Taifa Tanzania lapinga sababu 51 za Kikwete kutogombea 2010!

Unajaribu kusema nini? Kwamba Kikwete anafaa kwa sababu kapanda ngazi kutoka chini?

Umeona nilivyoeleza mwanzo kwamba Tanzania uongozi si lazima uendane na uwezo?

Ikiwa Mwinyi mwenyewe aliyemteua Kikwete ni failure aliyejiuzulu, na akarudi tena kwenye system na kupanda ngazi mpaka urais (mtu alishajiuzulu kwa uzembe) unategemea nchi hii kupanda ngazi kuwe na maana ya kwamba kunatokana na utendaji mzuri?

Katika hili tusidanganyane.

Nimekupata kabisa. It was just a joke trying to explain how he managed to reach there. Najuwa wewe na mimi tuko upande mmoja.

hapa umemnyamazisha kijana!AMEELEWA SOMO HUYO

Sometimes you need to read between the lines siyo kukurupuka tu. Swala si ushabiki hapa bali ni mjadala. Kama unataka kuelewa misismamo ya watu fuatilia mada siyo one posting!!!
 
Nadhani tuwe fair, tuseme JK hajatimiza ahadi zake kwa x% ambayo hiyo x ni kubwa kulizo 0%. the moment unavyosema hajafanya chochote (yaani 0%)... yet kuna habari kama hii..yeyote anayefanya hivyo anaonekana ana matatizo.

Habari yenyewe kwa wenye uvivu wa ku-click link.

UDOM ni matunda ya ahadi ya JK

RAIS Jakaya Kikwete leo anatimiza miaka minne tangu alipoingia Ikulu, ana kila sababu ya kujivunia utekelezaji wa ahadi zake ikiwemo ya kuratibu mchakato wa kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM).

Ni chuo cha aina yake nchini chenye eneo kubwa ambalo si rahisi kutembea kwa miguu na kulimaliza kwa vile lina ukubwa wa ekari 15,000.

Shughuli za awali za chuo zilianza katika jengo mashuhuri la CCM la Chimwaga, ambalo pia wakati fulani lilikusudiwa kuwa jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwandishi wa makala haya alipotaka kufahamu wapi lilipotoka wazo la kuanzishwa kwa chuo kikubwa namna ile, Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Idris Kikula anasema:

“Sisi ni wanataaluma, tumeandika kitabu kuhusu uanzishwaji wa Udom ambamo tumeeleza kwamba suala zima la Udom limetoka kwa Rais Jakaya Kikwete katika kampeni zake.

“Ingawa haikuainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM, lakini katika kampeni zake, aliahidi kuanzisha chuo kikubwa kama atashinda uchaguzi na kweli ametekeleza ahadi yake ambayo haikuwa kwenye Ilani ya Uchaguzi.

“Rais Kikwete amenipa ushirikiano mkubwa na anaendelea kufanya hivyo katika kuhakikisha kuwa Udom inafikia malengo yake na kinakuwa chuo cha mfano nchini, ndiyo maana unaona maendeleo haya ya majumba, mandhari na maelfu ya wanachuo, hadi ametuunganisha na kampuni ya IBM ya Marekani. Nitakueleza mengi, yote ni kazi ya Rais Kikwete”.

Profesa Kikula anasema Rais Kikwete ametoa ruhusa kwa Udom kutafuta wahadhiri ndani na nje ya nchi, ambapo hadi sasa chuo kimepata 19 kutoka India; Urusi na Cuba, na zimekubali kutoa walimu na hivi karibuni wataajiriwa.

Kutokana na ruhusa hiyo, Udom inaajiri wahadhiri wa muda kutoka nje ya nchi wenye sifa ya kufundisha, akiwamo Mwenyekiti wa Baraza la Udom, Dk. Mohamed Gharib Bilal ambaye ni gwiji wa Fizikia.

Yeye anafundisha kwa muda chuoni hapo. Watanzania wengine wenye sifa pia wanakaribishwa kufundisha kwa muda.

Katika kuonesha busara zake, Rais Kikwete ametekeleza ahadi ya kujenga chuo kikuu kwa faida ya Taifa na anasimamia ahadi yake hiyo kwa nguvu zake zote, tena katika mazingira magumu ya kutokuwa na fedha za kuendeshea mradi huu mkubwa nchini.

Mkuu wa Udom ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa, wakati Mwenyekiti wa Baraza la Udom ni mwanasiasa msomi na Dk Bilal ambaye pia ni Waziri Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Udom haina mfano wa kulinganishwa nao nchini na hata Afrika Mashariki kwa sababu nyingi tu, lakini Profesa Kikula anasema ndicho chuo kikuu pekee nchini ambacho kimeanzisha mafunzo ya Shahada za Lugha za Kijapani, Kikorea na Kichina.

Kama vile haitoshi, Udom ndicho chuo kikuu pekee nchini chenye mfumo wa utawala wa makao makuu na kuwa navyuo huru vinavyojitegemea ambavyo vinaratibiwa na ofisi ya makao makuu. Tayari vipo vyuo viwili na taasisi mbili, vyote vikitoa shahada, lakini lengo ni ifikapo mwaka 2012 chuo kiwe na vyuo sita vitakavyoratibiwa na ofisi ya makao makuu, anasema Profesa Kikula.

Lengo la chuo kikuu cha Udom ni kwamba ifikapo mwaka 2012 kiwe na uwezo wa kudahili wanafunzi 40,000 wa shahada mbalimbali.

Hadi sasa kuna jumla ya wanachuo 7,305 na kati yao, wanachuo 2,158 ni wanawake sawa na asilimia 30 ya wanachuo wote wa Udom hadi Julai mwaka huu. Kufikia Oktoba, idadi ilitarajiwa kuongezeka hadi 10,000 na kuifanya Udom kufikisha wanachuo 17,305.

Hiyo ni habari maalumu, anasema Baltazaar, ambaye ni Ofisa Uhusiano wa Udom. Profesa Kikula anasisitiza kuwa hii ni historia kubwa na ya kwanza kutokea, na kuongeza:

“Rais Kikwete atabaki katika vitabu vya kumbukumbu nzuri milele ya watu mashuhuri waliotoa mchango usiosahaulika kukuza elimu kwa kuzingatia mlolongo wake tangu msingi, sekondari na chuo kikuu”.

Maneno haya yanatoa changamoto kwa watu makini, kupima ukweli na uongo kwa vile utekelezaji unaonekana kwa macho na wala si kwa ramli ya mganga wa kienyeji.

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza anayetoka Kigoma, Vumi Omari anayechukua Shahada ya Biashara, anasema mjadala wa madai kuwa JK kashindwa kazi, waachiwe watoto wa wakulima wanaosoma Udom ambao watachambua pumba na mchele kwa wazazi, walezi, marafiki na jamii kwa jumla warudipo likizo na wakati mwafaka ukifika.

Chuo pia kimewezeshwa kuwa kituo cha Uenezi wa Taaluma ya Mawasiliano (IT) Tanzania, ambayo ni muhimu katika maendeleo ya kisiasa. Kutokana na jitihada za Rais Kikwete, chuo kimepata wataalamu kutoka kampuni ya IBM, Marekani.

Hapa ndipo lile suala la kulaumu safari za Rais nje ya nchi linapopatiwa jibu, kwamba Udom ina kituo chenye hadhi ya kutoa shahada za taaluma ya mawasiliano ambayo kinapata msaada wa kitaaluma ya mawasiliano kutoka IBM, mabingwa wa IT wa Marekani.

Tungepataje misaada hiyo haraka hivyo kama si kwa Rais mwenyewe kujishughulisha? Huu ni upande wa pili wa sarafu, hasa kwa wale wachache wanaodai Serikali ya Awamu ya Nne haijafanya kitu.

Kinachotakiwa kwa watu hao ni kuwaeleza kwa takwimu ili kubainisha kwamba wanayosema si sahihi na kwa yeyote anayepinga na aende Udom akaone maendeleo ya elimu ya juu.

