Elections 2010 TAKUKURU yamkamata Magreth Sitta Tabora; Aachiwa kwa dhamana

.

Jamani,
Hapo ndipo mnapotuchanganya sasa.
Taarifa inasema amekamatwa akitaka kutoa rushwa.Sasa kelele zote hizo za nini?.Si kuna mahakama na atakwenda kujitetea huko?Ushabiki gani huu wa kutotumia akili.

... wewe ungekuwa unatumia zako yaloandikwa juu yasingekuchanganya. Mahakama ipi? Zile theatre kunakochezwa maigizo na WASANII waloshika dola? Changanya na zako!
 
Sasa JF inakwenda kubaya badala ya kuchangia hoja jinsi ya kumaliza tatizo linalowasumbua wananchi wa uporaji kura kwa kutumia Rushwa sisi tunaleta Ushabiki kama wa Simba na Yanga kila Mshabiki anavutia kwake hata kama mabo yako vibaya. Kwa mtindo huu sijui kama kuna muelekeo mzuri na wenya tija huko mbeleni badala yake itakuwa klabu ya mashabiki wa kushabikia watu fulani.
 
Hii kitu iko pre-planned kwa baadhi ya watu ndani ya CCM wanaooneka ni tishio na hawatakiwi..
Sidhani kama ni bahati eti wamemkamata aki-taka kutoa rushwa..
Hivi kutoa T-shirt kulikofanywa na waziri mmoja anaegombea humuhumo Tabora sio rushwa..????
 
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Mama Sita amabaye ni waziri wa Wanawake Jinsia na watoto amekamatawa na kuhojiwa na TAKUKURU kwa kukutwa na simu nyingi amabazo zonashukiwa kwenda kutumika ktkt uchaguzi wa wabunge viti maalum-Tabora

Maoni binafsi:
-Pongezi TAKUKURU.. Ujasiri huo muendeleze muwakamate na watua rushwa Papa wa CCM
-CCM acheni TAKUKURU wafanye kazi yao, msitafute njia kumsafisha mtuhumiwa na ikiwezekana asishiriki kati uchaguzi huu.
 
kweli Tanzania ina matatizo makubwa, Organization zote zinafanya kazi kama ikiwa ni jambo la kisiasa tu, kuna kesi za maana sana za maMbo ya rushwa lakini hawa jamaa hawafatilii kabisa

sasa kama unataka kujua kuwa vyombo vya serikali vinafanya kazi huu ndio muda muafaka jaribuni kufuatilia nyendo za

1) TBC, DAILY NEWZ, HABARI LEO
2) USALAMA WA TAIFA
3) POLICE
4) TAKUKURU
HIZI ORGAN HAZINA KABISA HABARI NA MAENDELEO YA NCHI HII ZAIDI YA MAMBO YA KISIASA TU
 
Mama Sita? Tena saa nane usiku ? inamaana 6 mwenyewe alikuwa hajui mkewe yuko wapi mida hiyo.?duh kweli kikulacho ki nguoni mwako aiseeeeeeeee
 
Huyu mama kakutwa na Nokia Saba
Milioni moja kwenye pochi
Bahasha 154 sijui kama zilikuwa zinahusika na utoaji wa Rushwa
 
Ushahidi hautoshi kuthibitisha hilo, wangesubiri waone akizigawa, labda watumie ushahidi wa mazingira, na uthibitishwe,otherwise wanataka kumharibia jina.
 
Waziri Sitta amekamatwa kwa tuhuma ya kutaka kutoa rushwa na TAKUKURU mkoani Tabora. Sitta amekamatwa na fedha zaidi ya millioni moja na bahasha za kaki 140 na simu za mkononi aina ya Nokia. Sitta ameachiwa kwa dhamana.

Habari zaidi nikizipata

TBC imetangaza kwenye taarifa yao ya habari kuwa mke wa Spika Mama Magreth Sitta amekamatwa akitoa rushwa huko Tabora. Inavyoelekea TBC wameshabikia habari hiyo na kuzungumza moja kwa moja na Kaimu mkuu wa TAKA-KURU wa mkoa huo wakimdhihaki na kumhukumu kuwa ametoa rushwa.
Mbona hawa Takukuru hawaendi igunga ambapo yule muiran anachagiliwa tu kwa mlungula????
sijui nchi inaendaje

Kama ndiyo utaratibu Takukuru walio tumia basi wame shemsha na kuharibu mazingira ya kesi yao. Hapa sisemi kama Mama Sitta ana hatia au laa ila mazingira ya ishu nzima haiwezi kusimama mahakamani.

Sawa humu mama ina wezekana kakamatwa na milioni moja. Sawa huyu mama yawezekana kakutwa na bahasha 140. Sawa ana weza akawa kakamatwa na simu kibao. Lakini umiliki wa vitu hivyo pekee siyo rushwa. Ina maana sasa kila anayetembea na kiasi kikubwa cha pesa, bahasha au simu nyingi ana mpango wa rushwa?

Kama kweli walitaka kumkamata na kumshitaki ilikuwa lazima wamkamate akiwa anajaribu kutoa rushwa. Pasipo kumkamata mtu kujaribu kutoa rushwa basi hiyo si rushwa. Kwa maana hata elfu kumi yaweza kutumika kwa rushwa lakini hauwezi kumkamata mtu kwakuwa na elfu kumi mfukoni.

