Takukuru watawachunguza mawaziri watuhumiwa! Walikuwa wapi hadi mambo yanafika hapa?

Source Mwananchi

Boniface Meena
SAKATA la ufisadi ulioanikwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), limeingia sura mpya baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuanza kuwachunguza watendaji wote waliohusika, wakiwamo mawaziri.

Hatua hiyo ya Takukuru imekuja wakati tayari Kamati Kuu (CC) ya CCM imebariki uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kulisuka upya Baraza la Mawaziri kama hatua mojawapo katika kutekeleza maazimio ya Bunge kutaka mawaziri wanane na watendaji waliotajwa katika ripoti ya CAG wawajibishwe.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alisema jana kuwa pamoja na hatua ya Rais ya kufanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri, taasisi hiyo imeanza uchunguzi wake dhidi ya wahusika.

Dk Hoseah alisema ofisi yake imeshaanza kushughulikia tuhuma zote za rushwa zilizotolewa na CAG na baadaye kupigiwa kelele na wabunge ili watakaobainika wafikishwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

“Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka,” alisema Dk Hoseah.

Hata hivyo, Dk Hoseah alisema asingeweza kuwataja watu wanaowachunguza kwa majina, kwa kuwa sheria (Kifungu cha 37 cha Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007, kinazuia kuzungumzia mchakato wa uchunguzi).

Lakini, mawaziri waliotajwa katika ripoti hiyo ya CAG na hivyo kushinikizwa kujiuzulu ni William Ngeleja wa Nishati na Madini na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu.

Wengine ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), George Mkuchika; Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami.

“Siwezi kusema tunamchunguza nani kwani sheria hairuhusu ila elewa tu kwamba tuko serious (makini) na tunafanyia kazi tuhuma zote na wote tutahakikisha tunawafikia,” alisema Dk Hoseah.

CAG akiri

Kwa upande wake CAG, Ludovick Utouh alikiri kuwasiliana na Takukuru kuhusu kuwachunguza wote waliotajwa katika ripoti yake.

“Kimsingi ofisi yangu inafanya kazi kwa karibu na Takukuru na barua waliyotuandikia tunaendelea kuifanyia kazi. Sheria inatueleza kwamba katika ukaguzi wetu, tunapokutana na suala lolote la rushwa tuliwasilishe Takukuru na tumekuwa tukifanya hivyo,” alisema Utouh.

Awali, wakati sakata hilo likiwa bungeni, kuliibuka malumbano ya hapa na pale miongoni mwa mawaziri na wasaidizi wao huku watendaji hao wa wizara, wakitupiana mpira kuhusu kashfa mbalimbali zinazoelekezwa kwenye ofisi zao.

Kashfa za mawaziri
Waziri Nundu na Naibu wake, Athuman Mfutakamba kwa upande mmoja na Waziri Chami na Naibu wake, Lazaro Nyalandu walianza kutupiana mpira huku kila mmoja akijisafisha kiaina.

Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu katika utetezi wake alisema Naibu wake huyo amekuwa akishinikiza Kampuni ya China Communication Construction Company (CCCC), ipewe kazi ya kujenga gati namba 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa ilimgharamia safari kadhaa kwenda nje.

Waziri Nundu pia alishangazwa na shinikizo la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu chini ya Mwenyekiti wake, Peter Serukamba kuingia na kushinikiza CCCC ipewe kazi hiyo huku akihoji kuna nini?

Hata hivyo, Mfutakamba alipoulizwa kuhusu safari zake hizo za nje kugharamiwa na CCCC na baadaye kuandika ripoti akishinikiza ipewe kazi ya kujenga gati hizo, alikiri kusafirishwa na kampuni hiyo, lakini akasema alifuata taratibu zote za kiserikali.

Nyalandu kwa upande wake, alionekana kutua mzigo wa kashfa ulioigubika wizara hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege kudaiwa kuiingizia Serikali hasara ya karibu Sh30 milioni kwa ukaguzi hewa wa magari nje ya nchi akisema alimshauri Waziri wake, Dk Chami kumsimamisha kazi mkurugenzi huyo mapema.

