Elections 2010 Takukuru wafuata wagombea kwenye mabaa usiku

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Taarifa za jana usiku zinaeleza kwamba kuna watu wanaojiita maofisa wa Takukuru walikuwa wakipitia katika mabaa na kuwabughudhi wagombea wa CCM waliokua wakijipongeza kwa kunywa bia ama kula tena na watu ambao si wana CCM na watu wa kawaida, eti wanasema wananunulia watu bia ni sawa na rushwa... katika baa ya moja maarufu Dar, kukatokea zogo ambalo lilisababisha watu kuwazomea watu hao. Imebainika baadaye kwamba huenda watu hao ni MATAPELI na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hose anatarajiwa kutoa taarifa rasmi leo......

Kwa ujumla Takukuru sasa katika baadhi ya maeneo wanatumika.
 
Ngoja tuwasubiri kwenye main campaigne. na mtikiso wa Dr. Slaa, utasukuma wengi.
 
Wananchi wote wanatakiwa kuwa wangalifu sana wakati huu wa uchaguzi. Kuna matapeli wengi sana wataibuka kwa jina la takukuru, by the way is pccb allowed by law to work at night? PCCB is now used by some top government officials to frustrate some CCM candidates who are not inline with this officials. PCCP, stop being marrionets, stand to your principles and work ethics. Kumbuka sheria ni msumeno, one day you will be the dry timber, can you imagine how the saw will work on you?
 
Watz kwa kulalamika bila sababu hawajambo! Sheria ya Gharama za Uchaguzi inakataza wagombea kutoa shukrani hata baada ya uchaguzi! Kwa hiyo mambo ya "kujipongeza" wagombea wawe waangalifu sana! Haijalishi hata kama ni usiku!
 
Waacheni wafanye kazi yao. Kama unashuku walazimu wakuonyeshe vitambulisho vyao na chukua details zao kwa ufuatiliaji zaidi. Hata kama watashindwa kuwafungulia kesi washukiwa ni wazi kuwa uhai wao utasaidia angalao watu wakaanza kuogopa kujihusisha na rushwa na sio kama hali ilivyokuwa ambako wengi walifikia kuona ni jambo la kawaida kabisa. Tumewakashifu sana walipokuwa wamesinzia sasa wameamka tunauliza kwa nini wameamka.....Jamani ukombozi gharama
 
Ngoja tuwasubiri kwenye main campaigne. na mtikiso wa Dr. Slaa, utasukuma wengi.

Tarajia wapinzani kusumbuliwa kwa sana, na CCM hataguswa mtu. Hawa ni kama mbwa wakiambiwa uma yule wanauma, wangekuwa ni Simba basi wangeonesha kuwa huru zaidi.
 
Sasa kama mgombea ni mnywaji kuwapiga round wenzio si itatafsiriwa ni rushwa?na kama upo na washkaji kwenye meza ata kama kila mtu kajilipia bado watakuletea usumbufu tu!!
 
Buchanan, kwa kiwango kikubwa nakubaliana nawe.

Ni kweli mwanzoni itakuwa vigumu sana kutekeleza hii sheria mpya inayohusu fedha na matumizi yake wakati wa uchaguzi lakini ni bora kuanza hivyo na kuiboresha na kuiwekekea kanuni zinazopaswa na hata taasisi husika kwa kadri siku zinavyokwenda.

Ni bora Takukuru, Polisi, Usalama wa Taifa, Tume ya Uchaguzi, Viongozi wakuu wa vyama ya siasa na kamati zao, viongozi wa dini na NGO's KUENDELEA KUKEMEA KABISA SUALA HILI LA HONGO NA 'TAKRIMA' WAKATI WA KAMPENI NA UCHAGUZI WENYEWE.

Mimi hata yule asemaye sijui 'nilikuwa natekeleza ahadi yangu ya zamani' lazima tuangalie hiyo timing, why now! Hakuna kitu kibaya kama kuendesha uchaguzi huku unaruhusu wenye fedha wagawe fedha au zawadi kwa wapiga kura wakati wengine hawana huo uwezo!

Tumenyanyasika kiasi cha kutosha chini ya fedha (chafu) za wenye nazo! Hao watu si tu kuwa waenguliwe katika uteuzi au kubatilisha matokeo, bali wanatakiwa kushtakiwa na nikiwa mjengoni nitapendekeza kuwa kosa hilo lisiwe na dhamana na wakibainika wafungwe si chini ya miaka 40 (kumaliza kabisa ujana au uzee wao katika siasa) na pia kufilisiwa hutwo tu mali twao ambatwo wanatutukania wananchi tusio natwo!
 
Back
Top Bottom