yanafanana!! Wakina John Kisomo iliwabidi watumie viwanja vile Belinda... lasivyo Vijana Basketball club isingekuwa na stars kama wale enzi zile.... lol. viwanja tulitakiwa ku-share vile my dear.

Yule aliitwa Mwalimu Ndossi. Kipindi hicho ilikuwa ni Muhimbili, Olyimpio, Upanga na Bunge. Shule za watoto wa vigogo hizo. Ikifika saa nane unaona Marange rover, ONE TEN DEFENDER, Land cruiser zile za Salim za Jeshi zinaenda kuchukua watoto shule sie wa Tambaza tunaua boda. By the way Mabitozi wa Upanga walikuwa hawatupendi kulikuwa na ugomvi fulani wakati wa mashindano ya DON BOSCO. Jamaa alidai kuwa demu wake kapokonywa kofia . Kipindi hicho ukivaa kofia yenye chata za RAIDERS, CHICAGO BULLS au LAKERS unaonekana bonge la mjanja na mademu wote wako. Tambaza ilikuwa na mabitozi kama akina SAIGON kipindi hicho ila siku hizi anajifanya mgumu mara baada ya kurudi toka UK. Tambaza ilitisha kwenye buku ndio usisikie. AZANIA kulikuwa kuna ticha mmoja aliitwa KAZIBURE wa PHYSICS jamaa aliifagilia sana Tambaza . KAZIBURE anasema kwamba alisoma na NELKON. Mzee alikuwa anapiga EMBASSY sio mchezo siku moja akachanganya EMBASSY na chaki class . MUNGU AMWEKE MAHALI PEMA PEPONI. Huyu mzee alikuwa na bifu na Nyerere kipindi hicho Nyerere akaamua kumdemot.
 
Dar, kuna mwalimu mmoja pale Muhimbile P.Sch. alikuwa mashuhuri sana kwa elimu, ni mwanaume, naomba unikumbushie jina pls...

Zile shule zilitakiwa ziwe pamoja... shared pitches and everything. Hata majengo yake yanafanana!! Wakina John Kisomo iliwabidi watumie viwanja vile Belinda... lasivyo Vijana Basketball club isingekuwa na stars kama wale enzi zile.... lol. viwanja tulitakiwa ku-share vile my dear.

Huyo mwalimu atakuwa Ndossy maana anajulikana kushinda walimu wengine. Ukiongelea Muhimbili P.Sch. basi lazima ugusie Mwl. Ndossy. Ndo hilo jina ulilolisahau? Maana wengine kadhaa niwakumbukao kwa majina ni Walimu(Chuwa,Ndibalema,Msengeni,Gabone,Nchimbi,Tenga)

@Shared pitches
Tatizo baada ya zile vurugu zenu ikabidi uzio uwekwe kwa usalama tu. Ila bado outsiders wengine wengi tu walikuwa wanatumia viwanja hivyo na hata baada ya Tambaza kutulia..Maana ni kweli vile viwanja ni shared.
Nice memories, lol!.
 
Kama shule yenye wanafunzi iliyokuwa ikiongoza kwa wanafunzi wenye nicknames ni ile.

heheeeeeeee umenikumbusha kawawa (njemba manyoya) na Okello (yule jamaa wa mkoa wa mara)!!!!

HIVI SI KUNA MWALIMU ALIKUWA ANITWA AU NIMECHANGANYA??? PEPEYU YUKO WAPI??

TAMBAZA---THE GREATEST
 
Sikusoma Tambaza ila bro wangu na mshkaji wangu walikuwa wakisoma pale, ama
hakika vijana walikuwa wakorofi sana.

