Taifa kwanza: Rais na mawaziri 2015

- Dr. Harrison Mwakyembe; anafaa sana kuwa Rais, au Waziri Mkuu 2015, hana uoga wa kusema ukweli, ni msomi, mtendaji na muadilifu na pia mfuatiliaji na anaheshimu sana Sheria.

- Ninasema anafaa sana!

Willie @ NYC, USA.

na wewe naomba unishawishi zaidi.
 
Dr. Salim Ahmed Salim....

Sina haja ya kueleza wasifu wala sifa zake za utendaji kazi.........Zinajulikana sana
 
anayefaa ni baba yako mzee john samweli malecela;

sababu ni kuwa alipewa mapesa kibao na waarabu hadi kubadilisha dini kwa hiyo anatakiwa awe rais wa danganyika ili aweze kurudisha pesa za watu.

mkuu huna haja ya kukejeli! ngoja JF isionekane dangulo. tetea anayefaa kuwa rais wako 2015
 
anayefaa ni baba yako mzee john samweli malecela;

sababu ni kuwa alipewa mapesa kibao na waarabu hadi kubadilisha dini kwa hiyo anatakiwa awe rais wa danganyika ili aweze kurudisha pesa za watu.

- Well, thanks a lot ni wazo moja kati ya mawazo mengi, mkuu karibu sana maana lako ni wazo pia ha! ha! ha! ha! ha!!, ila nitoke kidogo nje ya mada anaendela vizuri sana na afya yake, sasa ni 80%, by next month atakuwa 100% na soon anarudi bongo!

- Karibu sana mkuu! ha! ha! ha!

Willie @ NYC, USA.
 
Dr. Salim Ahmed Salim....

Sina haja ya kueleza wasifu wala sifa zake za utendaji kazi.........Zinajulikana sana

tatizo umri umesogea zaidi, ila hata mimi sina shaka naye. kwa sasa Dr.Slaa ndo anatufaa kuirudisha hadhi na heshima ya Tanzania.
 
[/SIZE][/SIZE][/COLOR]

- Well, thanks a lot ni wazo moja kati ya mawazo mengi, mkuu karibu sana maana lako ni wazo pia ha! ha! ha! ha! ha!!, ila nitoke kidogo nje ya mada anaendela vizuri sana na afya yake, sasa ni 80%, by next month atakuwa 100% na soon anarudi bongo!

- Karibu sana mkuu! ha! ha! ha!

Willie @ NYC, USA.

mkuu tuendelee na mada, achana na watu wanaopoteza utamu wa thread. naomba unishawishi kuhusu Dr. Mwakyembe, kumbuka huyu alikuwa kambi moja na mzee! isije kuwa kuna maslahi hapo!!
 
umesema kuna majina ambayo yanatajwa kuelekea uraisi 2015 na yana kukatisha tamaa sana,si vibaya mkuu ukatuwekea hayo yanayokukatisha tamaa.....
 
- Dr. Harrison Mwakyembe; anafaa sana kuwa Rais, au Waziri Mkuu 2015, hana uoga wa kusema ukweli, ni msomi, mtendaji na muadilifu na pia mfuatiliaji na anaheshimu sana Sheria.

- Ninasema anafaa sana!

Willie @ NYC, USA.
Huyu ameathirika sana na U CCM. Bila ya huyu hoja ya Richmond ingekuwa historia. Akaamua kuilinda serikali kwa kutosema ukweli. Nilimwona shujaa sana wakati ule na nilifikiri alifaa kuwa Waziri Mkuu baada ya Lowassa lakini alipokubali hoja imalizwe kinyemela bungeni nikamwaona yeye, Samuel Sitta, Ole Sendeka, Kilango, Lembeli, Selelii, shelikindo (Bi&Bw), Mwambalaswa, Mengi,Membe,Zambi na Manyanya wote wasanii wanaoendeleza uhasama wa kimakundi. Kwenye list hii hata Nape anaingia. Mpendazoe tu ndio aliukana ufisadi kwa vitendo.
 
Mkuu mada hii naona huwa huiachi miaka yote unaipenda hahaha poa lakini wacha wachambuzi wakupe maneno yao juu ya Slaa naona wewe umsema huelewi maana ya kuwajali wananchi kwa Slaa .

- Mkuu Lunyungu, ukisoma mada zangu za nyuma kuhusu hii subject ndio utaelewa kwa nini taifa tumekwama maana toka BCS siku zote nilikuwa na hii mada nikasema wanaofaa na wasiofaa, ndio maana huwa ninaipenda sana hii subject ukienda kule nyuma ukapata archives utaona wale niliosema hawafai wakachaguliwa anyways, hakuna nilipokosea! ha! ha!

- Dr. Slaa niwe mkweli sana, ninamuona makini sana kwenye role ya uongozi wa upinzani bado sijaweza ku-transform jinsi gani mawazo yake yanaweza kulisaidia taifa as a President, nina heshimu sana mchango wake kwa taifa, lakini hapa ninaongelea kiongozi anayeweza kulisaidia taifa letu likasogea mbele kuliko tulipo sasa! au badala ya Rais tu as usual!

Willie @ NYC, USA.
 
