Taka ngumu na kuziba kwa mifereji

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Utupaji taka ngumu kwenye mifereji ya maji machafu ni tatizo sugu katika jiji la Dar es Salaam. Maeneo yanayokumbwa na tatizo la taka ngumu ni maeneo mengi yakiwepo Tandale, Manzese, Buguruni na maeneo mengine mengi. Taka hizi hutupwa kwenye mifereji hiyo nyakati za usiku wanaotupa taka wakiogopa kuonekana. Hii inaonyesha watupao taka wanajua ubaya wake ndio maana wanafanya usiku. Taka hizi hufanya mitaro mingi kuziba na wakati mwingine mitaro hiyo hutoa harufu mbaya ambayo ni chanzo cha magonjwa ya milipuko. Na wakati mwingine wananchi hutumia mifereji hiyo kuzibua vyoo vyao. Fikiria mtu amezibua choo chake akatiririsha maji hayo ya ****** kwenye mfereji halafu mfereji ukaziba, unafikiri nini kitatokea.

Utupaji taka ngumu ni tatizo sugu kwa sababu kwanza hakuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa au kukusanyia taka. Magari ya taka ni nadra sana kuyaona na wakati mwingine hayafuati ratiba ya kukusanya taka. Pia sheria zilizopo hazifuatwi au hazitekelezwi. Miundo mbinu ni mibovu katika kutatua tatizo la mifereji ya maji machafu kuziba.

Suluhisho ni: adhabu kali zitolewe kwa wanaokamatwa kwa kosa la kutupa taka ovyo. Pia pawepo na magari ya kukusanya taka na ratiba ya ukusanyaji taka ufuatwe. Wananchi waelimishwe juu ya adhari za utupaji taka ovyo.
 
Back
Top Bottom