Tahadhari ya wizi stand ya mkoa (ubungo)

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Naelewa fika kuwa watu wengi wanafahamu kuwa jiji hili lina vibaka wa kutupwa, ila napenda kuwakumbusha watanzania wenzangu hasa wanaomiliki magari kuwa mara wanaposindikiza ndugu au jamaa zao na wakalazimika kuingia ndani ya standi ya mabasi yanayokwenda mkoani(ubungo) wahakikishe kuwa wameacha mtu wa kuangalia gari. Leo hii nilidamka mapema kumsindikiza ndugu yangu, niliamini kuwa nimepaki gari langu kwenye eneo lenye usalama, haikuwa hivyo kwani niliporudi nilikuta site mirror imeshanyofolewa, hivyo kulazimika kwenda gerezani ili kupata nyingine. Nimeona niwakumbushe watanzania wenzangu kuwa hali ya usalama standi ya Ubungo ni ndogo sana hivyo pamoja na kuwa gari lako lina alarm hiyo haitazuia vibaka waliosheheni kuchukua wanachotaka kwenye gari yako. hivyo umakini wa hali ya juu unahitajika unapoingia kwenye stand hiyo aidha hao wanaojiita wanausalama kama wanapitia humu JF nawaomba waimalishe ulinzi kweenye stendi hiyo kwani uhalifu upo wazi kabisa na hakuna mtu anayejali.
 
pole sana uwe unawapahao wabeba mizigo alfu moja tu wanakuwa na number kweye nguo atakulindia hadi urudi hata ukimpa buku 2 sii mbaya.
 
Kweli kiongozi Ubungo pamezidi aisee, ni haohao wapiga debe na wanaokatisha tiketi wakiona biashara imewaendea kombo wanaanza kufanya uhalifu kama huo: Pole sana
 
Pole Anold.... yani kwa sasa hivi, sehem yoyote bongo ukiacha gari peke yake roho inakuwa haina amani, bora uache mtu tu, au kama alivosema mdau hapo juu, umlipe mtu akulindie...
 
Anold pole sana mpendwa sasa ulienda gerezani ukapata kile kile au ulikuwa hujaandika namba kwenye kioo.

Ila hako karangi mshikaji kafikirie kidogo wengine tunavaa miwani inakuwa shida kusoma.
 
pole mkuu ila una pesa sana wewe acha tu uibiwe. mimi sina hata mafuta ya kuweka kweye gari. wakiniibia chochote itabidi nipaki tu
 
Back
Top Bottom