TAKUKURU ni kama vinyago vya kwenye majaruba - Mbunge

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,396
7,968
Mh Ndasa Mbunge wa Sumve amewapiga dongo kali sana takukuru bungeni. Eti vinyago vya kwenye majaruba ndege waharibifu wanatua wanatest wakiona hakitikisiki wanajua ni kanyaboya wanaingia shambani kula huku kinyago kipo tu. Ha ha haa, Hosea upo hapo?
 
Anacho sema Ndasa ni kweli sababu yeye na Ramadhan Khijjah + Mkulo wana scandal na Takukuru wanaifahamu lakini hawaguswi..ni upuuzi
 
na wabunge nao ni 'kwelea kwelea'. wakiingia shambani hawaachi kitu!

Mh Ndasa Mbunge wa
Sumve amewapiga dongo kali sana takukuru bungeni. Eti vinyago vya kwenye
majaruba ndege waharibifu wanatua wanatest wakiona hakitikisiki wanajua
ni kanyaboya wanaingia shambani kula huku kinyago kipo tu. Ha ha haa,
Hosea upo hapo?
 
Dr. hosea ni pasua kichwa hakuna mfano...ni kkati ya watu walioshindwa kufanya kazi hapa tz kabisa....sijui takukuru ina faida gani hapa tz.......halafu cha ajabu, prosecutors wa takukuru ni wabovu ajabu, hawajui vizuri, hawana skills na uzoefu mzuri kulinganisha lets say na wale ma prosecutor walio chini ya dpp, ma state attorneys, ....kesi zao zilizonyingi ukiweka wakili wa kujitegemea mzuri hawawezi kabisa kushindana naye, tunapoteza kesi tu....na hawataki kabisa kupata maelekezo au kuwa chini ya ma state attorney katika kesi zao wakati wa prosecution.
 
na wabunge nao ni 'kwelea kwelea'. wakiingia shambani hawaachi kitu!
Ukiona hata kwelea kwelea wanashangilia kuwa wakienda shambani wanatest vinyago wakiona havitikisiki wanakula mpunga kwa kwenda mbele ujue hauvuni kitu hapo. Wabunge ni sehemu ya wala rushwa wazuri hivyo kuikashifu takukuru wana maanisha wanachokisema. JK sijui analielewa hili maskini
 
hivi kazi ya takukuru ni nini?
TAKUKURU ni taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa boss. Nadhani pia wanafanya uchunguzi wa makosa ya rushwa, ila cha kushangaza ni aina ya uchunguzi wanaofanya maana mfano mapolisi wanachukua rushwa kweupeeee haihitaji hata uchunguzi wala upelelezi. Nahisi tatizo ni Hosea himself
 
Mh Ndasa Mbunge wa Sumve amewapiga dongo kali sana takukuru bungeni. Eti vinyago vya kwenye majaruba ndege waharibifu wanatua wanatest wakiona hakitikisiki wanajua ni kanyaboya wanaingia shambani kula huku kinyago kipo tu. Ha ha haa, Hosea upo hapo?

Yaani kati ya watu ambao wanakula pesa za Nchi bila kazi ni hawa TAKUKURU sijui kwanini Bunge lisikomae wawaondoe waachie polisi tu. Kuhakikisha kuwa wao inawezekana wakawa miongoni mwa wapokea rushwa wapigwe investigation kwa mali walizonazo

Sitaki kuwasikia kabisa
 
TAKUKURU ni taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa boss. Nadhani pia wanafanya uchunguzi wa makosa ya rushwa, ila cha kushangaza ni aina ya uchunguzi wanaofanya maana mfano mapolisi wanachukua rushwa kweupeeee haihitaji hata uchunguzi wala upelelezi. Nahisi tatizo ni Hosea himself
Ukweli usiopingika wayatendayo Takukuru,binafsi siamini na sielewi kama ni taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa!!
Jamani nipeni maelezo zaidi! Ni mengi yanatendeka kweupee! lakin hawatii mguu wala kisigino! hawastahili hilo jina! sorry for that!!
 
Mchezaji wa mpira uwanjani akichemsha refa hana la kufanya isipokua coach lazima awajibike kwa kumtoa ama yeye mwenyewe coach afungashe virago timu inapohujumiwa.Kama hii haiwezekani masabiki hupiga kelele na kufanya fujo za kuwaondoa kamati yote ya ufundi
 
Back
Top Bottom