Taifa Stars Vs Sudan live updates & Results

Mpira umekwisha! 3-1 refa katubania sana kakataa goli 2 zetu ilikuwa tuwafunge 5 wamanga hawa!

Ebwana sasa naweza kupumzika maana hapatoshi. Anyway, binafsi nakupa big up sana maan umeweza kunisaidia mpaka nikafahamu nini kinaendelea huko home tena LIVE.
Thanks Masatu kwa kutuweka live japo tupo mbalia.
 
Bado kumalizia kazi ndogo tu kule Khartoum baada ya hapo mwezi Februari mwakani tupo kwenye Luninga kule Abidjan, cant wait....
 
Mkuu Mbalawata mimi nilikuwa critic mkubwa sana wa Maximo nakubali I was wrong mpira tuliocheza leo ni mkubwa sana tunatisha mazee. Bring on Brazil!
 
Mpira umekwisha! 3-1 refa katubania sana kakataa goli 2 zetu ilikuwa tuwafunge 5 wamanga hawa!

Asante kwa updates mkuu Masatu, sasa naweza kuanza kugonganisha glasi kwa kwenda mbele, niendelee na weekend.
 
Magoli ya Stars yamefungwa na Athumani Idd (Chuji) Jerisson Tegete ( Jerry ) na Kigi Makassi, sadly wote ni wachezaji wa Kandambili Yanga lakini poa tu tunashangilia ushindi.....

We Masatu behave yourself! yanga ndiyo team ya Taifa.
 
TIMU ya soka ya Tanzania, Taifa Stars jioni hii iliikandamiza Sudan ‘Mwewe wa Jangwani’ kwa mabao 3-1 katika mechi ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani (CHAN).

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam, Stars iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 20 lililofungwa kwa shuti kali na Jerry Tegete baada ya kuinasa pasi ya Mrisho Ngassa.

Hata hivyo furaha ya mashabiki wa Stars ilizimwa ndani ya dakika mbili tu baada ya kupata bao la kuongoza, baada ya Badreldin Eldod kupiga kona iliyotua kichwani kwa Seifdin Ali Idrisa aliyezitingisha nyavu za Stars na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.

Stars iliandika bao la pili katika dakika ya 60 mfungaji akiwa ni Athuman Idd ‘Chuji’. Juhudi za Stars zilizoandamana na pasi safi za uhakika zaidi ya 15 ziliiwezesha kuandika bao la tatu lililofungwa na Kiggi Makassy.

Habari kamili na vikosi vya timu gonga link hii NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
From Gazeti la Mwananchi


Safari ya Stars Ivory Coast yanukia baada ya kuikung'uta Sudan 3-1
Na Oliver Albert

NI raha, raha tupu. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya ushindi mzuri wa Taifa Stars wa mabao 3-1 dhidi ya Sudan katika mchezo uliofanyika jana kwenye Uwanja Mkuu wa Tanzania.


Ushindi huo umeifanya Tanzania kujiweka pazuri kwa mchezo wa marudiano na kuanza kupigia mahesabu safari ya Ivory Coast kwenye fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani, CHAN, Julai mwakani.


Stars sasa inahitaji sare ya aina yoyote iweze kukata tiketi ya fainali katika mchezo wa marudiano utakaofanyika kati ya Desemba 13 na 15.


Katika mchezo huo ambao Stars walianza kwa mashambulizi tangu dakika ya kwanza baada ya Athumani Idd kupaisha mpira akimwangalia kipa wa Sudan Akram Elhad.


Stars wakionekana kutulia na kupanga mashambulizi ya kushitukiza waliliandama lango dakika tano za kwanza lakini Jerry Tegete mara zote hakuwa makini.


Katika dakika ya 12, nusura Haruna Moshi 'Boban' aipatie Stars bao baada ya kupiga shuti kali na kipa wa Sudan, Elhad kulipangua.


Kadri muda ulivyokuwa unakwenda ndivyo Stars ilivyozidisha mashambulizi langoni mwa Sudan na kufanikiwa kuandika bao la kwanza katika dakika ya 25 lililofungwa na Tegete baada ya kazi ya Mrisho Ngasa aliyewatoka mabeki watatu wa Sudan na kutoa pasi kwa mfungaji.


Stars waliokuwa wakishangiliwa uwanja mzima huku wakiwa na uhakika wa kupata Sh1milioni kila mchezaji kutoka kwa wadhamini, Kampuni ya Bia ya Serengeti, SBL, walicheza kwa nguvu huku kila mmoja kuonekana kujituma vilivyo.


