Taifa linapoteza mwelekeo kwa ukimya wetu wa kutodai Katiba ya Jaji Warioba

Mambo ya msingi lazima yaingizwe kwenye katiba kama elimu iwe lazima mtu kusoma.
haswa si sasa mikopo imekuwa ya kulenga na manati wakati aliahidi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote.
CHADEMA kama kweli walikuwa wanataka Katiba Mpya wasingempokea mfadhili mkuu wa Katiba ya Sitta. Nani asiyejua bwana mkubwa alikuwa anataka kuwa raisi 'mwenye nguvu' na alikuwa anaamini hawezi 'kukatwa' kwa jinsi alivyokuwa amefanya harambee nchi nzima. Sasa kaeni na mgeni wenu.

imefadhiliwa serikali na katiba hii ni kwa maslahi mapana ya ccm
 
Katiba ya Warioba bado inamapungufu mengi sana mfano Waziri mwandamizi = Waziri Mkuu, Makamu wa kwanza wa Rais na wa pili, yote ya nini?
 
Taifa linapitia kipindi kigumu mno kiuchumi na kidemokrasia, Washika kalamu kufikisha ujumbe wanakamatwa wanafungwa au kuteswa kwa makosa ya mitandao ya kijamii huku yeye akiomba malaika washuke wafungie mitandao ambayo ni mfumo huru wa kufikisha ujumbe. Leo Watanzania hawajui nini dira ya taifa linapo elekea , watu wanazibwa midomo kuhoji , watu wamejazwa hofu ili tuu kumuogopa mtu binafsi kuliko utii wa katiba misingi na sheria zinazo ongoza taifa ,Binafsi nasema NO NO NO …. Hapana , Hapana hii ni hadharani na hata mafichoni huko kuliko na sifa za adhabu za kutwezwa ukiwa uchi wa mnyama ili ukirudishwa urudi nyuma katika mapambano , ukombozi unagharama ya hata damu kumwagika na fikra za mabadiliko hazifi kwa kukatisha uhai wa wachache waliojitoa kulitetea Taifa kama Marehemu Alphonce Mawazo , Mohamed Babu , Oscar Kambona.

Matokeo ya utawala wa JPM kulipeleka Taifa kama gari bovu ni ukimya wetu wakutodai katiba mpya tena katiba ya Tume ya Jaji Joseph Sinde Warioba. na katiba iliopo na hata ile ya Bunge, Mwl Nyerere 1963 aliwahi sema katika mahojiano na gazeti la landon observer “Katiba yetu inatofautiana na ile ya Marekani kwa sababu inamwezesha Rais kutenda kazi bila kulizwa ulizwa mara kwa mara ……Matakwa yetu si kudhibiti mwendo wa mabadiliko ya kijamii ……Tumetaka kuongeza mwendo kuwa na chombo chenye nguvu kuweza kuvunja umasikini na vizuizi vilivyo ndani ya jamii…..Kusema kweli, Katiba inanifanya dikteta kwa kigezo chochote kile”. Maneno haya ya Mwalimu yanapande mbili Moja wakati ule ni wa chama kimoja na Taifa lilipaswa kujengwa chini ya chama kimoja na Umoja wa Kitaifa, lakini pande wa pili Mwalimu alikiri katiba hii inampa nafasi ya Udikteta , pamoja na mabadiliko viraka ya katiba bado madaraka ya Rais ni makubwa na kiasi uchache wa Busura ukikosekana basi tusishangae udikteta na mambo ya hovyo yakitekelezwa maana Katiba inaruhusu chini ya madaraka ya sasa ya Rais.

Mambo haya yafuatayo ya Utawala huu wa JPM ndio msingi wangu wa kuwataka watanzania turudi katika agenda mama ya msingi ya Katiba ya Jaji warioba na tuache kupelekwa kimatukio. kama alivyo sema katibu Mkuu wa chama Changu Dr Vicent Mashinji ukomozi wa taifa hili ni kurudisha taifa katika misingi hivyo tudai katiba mpya .

1. Mihimili na Mamlaka ya Rais katika Bunge, Mapema sana mwa Utawala wa JPM ulianza kuturudisha nyuma miaka 50 ya kidemokrasia kama alivyosema Jenerali Ulimwengu, Hili limejidhihirisha wakati tume ya wataalamu ya jaji warioba ilipendekeza Rais asiwe sehemu ya bunge hivyo spika na naibu wake wasitokane na wabunge au mawaziri ili kuipa nafasi mijadala ya kidemokrasia JPM ALIAMUA BILA KUSHINIKIZWA KUMTEUA TULIA AKSON . Uhuru wa bunge ni muhimu sana kuliko jambo lolote ili kuweka Checks and Balance kama zilivyo katiba zote za kidemokrasia zinavyo hitaji , Matokeo ya utawala huu kumteua ubunge na kasha kumteua kuwa naibu spika ndipo hoja za hovyo za kuzima matangazo ya bunge live , kuleta na kujaribu kupitisha sheria kandamizi kwa uhuru wa vyombo vya habari , bajeti zisizo na vipaumbele kwa wananchi wa chini.