Lowassa. He is better than the rest of Magambas.

dude are u serious ...?! wajuwa kuna watu hata wapige msuaki vipi kinywa kitaendelea kutoa harufu mbaya...! basi ndio lowasa katika ulingo wa siasa na swala zima la ufisadi
 
mkuu tuendelee na mada, achana na watu wanaopoteza utamu wa thread. naomba unishawishi kuhusu Dr. Mwakyembe, kumbuka huyu alikuwa kambi moja na mzee! isije kuwa kuna maslahi hapo!!

- Mkuu unajua sio siri kwamba you are genius! ha! ha! ha! sawa sawa mkuu!

Willie @ NYC, USA.
 
Huyu ameathirika sana na U CCM. Bila ya huyu hoja ya Richmond ingekuwa historia. Akaamua kuilinda serikali kwa kutosema ukweli. Nilimwona shujaa sana wakati ule na nilifikiri alifaa kuwa Waziri Mkuu baada ya Lowassa lakini alipokubali hoja imalizwe kinyemela bungeni nikamwaona yeye, Samuel Sitta, Ole Sendeka, Kilango, Lembeli, Selelii, shelikindo (Bi&Bw), Mwambalaswa, Mengi,Membe,Zambi na Manyanya wote wasanii wanaoendeleza uhasama wa kimakundi. Kwenye list hii hata Nape anaingia. Mpendazoe tu ndio aliukana ufisadi kwa vitendo.

- Hapana mkuu, kama sio yeye a sitting Waziri Mkuu asingejiuzulu na mawaziri wengine Wawili, na kama sio Wapiganaji CCM isingejivua magambas, na Makamba angekua bado katibu mkuu mpaka leo!

- Infact, inapokuja kwenye matendo, Mwakyembe stands very tall ndani ya CCM kuliko wengine wengi!

ushawishi wako hauna mashiko! kwanini usiseme tarakimu6? kama wana misimamo kwanini walianzisha CCJ? ok. tuache la CCJ, mbona ameshindwa kutetea yale maazimio 21 ya kamati yake teule?
 
- Salaam wananchi wenzangu,

kuelekea uchaguzi wa 2015 ni muhimu sana wananchi tukaanza sasa kujadili wanaotufaa kwenye nafasi za uongozi wa juu yaani Rais na Mawaziri, na sababu; wasiotufaa pia tuwaambie kwa lugha ya Black and White yaani the truth bila kuchanganya maneno! na tujali Taifa kwanza vyama baadaye!

- Tanzania sio taifa la mtu mmoja au kikundi flani tu na tuanze kuambiana ukweli kuanzia sasa mapema sana ili maviongozi magoi goi waanze kujifikiria mapema kama wapo kwenye the right field au wajiondoe wenyewe, maana ninakatishwa tamaa sana na baadhi ya majina ya wanaotajwa kujipanga kuchukua fomu hasa za Urais 2015!

- Nani wanafaa na nani hawafai na sababu?

- Mungu Aibariki Tanzania!

William @ NYC, USA.

Hakuna haja ya kupoteza muda,kwa kifupi ni kwamba Taifa linahitaji chama mbadala kwa sasa.Miaka 50 ya utawala wa CCM kwa Taifa hili unatosha.Majina si hoja hapa.Nani alikuwa na sifa na jina zuri kama tuliye naye wakati anapendekezwa 2005? Kwa kifupi CCM ina mchoko wa mawazo na imechakaa,inahitaji chama mbadala.Tuache propaganda zisizo na maana kwa Taifa letu.Huyo Mwakyembe anaweza akawa kiongozi asiyefaa kuliko tulio nao sasa.Tatizo kubwa ni chama kilichochoka.
 
Willie nadhani the easiest ni kuweka list ya mawaziri wote kwa sasa, then kuchambua wasiofaa na baada ya hapo sasa kuweka hao wapya. Mimi ntaanza Nchimbi na Mhanga hawafai kabsaaaaaa!!!!!!
 
ok. bila kutaja chama taja mtu unayeona anafaa kuwa rais wako, inawezekana akawa CCM lakini akagombea chama chochote hata CCK, unachotakiwa hapa ni kutaja jina na sababu.
 
tatizo umri umesogea zaidi, ila hata mimi sina shaka naye. kwa sasa Dr.Slaa ndo
anatufaa kuirudisha hadhi na heshima ya Tanzania.

Sidhani kama umri utakuwa ni tatizo sana maana mwaka 2015 Dr. Salim atakuwa na miaka 73 na Dr. Slaa atakuwa na miaka 67.....Ina maana wote tuwaite wazee???.......

Rais Abdoullaye Wade wa Senegal aliingia madarakani akiwa na miaka 74....

NB.....Kwangu mimi ni vigumu kumtabiria kiongozi fulani kwamba ndiye atarekebisha matatizo ya nchi faulani......Huwa wanabadilika sana wakiingia madarakani....
 
Willie nadhani the easiest ni kuweka list ya mawaziri wote kwa sasa, then kuchambua wasiofaa na baada ya hapo sasa kuweka hao wapya. Mimi ntaanza Nchimbi na Mhanga hawafai kabsaaaaaa!!!!!!

maaaaaaama weeeeeee!! yaaani umemsahau NGELEJA??????
 
Back
Top Bottom