Tamaa ya Madaraka iliyovuka mipaka anayoiongelea Kikwete ni ipi?

Wana JF,

Jana Mkulu alipokuwa anaongea na sisi aliibua tahadhari kwa wananchi wa Igunga kutotumiwa na Wanasiasa kufanikisha maslahi binafsi na tamaa ya madaraka iliyovuka mipaka. Nimekuwa najiuliza, hao ni wanasiasa gani? Je, alikuwa akiwasema Magamba au Magwanda? Na kwamba, mipaka ya tamaa ya madaraka ni ipi ili yeye apime tamaa iliyovuka mipaka? Je, mipaka ni zile juhudu za chama kung'ang'ania madaraka hata kwa gilba, wizi na kuchakachua?

Mfa maji haachi kutapatapa...watasema kauli za kujaa debe lakini chamoto ni kesho....
 
Sure kesho ndiyo mwisho wa kelele zote. Kesho mida kama hii mambo yalishakuwa mambo. Ngoja tusubiri
 
Onyo la nini takeurabu?
magwanda wakishindwa kwenye uchaguzi huwa wanatamani kutumia nguvu ya umma ili kubadilisha matokeo hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani; sasa mkuu wa kaya anawatahadharisha msithubutu kufanya vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani, kwani mtajuta kuzaliwa!!!
 
Nimekuelewa mkuu. Ngoja tusubiri haya masaa machache yamebaki.

magwanda wakishindwa kwenye uchaguzi huwa wanatamani kutumia nguvu ya umma ili kubadilisha matokeo hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani; sasa mkuu wa kaya anawatahadharisha msithubutu kufanya vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani, kwani mtajuta kuzaliwa!!!
 
Anaongelea wanasiasa wahuni kama wa cdm ambao wapo tayari kuingia ikulu hata kwa kumwaga damu kama walivyoleta mungiki igunga!

Wahuni ni magamba wanaotuibia rasilimali zetu.Wanaiba kura na kutishia wa2 wasiseme.Maandamano yako pale pale kama uchakachuaji utafanyika
 
Nafasi inayogombewa Igunga ni moja tu na mshindi atakuwa mmoja, haiingii akilini Mkuu wa kaya anaposema tamaa ya madaraka ana maana ya wanaogombea nafasi ya ubunge igunga ndio wenye tamaa ya madaraka au vipi?
 
katika sifa nadra alizonazo jk ambayo hata wanaomkosoa walikuwa wakiikubali ni uvumilivu na kuonekana muungwana. sijui imekuwaje sasa ameanza kukosa sifa hizo na pengine wanaomshauri wanampeleka kubaya. katika hotuba yake ya mwsho wa mwez anawaita wapinzan wake wanye tamaa ya madaraka. hii si kaul inayotarajiwa kwa kiongoz kama yeye. alikuwa anatarajia nn ulipotangazwa uchaguz igunga. au alitaka vyama vinine visishrik ndiyo aone kwamba hawana tamaa ya madaraka

Mmeshindwa kumuelewa au mmeamua kupotosha kwa makusudi. Jamaa ametoa tahadhari ya jumla kwa wale wote wenye tabia za namna hiyo. Kama Magwanda wana sifa hiyo basi waache.
 
Wanasiasa kwasababu ya kupewa vipaza sauti mara kwa mara, mara nyingine wanaongea bila kupima uzito wala ujumbe wa maneno yao.
 
Wana JF,

Jana Mkulu alipokuwa anaongea na sisi aliibua tahadhari kwa wananchi wa Igunga kutotumiwa na Wanasiasa kufanikisha maslahi binafsi na tamaa ya madaraka iliyovuka mipaka. Nimekuwa najiuliza, hao ni wanasiasa gani? Je, alikuwa akiwasema Magamba au Magwanda? Na kwamba, mipaka ya tamaa ya madaraka ni ipi ili yeye apime tamaa iliyovuka mipaka? Je, mipaka ni zile juhudu za chama kung'ang'ania madaraka hata kwa gilba, wizi na kuchakachua?

Ni ile ya kutumia mpaka helikopta kadhaa na magari kedekede kutafuta kura wakati wakizama watu baharini hakuna hata helikopta moja inayopatikana kwa wakati.
 
Back
Top Bottom