2. Kuingiliwa kwa uhuru wa mahakama , hii ilijitokeza katika siku ya sheria Tanzania tarehe 4 february 2016 ambapo JPM aliwapatia fedha mhimili wa makama kwa malengo ya kutaka wote walio na kesi za madai ya kodi wafungwe na hukumu zao ziharakishwe kwa malengo ya kukusanya kodi ikiwa bila kujua watu hawa wana haki au la. Bila haya JPM aliyafanya akijua kuwa katiba ya sasa inampa kiburi husika , si kificho majaji kadhaa wamepandishwa vyeo kwa kuhukumu kesi dhidi ya wakosoaji mbalimbali ya mienendo ya serikali mfano Jaji Fedinand Wambali aliteuliwa kuwa jaji kiongozi tarehe 7/06/2016 baada tu ya hukumu ya kesi ya ubunge ya David kafulila .

3. Sasa taifa linajengwa kwa utashi wa mtu na si kuimarisha taasisi , si ajabu tena kwa utawala mtu kuacha ku refer ( kurejea misingi ya katiba,sheria sera na kanuni ) na badala yake kwa hofu na woga mtu anatimiza matakwa ya JPM , uonevu kwa watumishi unaofanywa na wakurugenzi , wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa eti tuu kutimiza matakwa ya bwana mkubwa bila kuja uwepo wa sheria na taratibu tulizo jiwekea. Gambo amefanya jambo la kipuuzi kabisa katika uwekaji jiwe wa mradi wa maendeleo wa mama na mtoto na amekaririwa akisema bwana mkubwa amempigia akimpongeza na akisapoti madudu yake.

4. Kufungiwa kwa mikutano ya hadhara, maandamano na mikutano ya ndani , Tarehe 7/ 06/ 2016 jeshi la polisi lililo chini ya JPM lilipata Baraka ya kufanya uchafu huu unaopingana na katiba za kidemokrasia moja kwa moja lakini yote haya ni matokeo ya katiba mbovu na kutunyima haki za msingi za kidemokrasia kuwawajibisha viongozi . Katiba ya Jaji Warioba imeweka vyena mipaka ya nguvu ya Raisi na mamlaka zilizo chini yake maana wote wanatokana na nguvu za wananchi kuwapa mamlaka.

5. Tumeshuhudia Teuzi za JPM zikiwapa nafasi makada wa CCM zaidi ya 70 kuwa wakurugenzi na zaidi ya 83 kuwa makatibu tawala . Watu ambao hapo baadae katika mchakato wa kura za maoni au uchaguzi ndio watakao kuwa na majukumu ya kusimamia chaguzi zetu. Hili kuliruhusu kutokea ni kukiri wazi JPM anaongoza taifa la wafu , Binafsi siwezi lifumbia macho kuona haki ya kidemokrasia ikapokwa na nika kaa kimya, Katiba ya Jaji warioba imependekeza katiba ambayo inaipa mamlaka Tume ya ajira Kuajiri kama chujuo la weledi , Uzoefu na uwezo usio na shaka na pia imemuondoa Rais katika teuzi za kati na chini ili kuondoa ukada na mambo kama haya hivyo wataalamu wale waliona haya ndio maana nasema katiba mpya ndio suluhu ya kudumu.

6. Uhuru wa vyombo vya habari, sasa ni dhahiri serikali hii haitaki hata kidogo kukosolewa , Vyombo kadhaa vya habari vimefungiwa na hata kufutwa Mfano Gazeti la Mawio lilifutwa rasmi januari 17, 2016 , huku Radio 5 ikifungiwa kwa miezi mitatu kwa sababu za kumhoji Mh Godbless lema ambaye kimsingi alikuwa anapaza sauti kutetea haki za kidemokrasia huku Clouds Tv ikifungiwa kipindi tu kilichorusha mahojiano ya Shoga ambacho ni dhahiri kilikuwa kikichochea mmomonyoko wa maadili , Wizara sasa inakwenda mbali kwa kuleta mswada wa sheria ya habari ambao unakwenda hadi katika magroup whatsapp, bloggers , vyombo vya habari vinaminywa kuripoti na ni mwendelezo wa kutufanya tufumbie macho maovu na kutuziba midomo watanzania kutufanya tusipaze sauti. Haya yote yanafanyika kwa kuwa mazingira ya katiba hii mbovu yanaruhusu.