Kuna siku nilimfuata mshkaji tukaenda kusubiri basi muhimbili na hiyo siku mvua ilikuwa
imenyesha so kulikuwa na madimbwi ya maji. tulikuwa kama wanne so wakati tunatokea
kulikuwa na abiria(wazee wazee) wakawa wananyoosha vidole kwetu huku wakilaani
vijana hawafai kabisa, basi yule mshkaji wangu akatumabia ngoja awashikishe adabu
kama masihara akatoka nduki na kujibwaga ndani ya dimbwi la maji misili ya mzigo yale
maji yakawarukia na kuwachafua wazee.

Nilicheka sana na tukatoka nduki, ama hakika TAMBAZA palikuwa na vichwa ngumu.
 
Mara ya kwanza niliposoma comments zake nilifikiri ni mtu wa Kinondoni Muslim, lakini kila nilipoendelea yawezakana kabisa mazee yule alisoma ile shule ya Almuntanzir pale Upanga... sijui kama spelling nimepatia. Ni shule fulani hivi wanafunzi wake walikuwa hawawezi kukatisha barabara pale UN road bila msaada kutoka kwa traffic police kutoka Salander bridge. Wanafunzi wa kike walikuwa wanavaa full cover, dizaini dizaini zile mtu unaweza kukutana nazo ukiwa Kabul.

KadaMpinzani naye nahisi alisoma shule hiyo... ngoja aje hapa a-substantiate... lol

Dongo hilo....
 
bibie ilikuweje ukasoma combination ngumu namna hio? PCB CBG unaonekana shori wa HKL HGK KLF hivi........

ila tambaza walikuwa machizi tu.....kujifanya magangwe gangwe usela wao ulizidi...kuna kijamaa kimoja eti alikuwa anajiita killer one......ukimuuliza kaua wangapi hata mbu hajaua.....
hahahhahahaah Yo Yo nilikuwa PCB ,unachikesha unaposema ulikuwa unatuona machizi tu, coz viceversa is true. Yo Yo weee unaonekana mtoto wa mama sana wale akina ' ze u know war am sayin? or kudo kudo this kudo that............., mtu kama wewe ukija TAMS lazima tukutimuee pale wagumu tuuu mambo ya kuimba nyimbo za RKelly na MJ hakuna pale watu wanaimba nyimbo Bob Marley , Alpha Blond , Lucky Dube na wengineo.......hahhaha najua utanimind kichizi
 
Hivi SteveD enzi zenu nazo mlikuwa mnaenda kucheza mechi mpira wa miguuu na kikapu shule ya PUGU? nimekumbuka kitu nimecheka mpaka basi ,mwana basi kuna moja ya mashindano flani hivi ilikuwa mechi kati Tams na Pugu tukaenda kuchezea kwao Pugu , tuliwafunga mpira wa kikapu na wa miguuuu eee bwanaeeee tulimwagiwa UPUPU wacha tukimbizane tukimbilie gari(Costa) tuliokuja nalo kumbe tulikuwa hatujui huko kwenye gari ndipo walipoanzia kuumwaga ,ilikuwa noma tulijikuna kama tuna ukurutu yaani wee acha tu ndo the first time naju upupu ndo nini in ma life ilikuwa noma, mie nilikuwa mmoja wa wahamasishaji tuu lakini duh.........
 
Ebwana nimemkumbuka Headmaster Mwl Kalumuna a.k.a Father Kalu. na msaidizi wake Mwaipopo. na Mwl Shija mchawi wa Chemistry.

Mi nilisoma A-Level pale.

O-Level walikuwa watukutu haswa. Mkienda mechi Tambaza wote mnajiamini kuwa hakuna wa kuwatisha.

Nakumbuka mambo ya Tambaza/Zanaki, ila wakiwaboa mnavuta ngamia toka Jangwani, mnawaumiza Azania.

Pia upinzani ktk sports hasa soccer na basketball. Don Bosco always palikuwa hapatoshi! Hapo nimemkumbuka sana Father Peter Paul!