Katika hali ambayo haikutarajiwa kabisa katika chuo chochote nchini, Udom imejipambanua vilivyo kwani hadi Julai mwaka huu, kimefundisha shahada mbalimbali 56 na lengo lake ni kutoa shahada 63 ifikapo mwaka 2012.

Haya ni maendeleo makubwa. Udom sasa ina vyuo vinne: Chuo cha Sayansi za Jamii na Lugha, Chuo cha Elimu, Chuo cha Sayansi za Kompyuta, na Chuo cha Sayansi Asilia na Hisabati.

Katika jitihada za kukabiliana na tatizo la walimu wa shule za sekondari hususani za kata, hadi Julai mwaka huu Udom ilikuwa na wanachuo 4,000 wanaosomea Shahada ya Ualimu. Udom pia imewezesha kuajiriwa wahadhiri wapatao 300 wakiwamo wa muda na watumishi wengine 200 wameajiriwa.

Shughuli za ujenzi wa chuo katika kipindi cha kati ya mwaka juzi na mwaka jana, zimewezesha kuajiriwa vibarua zaidi ya 10,000, anasema Baltazar.

Ili kujitosheleza kwa mahitaji ya wahadhiri, Udom inafundisha walimu wake ndani na nje ya nchi katika ngazi za Shahada za Uzamili na Uzamivu (PhD). Katika hali isiyokuwa ya kawaida, muundo wa Udom ni tofauti.

Katika eneo la chuo lipo kwa ajili ya shughuli za kitaaluma tu na wafanyakazi wote wanakaa nje ya chuo, na huu ndio mpango mkakati wake unavyoelekeza na kutenganisha maeneo ya vyuo vyake mbalimbali.

Kwa mujibu wa Profesa Kikula, mpango mkakati umeelekezwa pia katika kukifanya chuo kuwa kituo cha utalii mjini Dodoma na kwamba mkandarasi ameshapatikana wa kuweka mandhari itakayokifanya kufikia lengo hilo.

Kila mwanafunzi ana kitanda chake na amewekewa nafasi ya kusomea bila msongamano. Chumba kimoja kikubwa kinalaza wanafunzi wanne, kila mmoja akiwa na sehemu yake ya kusomea na kuweka kompyuta kwa ajili ya huduma za mtandao chumbani.

Kwa chuo kinachojengwa kwa thamani ya Sh bilioni 772.8, kati ya bajeti hiyo, tayari ujenzi umegharimu karibu nusu ya fedha hizo yaani Sh bilioni 300. Kwa mujibu wa utafiti, Udom imebadili shughuli za kiuchumi Dodoma ambazo sasa zimeshamiri.

Soko la Dodoma limekua na kuongeza shughuli mbalimbali za kibiashara tofauti na zamani ambapo tegemeo kubwa lilikuwa shughuli za Bunge ili kuboresha biashara, anasema Musa Jama, mwandishi mkongwe na mwakilishi wa Radio Uhuru mjini Dodoma.

Hivyo ujio wa Udom umekwenda sambamba na Ilani ya Uchaguzi katika kukuza uchumi, kupambana na umasikini na kutoa ajira, kwani magari mengi yamepata kazi ya kupeleka wafanyakazi na wanafunzi chuoni na kuwarejesha mjini.

Vifaa vya kuandikia na huduma mbali mbali hali kadhalika zimeongezeka, kama vile vyakula katika migahawa ya kawaida vinauzika.

Udom imechangamsha Dodoma, anasema mkazi wa barabara ya Saba, Joseph Mazengo. Pamoja na mafanikio yote hayo, Profesa Kikula anasema changamoto kubwa ya Udom hivi sasa ni uchanga wa chuo unaokifanya kuwa na uhaba wa walimu, ikifuatiwa na uhaba wa nyumba za walimu ukiwamo ukosefu wa nyumba ya hadhi kwa Makamu Mkuu wa Chuo na watumishi.

Changamoto nyingine ni upatikanaji wa maji safi, wingi wa wanachuo, miundombinu ya kutupa majitaka ya chuo na wizi.

Profesa Kikula anavishukuru vyombo vya habari nchini kwa kukitangaza vyema Chuo Kikuu cha Dodoma na kuwezesha mwaka juzi kupokea maombi ya udahili 15,000 na mwaka jana maombi 19,000 na mwaka huu maombi 29,000.

Udom itaanzisha shahada ya Taaluma ya Habari na Mawasiliano na Umma muda si mrefu, ujao ambao Profesa Kikula hakupenda kutoa tarehe rasmi.
 
Moja ya dawa muhimu ni kubadilisha katiba ili kipindi cha Urais kiwe kimoja tu kuanzia mwaka ujao, 2010. Mbunge jasiri akiamua anaweza kupeleka hoja binafsi bungeni ili zoezi lianze mapema na kwa kasi inayostahili. Hatuhitaji Rais kuwa madarakani kwa vipindi viwili. Kimoja kinatosha sana mtu kufanya yale aliyoyapanga na serikali yake kwa ajili ya nchi yetu. Namini uzoefu tunao wa kutosha katika hili.

Sidhani kuwa tatizo la uongozi wa nchi yetu liko katika vipindi mtu anavyotakiwa kuwa Rais wa nchi. Tatizo kubwa kabisa liko katika namna ya kumpata mtu anaefaa kushika wadhifa huo (uRais), na jinsi anavyopata uRais wenyewe. Vile vile, kuna tatizo katika udhibiti wa mamlaka ya Rais. Labda hayo ndio yanayohitaji kuangaliwa kwa makini zaidi.

Narudia tena (kama nilivyowahi kusema katika thread za nyuma) kuwa, Katiba ya nchi yetu haina manufaa kwa Taifa kabisa. Ni Katiba ambayo imepitwa na wakati, na inahitaji marekebisho makubwa sana. Nchi inahitaji Katiba ya kisasa inayoweza kutumika kuleta mabdiliko ya kisasa.
 
Wadau, mchomeko wa mada nyingine kwenye Taifa Tanzania inayohitaji kujadiliwa.

TUNAMJIBU M.M. MWANAKIJIJI:

...............[snip]
Kuna kundi dogo la watu ambao wana nongwa ya kuukosa Urais 2005 ..................[snip]

Walipofanikiwa kumg’oa Edward Lowassa hawakuridhika.

Kama kweli majibu kama haya yanatokana na 'brain' inayoaminika, basi tuna matatizo makubwa sana kiutawala.

Mwandishi huyu bado hadi leo ana amini Lowasa ni shujaa aliyezidiwa mbinu. Sababu ya makundi sasa inaonekana wazi maana kumbe bado Lowasa ni mtu mzuri kwa watu kama mwandishi huyu. Eti walipofanikiwa kumung'oa. Kumung'oa. Sema Lowasa aliposhindwa kujitetea kutokana na makosa yake,period.

Kama kweli CCM hakuna watu wenye uwezo zaidi ya JK, hilo ni tatizo jingine. Binafsi inanipa picha kwamba JK ndo kipimo cha best performance.

Angalia hata mchwa wana malkia! Kwa maana nyingine kila sehemu, bila kujali upungufu wa IQ ktk kundi lolote lile lazima kuwe na kiongozi. Shauri yenu.
 
Nadhani tuwe fair, tuseme JK hajatimiza ahadi zake kwa x% ambayo hiyo x ni kubwa kulizo 0%. the moment unavyosema hajafanya chochote (yaani 0%)... yet kuna habari kama hii..yeyote anayefanya hivyo anaonekana ana matatizo.

Habari yenyewe kwa wenye uvivu wa ku-click link.

UDOM ni matunda ya ahadi ya JK

RAIS Jakaya Kikwete leo anatimiza miaka minne tangu alipoingia Ikulu, ana kila sababu ya kujivunia utekelezaji wa ahadi zake ikiwemo ya kuratibu mchakato wa kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM).

Ni chuo cha aina yake nchini chenye eneo kubwa ambalo si rahisi kutembea kwa miguu na kulimaliza kwa vile lina ukubwa wa ekari 15,000.

UDOM.........UDOM...........UDOM...... nk.