7. Taifa halina malengo limepoteza dira hatujui tunajenga uchumi kwa sekta zipi ikiwa bandari inakauka , wanafunzi wanakosa mikopo ya elimu ya juu , kifupi kwa kipindi kama hichi kwa katiba ya Jaji warioba tungekuwa na haki ya kupima uwezo wa Rais katika kuliongoza taifa. Maisha ya watanzania yamekuwa magumu maradufu , hakuna dawa mahospitalini watu wanakufa kama kuku kwa kukosa madawa , watoto kukosa chanjo bila shaka ikitolewa ripoti isio na kuingiliwa na serikali vifo vya kina mama na watoto na wagonjwa wengine wakawaida vitakuwa vimeongezeka maradufu kuliko kawaida ndani ya miezi hii 3.

Ujumla wa mambo yanayotufanya sasa kama taifa kudai mustakabali wa taifa kwa zaidi ya miaka 100 ijayo ni mengi. Kiburi cha mtawala huyu ni katiba iliopo na si kingine, Taifa linakwenda mramba akijua wazi hakuna wa kumhoji na wote wanaomzunguka wana muabudi hadi katika makosa yake , akijua mamlaka alionayo yanamfanya kuwa dikteta wa kimaamuzi na kuacha misingi ya kidemokrasia . Niwaase watanzania wenzangu kama zipo nyakati tunapaswa kuidai katiba ya Jajii Warioba ni huu la sivyo ipo siku itatangazwa wote tulale saa saba mchana ili mtu mmoja tuu apime nguvu alionayo, WAKATI NI SASA DAI KATIBA MPYA bila hofu ya kufungwa , kuteswa kupigwa kwa ustawi wa taifa letu , kwa ustawi wa vizazi vyetu leo na kesho yako na yake asiejitambua sasa.

[HASHTAG]#JOIN[/HASHTAG] THE MOVEMENT

[HASHTAG]#DAI[/HASHTAG] KATIBA MPYA

[HASHTAG]#KATIBA[/HASHTAG] YA JAJI WARIOBA

NA HEMEDI ALI

MKUU WA IDARA UENEZI CHADEMA.
Mungu ibariki Tanzania .
 
Tizama nashauri turudi kwenye agenda BABU badala y agenda MAMA tufanye maandamano nchi nzima
 
Mkuu mtaani tunaongea lazima kuwe na watu wanaoochukua sura ya kitaifa kama vyama vya siasa na taasisi zisizo za serikali.Kwenye vijiwe tunaongea sana tu na watu wanahitaji.Hivi nimi ningetangaza UKUTA polisi wangefanya mazoezi kiasi kile?
Tuwaunge mkono wanaothubutu na si kuwavunja nguvu. Kumbuka viongozi wetu wengi wa ki Africa hawapendi upinzani wa dhati
 
Katiba ya Warioba bado inamapungufu mengi sana mfano Waziri mwandamizi = Waziri Mkuu, Makamu wa kwanza wa Rais na wa pili, yote ya nini?
upungufu huu haukupewa naafasi ya refining maana muundo wa serikali uliopendekezwa na wananchi
 
Uhakiki ni kazi ndogo chini ya Tume ya utumishi Tume ya Maji warioba iliona hili na kupendekeza kuwa chujio ... Tutengeneze taasisi...
Jon..

Tanzania yetu hakuna umakin kweny mambo ya msingi KATIBA imekula kodi zetu af hakuna kilicho fanyika.

JPM hata afanyeje hawez kulisimamia Hilo swala la katiba..
Mana katiba ya sasa bado inaonesha kumlinda kwa baadhi ya vifungu na kuendelea kuikanyaga kabisa.

TANZANIA... katiba mpya mpaka dunia Igeuke iwe inazunguka toka EAST to WEST
 
MU

Usirudi nyuma yaliofanywa yamefanyika ili tukate tamaa kudai haki zetu za msingi , wanayafanya wakijua wengi hawana elimu na walio na elimu watarudi nyuma tuu ...
 
Soma post vizuri uelewe ndo utoe maoni yako. Hii tabia ya watu kukurupuka kuandika comments za kishabiki naichukia sana. Jibu hoja kwa hoja
Hakuna hoja hapo kaka ni porojo tupu. Wewe kama unaona kuna hoja mjibu...Jamiiforums where we dare to talk openely.
 
Back
Top Bottom