Lakini Dk Chami alisema hadi Bunge linamalizika mjini Dodoma, alikuwa hajaiona ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge iliyomchunguza Ekelege ambayo alisema ingemsaidia kupata tuhuma zinazomkabili mkurugenzi huyo ili kuchukua hatua.

Mkulo ambaye alikuwa waziri wa kwanza kutakiwa ajiuzulu, anatuhumiwa kuvunja Bodi ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) ili kuficha tuhuma zake ikiwemo uuzaji wa kiwanja Na.10 kwa Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL).

Mkuchika alitakiwa aachie ngazi baada ya ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) kubaini mtandao mkubwa wa wezi wa mali za umma. Ripoti hiyo ilibainisha kuwa kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2010, Sh583.2 milioni zililipwa kama mishahara hewa, kiasi ambacho kingetosha kujenga madarasa 194.

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa mwaka mmoja wa fedha linafanya ununuzi wenye thamani ya Sh300 bilioni hadi Sh600bilioni, hivyo kumtaka Waziri Ngeleja awajibike.

Katika mwaka wa fedha 2009/2010, Tanesco ililitumia Sh1.8bilioni ukilinganisha na Sh65 milioni zilizokuwa zimepangwa katika bajeti ya ukarabati wa gati mojawapo katika Kituo cha Bwawa la Mtera na kuingia mikataba isiyo na tija kwa taifa.

Waziri Maige anakabiliwa na tuhuma za kutengeneza mazingira ya rushwa katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji, ambao inadaiwa ulitawaliwa na dosari nyingi ikiwa ni pamoja na kutangaza majina ya waliopata vitalu bila kuonyesha maeneo waliyopewa.

Pia, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili ilieleza kuwa kampuni 16 zilizopewa vitalu hivyo hazikuomba na kwamba vitalu hivyo vilikuwa vya daraja la kwanza na la pili.

Mbali na tuhuma hizo, Maige pia anakabiliwa na kashfa ya kununua nyumba kwa Dola za Marekani 700,000 iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, tuhuma ambazo alizipinga na kusema kuwa nyumba hiyo ameinunua kwa Dola 410,000, (wastani wa Sh600 milioni).

Waziri Mponda ametakiwa kuwajika baada ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), ambako ukaguzi maalumu wa MSD uliofanyika kubaini kuwapo tofauti ya Sh658.9 milioni ikiwa ni pungufu ya kiasi ambacho kilipokewa na kuripotiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwenda MSD na ushahidi wa kupokewa haukutolewa.

Pia kulikuwa na kiasi cha Sh100 milioni kilichopelekwa na MSD kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kikatumiwa na MSD bila kuwapo na mchanganuo wa matumizi.

Ukaguzi maalumu ulibaini pia kuwapo kiasi cha Sh4.5 bilioni zilizotoka Hazina kwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa vya hospitali, lakini ni kiasi cha Sh4.344 bilioni tu kilichopokewa na MSD ikiacha Sh196 milioni bila kuwepo na ushahidi wa kupokewa na MSD kutoka wizarani.

Ngoja tuone kama kweli wataweza au kama kawaida yao (jibwa koko)
 
ni bora wewe Edward Hosea ukaongee na mbwa vichaa wenye vichwa vibovu kuliko kuongea na watu kama sisi. Hii yote unawatishia hao mawaziri wezi et nao wakupe mgao au utawalipua ki ukweli kweli. Usitumie jamiii ya kitanzania ili kuombea rushwa.
 
Mambo ya kisheria si ya kukurupuka. Takukuru wanajitahidi kadiri ya uwezo wao. Hata hivyo inabidi wafanye kazi zao kwa mujibu wa sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya ushahidi,sheria ya mwenendo wa mashtaka, mutual legal assistance (kwa kupata ushahidi ulio nje ya nchi) nk. Hivyo uchunguzi si kitu cha kuisha kwa siku moja kama wengi humu ambavyo wangetaka. Kuhusu hoja walikuwa wapi hadi mambo yanafika hapa ikumbukwe rushwa ni kama ngono. hufanywa kwa siri. hivyo hujulikana baada ya madhara kujitokeza.