Hata hivyo, Sudan walichafua gazeti baada ya kusawazisha bao dakika 27 kupitia kwa Saifeldin Ali Idris.


Kipindi cha pili, Stars ilibadilika hasa katika kiungo na kukamata kila idara ya Wanubi hao na katika dakika ya 59, Athuman Idd 'Chuji' ambaye katika mchezo huo hakuwa katika kiwango chake aliipatia Stars bao la pili kwa shuti la umbali wa mita 40 na kuamsha hoi hoi na nderemo kwa mashabiki.


Kigi Makasy ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Henry Joseph ambaye aliumia mguu aliifungia Stars bao la tatu dakika ya 67 kilaini akipokea pasi ya Tegete hivyo kumuacha kipa wa Sudan akishindwa la kufanya.


Licha ya Sudan kutaka kusawazisha mabao yao ilishindwa kutokana na umakini wa mabeki wa Stars wakiongozwa na Salum Sued na kipa Shaaban Dihile ambaye ni mechi yake ya pili ya kimataifa kuidakia Stars.


Sudan walipata pigo dakika ya 90 ya mchezo baada ya kipa wao Elhad kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi Mnkant Ntaban kutoka Zimbabwe baada ya kumkata mtama Ngassa aliyempiga chenga na kuelekea kufunga bao la nne.


Kocha mkuu wa Stars, Marcio Maximo aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo, lakini akasema bado wana kazi ngumu kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki mbili zijazo nchini Sudan.


" Timu imecheza vizuri hasa wachezaji wangu vijana, tunafurahia ushindi lakini lazima tutambue kuwa tuna kazi bado tena mara mbili tukifika kwao, kwani Sudan ni timu nzuri yenye uzoefu mkubwa na ngumu kufungika kwao lakini tutapambana," alisema Maximo.


Naye kocha wa Sudan Mohamed Abdallah aliwasifu Stars kwa mchezo mzuri waliouonyesha lakini akaahidi kushinda mabao 2-0 mchezo wa marudiano mjini Khartoum.


Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko safarini Doha, Qatar, ametuma salaam za pongezi kwa vijana wake kutokana na ushindi huo.
 
Check live update hapa JF


Wapi hapo mkuu......au mazingaombwe haya...maana nimeikodolea macho posti yako kwa dakika kadhaa sioni kitu. Kuwa muwazi zaidi mkuu....


Kuwa na subra basi....


Link ni uwanja mkuu wa taifa na sioni peke yangu tupo over 50,000 humu ndani.....


Magoli ya Stars yamefungwa na Athumani Idd (Chuji) Jerisson Tegete ( Jerry ) na Kigi Makassi, sadly wote ni wachezaji wa Kandambili Yanga lakini poa tu tunashangilia ushindi.....


Masatu huyo akiwa kwenye anga zake. Bado anakumbuka kandambili na raizon
 
Hosts Taifa Stars clobbered their chest-thumping guests, Sokoor Al-Jediane (Desert Hawks) of Sudan 3-1 at the National Stadium in Dar es Salaam yesterday.

The victory puts the home boys in a good position as they battle for honours in the 2009 African Cup of Nations tournament. The tournament features only home-based players.

The first goal was slotted into the Hawks` net by Jerry Tegete, in a spectacular tactic in the 26th minute, which left the guests utterly confused.

The Stars� joy as well as that of their cheering supporters was however short-lived, as the Hawks equalised two minutes later through a hat trick by Salfeldin Alildris.

The encounter was billed as the final before the real final, although both teams had polished up on their defects. Stars have scraped through to this stage with performances well below their capabilities.

Although both teams were given chances to perform well, it is Stars which, was highly expected to win the match after they were promised a Sh30million reward by NMB.

But in the 58th and 66th minute goals by Athumani Iddi`s and Kigi Makassy respectively, proved that the home side had all the advantage it needed to show its might against the Sudanese, who despite their country being war torn, have proved to be a football giant in the sub-Saharan region.

They will play a return match in Khartoum in a match which will automatically decide who qualifies for the tournament next year.

Taifa Stars are still the favourites for the championship in their group after their composure and all-round talents were emphatically successful in knocking Kenya and Uganda from the preliminary matches mid this year.

With just two weeks before their final encounter, the Stars will be hard-pressed to adjust for a win to sail through to the next phase, recovering from the gruelling series of losing most of its international encounters.

The second leg matches have been scheduled for the weekend of December 12 to 14 with the winners joining hosts Ivory Coast for the finals fixed for February 22 to March 8, 2009. What a sweet revenge it could be.
 
Back
Top Bottom