Mafanikio ya UDOM tunayasubiri huko maofisini baada ya wanafunzi hao kumaliza masomo yao. Usitaje mambo ya idadi, majengo, wahindi, warusi na yote yasiyohusiana na elimu. Mbona hutaji jinsi chuo kinavyoshindwa ku-retain staff. Kila leo kuna exodus ya walimu kwenda vyuo vingine. Kuna uchafu gani hapo?

Mambo ya UDOM tulishayajadili kwa kirefu sana ktk kipindi kilichopita. Unaweza ukatusaidia sana kama utajibu maswali ya siku zile kuliko kuanza tena kusifia UDOM x1000.

Kama wewe ni Rais wa nchi, unaweza ukatumia ujenzi wa chuo kimoja cha wanafunzi 40,000 kwa miaka mitano kama agenda kubwa kabisa ya maendeleo? Unanikumbusha mavuno ya kwetu uzalamoni yanayotufanya tucheze ngoma miezi mitatu.
 
Wadau, mchomeko wa mada nyingine kwenye Taifa Tanzania inayohitaji kujadiliwa.

TUNAMJIBU M.M. MWANAKIJIJI:

Sababu 102 kwa nini Jakaya Kikwete agombee 2010 na aendelee kuongoza

MWANDISHI WETU

Wana CCM milioni 4 (kasoro Nungayembe wa kisiasa) na wapiga kura kwa mamilioni, wanatambua uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Hao waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu 2005, pamoja na wapiga kura wapya tuna hakika, hawajaona au hawategemei kuona mbadala kwa nafasi ambayo Kikwete anayoishikilia. Kwa nini tunaona hivyo?

Hali iliyopo kwa watu wanaofanya shughuli zao za kuzalisha mali na katika kujenga taifa inaridhisha tofauti na ramli za kutabiri mwisho wa dunia ya Tanzania yenye amani zinazopigwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Kuna kundi dogo la watu ambao wana nongwa ya kuukosa Urais 2005 na wengine ambao hawana uwezo wa kuchambua matukio, michakato na mienendo ya kisiasa na kijamii wanaendeshwa na kuamini katika hisia zao, ambazo zinawatuma kuandika vitu vya kubuni na alnacha.

Walipofanikiwa kumg’oa Edward Lowassa hawakuridhika. Wamekuwa wakijidanganya kwamba wanaweza kutimiza ndoto yao ya kumng’oa na Kikwete na kuzika kizazi hicho cha uongozi. Katika Gazeti la Mwanahalisi, toleo Na. 167 Jumatano Desemba 16-22, 2009 makala ya M.M. Mwanakijiji (sababu 51 za kumkwamisha Kikwete) mwandishi anaonyesha alivyokosa cha kuandika, akalazimisha hoja na sababu kwa nini Rais Kikwete asigombee nafasi ya Urais mwaka 2010.

Kwanza kabisa hakuna mwanachama ndani ya CCM anayeweza kutaka kugombea na akawa tishio kwa Rais Kikwete. Kikwete alishapitia tanuru la moto mwaka 1995 na 2005.

Hakuna watu wenye nguvu na uwezo wa kila hali ambao wanaweza kujitokeza sasa kuliko wale ambao aliishashindana nao huko nyuma. Majina ya akina John Samwel Malecela, Frederick Sumaye, Profesa Mark Mwandosya, Cleopa Msuya, Benjamen Mkapa, Jaji mstaafu Mark Bomani, Salim Ahmed Salim na mengineyo ni majina makubwa. Alishindana nao na akawashinda.

Kikwete kugombea Urais siyo kwa maslahi ya wapambe, kuna mambo makubwa zaidi ya wapambe ambayo yanamfanya mtu agombee nafasi kuu ya Urais. Tamaa ya mtu katika nafsi yake kutaka kugombea uongozi ni kwamba ana uwezo fulani na anataka atekeleze mambo fulani nje ya nafsi yake. Wako watu wengi katika uwanja wa siasa ambao hawafikii hatua hiyo.

Ukweli wa mambo ni kwamba tangu achukue madaraka 2005, mambo mengi yamekuwa yanafanyika hapa nchini. Miradi imekuwa inatekelezwa na serikali watu katika sekta binafsi, mashirika makubwa ya kimataifa na mashirika ya kidini. Kusema kwamba wanaotaka Kikwete agombee ni wale ambao wanakariri kikasuku msemo wa “kuendeleza umoja, utulivu, amani na mshikamano” wa nchi yetu, ni fikra za mtu ambaye akili yake imedumaa na kukwama kutokana na kutotaka kujifunza mabadiliko yanavyotokea katika mazingira na nani analeta mabadiliko hayo.

Kwa upande mwingine dhana ya utulivu wa kisiasa (political stability) imepitwa na wakati. Wanataaluma na watunga sera, sasa hivi wanazungumzia utulivu utokanao na mkusanyiko wa sababu mbalimbali za maendeleo katika sekta za uchumi na ustawi wa jamii (structural stability). Kwamba watu hawali maneno matupu na nadharia za siasa.

Utulivu kimfumo una nafasi kubwa kutokana na sekta mbalimbali kutegemeana ili kuleta maendeleo yenye ulinganifu, hivyo ni wazi kwamba sera zote zinazotungwa na miradi inayotekelezwa inakuwa imepangwa kimtambuka kiasi kwamba yanayotokea sekta moja yanaathiri maendeleo yatakavyokuwa katika sekta nyingine.

Kwa namna moja au nyingine watanzania walio wengi katika sekta mbalimbali wanaguswa na kufikiwa na miradi ya maendeleo ya kubadilisha maisha yao . Yawezekana kwamba kasi ya maendeleo inazidiana. Lakini kwa namna moja au nyingine kuna mabadiliko ya msingi kule wanapoishi watu.

Watu wasioelewa hali inavyobadilika wanakuwa wa kwanza kupiga mayowe jinsi serikali ilivyoshindwa kuwaletea watu maendeleo, bila kutambua ukweli wa mambo kwamba watu wenyewe ndiyo watajiletea maendeleo na kazi hiyo ndiyo wameshaianza. Kwa waandishi wapiga ramli, kwa sababu wanataka kuonyesha msimamo wao wa “kupinga kila kisemwacho au kufanywa na hasimu wao”, wanakuwa na watu wao ambao wanawaumba na kuwatengenezea mazingira.

Wanapoanzia siyo kuonyesha uwezo wa kiongozi wao wa kufikirika bali ni kubuni na kuzua mambo, na kujaribu kugeuza mkondo wa maji utoke ziwani na kupanda mlima. Kwa hili la Kikwete kugombea 2010 tunasema binadamu ana uwezo mkubwa, lakini hawezi kuzuia jua kuchwa!

Katika jamii inayokua kwa misingi ya kidemokrasi wapiga kura na raia kwa ujumla wana nafasi yao katika mchakato wa siasa, uchumi na maendeleo ya jamii. Nchi inaweza ikawa katika matatizo makubwa ya kiuchumi lakini hakuna matukio ya uvunjivu wa sheria wa makusudi kutoka kwa watu wengi. Tanzania ilipitia vipindi vigumu ambapo uchumi wa nchi ulikuwa mbaya. Hakuna fujo zilizotokea ambao zilitishia usalama wa watu na mali zao.
Kuna sababu 102 ambazo tunaona kwa nini Rais Kikwete agombee Urais 2010. Tutazitolea maelezo machache baadhi ya sababu kila panapokuwa haja.

Tunaanza na sababu 3:

Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele wa kutaka kuwepo utawala wa sheria. Utawala wa sheria ndiyo msigi mkuu wa utawala wa kidemokrasia, Tanzania ni nchi mojawapo miongoni mwa nchi changa kuwa na asasi zenye mamlaka zinazofanya kazi kwa uhuru kamili.

Hivi sasa ni wazi kwamba nchini Tanzania hakuna mtu anayekuwa juu ya sheria; awe ni raia wa kawaida, kiongozi mkuu serikalini au watendaji wakuu waandamizi. Matukio ya kutaka sheria ichukue mkondo, yako wazi na sasa tunaweza kusema sheria inatawala na watu wanaongoza. Tanzania haitumii utawala kwa sheria.