Kwa hiyo kama hizi ndiyo mbinu zao basi wataendelea kupoteza hata kesi za watu ambao kweli walikuwa na mpango wa kutoa rushwa. Hawa watu hawajui mbinu za upelelezi?
 
Kwa hali hii tumekwisha kabisa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Kila kukicha CCM! CCM! CCM! Nao KANU walikuwa hivi hivi na sasa nyakati na enzi ni za nani Kenya?? "CHADEMA JUU, JUU, JUU ZAIDI". CCM PWAA, PWAAA, PWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA..........
 
... wewe ungekuwa unatumia zako yaloandikwa juu yasingekuchanganya. Mahakama ipi? Zile theatre kunakochezwa maigizo na WASANII waloshika dola? Changanya na zako!


Bongo hapatoshi sasa. Na huyu mama Sitta angekaa aachane na siasa ya nini kung'ang'ania jamani ubunge kila wakati?? hela zimeshawatosha hizo!! waondokee.

Heri yake anayo hiyo milioni ya kutoa rushwa. Watanzania wanawake wenzake hawana hata ya kujifungulia mtoto pale hospitali si angewagawia tuu kina mama wenzake wa mtaani kulikoni kutoa hiyo rushwa?? Aibu tupu
 
TBC imetangaza kwenye taarifa yao ya habari kuwa mke wa Spika Mama Magreth Sitta amekamatwa akitoa rushwa huko Tabora. Inavyoelekea TBC wameshabikia habari hiyo na kuzungumza moja kwa moja na Kaimu mkuu wa TAKA-KURU wa mkoa huo wakimdhihaki na kumhukumu kuwa ametoa rushwa.
Mbona hawa Takukuru hawaendi igunga ambapo yule muiran anachagiliwa tu kwa mlungula????
sijui nchi inaendaje
Muirani ndiye anaye ongoza TBC na vyombo vingine vyote vya habari vilivyopo chini ya TBC na hii ni hatari sana kwa nchi sijui kiongozi wetu yuko wapi jamani,ruwanda vyombo vya habari ndivyo vilivyo chochea mauwaji,ee Mungu baba mfungue Raisi wetu aone hila hizi! mungu ibariki tanzania ,
 
Itaprecedent kiasi cha pesa taslimu mtanzania anachotakiwa kuwa nacho, credit/debit cards use etc.
 
kweli Tanzania ina matatizo makubwa, Organization zote zinafanya kazi kama ikiwa ni jambo la kisiasa tu, kuna kesi za maana sana za maMbo ya rushwa lakini hawa jamaa hawafatilii kabisa

sasa kama unataka kujua kuwa vyombo vya serikali vinafanya kazi huu ndio muda muafaka jaribuni kufuatilia nyendo za

1) TBC, DAILY NEWZ, HABARI LEO
2) USALAMA WA TAIFA
3) POLICE
4) TAKUKURU
HIZI ORGAN HAZINA KABISA HABARI NA MAENDELEO YA NCHI HII ZAIDI YA MAMBO YA KISIASA TU
asante mkuu ukweli mtupu huo, lkn wajue ipo siku watoto wa paka watapofoa macho itakuwa kazi kuwazuia,
 
Wagombea wa Dar mbona hawakamatwi na wanagawa rushwa hiyo kweupeeeeeeeeee.
Mi nilikataa bia za mtangaza NIA niliwatafuta takukuru lakini jamaa anapeta tu
 
Ladies & Gentlemen,

Rushwa ni ADUI wa HAKI, mtu yeyote yule ASITOE wala ASIPOKEE RUSHWA.

Iwe ni Waziri, DC, RC, kiongozi wa dini, wafanyabiashara wakubwa na watu wa kawaida wanatakiwa wakamatwe mara moja bila upendeleo na kufikishwa mahakamani kama kuna ushahidi wa ushiriki wao kwenye vitendo vya rushwa.
Kipaumbele kwa sasa ni kupambana na rushwa hasa kwenye uchaguzi kwa kuwa watakaochaguliwa ndiwo watakaoongoza vita hiyo kwenye idara na taasisi za serikali.
Waacheni PCCB wafanye kazi zao, watahukumiwa baada ya kuona matokeo.
WanaJF tuache ushabiki linapojadiliwa jambo la msingi kwa jamii yetu!
 
Hivi watanzania wataamka lini ili waone true colour ya CCM, rushwa ndo utamaduni wao, na hao wanaoingia kwa kutoa rushwa watahitaji kurudisha pesa zao ,sasa unategemea nini kwa chama ambacho viongozi wake wanapatikana kwa rushwa? wataweza kweli kufikiria kuleta maendeleo kwa mtanzania wa kawaida? jibu ni NO, mimi nawaomba watanzania tuamke, tuachane na CCM kwani hawana political committment ya kuwasaidia watanzania, haya wanayoita maendeleo ni sehemu kidogo sana ya kile walichotakiwa kudeliver.SAA YA UKOMBOZI NI SASA.
 
Hata Sitta, aibu gani hii!!!

.... UKISTAAJABU HII, NGOJA TAKUKURU WAKAMATE WANAOTOA RUSHWA YA NGONO. Wakuteuliwa waliambiwa wakagombee hukoo. Kura za maoni zilitanguliwa na kampeni za chini chini kutafuta endorsements. Chupi zimekuwa nje nje. TAKUKURU mpo?
 
Back
Top Bottom