Watakamatwa wengi na kampeni hizi!...
Mkuu hii issue ya TAKUKURU kukamata wagombea wa CCM mwisho ni tarehe 31 mwezi huu. Baada ya hapo hutosikia mgombea yeyote wa CCM anakamatwa na TAKUKURU kwa kutoa rushwa kwa wapiga kura, kununua shahada au kulisha watu wali. Kwani kwa kufanya hivyo kutakuwa ni kukosesha CCM jimbo. Tegemea wapinzani wengi kukamatwa na TAKUKURU wakati wa kampeni hasa maeneo CCM inapokuwa hoi bin taaban. Believe me haya ni maandalizi ya kuukandamiza upinzani wakati wa kampeni za kuelekea october. MARK THIS POST!!!!
Kwa nini TAKUKURU wanafanya hivi?
1. Kuudanganya ulimwengu kuwa CCM inapiga vita rushwa.
2. Majungu yanayoendelea miongoni mwa wana - CCM wenyewe kwa wenyewe
3. Part of revenge ya Hosea baada ya kumshikia bango, Huwezi kumkamata mtu akiwa na keshi au bahasha halafu useme alikuwa anataka. Unatakiwa kumkamata wakati anatoa rushwa. Kama bahasha zake na hela ni zake halali kuna kosa gani?
Unajua nilisoma jama eti wamemkamata mkuu wa wilaya ya kasulu betty Machangu akiwa chumbani hotelini, swala la kujiuliza ni kwamba kuna kosa gani mtu kukodi chumba hotelini na kukaa na wapambe wake wawili?. Yaani TAKUKURU ni big mchemko na inaonesha wazi kuwa wameshindwa mbinu za kikachelo matokeo yake wanatumia mbinu za kivamizi sasa. Tushangilie haya yanatokea sasa kwa CCM wenyewe kwa wenyewe lakini tujiandae kulia sana pale tutakapoona wagombea wenye nguvu wa upinzani wapoondolewa uwanjani - Kumbuka ya Shitambala
Wakati wa kuwakemea TAKUKURU ni huu. Baadae watasema mbona wana CCM walipokuwa wakikamatwa mlikuwa kimya?