TAJENI majina JF

Mimi nadhani hili ni wazo zuri na kwa vile ni wazo zuri kutaja majina nadhani tuanze kutaja majina yetu sisi wenyewe kabla hatujayataja ya wale wengine. Kwa sababu JF ni "where we dare talk openly"!
 
...mimi naona mnalazimishana vitu ambavyo ni hypothetical. kila habari na kila fununu ina circumstances zake. si hivyo tu, lakini pia kila mwandishi wa habari na kila mtoa habari ana ujuzi wake...

... katika forum kama JF hakuna mambo ya kulazimishana, alimradi habari inaeleweka na ina ukweli hasa katika mambo ya siasa, mambo mengine yote ni ya kumalizia au kukamilisha jedwari tu... tusilazimishane, hiari na malengo ni muhimu zaidi....
 
Duu. Hapa sasa naona kuna hoja mbili, kwanza kutaja majina ya watu unaowatolea habari mfano Msesewe anamiliki majumba ya kifahari ambayo hatujui kayapata vipi, na pia Msesewe ataje jina lake halisi kuwa mtoa taarifa hii ni mimi Rafael John nikiripoti kutoka Mbeya.

Kwa mtazamo wangu kama habari mtu unayoiweka hadharani una uhakika nayo kabisa sioni tabu kwa nini mtu usimtaje mhusika ni nani, ikiwa pia kutaitajika mtu kusema jina la mleta habari sii vibaya ila kuna ushahidi gani kuwa Rafael ni yeye kweli?
 
Watu wamekalia ngangari kupata umaarufu kupitia JF wakati wao wenyewe ndio wa kwanza katika kuchafua topic pale wanapoona ni muafaka kwao kufanya hivyo. Lets concentrate with MAFISADI kwani ukitaka kusema tabia hii imeanza ..........................................you better be specific ili tuchambue pumba ni zipi na upi mchele.

Mbona mleta hoja (GT) hajatoa mfano? Ina maana unaogopa kuweka hiyo mifano ambayo iko hapa JF! What a crap I would imagine if you can't dare to talk openly with your nick name?
 
Mimi naamini tunavyoendelea sasa we are just fine, wanaotaka kuweka majina wataweka, wasiotaka hawatataka, na kama mtu atayataja majina toka ndotoni basi ana haki hiyo.

Tunaposema uhuru wa maoni ni pamoja na uhuru wa maoni ya kijinga au ya ndotoni.
 
MY SUGGESTION ON THIS IS......."TUYATAJE MAJINA YA WAHUSIKA,......NA TUSITAJE YAKWETU...."
 
MY SUGGESTION ON THIS IS......."TUYATAJE MAJINA YA WAHUSIKA,......NA TUSITAJE YAKWETU...."

kwanini sisi tuwe special? hii inaonekana kama sheria za "Shamba la Wanyama" ambako wanyama wote wana haki lakini wengine wana haki zaidi!
 
1. Careful na majina ya watu, so far so good, we are doing just fine, mimi sijawahi kusoma hapa nikashindwa kuelewa anayesemwa ni nani, au ni kiongozi gani,

2. Wazo la GT ni sawa kabisa, na halina ubaya wowote, isipokuwa so far ni wazo, anayetaka anaweza kulikubali na kuanza kuweka majina, au kumtumia majina huko pm, au kukataa,

3. the bottom line ni kuwa ukiweka jina la kiongozi au mwanachi, bila mpangilio au uhakika wa unachofanya, hiyo ni responsibility yako wewe mwenyewe, na wamiliki wa JF, lets be real on that,

Otherwise, tujifunze kutumia pm, maana ndio hasa kazi yake, kuuuliza usichoelewa kwenye uwanja kabla hujakurupuka, idea ni nzuri sana mkulu GT, ila wanaotaka kufanya hayo wahahkikishe wana ubavu, hakuna asiyependa kutaja majina, lakini kila ishu ina season na time yake, ndio maana huwa tuna dataz nyingi sana believe me tukiamua kuziweka hapa hapatatossha, lakini huwa kuna kusubiri timing, na pia kama wewe huwezi ni kumpa mwingine aziweke, sifa ni kwa JF kwanza sisi baadaye!

Ahsante Wakuu!
 
kuna majina ambayo hayatajwi kwa sababu ni kinyume na sheria; mnakumbuka ya Valerie Plamer..? so tread careful
 
Kama kuna mtu anaogopa kutaja majina anipe niyataje mimi.Unafiki hatutaki biashara hizi za kutoa ndizi Mwanza na kupeleka Bukoba hatutaki JF.
 
Nimeanza kusoma post moja hadi nyingine nikawa sielewi anachozungumzia hapa GT, hadi aliposema haya.

Huwezi kuamini how long it took us wengine kujua kama CHENGE ndiye watu humu walikuwa wanasema eti(jina linahifadhiwa)what ever hapenned to JF kuset the agenda?

Badala magazeti kujadili reference zetu utashangaa tunajadili yaliyoandikwa na hayo magazeti ambayo yanakuja kucopy data humu

Hoja anayoijadili hapa GT ni kwamba habari iliyokua ikijadiliwa kuhusu Chenge haikuwa imetokana na post ya JF bali ni habari iliyochapwa katika gazeti la Thisday na kuwekwa JF, ndipo watu wakawa wanamtaja Chenge kuwa ndiye waziri aliyefichwa jina na THISDAY. Kwa kifupi anachosema GT humu si cha kweli kwani walioficha njina ni THISDAY si JF kwani ndani ya JF jina la Chenge lilitajwa na wengi wakijadili hiyo habari ya THISDAY na mimi nikawaambia wazi nikimjibu Kitila kwamba ndani ya siku tatu jina la Chenge litatajwa hadharani tena kutokea nje ya nchi na hiyo ni baada ya kuzungumza na wapelelezi ambao nilikutana nao katika ndege nikielekea Nairobi na wao wakienda London wakiwa na hizo data na wakasema tayari wamewapa hizo taarifa waandishi wa The Guardian la Uingereza ambao wangezichapisha siku si nyingi. Sasa GT labda aanze kujadili THISDAY kwa kutotaja jina na si JF. JF walimtaja Chenge moja kwa moja baada ya watu kujadili THISDAY na yote yaliyojadiliwa JF yametokea kwa kipindi kilichotajwa na JF kwa kuwa JF siku zote MBELE DAIMA
 
Majina.....leo Mwanahalisi wamemtaja 'ofisa mwandamizi mmoja aliyekua benki kuu miaka kadhaa iliopita na ambaye kwa sasa anaongoza shirika la umma'ambaye account yake ilipokea dola 600,000 kutoka kwa Chenge,sasa huyu si Dr Idris Rashid tu,au kuna mwingine?
 
Back
Top Bottom