Tamasha la Umeme wa Upepo Duniani

Haya tuangalia maskini wenzetu wa maldives wanafanya nini kwenye hii ishu. Wakati sisi tunabakia kuota ndoto za alinacha za nyuklia wenzetu wanafanya kweli!

Carbon-neutral goal for Maldives
Beach in the Maldives
One-third of the Maldives' economy depends on tourism

The Maldives will become carbon-neutral within a decade by switching completely to renewable energy sources like wind and solar power, its leader has said.

Kutoka hapa:BBC NEWS | Science & Environment | Carbon-neutral goal for Maldives

Mimi niko kwa Mchungaji kwenye hili. Utaalamu si kusomea kitu kama mojawapo ya masomo unayohitaji kufaulu ili upate digrii ya kwanza. Mtaalam ni yule aliyejikita zaidi katika particular subject. Kwa hali kuwaita electrical injiniaz wote kuwa wataalamu wa nishati ni kosa. Kama vile si civil injiniaz wote ni wataalamu wa structures! Kwa hali hiyo sidhani kama tuna wataalamu wa alternative energies Tanesco. Kuna electrical injiniaz kibao lakini hii haiwafanyi kuwa wataalamu wa hizi nishati mbadala.

Amandla.
 
wataalam tunao na binafsi nilikutana nao pale Tanesco. Kishoka this is a good thread

....................................................

..............................................

On a flip side hivi unajua nani aliweka zile wind turbines kule Singida? na ni nani alifund that project?

.................................

Kuna thread nyingine humu ndani inayosuggest kuwa kuna conflict of interest because Mwakyembe is part of a company that is looking into wind power generation and him being the voice against Richmond and Dowans. Apparently this company has set up trails in Makambako and Singida.......
 
Unaweza kuwa upande wa Kishoka vyovyote utakavyo (kwanza haya si mashindano na hata kama ni mashindano sitegemei uwe on my side), point yangu ni simpo sana....tatizo si utaalamu, bali waroho wa 10% ambao wengi wao ni mangwini!!! Isitoshe, technologia ya wind power sio ngumu kama unavyotaka kutishia watu hapa...hata kama wataalamu wa Tanesco hawajui, basi vikozi vya miezi sita vinaweza kufanya tofauti kubwa mno.....

Sasa hiyo article ya Maldive nani amefanya waweze?? Na nani anafanya sisi Tanzania tushindwe?? Ukielewa hapo basi ndio mzizi wa point yangu!!! Mangwini wasikilize wataalamu, waache uroho wa 10% then kila kitu kinawezekana ktk Tanzania.

Jumatatu njema!

Tatizo ni kuwa hao unaowaita wataalamu hawasemi na sio kuwa hawasikilizwi! Lini umesikia mtaalamu amejiuzulu kwa sababu ushauri wake haukusikilizwa. Wataalamu wetu wamejiunga na wanasiasa kiasi ambacho hauwezi kuwatofautisha. Wao nao wako katika mkao wa kula kama walivyo hao uliowashikia bango! Badala ya ushauri wanasema kile ambacho wanadhani wakuu wao wangependa kusikia. Wao nao ni sehemu ya tatizo na si solution! So called wataalmu tumeji-prostitute kwa kupenda vyeo na rupia!

Wind energy ni sehemu tu ya possible solution. Tunahitaji watu watakaoweza kuangalia picha yote na kutushauri wapi tuelekee. Utaalamu tunaohitaji si wa kutengeneza mapanga boi au majiko ya kutumia jua bali ni ule wa kuanganisha yote haya kuwa policy! Tunahitaji visionaries zaidi ya mafundi mchundo.

Tofauti na unavyopenda kufikiri, sina ugomvi na wewe. Kwenye ishu hii, arguments za Mchungaji zimenivutia kuliko za kwako. Ni hilo tuu

Amandla........
 
Last edited:
Tatizo ni kuwa hao unaowaita wataalamu hawasemi na sio kuwa hawasikilizwi! Lini umesikia mtaalamu amejiuzulu kwa sababu ushauri wake haukusikilizwa. Wataalamu wetu wamejiunga na wanasiasa kiasi ambacho hauwezi kuwatofautisha. Wao nao wako katika mkao wa kula kama walivyo hao uliowashikia bango! Badala ya ushauri wanasema kile ambacho wanadhani wakuu wao wangependa kusikia. Wao nao ni sehemu ya tatizo na si solution! So called wataalmu tumeji-prostitute kwa kupenda vyeo na rupia!

Wind energy ni sehemu tu ya possible solution. Tunahitaji watu watakaoweza kuangalia picha yote na kuangalia wapi tuelekee. Utaalamu tunahitaji si wa kutengeneza mapanga boi au majiko ya kutumia jua bali ni ule wa kuanganisha yote haya kuwa policy! Tunahitaji visionaries zaidi ya mafundi mchundo.

Tofauti na unavyopenda kufikiri, sina ugomvi na wewe. Kwenye ishu hii, arguments za Mchungaji zimenivutia kuliko za kwako. Ni hilo tuu

Amandla........

Acheni siasa.maneno mingi mingi Mainjinia+Magwini,then what?? mnatishiana shule.au ecosystem(natural balance) haipandi nini??
 
Una amini kabisa kwamba Tanesco hawana habari za mikutano hii....!!? Kama ma-injinia wa kibongo hawatakuwepo huko Jo'burg na/au Chi-town basi ni kwasababu "mangwini" wamekataa kutoa funds za wao kusafiri na kujikimu wakti wakiwa ktk mikutano hii na si vinginevyo!!

Wasomi wa Tanzania ndio maana wanasemwa wana matatizo hivi kuhudhuria kozi lazima mwajiri akupe funds? Ukiona ni nzuri kuongeza upeo wako wa kujua mambo kwa nini usijigharimie mwenyewe ukaenda kwa savings zako.Wala si lazima uende na ndege waweza enda Afrika kusini kwa basi ukalala guest house ya bei poa uswahilini ukila kwa mama ntilie lakini ukarudi na elimu kubwa ya kukusaidia.

Nakutana na wakenya na wanigeria kwenye kozi nyingi za kimataifa wakiwa wanajilipia wenyewe.Wao hu-save pesa za personal development through international courses .wasomi wa Tanzania wanaudhi sana kila kitu mwajiri mwajiri ndio maana wengi wana knowledge outdated shauri ya kusubiri mwajiri na hata wakistaafu wanakuwa rejects ambazo hazihitajiki katika jamii maana hawako current kielimu.

Ukiona kozi nzuri chukua hata likizo ondoka nenda wacha blabla za mwajiri.
 
...tatizo la umeme ni policy zetu za kikoloni ambazo zinaleta rushwa zote za Dowans na IPTL na ndio sumu yote ya matatizo yote (nawashauri mziangalie labda mnaweza kuelewa nina maana gani),Wind na Gas tumebarikiwa na vinaweza kutupatia energy 100% kwa miaka mingi sana ijayo bila matatizo kama tukiweka policy zetu vizuri na tukapata serious leadership inayoelewa umuhimu wa investment na good policy katika energy....sijui kama mnajua Artumas(kampuni ya umeme wa gas kule mtwara) wamezalisha umeme na wanashindwa kuuza huku tukiambiwa hakuna umeme na waliomba kuzalisha 300MW lakini wakanyimwa kwa sababu stupi-d serikali/Tanesco hawawezi kununua huo umeme/hawahitaji huku wakituletea migawo,tanzania hatuna shida ya umeme ni bogus leadership tuu inatufanya tuishi kwa tabu za umeme expensive na migawo isiyokwisha amabyo effect yake kila kitu bei juu na maisha magumu kwa sababu gharama za uzalishaji ni kubwa sana,Gas tuliyonayo,Wind,hydro ni zaidi tunavyohitaji kumaliza shida ya umeme lakini serikali vilaza ya CCM ndio poison ya umaskini wetu.
 
Back
Top Bottom