Taifa Lina Viongozi Wenye Sura Mbili - Sitta

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,193
WAZIRI wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samwel Sitta amesema taifa linakabiliwa na viongozi wenye sura mbili ambao ni wale wasio waadilifu wanaofikiri kwa kutumia matumbo kwa kujilimbikizia mali na viongozi wachache wanaofikiri kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

“Msishangae, tuna viongozi wenye sura mbili, wapo wanaofikiri kwa kutumia matumbo yao jinsi ambavyo wataneemeka na kujinufaisha wenyewe, hawa ni wale wabinafsi lakini wapo viongozi ambao wanatumia ubongo katika kufikiri jinsi ambavyo watatumia uwezo wao wote katika kuwatumikia wananchi, mimi ni miongoni mwa hawa,” alisema Sitta.

Source: Mwananchi

My Take: Je ni kweli ndani ya ccm Sitta ni msafi?
 
Mzee Sita ni pekee mwenye msimamo.
Tunamhukumu Mzee Sita kwa ajili ya nini zaidi ya kuinusuru Serikali kwenye kashfa ya Richmond? Kwa ajili ya maslahi ya chama chake ilibidi afanye vile ingawa amegundua kuwa Serikali ya Jk ni lakuvunda ambalo halina ubani.
Ingawa tunamwona vile, Sitta ni kati ya viongozi wachache wa CCM wenye msimamo.
 
Samweli Sura 2 mstari wa SITA
Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo.
 
Mzee Sita ni pekee mwenye msimamo.
Tunamhukumu Mzee Sita kwa ajili ya nini zaidi ya kuinusuru Serikali kwenye kashfa ya Richmond? Kwa ajili ya maslahi ya chama chake ilibidi afanye vile ingawa amegundua kuwa Serikali ya Jk ni lakuvunda ambalo halina ubani.
Ingawa tunamwona vile, Sitta ni kati ya viongozi wachache wa CCM wenye msimamo.

nakubaliana na wewe mkuu.kula like yangu kwa roho safiii.
 
Samweli Sita.
Wewe ni kiongozi shujaa na si muoga. Kila mara unajitahidi kutoa kauli za kuonya na muda mwingi kwa chama chako mwenyewe. Ni moyo mzuri ambao tutaukosa baada ya miaka kama 10 ijayo just Filikunjombe hana bei ya kununuliwa au Shibuda angekua bado CCM.
Bahati mbaya sana Mh Sita, inaonekana huna ule mvuto ambao sisi wajinga wengi wa tanzania tunauhitaji ili tukupigie kura. Kama tungalikua tunastand on issues lazma wewe ni mtu unaetufaa ila kwa ustaarabu wetu wa kuangalia mvuto! haitowezekana
Tanzania hatufkirii sawasawa
 
Sitta ni mwanasiasa kwa ajali tu, ila yeye nafikiri ni mtekelezaji zaidi au technocrat kukiwa na tatizo ataita watu wataalam wakae na waje na uamuzi wa kutekelezwa..kama ulivyosema mkuu watanzania wanataka mwmanasiasa mtu wa maneno mengi na "mvuto" fulani. Hawajui kua Tanzania inahitaji mtu pragmatic, a technocrat kama Mkapa ila asiye mwizi.
 
Ndo maana mimi nimewekeza moyo wangu kwa Yesu kristo mwenye haki na si haya masi hasa.
.
"HERI KIJANA MASKINI MWENYE HEKIMA, KULIKO RAIS MWENYE MALI NYINGI ALIYE MPUMBAVU".
 
Back
Top Bottom