TAKUKURU; Lowassa Kawakosea nini?

Mwaka mzima huu hamjakamata rushwa hata moja hadi uchaguzi wa Arumeru ulipowadia. Cha kushangaza mko BIAS hadi kila mtu anaona kuwa mmetumwa kukomalia upande mmoja. Kitendo cha kuwakamata watu walio karibu na Lowassa na kuvamia kituo chake cha redio huku kambi ya Sarakikya haiguswi kinaleta picha kuwa TAKUKURU ni mtaji wa kisiasa wa watu fulani.

Uchaguzi wa 2010 mliiandamana kambi ya Sitta na mkamkamata mkewe na kumbambikizia kesi. Wakati huo Sitta na Baba M hawakuwa wanaiva, na wakati huu ambapo inaonekana Lowasa na Baba M hawaivi nyie mnawanyanyasa watu wake. Inatufanya sisi watanzania tulioumizwa sana na ufisadi wa Lowassa kuwa na SYMPATHY naye kuwa huenda mambo yote dhidi yake anapakaziwa.

Ushauri: TAKUKURU tumieni akili kidogo kufanya mambo yenu, msionyeshe kila mtu kuwa mnatumiwa. Rushwa imetapakaa kila kona na mlitoa ripoti kuwa Polisi ndio wanaongoza lakini mmeshindwa kukamata, uwezo wenu ni rushwa za uchaguzi tu au kila aina ya rushwa? Mnatumia vibaya kodi zetu. Acheni nature ichukue nafasi yake, yani NAPE AKAMPIGIE KAMPENI MKWEWE LOWASSA, si ndio demokrasia...

Mkuu, sentensi yako ya pili ni vema isomeke: "Cha kushangaza mko BIASED" badala ya "Cha kushangaza mko BIAS". Vilevile, matumizi ya neno "nature" kwenye sentensi yako ya mwisho si sahihi, yanatoa picha nyingine kabisa ya uliyotarajia. Mwalimu Msonda
 
Wewe Lowassa unamhurumia kwa nini? Kwani Lowassa siyo fisadi? Kwani hajatoa Rushwa? Mbona yeye hajalalamika?
 
Mtoa mada ungeenda kuripoti takukuru juu ya uhalifu wake huo. Yaani unataka kuhalalisha hoja kwa kuhalalisha kosa (rushwa)?
 
Back
Top Bottom