Wadau, mchomeko wa mada nyingine kwenye Taifa Tanzania inayohitaji kujadiliwa.
TUNAMJIBU M.M. MWANAKIJIJI:
Sababu 102 kwa nini Jakaya Kikwete agombee 2010 na aendelee kuongoza
MWANDISHI WETU
Wana CCM milioni 4 (kasoro Nungayembe wa kisiasa) na wapiga kura kwa mamilioni, wanatambua uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Hao waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu 2005, pamoja na wapiga kura wapya tuna hakika, hawajaona au hawategemei kuona mbadala kwa nafasi ambayo Kikwete anayoishikilia. Kwa nini tunaona hivyo?
Hali iliyopo kwa watu wanaofanya shughuli zao za kuzalisha mali na katika kujenga taifa inaridhisha tofauti na ramli za kutabiri mwisho wa dunia ya Tanzania yenye amani zinazopigwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Kuna kundi dogo la watu ambao wana nongwa ya kuukosa Urais 2005 na wengine ambao hawana uwezo wa kuchambua matukio, michakato na mienendo ya kisiasa na kijamii wanaendeshwa na kuamini katika hisia zao, ambazo zinawatuma kuandika vitu vya kubuni na alnacha.
Walipofanikiwa kumgoa Edward Lowassa hawakuridhika. Wamekuwa wakijidanganya kwamba wanaweza kutimiza ndoto yao ya kumngoa na Kikwete na kuzika kizazi hicho cha uongozi. Katika Gazeti la Mwanahalisi, toleo Na. 167 Jumatano Desemba 16-22, 2009 makala ya M.M. Mwanakijiji (sababu 51 za kumkwamisha Kikwete) mwandishi anaonyesha alivyokosa cha kuandika, akalazimisha hoja na sababu kwa nini Rais Kikwete asigombee nafasi ya Urais mwaka 2010.
Kwanza kabisa hakuna mwanachama ndani ya CCM anayeweza kutaka kugombea na akawa tishio kwa Rais Kikwete. Kikwete alishapitia tanuru la moto mwaka 1995 na 2005.
Hakuna watu wenye nguvu na uwezo wa kila hali ambao wanaweza kujitokeza sasa kuliko wale ambao aliishashindana nao huko nyuma. Majina ya akina John Samwel Malecela, Frederick Sumaye, Profesa Mark Mwandosya, Cleopa Msuya, Benjamen Mkapa, Jaji mstaafu Mark Bomani, Salim Ahmed Salim na mengineyo ni majina makubwa. Alishindana nao na akawashinda.
Kikwete kugombea Urais siyo kwa maslahi ya wapambe, kuna mambo makubwa zaidi ya wapambe ambayo yanamfanya mtu agombee nafasi kuu ya Urais. Tamaa ya mtu katika nafsi yake kutaka kugombea uongozi ni kwamba ana uwezo fulani na anataka atekeleze mambo fulani nje ya nafsi yake. Wako watu wengi katika uwanja wa siasa ambao hawafikii hatua hiyo.
Ukweli wa mambo ni kwamba tangu achukue madaraka 2005, mambo mengi yamekuwa yanafanyika hapa nchini. Miradi imekuwa inatekelezwa na serikali watu katika sekta binafsi, mashirika makubwa ya kimataifa na mashirika ya kidini. Kusema kwamba wanaotaka Kikwete agombee ni wale ambao wanakariri kikasuku msemo wa kuendeleza umoja, utulivu, amani na mshikamano wa nchi yetu, ni fikra za mtu ambaye akili yake imedumaa na kukwama kutokana na kutotaka kujifunza mabadiliko yanavyotokea katika mazingira na nani analeta mabadiliko hayo.
Kwa upande mwingine dhana ya utulivu wa kisiasa (political stability) imepitwa na wakati. Wanataaluma na watunga sera, sasa hivi wanazungumzia utulivu utokanao na mkusanyiko wa sababu mbalimbali za maendeleo katika sekta za uchumi na ustawi wa jamii (structural stability). Kwamba watu hawali maneno matupu na nadharia za siasa.
Utulivu kimfumo una nafasi kubwa kutokana na sekta mbalimbali kutegemeana ili kuleta maendeleo yenye ulinganifu, hivyo ni wazi kwamba sera zote zinazotungwa na miradi inayotekelezwa inakuwa imepangwa kimtambuka kiasi kwamba yanayotokea sekta moja yanaathiri maendeleo yatakavyokuwa katika sekta nyingine.
Kwa namna moja au nyingine watanzania walio wengi katika sekta mbalimbali wanaguswa na kufikiwa na miradi ya maendeleo ya kubadilisha maisha yao . Yawezekana kwamba kasi ya maendeleo inazidiana. Lakini kwa namna moja au nyingine kuna mabadiliko ya msingi kule wanapoishi watu.
Watu wasioelewa hali inavyobadilika wanakuwa wa kwanza kupiga mayowe jinsi serikali ilivyoshindwa kuwaletea watu maendeleo, bila kutambua ukweli wa mambo kwamba watu wenyewe ndiyo watajiletea maendeleo na kazi hiyo ndiyo wameshaianza. Kwa waandishi wapiga ramli, kwa sababu wanataka kuonyesha msimamo wao wa kupinga kila kisemwacho au kufanywa na hasimu wao, wanakuwa na watu wao ambao wanawaumba na kuwatengenezea mazingira.
Wanapoanzia siyo kuonyesha uwezo wa kiongozi wao wa kufikirika bali ni kubuni na kuzua mambo, na kujaribu kugeuza mkondo wa maji utoke ziwani na kupanda mlima. Kwa hili la Kikwete kugombea 2010 tunasema binadamu ana uwezo mkubwa, lakini hawezi kuzuia jua kuchwa!
Katika jamii inayokua kwa misingi ya kidemokrasi wapiga kura na raia kwa ujumla wana nafasi yao katika mchakato wa siasa, uchumi na maendeleo ya jamii. Nchi inaweza ikawa katika matatizo makubwa ya kiuchumi lakini hakuna matukio ya uvunjivu wa sheria wa makusudi kutoka kwa watu wengi. Tanzania ilipitia vipindi vigumu ambapo uchumi wa nchi ulikuwa mbaya. Hakuna fujo zilizotokea ambao zilitishia usalama wa watu na mali zao.
Kuna sababu 102 ambazo tunaona kwa nini Rais Kikwete agombee Urais 2010. Tutazitolea maelezo machache baadhi ya sababu kila panapokuwa haja.
Tunaanza na sababu 3:
Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele wa kutaka kuwepo utawala wa sheria. Utawala wa sheria ndiyo msigi mkuu wa utawala wa kidemokrasia, Tanzania ni nchi mojawapo miongoni mwa nchi changa kuwa na asasi zenye mamlaka zinazofanya kazi kwa uhuru kamili.
Hivi sasa ni wazi kwamba nchini Tanzania hakuna mtu anayekuwa juu ya sheria; awe ni raia wa kawaida, kiongozi mkuu serikalini au watendaji wakuu waandamizi. Matukio ya kutaka sheria ichukue mkondo, yako wazi na sasa tunaweza kusema sheria inatawala na watu wanaongoza. Tanzania haitumii utawala kwa sheria.
Rais Kikwete anajali mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mikuu mitatu
Sasa hivi mgawanyo wa madaraka kati ya utawala wa dola, mabaraza ya utungaji sheria na Mahakama uko wazi. Kila mhimili una eneo lake na mipaka yake utawala wa dola unafanya kazi ya utendaji katika mfumo wa dola. Utumishi wa umma, majeshi ya ulinzi na usalama na srikali za mitaa zote ni asasi za mamlaka. Uhuru wa Mahakama ni jambo lisilo la kubishaniwa. Tangu miaka ya 1960 bunge la Tanzania limekuwa linajaribu kuwa muhimili usiothibitiwa. Sasa hivi hilo limewezekana kutokana na Rais Kikwete kujali na kutaka kila mhimili uwe huru kufanya mambo yake na yote kwa maslahi ya taifa.
Rais Kikwete anajali na kutambua ulazima wa utawala bora kwa maendeleo ya taifa Utawala bora ni dhana mpya ambayo imebuniwa katika jitihada za dola kukabiliana na hali mpya inayotokana na matakwa mapya kadri mazingira ndani na nje ya jamii yanavyokuwa na matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi. Utawala bora una maana ya ushirikishwaji wa wadau na dola kuwa chombo cha kuelekeza matumizi ya raslimali. Na hivyo utawala (bora) ni pamoja na njia zilizo bora za kudhibiti na kuratibu shughuli zinazolenga kuwapa watu uhuru zaidi na uwezo wa kuthibiti mazingira.
Rais Kikwete anathamini mashauriano kati ya wadau juu ya utungaji sera Rais Kikwete anajali usawa wa kijinsia.
Ametunza lengo la kuendeleza sera za kuvutia wawekezaji
Amekubali ushauri wa kufanya mabadiliko katika sera na sheria za madini (kuleta ulinganifu)
Ni kiongozi anayekubali ushauri katika miswada ya serikali inayopelekwa bungeni
Ni kiongozi mwenye kuwa na ubunifu katika utungaji sera za maendeleo mfano mzuri ukiwa ni sera ya Kilimo Kwanza.
Source: TAIFA Tanzania , Desemba 18, 2009
( Mambo yamepamba moto. Nyingine hii nimeinasa kutoka mtandao wa kwanzajamii.com)