Tanzania nchi ya usanii na kudanganyana. Nani angeamini kuwa TAKUKURU ingekuja na kamba kuwa itawachunguza mawaziri watuhumiwa wa ripoti ya CAG. Hivi Takukuru walikuwa wapi wakati wote huu au wanatafuta kuwatoa chochote kitu? Je Takukuru licha ya kupaswa kuvunjwa ina udhu wa kumchunguza mtu tena kigogo wa CCM na serikali? Nani anamdanganya nani?
Vyombo vya habari vilimnukuu mkurugenzi wa Takukuru Edward Hosea akisema, “Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka
 
Wanataka kuchunguza kitu gani wakati walishindwa mpaka cag akafanya kazi yake? Huyo osea edward ni wakufukuza hakuna kitu wanachofanya pamoja na tume yake..hakuna wala rushwa wakubwa nchi hii kama edward hosea na watu wake wote wa takukuru... Eti mtanataka kuchunguza,,,,,,,, mchunguze kitu gani mbwa nyie msio nahaya wala mshipa wa aibu? Mmeishiwa sasa mnataka serikali itoe fedha kwaajili ya upumbavu wenu mnaotaka kuufanya kiini macho hichoo........ Ingekuwa ni amri yangu hosea angekiona cha mtema kuni...pumbapuuuuuu!
 
Tanzania nayo! Huyu mbabaishaji anayeitwa Dr. Hosea sijui imemuokotea wapi. Si mpinga rushwa...ni mfadhili wa wala rushwa. Hakustahili kabisa kuiongoza PCCB
 
TAKUKURU ni Chama cha siasa kama vilivyo CCM, CDM, CUF etc, Mwenyekiti wake ni Hosea ila tu hakijasajiliwa rasmi ingawa kinaruhusiwa kufanya siasa.
 
Yani mmoja kati ya Taasisi nisizo na imani nazo ni TAKUKURU,na hasa huyo Mkurugenzi wake,yaani hatukupendi hatukupendi Hosea maana unalea tu rushwa,ni bora ujiuzulu tu,..hivi taratibu za vyuo zinasemaje?kama mmemtunukia mtu Phd,then anafanya mambo ya ajabu kwenye field yake,Chuo kinaweza kuchukua hatua gani?..kama kuna uwezekano,basi UDSM mumvue huyu Hosea hiyo Phd mliyomtunuku maana anakidhalilisha chuo na wasomi wote nchini..
 
TAKUKURU shame on you. Binafsi huwa sisomagi habari zao kwani napatwa na kichefuchefu, No value for money kwa taasisi hii.
 
mi nashauri Kiundwe chombo maalumu cha kuwachunguza Usalama wa ccm na takukuru hasa wakubwa wao kuanzia kwenye mali hadi kwenye akaunti zao sababu inaonekana wao ndio wanaongoza kwa rushwa.. na hakuna wa kuwachunguza
 
“Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka[

CAG anapeleka ripoti yake kwa Rais na bunge. Kimsingi taasisi ya Urais au bunge ndio wanaweza kupeleka taarifa hizo takukuru. inamaana makazini vitengo vya internal audit wakigundua fraud wanapeleka takukuru/polisi? Hawa vipi si ni menejementi au bodi ndio inaamua hatua za kuchukua?
 
Tanzania nchi ya usanii na kudanganyana. Nani angeamini kuwa TAKUKURU ingekuja na kamba kuwa itawachunguza mawaziri watuhumiwa wa ripoti ya CAG.

Hivi Takukuru walikuwa wapi wakati wote huu au wanatafuta kuwatoa chochote kitu? Je Takukuru licha ya kupaswa kuvunjwa ina udhu wa kumchunguza mtu tena kigogo wa CCM na serikali? Nani anamdanganya nani?

Vyombo vya habari vilimnukuu mkurugenzi wa Takukuru Edward Hosea akisema, “Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka

Yaani the main objective ya CCM ni kuiba, kuua na kuharibu.

1. Kuiba

Kila anayewekwa kwenye position yoyote cha kwanza lazima awe na uwezo wa kuiba, kama huna nia na uwezo huo usikubali position kwa kwa sababu ni kwenda kinyume na interests za wana CCM.