Rais Kikwete anajali mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mikuu mitatu

Sasa hivi mgawanyo wa madaraka kati ya utawala wa dola, mabaraza ya utungaji sheria na Mahakama uko wazi. Kila mhimili una eneo lake na mipaka yake utawala wa dola unafanya kazi ya utendaji katika mfumo wa dola. Utumishi wa umma, majeshi ya ulinzi na usalama na srikali za mitaa zote ni asasi za mamlaka. Uhuru wa Mahakama ni jambo lisilo la kubishaniwa. Tangu miaka ya 1960 bunge la Tanzania limekuwa linajaribu kuwa muhimili usiothibitiwa. Sasa hivi hilo limewezekana kutokana na Rais Kikwete kujali na kutaka kila mhimili uwe huru kufanya mambo yake na yote kwa maslahi ya taifa.

Rais Kikwete anajali na kutambua ulazima wa utawala bora kwa maendeleo ya taifa Utawala bora ni dhana mpya ambayo imebuniwa katika jitihada za dola kukabiliana na hali mpya inayotokana na matakwa mapya kadri mazingira ndani na nje ya jamii yanavyokuwa na matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi. Utawala bora una maana ya ushirikishwaji wa wadau na dola kuwa chombo cha kuelekeza matumizi ya raslimali. Na hivyo utawala (bora) ni pamoja na njia zilizo bora za kudhibiti na kuratibu shughuli zinazolenga kuwapa watu uhuru zaidi na uwezo wa kuthibiti mazingira.

Rais Kikwete anathamini mashauriano kati ya wadau juu ya utungaji sera Rais Kikwete anajali usawa wa kijinsia.

Ametunza lengo la kuendeleza sera za kuvutia wawekezaji

Amekubali ushauri wa kufanya mabadiliko katika sera na sheria za madini (kuleta ulinganifu)

Ni kiongozi anayekubali ushauri katika miswada ya serikali inayopelekwa bungeni

Ni kiongozi mwenye kuwa na ubunifu katika utungaji sera za maendeleo mfano mzuri ukiwa ni sera ya Kilimo Kwanza.

Source: TAIFA Tanzania , Desemba 18, 2009
( Mambo yamepamba moto. Nyingine hii nimeinasa kutoka mtandao wa kwanzajamii.com)

Mimi nina wasiwasi CCM au JK Mwenyewe amempa tenda huyu jamaa aandike kujaribu kuwasafisha lakini ukweli unabaki pale pale na UOZO WA CCM na viongozi wake unaonekana. KWANINI TUWACHAGUE TENA? Mkome kabisa!!!! Ondokeni madarakani tunataka nchi iendelee na sio baadhi ya watu wachache wa CCM.
 
Mkongo;Kama atakuwa amepewa kazi,basi machoni pa wachambuzi wengi kaandika upupu zaidi,kwanza ngoja tuanze na hii quote hapo chini....Mwandishi anapodai kuwa walifanikiwa kumng'oa Lowassa,basi ana maanisha kuwa ilikuwa ni kinyume cha matakwa ya JK,je ni kweli?Na hizi rumours kwamba EL anataka kurudi na kujisafisha,je atakuwa anapambana na nani kwenye harakati zake hizo?Mwandishi anaelekea kuamini kwamba JK na EL bado wapo pamoja na kwamba nia mbaya ipo ya kuzika kizazi hicho cha uongozi,sasa sijui ni kizazi hiki cha baraza jipya ama kizazi cha kina EL?Mwandishi anaonekana amebase uchambuzi wake kiupambe upambe zaidi,na kwajinsi ninavyoona,kwa Mwanakijiji huyu ni sisimizi tu,huyu ni size yetu sisi huyu si Mwanakijiji,hivyo kama ni mpambano wa hoja,ni wazi MKJJ ataprevail...Na inaonekana kama mwandishi amemtaja MKJJ mara baada ya kusema "walimng'oa Lowassa" na kwahivyo basi huyu atakuwa ni victim wa baraza la zamani na hivyo jazba zake bado zinamsumbua,kimawazo bado yuko kwenye baraza la zamani la mawaziri,ama kama sivyo yuko kwenye payroll.

Walipofanikiwa kumg'oa Edward Lowassa hawakuridhika. Wamekuwa wakijidanganya kwamba wanaweza kutimiza ndoto yao ya kumng'oa na Kikwete na kuzika kizazi hicho cha uongozi. Katika Gazeti la Mwanahalisi, toleo Na. 167 Jumatano Desemba 16-22, 2009 makala ya M.M. Mwanakijiji (sababu 51 za kumkwamisha Kikwete) mwandishi anaonyesha alivyokosa cha kuandika, akalazimisha hoja na sababu kwa nini Rais Kikwete asigombee nafasi ya Urais mwaka 2010.
 
Mafanikio ya UDOM tunayasubiri huko maofisini baada ya wanafunzi hao kumaliza masomo yao. Usitaje mambo ya idadi, majengo, wahindi, warusi na yote yasiyohusiana na elimu. Mbona hutaji jinsi chuo kinavyoshindwa ku-retain staff. Kila leo kuna exodus ya walimu kwenda vyuo vingine. Kuna uchafu gani hapo?

Mambo ya UDOM tulishayajadili kwa kirefu sana ktk kipindi kilichopita. Unaweza ukatusaidia sana kama utajibu maswali ya siku zile kuliko kuanza tena kusifia UDOM x1000.

Kama wewe ni Rais wa nchi, unaweza ukatumia ujenzi wa chuo kimoja cha wanafunzi 40,000 kwa miaka mitano kama agenda kubwa kabisa ya maendeleo? Unanikumbusha mavuno ya kwetu uzalamoni yanayotufanya tucheze ngoma miezi mitatu.

This should be read at a high volume.

Preferrably, in a residential area.
 
hii nchi kwa kutea viongozi wabovu kiboko.watu wanatetea sera ambazo hata zijatekelezwa kwa vitendo imradi mtu alisema kitu tu.
 
Mwandishi huyu yuko very shallow, JK has done more than any presidency in the country for four years!

There are so many things worth mentioning lakini mwandishi hakusema anahitaji kufanya utafiti wa kutosha ameacha kusema mambo mengi ya maana kama barabara, mishahara (increase), shule na mahospitali nk
 
Tatizo ni kwamba Rais anashidwa kufanya kuwajbisha watendaji kibao ambao wanaimaliza Bongo na ushaidi upo kwa baadhi ya watendaji wake kuwa mafisadi,ruswa,kutumia mali za umma vibaya .kwa mtaji huo hafai kabisa kugombea urais,tunataka mchapa kazi ammbaye atahakikisha hakuna mafisadi,na watu wote wanaoifirisi Tanzania hivyo namuunga mkono mwanakijiji 100%
 
Wadau, mchomeko wa mada nyingine kwenye Taifa Tanzania inayohitaji kujadiliwa.

TUNAMJIBU M.M. MWANAKIJIJI:

Sababu 102 kwa nini Jakaya Kikwete agombee 2010 na aendelee kuongoza

MWANDISHI WETU

Wana CCM milioni 4 (kasoro Nungayembe wa kisiasa) na wapiga kura kwa mamilioni, wanatambua uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Hao waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu 2005, pamoja na wapiga kura wapya tuna hakika, hawajaona au hawategemei kuona mbadala kwa nafasi ambayo Kikwete anayoishikilia. Kwa nini tunaona hivyo?

Hali iliyopo kwa watu wanaofanya shughuli zao za kuzalisha mali na katika kujenga taifa inaridhisha tofauti na ramli za kutabiri mwisho wa dunia ya Tanzania yenye amani zinazopigwa na baadhi ya vyombo vya habari.

- Huyu muandishi naye ni misguided kama waandishi wa habari anaowalaumu, asingekua basi angekuwa ana-record kwamba amani ya Tanzania, iliharibika pale wananchi wasio hatia walipopigwa Mwembe Chai na wengine kuuliwa Pemba, katika serikali ambayo Rais wa sasa alikua waziri wa nje na kama ana kumbu kumbu nzuri basi angekuwa anajua kuwa hata rais wa wakati huo Mkapa, katika hotuba yake baada ya mauaji yale alisema wazi kwamba amani ya Tanzania imeingia dosari tayari.

- Kwa hiyo utabiri wa waandishi kuwa amani ya Tanzania inaelekea ukingoni ni sawa sawa maana kuna facts zipo za ku-back up the claim, as opposed na maneno ya huyu muandishi ambayo simply ndio hasa ramli yenyewe anayoisema!

Kuna kundi dogo la watu ambao wana nongwa ya kuukosa Urais 2005
- Misguided au simply stupid, Mwanakijiji, Butiku, na Quaresi hawakugombea urais anytime, na hasa Mwanakijiji ambaye ndiye hasa the focus wa hii nonsense article sikumbuki wakati wowote amewahi kugombea anything Nationally

na wengine ambao hawana uwezo wa kuchambua matukio, michakato na mienendo ya kisiasa na kijamii wanaendeshwa na kuamini katika hisia zao, ambazo zinawatuma kuandika vitu vya kubuni na alnacha.
- Misguided and foolish, kama hawa wachambuaji kama Mwanakijiji hawana uwezo wa kuchambua then why waste your precious time kuwajibu tena na mu-article mrefu kama unaomba viza ya US, please hatujazaliwa jana hapa JF! Nenda muwaambie waliowatuma kwamba tupo macho sana!

Walipofanikiwa kumg'oa Edward Lowassa hawakuridhika. Wamekuwa wakijidanganya kwamba wanaweza kutimiza ndoto yao ya kumng'oa na Kikwete na kuzika kizazi hicho cha uongozi.

- Another misguided point, Lowassa amejing'oa mwenyewe kwa wizi wake, kwanza ashukuru kwamba Rais ni rafiki yake, otherwise alitakiwa awe Segerea as opposed na bungeni aliko sasa.

- Kikwete, anataka kujing'oa mwenyewe kwa kushindwa kufanya aliyoayaahidi akipewa urais, na who said that hao wawili ndio kizazi hicho cha uongozi, nonsense sasa how come sio wawili tu wanaongoza Tanzania sasa hivi, I mean hata muandishi anaonyesha the fear kwamba Tanzania tunaweza tukaishi bila hao wawili, ndio maana amekuja mbio kumjibu member wa JF mwenye uwezo mdogo sana wa kuchambua mambo ya siasa na uongozi, lakini akawaacha wachmbuzi wakubwa sijui wapi huko1 Bwa! ha! what a big joke!

Katika Gazeti la Mwanahalisi, toleo Na. 167 Jumatano Desemba 16-22, 2009 makala ya M.M. Mwanakijiji (sababu 51 za kumkwamisha Kikwete) mwandishi anaonyesha alivyokosa cha kuandika, akalazimisha hoja na sababu kwa nini Rais Kikwete asigombee nafasi ya Urais mwaka 2010.
- Muandishi anaonyesha jinsi alivyokosa cha kuandika, lakini wewe mwenye something good cha kuandika ukaamua to waste all you time kuandika mu-article wote huu kujibu hoja za kulazimisha za Mwanakijiji? Bwa! ha! ha! yaani inafurahisha sana! I mean hawa watu wa namna hii ndio wamemzunguka Rais wetu, Bwa! ha! ha!

Kwanza kabisa hakuna mwanachama ndani ya CCM anayeweza kutaka kugombea na akawa tishio kwa Rais Kikwete. Kikwete alishapitia tanuru la moto mwaka 1995 na 2005.Hakuna watu wenye nguvu na uwezo wa kila hali ambao wanaweza kujitokeza sasa kuliko wale ambao aliishashindana nao huko nyuma. Majina ya akina John Samwel Malecela, Frederick Sumaye, Profesa Mark Mwandosya, Cleopa Msuya, Benjamen Mkapa, Jaji mstaafu Mark Bomani, Salim Ahmed Salim na mengineyo ni majina makubwa. Alishindana nao na akawashinda.

- Hapa anajaribu kuficha fear zake, vipi lini Kikwete aliwahi kugombea urais na Lowassa, ambaye ndiye hasa tatizo lake sasa au anafikiri hatujui, kwa sababu kama kungekwua hakuna a threat ndani ya CCM, basi Kikwete angekwenda Denmark na asingepoteza muda wake kuwajibu Butiku na Lowassa, na huyu muandishi pia asingepoteza muda kujibu Mwanakijiji huku JF,

- Haya majibu maana yake ni moja tu, kwamba sasa JF tumeanza kuwatesa tena huko Magogoni kama zamani, sasa JF tuzidishe mashambulizi tu hakuna suluhu, either waondoke wawaaachie wengine au wajirekebishe!

Kikwete kugombea Urais siyo kwa maslahi ya wapambe, kuna mambo makubwa zaidi ya wapambe ambayo yanamfanya mtu agombee nafasi kuu ya Urais. Tamaa ya mtu katika nafsi yake kutaka kugombea uongozi ni kwamba ana uwezo fulani na anataka atekeleze mambo fulani nje ya nafsi yake. Wako watu wengi katika uwanja wa siasa ambao hawafikii hatua hiyo.
- Ona sasa, sheria ya jamhuri yetu inasema hivi Rais apewe miaka mitano kutimiza hiyo tamaa yake ya kutaka kutekeleza mambo flani na baada ya hapo wananchi waaamue kama amefanikiwa au hapana, sasa Kikwete tulimpa saa imefika sasa ya sisi wanachi kutoa maoni yetu kulingana na facts at hand za uongozi wake in five years, Mwanakijiji ametoa sababu 51 kwamba kwa nini Rais wa sasa ameshindwa, sasa ulikuwa ni wajibu wa aliyejibu kutoa sababu 51 kwamba kwa nini Rais wa hakushindwa,lakini kumshambulia Mwanakijiji kwamba hana uwezo wa kuchambua mambo ya uongozi na siasa, huku wamekimbia mbio hapa kumjibu sounds like sour losers!

Ukweli wa mambo ni kwamba tangu achukue madaraka 2005, mambo mengi yamekuwa yanafanyika hapa nchini. Miradi imekuwa inatekelezwa na serikali watu katika sekta binafsi, mashirika makubwa ya kimataifa na mashirika ya kidini. Kusema kwamba wanaotaka Kikwete agombee ni wale ambao wanakariri kikasuku msemo wa "kuendeleza umoja, utulivu, amani na mshikamano" wa nchi yetu, ni fikra za mtu ambaye akili yake imedumaa na kukwama kutokana na kutotaka kujifunza mabadiliko yanavyotokea katika mazingira na nani analeta mabadiliko hayo.

- Sijawahi kuona pumba kiasi hiki katika maisha yangu yote ya siasa, I mean watu katika sekta binafsi, mashirika makubwa ya kimatafia, na mashirika ya dini ndiye yaliyomchagua Rais wetu, sasa hapa muandishi anatuambia mwenyewe kwamba ni kwa nini Rais wetu ameshindwa kazi, kumbe hawa ndio anaojaribu kuwa-please, badala ya kulinda sheria za jamhuri na hasa sisi wanachi tuliomchagua?

Kwa upande mwingine dhana ya utulivu wa kisiasa (political stability) imepitwa na wakati. Wanataaluma na watunga sera, sasa hivi wanazungumzia utulivu utokanao na mkusanyiko wa sababu mbalimbali za maendeleo katika sekta za uchumi na ustawi wa jamii (structural stability). Kwamba watu hawali maneno matupu na nadharia za siasa.

Utulivu kimfumo una nafasi kubwa kutokana na sekta mbalimbali kutegemeana ili kuleta maendeleo yenye ulinganifu, hivyo ni wazi kwamba sera zote zinazotungwa na miradi inayotekelezwa inakuwa imepangwa kimtambuka kiasi kwamba yanayotokea sekta moja yanaathiri maendeleo yatakavyokuwa katika sekta nyingine.

- Maskini ya Mungu anakataa na kukubali yale yale, sekta ya sheria imemshinda Rais wa sasa, sasa anashindwa vipi kuelewa kwamba ndio sababu hasa ya msingi kwa sekta zingine kukwama Tanzania katika miaka mitano ya urais wa Kikwete?

Kwa namna moja au nyingine watanzania walio wengi katika sekta mbalimbali wanaguswa na kufikiwa na miradi ya maendeleo ya kubadilisha maisha yao . Yawezekana kwamba kasi ya maendeleo inazidiana. Lakini kwa namna moja au nyingine kuna mabadiliko ya msingi kule wanapoishi watu.

Watu wasioelewa hali inavyobadilika wanakuwa wa kwanza kupiga mayowe jinsi serikali ilivyoshindwa kuwaletea watu maendeleo, bila kutambua ukweli wa mambo kwamba watu wenyewe ndiyo watajiletea maendeleo na kazi hiyo ndiyo wameshaianza. Kwa waandishi wapiga ramli, kwa sababu wanataka kuonyesha msimamo wao wa "kupinga kila kisemwacho au kufanywa na hasimu wao", wanakuwa na watu wao ambao wanawaumba na kuwatengenezea mazingira.Wanapoanzia siyo kuonyesha uwezo wa kiongozi wao wa kufikirika bali ni kubuni na kuzua mambo, na kujaribu kugeuza mkondo wa maji utoke ziwani na kupanda mlima. Kwa hili la Kikwete kugombea 2010 tunasema binadamu ana uwezo mkubwa, lakini hawezi kuzuia jua kuchwa!

- Muandishi mwenyewe hana uhakika na anayoyasema, anasema "inawezekana" ni kwa sababu anajua kuwa haiwezekani, I mean ukisoma Bibilia kuna kifungu Mungu anasema "ikiwezekana ishi kwa amani na kila binadam", unajua ni kwa nini anasema "ikiwezekana?" ni kwa sababu anajua kwua haiwezekani,

- Halafu another point, muandishi anasema binadam hawezi kuzuia jua, meaning kwamba anakubali kwamba anayemtetea ana problems kama zlivyosema Mwanakijiji, lakini anashindwa kukubali kwamba Rais hakulazimishwa kuwa Rais, aligombea mwenyewe na kutuahidi kwamba anaweza kazi kuliko wengine wote walioogombea, sasa ya kushindwa kuzuia jua yametoka wapi? Eti ni wapi katiba yetu inasema Rais lazima azuie jua? Pumba tupu!

- Katiba yetu inasema Rais ndiye The Chief Law Enforcer, moja ya kazi zake za kila siku katika miaka mitano ni kulinda kwa nguvu zake zote tulizompa kisheria, katiba na sheria za jamhuri, lakini bado ameshindwa sasa tutampaje task ya kuzuia jua kama ameshindwa kulinda sheria tu, kwa sababu sisi tulijua kwamba kwa nguvu zake za kibnadam hawezi kulinda sheria zetu, tukampa nguvu zaidi za kisheria yeye ni kujali facts na kusema tu, hawezi ameshindwa sasa itakua ya jua?

Katika jamii inayokua kwa misingi ya kidemokrasi wapiga kura na raia kwa ujumla wana nafasi yao katika mchakato wa siasa, uchumi na maendeleo ya jamii. Nchi inaweza ikawa katika matatizo makubwa ya kiuchumi lakini hakuna matukio ya uvunjivu wa sheria wa makusudi kutoka kwa watu wengi.
- Ndio ninasema huyu muandishi ni kichaka sana, yaani mtupu kabisaa look anasema kwamba katika jamii wananchi wana nafasi yao kisiasa katika mchakato kama huu unaokuja wa Rais, lakini ana tatizo na mawazo ya Mwanakijiji ambayo yanatakliwa kuwepo kwenye hiyo hiyo nafasi anayoisema kwenye jamii kuhusu wananchi kuwa nafasi yao, and then anasema hakuna uvunjifu wa sheria, I mean kama Mwanakijiji mwananchi ana nafasi katika jamii katika mchakato wa siasa, then kwa nini muandishi ana tatizo na mawazo ya Mwanakijiji kuhusu kushindwa kwa Rais wa sasa kama alivyotoa sababu 51?

Tanzania ilipitia vipindi vigumu ambapo uchumi wa nchi ulikuwa mbaya. Hakuna fujo zilizotokea ambao zilitishia usalama wa watu na mali zao.
Kuna sababu 102 ambazo tunaona kwa nini Rais Kikwete agombee Urais 2010. Tutazitolea maelezo machache baadhi ya sababu kila panapokuwa haja.

Tunaanza na sababu 3:

Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele wa kutaka kuwepo utawala wa sheria. Utawala wa sheria ndiyo msigi mkuu wa utawala wa kidemokrasia, Tanzania ni nchi mojawapo miongoni mwa nchi changa kuwa na asasi zenye mamlaka zinazofanya kazi kwa uhuru kamili.

Hivi sasa ni wazi kwamba nchini Tanzania hakuna mtu anayekuwa juu ya sheria; awe ni raia wa kawaida, kiongozi mkuu serikalini au watendaji wakuu waandamizi. Matukio ya kutaka sheria ichukue mkondo, yako wazi na sasa tunaweza kusema sheria inatawala na watu wanaongoza. Tanzania haitumii utawala kwa sheria.

- Pumba zaidi, Tanzania tayari wananchi wamekufa kwa kutaka mabadiliko kule Pemba na huku Mwembechai wakapigwa sana na polisi, halafu kama Rais wa sasa anajali sheria, then mafisadi wametokea wapi?

- I mean haoni hata aibu kwamba Rostam, Lowassa, Karamagi, kwamba hawa wako juu ya sheria na yes Tanzania hatutumii utawala wa kisheria kwa sababu Rais wa sasa anawaogopa marafiki zake ambao ndio hasa wavunja sheria!

Rais Kikwete anajali mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mikuu mitatu

Sasa hivi mgawanyo wa madaraka kati ya utawala wa dola, mabaraza ya utungaji sheria na Mahakama uko wazi
. Kila mhimili una eneo lake na mipaka yake utawala wa dola unafanya kazi ya utendaji katika mfumo wa dola. Utumishi wa umma, majeshi ya ulinzi na usalama na srikali za mitaa zote ni asasi za mamlaka. Uhuru wa Mahakama ni jambo lisilo la kubishaniwa. Tangu miaka ya 1960 bunge la Tanzania limekuwa linajaribu kuwa muhimili usiothibitiwa. Sasa hivi hilo limewezekana kutokana na Rais Kikwete kujali na kutaka kila mhimili uwe huru kufanya mambo yake na yote kwa maslahi ya taifa.

Rais Kikwete anajali na kutambua ulazima wa utawala bora kwa maendeleo ya taifa Utawala bora ni dhana mpya ambayo imebuniwa katika jitihada za dola kukabiliana na hali mpya inayotokana na matakwa mapya kadri mazingira ndani na nje ya jamii yanavyokuwa na matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi. Utawala bora una maana ya ushirikishwaji wa wadau na dola kuwa chombo cha kuelekeza matumizi ya raslimali. Na hivyo utawala (bora) ni pamoja na njia zilizo bora za kudhibiti na kuratibu shughuli zinazolenga kuwapa watu uhuru zaidi na uwezo wa kuthibiti mazingira.

Rais Kikwete anathamini mashauriano kati ya wadau juu ya utungaji sera Rais Kikwete anajali usawa wa kijinsia.

Ametunza lengo la kuendeleza sera za kuvutia wawekezaji

Amekubali ushauri wa kufanya mabadiliko katika sera na sheria za madini (kuleta ulinganifu)

Ni kiongozi anayekubali ushauri katika miswada ya serikali inayopelekwa bungeni

Ni kiongozi mwenye kuwa na ubunifu katika utungaji sera za maendeleo mfano mzuri ukiwa ni sera ya Kilimo Kwanza.
- Yaaani nimeishiwa nguvu na huyu jamaa more pumba, kwa kweli inatia kinyaa, anasema Kikwete ni kiongozi anayekubali ushauri, lakini akishauriwa na kina Butiku na Quaresi, anadai wana chuki za binafsi! Kikwete tulikwambia mapema fukuza hawa washauri njaa, maana sio siri hawa wanaoandika hizi nonsense ndio washauri wako wakuu, pole sana mkuu uongozi ni maneno kwanza halafu vitendo,

- Tulijua yatakuja kuwafika shingoni tu, kuchafua watu, kuwalipa wabunge wasilze maswali kwenye bajeti zenu, kuwalipa wabunge wawachafue msiowataka, sasa yamewafika shingoni na bado, hapa wananchi tutaendelea tu kutumia haki yetu kusema ukweli bila ya kuogopa, uamuzi ni wenu msuke au mnyoe, meaning kwamba kama hamuwezi kama mnavyoonyesha tayari achieni ngazi, wananchi tumechoka sana ikibidi sasa hata shetani Lowassa na awe tu!

Respect.

FMEs!
 
Ingawa sikusoma hiyo article wa mwanakijiji, nina imani kuwa huyu alieandika article hii ni Kilaza mkubwa na anaonyesha kuwa ni mmoja wa wafuata upepo bila kuangalia kama upepo huo pia umebeba vumbi ndani yake. Sehemu kubwa ya article imejaa kejeli na madai ya kuwa wanomkosoa Kikwete wanamuonea wivu eti kwa sababu ya "kuukosa uraisi." Amenichosha zaidi kwa kudai kuwa watu hao ndio waliomuondoa Lowasa madarakanai na bado hawajatosheka; yaani anasahau kuwa Lowasa alijizuu mwenyewe baada ya kuona maji yamefika shingoni.

Upungufu mwingine ni kutangaza hapa kuwa katika CCM yote hakuna kiongozi mwingine aliye bora zaidi ya Kikwete: give me a break!!

"
Kuna kundi dogo la watu ambao wana nongwa ya kuukosa Urais 2005 na wengine ambao hawana uwezo wa kuchambua matukio, michakato na mienendo ya kisiasa na kijamii wanaendeshwa na kuamini katika hisia zao, ambazo zinawatuma kuandika vitu vya kubuni na alnacha.

Walipofanikiwa kumg'oa Edward Lowassa hawakuridhika.
Wamekuwa wakijidanganya kwamba wanaweza kutimiza ndoto yao ya kumng'oa na Kikwete na kuzika kizazi hicho cha uongozi. Katika Gazeti la Mwanahalisi, toleo Na. 167 Jumatano Desemba 16-22, 2009 makala ya M.M. Mwanakijiji (sababu 51 za kumkwamisha Kikwete) mwandishi anaonyesha alivyokosa cha kuandika, akalazimisha hoja na sababu kwa nini Rais Kikwete asigombee nafasi ya Urais mwaka 2010.

Kwanza kabisa hakuna mwanachama ndani ya CCM anayeweza kutaka kugombea na akawa tishio kwa Rais Kikwete. Kikwete alishapitia tanuru la moto mwaka 1995 na 2005.

Hakuna watu wenye nguvu na uwezo wa kila hali ambao wanaweza kujitokeza sasa kuliko wale ambao aliishashindana nao huko nyuma.
Majina ya akina John Samwel Malecela, Frederick Sumaye, Profesa Mark Mwandosya, Cleopa Msuya, Benjamen Mkapa, Jaji mstaafu Mark Bomani, Salim Ahmed Salim na mengineyo ni majina makubwa. Alishindana nao na akawashinda."
 
Hizi nyingine sio sumaku tunazojua zenye kunasa chuma, ni sumaku zinazikusanya upuuzi usio kifani na kutaka kutugawia ndani ya akili zetu
 
FMES,

I wanted to give the toe to toe Bluray tradition to this so called article, now that you killed it, there is no need to murder machete it.

That would be like beating the proverbial dead horse.

And unless somebody attempts something on the personal level (where not even beating a dead horse is enough), beating a dead horse is never the Bluray tradition. I mean it is just so not benevolent and so against the Geneva Convention. Plus Shakespeare and Mkwawa would not have approved.

Bado hawaja perfect hata rhetoric.
 
Wadau, mchomeko wa mada nyingine kwenye Taifa Tanzania inayohitaji kujadiliwa.

TUNAMJIBU M.M. MWANAKIJIJI:

Sababu 102 kwa nini Jakaya Kikwete agombee 2010 na aendelee kuongoza

MWANDISHI WETU

Wana CCM milioni 4 (kasoro Nungayembe wa kisiasa) na wapiga kura kwa mamilioni, wanatambua uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Hao waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu 2005, pamoja na wapiga kura wapya tuna hakika, hawajaona au hawategemei kuona mbadala kwa nafasi ambayo Kikwete anayoishikilia. Kwa nini tunaona hivyo?

Hali iliyopo kwa watu wanaofanya shughuli zao za kuzalisha mali na katika kujenga taifa inaridhisha tofauti na ramli za kutabiri mwisho wa dunia ya Tanzania yenye amani zinazopigwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Kuna kundi dogo la watu ambao wana nongwa ya kuukosa Urais 2005 na wengine ambao hawana uwezo wa kuchambua matukio, michakato na mienendo ya kisiasa na kijamii wanaendeshwa na kuamini katika hisia zao, ambazo zinawatuma kuandika vitu vya kubuni na alnacha.

Walipofanikiwa kumg’oa Edward Lowassa hawakuridhika. Wamekuwa wakijidanganya kwamba wanaweza kutimiza ndoto yao ya kumng’oa na Kikwete na kuzika kizazi hicho cha uongozi. Katika Gazeti la Mwanahalisi, toleo Na. 167 Jumatano Desemba 16-22, 2009 makala ya M.M. Mwanakijiji (sababu 51 za kumkwamisha Kikwete) mwandishi anaonyesha alivyokosa cha kuandika, akalazimisha hoja na sababu kwa nini Rais Kikwete asigombee nafasi ya Urais mwaka 2010.

Kwanza kabisa hakuna mwanachama ndani ya CCM anayeweza kutaka kugombea na akawa tishio kwa Rais Kikwete. Kikwete alishapitia tanuru la moto mwaka 1995 na 2005.

Hakuna watu wenye nguvu na uwezo wa kila hali ambao wanaweza kujitokeza sasa kuliko wale ambao aliishashindana nao huko nyuma. Majina ya akina John Samwel Malecela, Frederick Sumaye, Profesa Mark Mwandosya, Cleopa Msuya, Benjamen Mkapa, Jaji mstaafu Mark Bomani, Salim Ahmed Salim na mengineyo ni majina makubwa. Alishindana nao na akawashinda.

Kikwete kugombea Urais siyo kwa maslahi ya wapambe, kuna mambo makubwa zaidi ya wapambe ambayo yanamfanya mtu agombee nafasi kuu ya Urais. Tamaa ya mtu katika nafsi yake kutaka kugombea uongozi ni kwamba ana uwezo fulani na anataka atekeleze mambo fulani nje ya nafsi yake. Wako watu wengi katika uwanja wa siasa ambao hawafikii hatua hiyo.

Ukweli wa mambo ni kwamba tangu achukue madaraka 2005, mambo mengi yamekuwa yanafanyika hapa nchini. Miradi imekuwa inatekelezwa na serikali watu katika sekta binafsi, mashirika makubwa ya kimataifa na mashirika ya kidini. Kusema kwamba wanaotaka Kikwete agombee ni wale ambao wanakariri kikasuku msemo wa “kuendeleza umoja, utulivu, amani na mshikamano” wa nchi yetu, ni fikra za mtu ambaye akili yake imedumaa na kukwama kutokana na kutotaka kujifunza mabadiliko yanavyotokea katika mazingira na nani analeta mabadiliko hayo.

Kwa upande mwingine dhana ya utulivu wa kisiasa (political stability) imepitwa na wakati. Wanataaluma na watunga sera, sasa hivi wanazungumzia utulivu utokanao na mkusanyiko wa sababu mbalimbali za maendeleo katika sekta za uchumi na ustawi wa jamii (structural stability). Kwamba watu hawali maneno matupu na nadharia za siasa.

Utulivu kimfumo una nafasi kubwa kutokana na sekta mbalimbali kutegemeana ili kuleta maendeleo yenye ulinganifu, hivyo ni wazi kwamba sera zote zinazotungwa na miradi inayotekelezwa inakuwa imepangwa kimtambuka kiasi kwamba yanayotokea sekta moja yanaathiri maendeleo yatakavyokuwa katika sekta nyingine.

Kwa namna moja au nyingine watanzania walio wengi katika sekta mbalimbali wanaguswa na kufikiwa na miradi ya maendeleo ya kubadilisha maisha yao . Yawezekana kwamba kasi ya maendeleo inazidiana. Lakini kwa namna moja au nyingine kuna mabadiliko ya msingi kule wanapoishi watu.

Watu wasioelewa hali inavyobadilika wanakuwa wa kwanza kupiga mayowe jinsi serikali ilivyoshindwa kuwaletea watu maendeleo, bila kutambua ukweli wa mambo kwamba watu wenyewe ndiyo watajiletea maendeleo na kazi hiyo ndiyo wameshaianza. Kwa waandishi wapiga ramli, kwa sababu wanataka kuonyesha msimamo wao wa “kupinga kila kisemwacho au kufanywa na hasimu wao”, wanakuwa na watu wao ambao wanawaumba na kuwatengenezea mazingira.

Wanapoanzia siyo kuonyesha uwezo wa kiongozi wao wa kufikirika bali ni kubuni na kuzua mambo, na kujaribu kugeuza mkondo wa maji utoke ziwani na kupanda mlima. Kwa hili la Kikwete kugombea 2010 tunasema binadamu ana uwezo mkubwa, lakini hawezi kuzuia jua kuchwa!

Katika jamii inayokua kwa misingi ya kidemokrasi wapiga kura na raia kwa ujumla wana nafasi yao katika mchakato wa siasa, uchumi na maendeleo ya jamii. Nchi inaweza ikawa katika matatizo makubwa ya kiuchumi lakini hakuna matukio ya uvunjivu wa sheria wa makusudi kutoka kwa watu wengi. Tanzania ilipitia vipindi vigumu ambapo uchumi wa nchi ulikuwa mbaya. Hakuna fujo zilizotokea ambao zilitishia usalama wa watu na mali zao.
Kuna sababu 102 ambazo tunaona kwa nini Rais Kikwete agombee Urais 2010. Tutazitolea maelezo machache baadhi ya sababu kila panapokuwa haja.

Tunaanza na sababu 3:

Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele wa kutaka kuwepo utawala wa sheria. Utawala wa sheria ndiyo msigi mkuu wa utawala wa kidemokrasia, Tanzania ni nchi mojawapo miongoni mwa nchi changa kuwa na asasi zenye mamlaka zinazofanya kazi kwa uhuru kamili.

Hivi sasa ni wazi kwamba nchini Tanzania hakuna mtu anayekuwa juu ya sheria; awe ni raia wa kawaida, kiongozi mkuu serikalini au watendaji wakuu waandamizi. Matukio ya kutaka sheria ichukue mkondo, yako wazi na sasa tunaweza kusema sheria inatawala na watu wanaongoza. Tanzania haitumii utawala kwa sheria.

Rais Kikwete anajali mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mikuu mitatu

Sasa hivi mgawanyo wa madaraka kati ya utawala wa dola, mabaraza ya utungaji sheria na Mahakama uko wazi. Kila mhimili una eneo lake na mipaka yake utawala wa dola unafanya kazi ya utendaji katika mfumo wa dola. Utumishi wa umma, majeshi ya ulinzi na usalama na srikali za mitaa zote ni asasi za mamlaka. Uhuru wa Mahakama ni jambo lisilo la kubishaniwa. Tangu miaka ya 1960 bunge la Tanzania limekuwa linajaribu kuwa muhimili usiothibitiwa. Sasa hivi hilo limewezekana kutokana na Rais Kikwete kujali na kutaka kila mhimili uwe huru kufanya mambo yake na yote kwa maslahi ya taifa.

Rais Kikwete anajali na kutambua ulazima wa utawala bora kwa maendeleo ya taifa Utawala bora ni dhana mpya ambayo imebuniwa katika jitihada za dola kukabiliana na hali mpya inayotokana na matakwa mapya kadri mazingira ndani na nje ya jamii yanavyokuwa na matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi. Utawala bora una maana ya ushirikishwaji wa wadau na dola kuwa chombo cha kuelekeza matumizi ya raslimali. Na hivyo utawala (bora) ni pamoja na njia zilizo bora za kudhibiti na kuratibu shughuli zinazolenga kuwapa watu uhuru zaidi na uwezo wa kuthibiti mazingira.

Rais Kikwete anathamini mashauriano kati ya wadau juu ya utungaji sera Rais Kikwete anajali usawa wa kijinsia.

Ametunza lengo la kuendeleza sera za kuvutia wawekezaji

Amekubali ushauri wa kufanya mabadiliko katika sera na sheria za madini (kuleta ulinganifu)

Ni kiongozi anayekubali ushauri katika miswada ya serikali inayopelekwa bungeni

Ni kiongozi mwenye kuwa na ubunifu katika utungaji sera za maendeleo mfano mzuri ukiwa ni sera ya Kilimo Kwanza.

Source: TAIFA Tanzania , Desemba 18, 2009
( Mambo yamepamba moto. Nyingine hii nimeinasa kutoka mtandao wa kwanzajamii.com)

Sasa huyu Mwandishi ni nani mbona Mwanakijiji alijisema yeye anajificha nini si aseme tu na tumjue ?
 
Shkespeare na mkwawa???????
How is it so????????

Shakespeare na Mkwawa wote walikuwa wana observe The Geneva Convention hata kabla haijawa ratified.Strict honor code, kamikaze style. I draw from them, Shakespeare as a literary scribe and Mkwawa as a warrior chief.
 
Sasa huyu Mwandishi ni nani mbona Mwanakijiji alijisema yeye anajificha nini si aseme tu na tumjue ?

- Unajua mkuu haya ndio hasa masilahi ya taifa, hawa Mtandao wamefikwa na maji shingoni sasa wanajaribu kama kawaida kulaumu kila mtu badala ya kubeba msalaba, zile rushwa sasa zinawatokea puani kwenye kutafuta urais walifika mahali hata walikuwa wanawalipa wabunge ili wamshambulie bajeti ya Mwandosya, lakini wasiulize maswali kwenye bajeti ya nje! Bwa! ha! ha!

- Kuna siku walimlipa mbunge mmoja njaa anaitwa Nyami, ili amchafue balozi wetu London then ambaye walikuwa na tatizo naye sana, Mbunge Nyami akadai bungeni kuwa yule balozi anaringa sana, uchunguzi kufanyika kumbe huyu Mbunge hajawahi hata kufika London, sasa akaulizwa bungeni kule kwamba alijuaje mambo ya ubalozi wa London ambako hajwahi kufika? Wakafuta hoja!

- Ndio maana ninasema haya mengine tuliyataka wenyewe, I mean hakukuwa na a serious scrutiny kabisaa, tukawaachia hawa Mtandao wakashika nchi kwa visingizio vya Vijana, sasa tizama walipolifikisha taifa! Kiongozi wao akishauriwa anadai anaonewa wivu na chuki binafsi, halafu washauri wake ndio hawa watupu kabisaaa vichwani hata kusema majina yao wanaogopa, dawa ni kuendelea kuwatwanga tu na kwa sababu wanajibu maana yake ni moja tu kwamba kumbe message sasa inafika, saafi sana!

- Ni kupiga mawe tu mpaka kieleweke!

Respect.

FMEs!
 
Back
Top Bottom