Wimbo wa kutengeza ajira hasa kwa vijana umekuwa wa muda mrefu sana sasa.Hata hivyo hatujasikia mafanikio yoyote yaliyo patikana ya kutia moyo.Tamko la sasa kwamba serikali imepatia wanachi wake ajira millioni moja ni za kutiliwa mashaka sana, hasa ukizingatia historia mbaya ya serikali yetu ya kutojali wananchi wake.
Ni miaka takribani minne sasa tangu Kikwete aingie madarakani lakini haionekani kwamba serikali ina nia ya dhati ya kuwapatia wanachi wake ajira.Kwanza mimi binafsi najiuliza mara nyingi, hivi serikali inaposema itatengeneza ajira, ina maana gani hasa.Kwanza ina uwezo gani wa kufanya hivyo.Kwa sababu sehemu ambayo serikali ingeweza kutengeneza ajira ni katika taasisi za uma, na hata huko ufisadi unafanya kazi hiyo kuwa ngumu sana.
Kusema kweli serikali haiajiri siku hizi kabisa, na ukiona inafanya hivyo ujue upo msukumo wa kisiasa!Mbaya zaidi ni kwamba serikali imezusha mtindo wa kuajiri kwa contract waastahafu siku hizi, kana kwamba hakuna vijana wenye sifa za kuajiriwa.Hivi kwa mtindo huu tutafika kweli.Na hawa nao ukomo wao wa kufanya kazi ukifika itakuwaje?
Inasikitisha kwamba hata serikali inapoajiri vijana, maslahi yanakuwa duni mno kiasi kwamba vijana wanaoajiriwa wanaamua kujiondokea kutafuta kazi kwenye vyombo binafsi.Sasa serikali inaposema kwamba ime create employment opportunities millioni moja,ime create wapi.Ni bora wakawa wazi wakatuambia sisi wanachi ili tujue sehemu ambazo ajiri hizo zimepatikana.Vinginevyo tutaaamini kwamba takwimu serikali ilizotoa ni za kughushi.
Napenda niseme jambo moja la msingi,kwamba uchaguzi haupo mbali sana ,ni mwaka ujao tu.Sasa rhetoric hizi zote ni za kujaribu kuwa hadaa watanzania ili waamini kwamba serikali yao inawajali.Kama ingewajali ingeanza na kutokomeza ufisadi,achilia mbali vifo vinavyotokana na sumu kule North Mara ambako wanachi wanakufa na serikali haijali kabisa.
Ni vema kwa hiyo tukawa makini sana, vinginevyo hawa jamaa wataendelea kutuingiza mkenge.Mungu ibariki Tanzania.