Ile issue ya kumuua konda maeneo ya Keko baada ya mechi kule Taifa ndio iliyoifuta O'Level. As a result Serikali ikawatawanya wana-Tambaza kuwapeleka wakaendelee na O'Level yao ktk shule mbalimbali nchini. Ndio hatimaye Tambaza ikawa Full A'Level ikiwa na combinations kibao, siyo PCM na PCB pekee kama zamani.

Mambo ya Azania vs Tambaza academically, mi naona Azania walikuwa wakali zaidi O'Level, ila Tambaza nao A'Level walikuwa super.

Just reminiscing...
 
...kuna moja ya mashindano flani hivi ilikuwa mechi kati Tams na Pugu tukaenda kuchezea kwao Pugu , tuliwafunga mpira wa kikapu na wa miguuuu eee bwanaeeee tulimwagiwa UPUPU wacha tukimbizane tukimbilie gari(Costa) tuliokuja nalo ....

Tambaza ya mwaka gani hiyo mkapigwa na Pugu nyinyi wazembe nyinyi? aaaaah!

Hiyo itakuwa Tambaza ya 2000 ya kina marehemu Amina Chifupa!

Huko Pugu kulikuwa na mwalimu mmoja fisadi eti ana reputation ya kutunga mitihani ya taifa ya Physics form six ( what's his name again?), basi inabidi mwende tuition kwake, all the way from city center mnapanda vichai-maharage vya Gongo la Mboto (Tambaza Physics walimu walikuwa watupu, kama alumni mmoja alivyosema hapo juu...) Wanafunzi wa Pugu tulikuwa tunawaona wakulimaaaa, tuko ugenini halafu wanatuogopa.

What's funny ni kwamba mwalimu mtunga mitihani wa NECTA eti anafundisha practical physics ubaoni, sio lab, darasani, kwa lecture!!!!! Elimu yetu Bongo duuuuh!
 
wee hebu tupishe hapa! we're talkin bout stuffs done when we were teenagers...too ashamed au hukupitia hiyo stage?? kama wewe ulipokuwa form two ulikuwa na miaka 22 tayari, huo mzigo usitake kututwisha sisi. kama wewe shule yenu was a bunch of mommy's boy woosies then u can talk about that too, kama mlikuwa mnafungwa bib na kunyweshwa maziwa mkiwa form three basi wewe ongelea hilo, labda kuna wengine wapo wanaoshare experience kama hiyo. if you're too shy to recount ya stuffs on this thread, feel free to start a new one. Btw, if you don't mind, shule gani vile tena ulisoma secondary?!

Tambaza ilikuwa na best teachers na wanafunzi wake walikuwa top performers. Hili halina ubishi. Kuna mwalimu gani tena mwingine alikuwa top Dar na Bongo kwa geography ukiachilia mama Msuya? Nitajie....!! Practicle gani nyingine ya chemistry na biology Bongo ilikuwa top class ukiondoa iliyofanyika kwenye laboratories za Tambaza? (Physics sawa, hatukujaliwa sana, some of us had to go kwa mwalimu Mkichwe pale Jangwani). But as Tambaza stands, kila leo tulikuwa tunaona wanafunzi kutoka Shabaan Roberts, Aghakhan Mzizima, watoto kutoka boarding schools kila walipofunga walikuwa lazima wajiandikishe tuition pale. n.k.. wakimiminika kwenye corridors za ATC, what another encounter could better elaborate the academic performance of Tambaza??!

Yakhe, mbona mihasira namna hiyo eh? Well sijui lolote kuhusu Tambaza kwa kifupi sijui mengi kuhusiana na shule nyingi za mjini hapa unless nilikuwa nafuata chicks (Jangwani, Zanaki, Shaban Robert na Mzizima). Ila nakumbuka jinsi cousins wangu walivyokuwa wanaogopa kwenda shule kisa wanafunzi wa Tambaza wanatishia kuwafanyia fujo eti hao ndio viongozi wetu siku zijazo.

Mkuu wakati wewe uko 22 probably mimi nilikuwa nachezea bakora za first lady darasa la tatu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom