Taifa Stars yalala moja nunge na JK akosa mtaji wa kisiasa katika kampeni

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Baada ya Ng'wanangwa kupost uzi wenye kichwa cha habari: "Kikwete Mgeni rasmi? Taifa stars itarajie kichapo", baadhi ya watu walichukia na kuanza kushabikia kuwa Ng'wanangwa awe banned kwa hoja kwamba anaendekeza udini (lakini watu wenyewe walikuwa wanaficha hoja iliyokuwa mioyoni mwao).

Stars imekalia kichapo. Je, Mods muta-lift ban ya Ng'wanangwa???
 
bora unyimwe mali kuliko akili,eti leo jk kuwa mgeni rasmi kwenye mechi ya stara na moroco iliandaliwa makusudi kama jukwaa la kampeni na kama stars ingeshinda angezungushwa uwanla mzima,
 
Ingependeza sana kama Stars ungeshinda ili Mh. JK awapungie washabiki!!!!!! Nadhani kwa kufungwa mission ya kuwepo pale haikufauli
 
Baada ya Taifa Stars kutoka sare kule Morocco, JK na wapambe wake walitegemea nyumbani mambo kuwaendea vizuri na alijidamka mwenyewe kwenda uwanjani kwa matarajio kama Stars wangelishinda basi wapenzi wa soka wangelimkumbuka kwa kufanikisha soka.

Lakini kuhudhuria kwake JK yaelekea ulikuwa ni mkosi kwa Stars kwani hata ile ya sare waliyoipata ugenini walishindwa kuilinda na matokeo yake wamelala bao moja bila ya majibu.


Jitihada za JK kuona maendeleo ya soka yataletwa kutoka juu badala ya kuviimarisha vilabu kwa ruzuku tosheleza sasa ni mzigo mkubwa kwake kisiasa kwa sababu wanamichezo wamechoka kuona Tanzania bado yaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu.

Mbaya zaidi kwa JK, mipango yake ya kuiendeleza soka haijawahi kutafuta maoni ya wapenzi wa soka na hivyo kubashiria ya kuwa kutowashirikisha wadau wa mchezo huo ni sababu kubwa ya mabilioni yaliyotumbukizwa kuinua soka kupotea bure.

Dr. Slaa ameahidi kuvipa ruzuku vilabu vya mpira na kuvishirikisha katika kuweka program ya kuendeleza michezo yote. Hii ndiyo itakuwa muarobaini wa sisi kuacha kuishia kuwa wasindikizaji kama CCM itakavyokuwa msindikizaji katika uchaguzi huu.

 
bora unyimwe mali kuliko akili,eti leo jk kuwa mgeni rasmi kwenye mechi ya stara na moroco iliandaliwa makusudi kama jukwaa la kampeni na kama stars ingeshinda angezungushwa uwanla mzima,

we unaeletewa kiongozi anaongozwa na majini unatarajia nini ?????
 
Yep mtani wangu Junius,

Litimu la Kikwete limefungwa leo. Wangelivaa kabisa Kijani na njano ndiyo ingelinoga zaidi.

Kikwete atakuwa kafurahi maana goli hilo moja litaonyeshwa dunia nzima. Mbaya kama tungelitoka Sare.
 
Na hii ndo mechi ya mwisho yeye kama rais, nirudie tena nililosema nilipomwona kikwete akiingia {via ss3 and four} niliwaambia jamaa tulokuwa kunacheki nao, tumeumia leo. kama sikosei hatujawahi kushinda Kiwete akiwa mgeni rasmi!
 
Na hii ndo mechi ya mwisho yeye kama rais, nirudie tena nililosema nilipomwona kikwete akiingia {via ss3 and four} niliwaambia jamaa tulokuwa kunacheki nao, tumeumia leo. kama sikosei hatujawahi kushinda Kiwete akiwa mgeni rasmi!

ulijuaje ulikuwa pemben yangu nini mi nilisema hivyo nikaoona mijaamaa inaniangali aikuchukua dk 5 jamaa wanafunga nikaama na kiti nikasema hii miusalama nini isije nipa kazi ya ziada weekend na si unajua ukiingia mpaka jumatatu labdatuliemtaja atutoe kwa msamaha
 
Ama kweli chuki za kisiasa zinaongeza munkari hata pahali ambapo hapahitaji siasa.

Hivi leo tena hiyo taifa stars kufungwa imekuwa JK, kwani mara ngapi imefungwa???????

Mimi sio shabiki wa siasa lakini hii naona toooooooo much!
 
Back
Top Bottom