Takukuru washindwa kuwachunguza mafisadi sasa wawageukia maaskofu?

Kama mtu katafuna sadaka atajuana na waumini wake mwenyewe.kodi yetu sio ya kufuatilia visa vya matumizi yasadaka isiyotozwa kodi.Tafadhali PCCB tunataka mshughulikie ufisadi wa kodi zetu kama kwenye fuko la EPA ila kama mmeshaandika ripoti ya huyo askofu naomba mkawasomee waumini wake huko kanisani.
 
Acheni takukuru ifanye kazi yake kama hana makosa siitajulikana? wewe unayemtetea ni kama nani? Tumesikia mangapi juu ya hao makasisi. Wamekuwa wakwepaji kodi wazuri tu, wengine wametuhumiwa kwa wizi (rejea kesi ya mzee wa upako na zingine), wengine wamehusishwa na viungo vya binadamu (rejea kesi ya mbeya), wengine na kulawiti (karibia sehemu yote ya dunia), Nashangaa wewe unayemtetea. Acha ukweli uwe hadharani. Kosa moja halihalalishi lingine. kama takukuru hawawachunguzi akina lowasa na chenge haina maana ndo exceptional ya wengine. haya tuyaseme na mengine yaendelee kama kawa.
Takukuru fanya kazi yako lakini pia usisahau akina lowasa et al.
 
Mleta mada habari yako iko nusunusu. hujui hasa huyo kasisi wa kanisa anachohojiwa. wewe unachotafuta humu ni huruma tu. Lete data zenye mashiko tuzijadili. sio huu upupu unaomwaga humu usiokuwa na mbele wala nyuma au kichwa wala miguu.
so go back and re-write it again and come with well structured thread.
 
Hao TAKUKURU inabidi wajichunguze wao kwa wao. La sivyo mambo itawageuka cku si nyingi.
 
Kama una-details za huyo Bukuku ziongeze hapa, hawa jamaa katika kura za maoni za CCM walikuwa wanakama watu kwa kuchagua wale walikuwa kundi la Lowasa na Kikwete walikuwa wanatoa hongo adharani na mchana bila woga.

PCCB ilikufa siku nyingi Mkapa aliondoka nayo, maana hii ya Hoseah ilikuwa katika kampeni za uchaguzi na kumchafua Mr. Zero kwenye magazeti ya RAI kila siku Hoseah akitangaza kuwa wanamchunguza Sumaye kumbe hakuna kitu kampeni za CCM kura za maoni baada ya hapo kapewa Ukurugenzi anakula kwa mlija kamaliza kumchunguza Sumaye hakuna tena habari yoyote tena mpaka leo.
 
kanisa linaendeshwa kwa pesa za walipakodi rejea pesa serikali imetoa kwa kanisa majuzi bilioni 60.so takukuru wana haki kisheria kufuatilia kama hao maskofu wanatumia vibaya hela hiyo lazma wawajibike

Nadhani ni kazi ya CAG na sio TAKUKURU.
lakini nijuavyo mimi hizo hela za serekali haziendi kuendesha ibada, zinaenda kuendesha huduma za jamii mahospitali na mashule!
 
kanisa linaendeshwa kwa pesa za walipakodi rejea pesa serikali imetoa kwa kanisa majuzi bilioni 60.so takukuru wana haki kisheria kufuatilia kama hao maskofu wanatumia vibaya hela hiyo lazma wawajibike


Tupe majina ya mashirika ya kidini yalio pokea hizo pesa. Wacha kutetea ufisadi.
 
Hii ni kweli tupu!Ila kinachonikera ni hii tabia ya Kina Hosea Kujivika utakatifu ghafla na kuanza kuwahukumu wenzao wakati hata yeye mwenyewe anajua kwamba watanzania wanajua jinsi alivyotoa taarifa zisizo sahihi pale alipotakiwa kuchunguza Mchakato wa zabuni za ki-Shetani za Richmind-Dowans zinazoicost Nchi mpaka sasa.Huyu naye ni shetani msaidizi na kwa hiyo kimaadili hatakiwi kuwa pale!
Ninaandika nikiwa sifungamani na upande wowote. TAKUKURU kama wamepokea taarifa kwamba mtumishi wa Bwana anamiliki kiasi cha mali ambacho hakilingani na vipato vyake vyote halali, ina jukumu,kisheria, kufanya upelelezi kwa lengo la kukusanya ushahidi (ikiwa ni pamoja na kumhoji mtuhumiwa) ili kuithibitisha au kutoithibitisha taarifa pokelewa. TAKUKURU kama wamezikalia taarifa za mafisadi kutenda vitendo vya ruswa ni kosa, lakini kosa hili haliwezi kuhalalisha kuwa taarifa ya mtumishi wa Bwana kujilimbikizia mali isifanyiwe upelelezi.
 
Lifeofmshaba
Naungana na wewe kuhusu kuwatenga hawa vibaraka wa JK - TAKUKURU na kuwanyima ushirikiano kabisa, kwani utendaji wao wa kazi hauonyeshi nia ya dhati ya kuwashughulikia MAFISADI WENYE MAGAMBA na wala Rushwa wanaojulikana, bali wanatumikia matakwa ya chama tawala kwa kuwaandama watetea haki za watanzania. Sasa kibaya zaidi, wameanza kuwaingilia MAASKOFU jambo ambalo ni hatari sana kwa mstakabali wa Taifa letu. Maana kutangaza vita dhidi ya viongozi wa dini ni kutangaza vita dhidi ya jamii nzima ya watanzania.
Tunajua kwamba MWANZA (ROCK CITY) wameikataa CCM ndio maana wanawasakama Maaskofu wa huo mji.
 
nshimba

Ninayaunga mkono maoni yako kuwa huu ni mwanzo wa mwisho wa utawala wa kifisadi. Watanzania wanazidi kufunguka ki akili kila iitwavyo leo na kuungana pamoja hatimaye tutaikomboa nchi yetu kutoka katika mikono ya watu wasio itakia mema. Kwa kweri ina udhi sana unapoona chombo kama hiki "TAKUKURU" kikitumika vibaya namna hii. Mimi sipingi wao kumwita mtu yeyote yule kwa ajili ya kumhoji ikiwa kunataarifa za kimsingi juu yake. Kitu ambacho hakiingii akilini kwangu ni vile ambavyo wamefumbia macho taarifa za wazi juu ya watuumiwa wote wa ufisadi, ikiwa ni pamoja na rushwa iliyofanywa wazi wazi wakati wa kula za maoni za wagombea wa CCM, harafu eti wanaandama maaskofu ????. Hii serikari kweri itaweza kujiepusha na raana ya anguko iliyo mbele yake?. I doubt.
 
Kuna matumizi mabovu sana ya madaraka katika nchi yetu. Nawasikitia sana hao viongozi wa Takukuru walioshindwa kazi, au wasiojua cha kufanya na wanajikuta wanawanyanyasa watumishi wa Mungu. Hawajui wanajishughulisha na mamlaka ipi. Mamlaka ya Mungu ni kubwa zaidi ya hii ya duniani. Wanatakiwa kuwa na heshima ya hali ya juu. Hatukatai, wapo wasio waaminifu, ila wangeanza kwanza na uchafu ulio ndani ya serikali, ambao umekithiri kupita muda mwingine wowote. Mungu atawaadhibu na itakuwa majuto kwao.
 
Wenyewe TAKUKURU ni washenzi hawaoni aibu wanakula bure hela za wavuja jasho. kila mwezi wanajilipa Extra duty allowance na investigation allowance sijui kwa kazi ipi? Pumbavu zenu TAKUKURU
 
Ngwendu, mbona unakuwa harsh kiasi hicho? Au na wewe uko Takukuru? Mtoa mada, sisi wengine tumemuelewa vizuri sana na tumeshaanza kumhisi huyo Askofu ni nani. Kwa taarifa yako, huyo Askofu ni muadilifu sana, na baada ya huo uchunguzi wenu usiokuwa na maana, mtagundua. Tunachokihoji hapa, is it wise kutumia nguvu yote hiyo, wakati zipo sehemu ambazo hata sisi wananchi wa kawaida, tunajua kwamba ufisadi upo, tena wa hali ya juu, kutokana na kazi nzuri ya vyombo vichache vya habari? Kwa nini tusiwahoji mafisadi, na tukafanikiwa ku recover pesa inayoshukiwa kuibwa nao? Usidhani hii mada haina maana, kwa upeo wako finyu, unamu attack mtoa mada. You are the one to zip up as you don't know the consequense of this.
 
Maaskofu wanaweza kuwa mafisadi maana nao ni binadamu tu. Swali la kujiuliza ni kuwa je, TAKUKURU ndio chombo cha kukagua mali za taasisi za dini? Taasisi za dini ni aina ya NGOs ambazo zina mifumo yake ya kudhibiti watu na mali zao. Kwa hiyo kuwaona TAKUKURU huko ni dalili ya kuwa wametumwa kwa mission maalumu ya kumkandamiza mtu!
 
kanisa linaendeshwa kwa pesa za walipakodi rejea pesa serikali imetoa kwa kanisa majuzi bilioni 60.so takukuru wana haki kisheria kufuatilia kama hao maskofu wanatumia vibaya hela hiyo lazma wawajibike
TAKUKURU wana-swap na PPRA if indeed ni wajibu wao?
 
Back
Top Bottom