Takukuru wameshindwa kazi au wamelala?

Rogate

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
215
45
Madhara ya rushwa ni makubwa zaidi pale yule anayeidai anapochelewesha huduma au kuifanya kwa kiwango cha chini ili tu kusababisha apewe rushwa. Taratibu sheria na kanuni ndio sumu ya kummaliza huyu mdudu aliyewaingia watz. Mfano halisi ni leo ambapo nilikwenda mahakama ya Ilala samora avenue ambayo kwa sasa ipo Lumumba. Imenigharimu masaa 3 kupata mhuri wa mahakama. Wakati huo huo mwengine aliyetaka mhuri kwa sababu kama zangu aliupata kwa dk 30. Mazingira ya rushwa! Sikutakiwa kulipia chochote wakati huyu mwingine alitakiwa kulipia elfu 1 ya file. Utaratibu!
 
Kweli Tanzania ni Taifa la walalamikaji! Mkubwa kwa nini usingethubutu kuchukua hatua kuwaeleza hao uliwataja au unapenda kulalamika tu.
 
Hata ma mods wa JF ukiwa na mashtaka wanakwambia wasaidie kwa kubofya "Report Abuse". Inabidi wewe uwasaide TAKUKURU kwa kuwapelekea hayo malalamiko na kisha kama hawajayafanyia kazi uje kuushtakia umma.
 
Hata ma mods wa JF ukiwa na mashtaka wanakwambia wasaidie kwa kubofya "Report Abuse". Inabidi wewe uwasaide TAKUKURU kwa kuwapelekea hayo malalamiko na kisha kama hawajayafanyia kazi uje kuushtakia umma.

nimechukua hatua mkuu, kuleta hapa nikuwaambia wa tz wenzangu yanayoendelea
 
Kweli Tanzania ni Taifa la walalamikaji! Mkubwa kwa nini usingethubutu kuchukua hatua kuwaeleza hao uliwataja au unapenda kulalamika tu.

Hatua nimechukua mkuu, tatizo muda wakufwatilia.
 
Tujadili nini kifanyike kudhibiti hili tatizo. Takukuru wanafanya kazi ya kupeleleza na kushtaki nk.... Wanamipango gani yakuondoa na kidhibiti!!? Ndani ya hayo masaa matatu niliyokaa hapo mahakamani nimeona mambo hekaheka nyingi za kuweka hela kibindoni kwenye kona mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumsikia mmoja wa makarani akimwambia MWANASHERIA" wewe kajipange uje na laki moja hiyo doc itatoka na utapata stop oder yako..." Kama mimi mwananchi wakawaida naweza kuspot hivyo vitu kwa muda mfupi inamaana kuna zaidi yanaendelea na wanaotakiwa kuzuia wamelala.

Mytake; Kwenye sekta za uma kuwe na machapisho yanayotoa muongozo na taratibu za utendaji kwenye kitengo husika.
Sheria, Taratibu na Kanunu. Ijulikane huduma flani inatolewa siku zipi katika wiki, muda gani, na muda wa kusubiri huduma bila kusahau Escalation level kama hujapata huduma bora baada ya muda uliopangwa.
 
Back
Top Bottom