TAKUKURU yakamata wana-CCM Arumeru Mashariki

BigMan

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,096
135
Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa{TAKUKURU} mkoani Arusha imewakamata watu wanne wanaodaiwa kwa ni wafuasi wa Chama Cha mapinduzi,CCM kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa wajumbe wa mkutano wa jimbo la Arumeru

Mashariki
Chama hicho kinarudia upigaji wa kura kutokana na uamuzi wa kamati kuu{CC} ya CCM kwa wagombea wawwili Sioi Sumari aliyepata kura 361 na Williamu Sarakikya alifanikiwa kupata kura 259.

Watu hao ambao inadaiwa kuwa ni wafuasi wa mmoja wa wagombea ubunge wa jimbo hilo wamekamatwa akiwemo katibu wa jumuiya ya vijana ya chama cha mapinduzi wilaya ya Monduli {UVCCM}Ezekiel Mollel.

Watuhumiwa hao inadaiwa kuwa waliwekwa ndani kwanza katika kituo cha polisi cha mji mdogo wa Usa river kabla ya kupelekwa makao makuu ya taasisi hiyo yaliyopo Jijini Arusha kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha Mbengwa Kasomambuto amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao ni wanachama wa UVCCM katika wilaya za Arumeru,Mondulu na Arusha.

Aidha taarifa za uchunguzi utoka Arumeru zimebaini kwamba vijana wawili wa UVCCM Arumeru na mmoja aliyewahi kuwa kiongozi wa jumuiya hiyo jijini Arusha walifanikiwa kutimua mbio na wanasakwa na Takukuru.
 
Tutarajie mengi kipindi hiki kwani mbali na ushindani kati ya ccm na wapinzani, pia kuna CCM vs CCM monduli team.
Na hii ni trailer movie bado.
 
Lowassa in action!!! Mwaka huu atagawa sana pesa mpaka sitamwishia, lakini mambo yote ni 9, 10 cdm kuchukuwa ushindi. Tusubiri tuone!
 
Hao waliokamatwa tutegemea nin? Mi naona ni vunga tu kesi yao itaisha kimyakimya na sababu kubwa hapa ni mag.amba watawachuwa watu wao leo leo.
 
Tatizo nkwamba wananchi hawackii haya yajiriyo kilacku. Wangeshaamuaga.
 
Hao waliokamatwa tutegemea nin? Mi naona ni vunga tu kesi yao itaisha kimyakimya na sababu kubwa hapa ni mag.amba watawachuwa watu wao leo leo.

Sahihi kabisa, hakuna lolote hapo ni sasa tu ili ujumbe uende kwa wananchi kwamba jamaa alitoa rushwa na hivo wabadilike ktk kura za marudio, baada ya hapo kimyaaaaaa!Takukuru walikuwa wapi tokea uchaguzi umefanyika ndo wanakamata leo?wanatumika tu!
 
Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa{TAKUKURU} mkoani Arusha imewakamata watu wanne wanaodaiwa kwa ni wafuasi wa Chama Cha mapinduzi,CCM kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa wajumbe wa mkutano wa jimbo la Arumeru

Mashariki
Chama hicho kinarudia upigaji wa kura kutokana na uamuzi wa kamati kuu{CC} ya CCM kwa wagombea wawwili Sioi Sumari aliyepata kura 361 na Williamu Sarakikya alifanikiwa kupata kura 259.

Watu hao ambao inadaiwa kuwa ni wafuasi wa mmoja wa wagombea ubunge wa jimbo hilo wamekamatwa akiwemo katibu wa jumuiya ya vijana ya chama cha mapinduzi wilaya ya Monduli {UVCCM}Ezekiel Mollel.

Watuhumiwa hao inadaiwa kuwa waliwekwa ndani kwanza katika kituo cha polisi cha mji mdogo wa Usa river kabla ya kupelekwa makao makuu ya taasisi hiyo yaliyopo Jijini Arusha kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha Mbengwa Kasomambuto amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao ni wanachama wa UVCCM katika wilaya za Arumeru,Mondulu na Arusha.

Aidha taarifa za uchunguzi utoka Arumeru zimebaini kwamba vijana wawili wa UVCCM Arumeru na mmoja aliyewahi kuwa kiongozi wa jumuiya hiyo jijini Arusha walifanikiwa kutimua mbio na wanasakwa na Takukuru.

Hiyo ndo janja pekee ya ccm ambayo wananchi wamekwisha itambua kwani sasa wanaichukua hiyo rushwa na kura hawawapigii
 
wakuu,

Nilishasema CCM kwa sasa Mungu amewafitinisha ndio maana hawaelewani wao kwa wao, wanawekeana sumu, wanatishiana maisha,wabunge wao wanatishia kumpigia rais wao kura ya kutokuwa na imani naye,yaani ni kama wanajenga mnara wa babeli, hawawezi kubaki salama.
Kumbuka salama yetu lazima CCM ianguke na dalili zenyewe ndio hizi, kajimbo kamoja kanawasumbua hivi.
Na ubunge wataukosa. CDM wanachukua kama Joshua ameoa maana wakati ule hakupata kwa sababu kimila alikuwa hana boma.
 
hamna lolote hapo wanapoteza muda hao TAKUKURU kwanza ni wanafiki wakubwa cku zote walikua wapi kuwakamata, hiyo ni vita ya makundi dhidi ya EL lkn hawamuezi akiona anaelemewa anamuita mwanae RA aje ampe tough, alf utaonma jk anasalimu amli huyo ndo ngoyai bwana
 
wakuu,

Nilishasema CCM kwa sasa Mungu amewafitinisha ndio maana hawaelewani wao kwa wao, wanawekeana sumu, wanatishiana maisha,wabunge wao wanatishia kumpigia rais wao kura ya kutokuwa na imani naye,yaani ni kama wanajenga mnara wa babeli, hawawezi kubaki salama.
Kumbuka salama yetu lazima CCM ianguke na dalili zenyewe ndio hizi, kajimbo kamoja kanawasumbua hivi.
Na ubunge wataukosa. CDM wanachukua kama Joshua ameoa maana wakati ule hakupata kwa sababu kimila alikuwa hana boma.

Kumbe BOMA ni MWANAMKE...mi nilidhani nyumbani kwako unapoishi na mifugo yako!
 
Jimbo li wazi kwa ccm hata wakilisimamisha jiwe litashinda!

Nyoooooooooooooooooo times million.CDM hata wakiweka a piece of dust wataikamerun CCM,Hhata ww usiwabeep proCDM watakukamerun fasta baada ya kukutwangia
 
Arumeru imewakalia vibaya awamu hii.
Game ipo kati ya Edward Lowassa vs CCM
 
Back
Top Bottom