2. Kuua

Kwa kuiba mali za umma obviously kuna massive consequences ikiwemo kukosekana kwa huduma muhimu kama afya, maji safi, barabara nzuri, n.k Matokeo ya haya yote ni ni vifo visivyo na sababu kwa watanzania. Sasa kuua ni indirect lakini ni part of the objective.

3. Kuharibu

Viongozi wa CCM wamehusika sana na uharibifu wa morals za watanzania, mathalan mtu anapopata position anawaza namna ya kutajirika kwa njia zisizo halali. Vijana kwa wazee wanafikiria kuishi superstar lifestyle baada ya kuwa viongozi wa serikali. Hii ni hatari sana kwa mustakabali kwa taifa letu.
 
Takukuruuuu mnaamka saa hizi??kweli usingizi mtamu jamani!!!mnaonea watendaji wa vijiji na watendaji wilayani mafisadi papa yanaranda tu mijini ,kweli kazi ipo!!

Liyumba, Mramba, Yona, Mgonja, Mahalu, Jengo, Jeetu Patel, Baghdad na wengine kama hao ambao Takukuru imeshawafikisha kwa Pilato nao ni watendaji wa vijiji?
 
Ni aina nyingine ya usanii na ujinga kutoka TAKUKURU.Wanajidhalilisha tu.Tunajua wanalofanya.
Tanzania nchi ya usanii na kudanganyana. Nani angeamini kuwa TAKUKURU ingekuja na kamba kuwa itawachunguza mawaziri watuhumiwa wa ripoti ya CAG.

Hivi Takukuru walikuwa wapi wakati wote huu au wanatafuta kuwatoa chochote kitu? Je Takukuru licha ya kupaswa kuvunjwa ina udhu wa kumchunguza mtu tena kigogo wa CCM na serikali? Nani anamdanganya nani?

Vyombo vya habari vilimnukuu mkurugenzi wa Takukuru Edward Hosea akisema, “Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka
 
Tanzania nchi ya usanii na kudanganyana. Nani angeamini kuwa TAKUKURU ingekuja na kamba kuwa itawachunguza mawaziri watuhumiwa wa ripoti ya CAG.

Hivi Takukuru walikuwa wapi wakati wote huu au wanatafuta kuwatoa chochote kitu? Je Takukuru licha ya kupaswa kuvunjwa ina udhu wa kumchunguza mtu tena kigogo wa CCM na serikali? Nani anamdanganya nani?

Vyombo vya habari vilimnukuu mkurugenzi wa Takukuru Edward Hosea akisema, "Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka

:tape::A S-fire1::angel:Takukuru ni Jibwa lisilokuwa na meno,kwanza wapo pale kwa maslahi ya mafisadi,hivi nauliza msaidizi,wa waziri mwenye Nundu wakati anapewa hizo rushwa na wachina kwani Takukuru waliojaa kila mahali walikuwa wapi?
Bora Takukuru ivunjwe,wanalipwa mishahara ya bure kutoka kwenye kodi za walala hoi wa Tanzania.
:kev::love:
 
mpayukaji lazima kuna dosari katika mfumo wa utawala na uwajbikaji ndani ya serikali kwa sababu taarifa za mkaguzi mkuu zilizozua mambo bungeni Mh Raisi alikabidhiwa taarifa hizo Mwezi April 2011; inashangaza Mh Raisi na Wizara husika hazikufanya chochote juu ya taarifa zote hadi kamati za Bunge zilipoleta maoni yake Bungeni ikiwa ni mwaka mmoja tokea taarifa hizo alipokabidhiwa Mh. Raisi. Inawezekana Raisi hana mshauri kwenye masuala ya usimamizi wa fedha za umma vinginevyo angekuwa hata anawauliza mawaziri wake wamechukua hatua gani kuhusu yaliyomo ndani ya taarifa za CAG.

Wanausalama mliomo humu ndani mshaurini Mh Raisi atafute mshauri wa maswala usimamizi wa fedha za umma ili awe anamshauri "Implication" ya taarifa anazopokea tofauti na ilivyosasa ambapo yeye hufahia kupiga picha na CAG bila hatua yoyote
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom