Tamaduni zetu zinasemaje, matendo haya ni sahihi kufanyika TZ?

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52







Mimi katika mtazamo wangu tamaduni kama hizi, watoto wa watu kuwaweka nusu uchi, wanaoangalia ni wananume siuafiki, sielewi ni ushamba umenizidi au ni ulimbukeni. nisaidieni
 
Mkuu kaitaba, kweli sasa hivi kuvaa nusu uchi si sahihi lkn utamaduni wetu ni kukaa km hivyo. wamasai si unawaona wanavyovyaa? huo ndo utamaduni wetu sasa kwa taarifa yako. Umewaona wale wasandawe? ule ndo utamaduni wa mwafrika mkuu. Nina picha ambazo wajerumani walipiga enzi hizo Moshi huko wakati wanaingia TZ kuna mama na watoto wawili wa kike palipofichwa ni kiunoni tuu lkn matiti yote yako nje yaani asilimia 95 ni uchi wa mnyama. hatukuwa na NGUO, bali magome ya miti tu. Na ndio maana kwenye festival zote zinazohusu utamaduni utaona mwafrika anavaa nguo za kiasili takribani asilimia tisini inakuwa yuko nusu uchi. Uliona picha za sherehe ya Jacob Zuma? alivaa kitamaduni na harusi ilikuwa ya kitamaduni na ule ndo UTAMADUNI wa mwafrika- ni kiuno ndo kilikuwa kimefunikwa lkn sehemu nyingine zilikuwa wazi. so huo ndo utamaduni wetu lkn sasa hivi tumestaarabika tunajisitiri na NGUO
 


Mimi katika mtazamo wangu tamaduni kama hizi, watoto wa watu kuwaweka nusu uchi, wanaoangalia ni wananume siuafiki, sielewi ni ushamba umenizidi au ni ulimbukeni. nisaidieni

Hapo kwenye RED... Understood!!

Ingine mi bado elewa
 
mwanamke daima aliubwa kumfurahisha mwanaume hivyo hapo walipo wanatimiza jukumu lao,wacha wasifu uumbaji
 
Ama kweli !!!!Kambarage aliweza kuwakantroli Watanganyika, leo wapi ?watu wanakwenda utupu kama ndio kwanza wapo katika wodi ya wazazi .
 
Labda tusadiane, utamaduni wa mtanzania ni upi hasa????? Yapo makabila ambayo ni afadhali hao mamiss walivyovaa, wenyewe ni 3/4 uchi afadhali hiyo nusu uchi. Utamaduni wetu kama waTZ ni upi katika mavazi????????????????????
 
Nadhani ile falsafa ya utandawazi ndio inayopelekea haya yote. Jamii inalazimishwa kuamini kuwa watu hawatakiwi kuishi kama kisiwa eti lazima waendane na upepo wa kidunia. Kiukweli kabisa si jambo jema kwa mfano kwa baba kumuangalia binti yake yuko mwili wazi kwa 80% eti urembo....na huu ujasiliamali nao umechangia hili tatizo pia. Watu wanatengeneza pesa kwa kuwaanika watoto wa wenzao uchi hadharani...Leo mwambie Lundenga avue shati tu akasimame kifua wazi mbele ya kadamnasi uone kama atakubali....Tunapenda ku-copy na ku-paste mno!!!
 
Loh! watoto wazuri hawa nashindwa hata nichague yupi niache yupi...hebu weka picha zaidi bana
 
Nguo tumeletewa na hao hao wazungu na wauza watu(waarabu) sisi enzi zetu ahaa twatembea tuyu bila nguo bila tatizo, sasa twataka kujifanya kujua ustaarabu wa kigeni kuliko waliotuletea ni NOMAAAAAAAAAAA
 
Tatizo liko wapi hapo na nyinyi bana aaah...mbona hamsemagi kitu kuhusu wale wasichana wa Mfalme Mswati....
 
kwa kweli utamaduni wetu sijui ni kuvaa baibui,gauni,suruali au whatever,but personally napenda kuwaona mabinti wakivaa hivi hasa wakiwa warembo wa surana maumbile kama hawa,napenda wakionyesha walichopewa na muumba
 
Tatizo liko wapi hapo na nyinyi bana aaah...mbona hamsemagi kitu kuhusu wale wasichana wa Mfalme Mswati....

Jalia ni ndugu yako wa kike baba moja mama moja anakupitia kama hivyo nusu uchi mbele uso wako ukiwa na marafiki zako au peke yako(wati wili goingi baki ini yowa maindi?)
 
ndo maana yakaitwa mashindano ya urembo....urembo sio sura tu ni muhimu pia kuonyesha maeneo flan flan ili watazamaji washuhudie yalivyorembeka.Kama vile miguu,mapaja,tumbo,eneo la nyonga maumbile kwa ujumla.Kama yataendelea kuitwa mashindano ya urembo yes ni sahihi kufanya hivyo.Hayo si mashindano ya kuuenzi utamaduni wetu
 
Loh! watoto wazuri hawa nashindwa hata nichague yupi niache yupi...hebu weka picha zaidi bana

NGABU....!Hebu weka dhana kuwa huyo ni binti yako wa kumzaa mwenyewe,ambaye ametoroka na kwenda kushiriki hayo mashindano..pasipo wewe kujua kuwa ni bintiyo....ONA MATE YA UCHU WA MAUNGO YA BINTI YAKO YANAVYOKUTOKA....!siku za nyuma nilifurahi sana pale wazazi wa binti mmoja wa KIISLAMU walipokataa binti yao kuwa kati ya wanawake wanaowavutia wanaaume kingono....!
 
Hapa kinachotafutwa ni pesa tu, ndio maana kuna muigizaji mmoja alisema kama atapewa pesa anaweza kujifungua mbele ya camera akirekodiwa live.
 
Kama ndio mila zetu,
mbona wanaoangalia wamevaa vizuri? na je
ni kwa nini wote wasiwe kama hawa watoto?, na
haya mashindano yana faida gani zaidi ya kuhamashisha hisia za ngono?,
hivi yakifutiliwa mbali tutapata hasara gani?
 
Back
Top Bottom