Tamasha tgnp

Mutekanga

Member
Aug 26, 2007
34
3
Tamasha la jinsia, lilifunguliwa jana kwenye viwanja wa TGNP. Nashangaa kimya hakuna anayetupasha juu ya TAMASHA hili. Jana nilikwenda na leo nimekwenda. Kuna mada nzuri na za kufikirisha. Bado siku zipo, hadi Ijumaa. Twendeni tujadiliane na kupanuana mawazo!
 
Si ndio hivyo unatupasha? Au ungependa atupashe nani ? Kwani wewe sio mwana JF bana?
 
Mkuu, tamasha kama hilo ni kupoteza muda asilani.Wanawake wengi walioamua kujikita katika matamasha kama hayo ya kujidai kudai haki zao wameishia kuvunja ndoa zao na kubaki wanaharakati, siwapendi haooo!
 
Mkuu umekuwa tooooooo general aaaaaaaaggggggggggrrrrrrhhhh!!!
Huwapendi wanawake wanaharakati hata kama ni wa kusaidia haki itendeke Tanzania? TGNP kama ilivyo mitandao mingine ya wanaharakati kuna wanaume kibao tena vijana, nao ndoa zao zimevunjika au zitavunjika? Kuna wanawake tena vijana kabisa na ndoa wanazo, sasa wewe unawazungumzia wote ama baadhi? Maisha ni ndoa tu mkuu?

Unajua hao usiowapenda ndio wametoka Loliondo majuzi na habari za kuwepo 'dola nyingine ndani ya dola ya Tanzania'? Au hata walivyokwenda Loliondo hupendi?
 
Back
Top Bottom