Tahadhari ya utapeli: Wizi wa fedha kupitia "mobile banking"

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Leo yamenifika, na ninapenda kutoa tahadhari hii kama hili halijawahi kukumba. Leo asubuhi kuna jamaa alinipigia simu akidai kuwa anatoka kitengo cha NMB mobile banking akaniambia kuwa airtel wanatoa bonus kwa wateja wazuri wanaotumia service hiyo. Sasa bila kujua hili wala lile nikatoa taarifa za simu yangu na hata za account yangu.

Guess what?

Baada ya muda nikarealise kuwa line yangu imekuwa blocked na ndipo niliposhtuka na kujua kuwa nimeliwa!

Nilipiga simu kwa Bank Manager na kumweleza suala hilo na baadaye alinidhhirishia kuwa account yangu imekombwa yote. Hivyo nikamwambia wai-block, kitu ambacho pia kilikuwa kinawapa shida kwa sababu line ilikuwa imeshachakachuliwa. Kama isitoshe, wakaanza kupiga simu kwa watu ambao awali walitaka niwape namba tano za watu ninaowapigia simu mara kwa mara, wakiwataka hao watu wanitumie pesa na kwa sababu simu ilionyesha kuwa inatoka kwangu wengine walikuwa karibu waanze ku-act.

Kwa hiyo ni kuwa zile information za simu yangu ziliwasaidia ku-disable line yangu toka kwenye simu card yangu na na kuziweka kwenye simu card yao maana pia walihitaji ICC number ya sim card yangu, hivyo kuweza kuwasiliana na watu waki-impose kuwa ni mimi. Pili details za benki ziliwapa access kwenye account yangu na kuikwangua yote.

Kwa hiyo ndugu, kama hujawahi tokewa na hili au ulikuwa unalisikia tu kwa mbali leo hii mimi ninakuwa shahidi kwako na tafadhali usotoe taarifa zako zozote kupitia simu kama nilivyofanya mimi. Teknologia ina faida na hasara zake kwa hiyo siyo mbayo kushiriki vyote ila pale iwezekanapo jaribu kuepuka hasara. Kama utataka kujua mbinu waliyotumia unaweza kuuliza nikujuze ili uwe makini kitokea mtu akakupigia simu kama hiyo.

Mungu awabariki sana!

Wenu Mhanga wa Teknolojia

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz1lzwK4Uct
 
Hali hiyo inaweza kumkumba yeyote kati yetu kutokana na Imani tuliyonayo miongoni mwetu na kwenye asasi zinazotuhudumia. Kwa jinsi ilivyoelezwa naweza kuhisi machungu aliyonayo huyo mhanga!

Habari mbaya sana hiyo.
 
Pamoja na kwamba hadithi yako inaacha maswali mengi lakini ukweli unabaki
kuwa ni kweli maendeleo ya teknolojia yameambatana na maendeleo ya wizi.
Wizi huu unarahisishwa na ulegelege wa TCRA kutosimamia sheria ya kusajili
simu. Pia makampuni ya simu yamechangia kufanikisha wizi huu kwa vile wa-
mekuwa hawatoi ushirikiano ili kuwakamata wezi wa njia ya mtandao...
Aidha tatizo kubwa lipo kwenye benki...haipo wazi jinsi fedha za mteja zinavyolindwa
je pesa iliyoibiwa ni mali ya nani? benki au mteja?
Jaji Atkins alifafanua vema katika kesi ya Libya Arab Foreign Bank dhidi ya Bankers
Trust ya mwaka 1989 QB ukurasa728, na 748 kuwa mahusiano kati ya benki na mteja
ni yale mkopaji na mkopeshaji.
Natoa wito kwa victims kuishitaki benki mahakamani kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake
wa kulinda fedha za wateja ili tuweze kupata msimamo wa kisheria hapa Tanzania...na pia
kutoa funzo kwa mabenki. Kuendelea kutegemea Polisi wapeleke kesi ya jinai mahakamani
ni kupoteza muda na hapatakuwa na manufaa ya kutosha kwa vile nchi hii haina sheria
dhidi ya wizi wa mtandao na makosa mengine ya kimtandao.
 
wewe si mzima wewe umeibiwa kizembe sana huitaji hata kuonewa huruma
 
Hii mambo ya teknolojia bongo tumebakwa tu! Aaaggghhhrrr!
Kuna mdada aliibiwa na mumewe
 
Angalizo limetolewa.unachotakiwa kuwa makini na mambo mengine yatafata.
 
angekuwa binadamu ningesema umebakwa mpwa ila kwa simu sijui niiitaje
 
wewe si mzima wewe umeibiwa kizembe sana huitaji hata kuonewa huruma


kwani ulitaka aibiwe kivipi,aibiwe kikomandoo ama kivitavita ndio ujue kuwa jamaa sio mzembe?

kuwa mwelewa leo kwake kesho kwako,take care
 
Pole mkuu ila nadhani tuwe makini sana na watu tusiowafahamu wanapotupigia na kuhitaji taarifa zozote ambazo ni siri yako
 
Mi pia juzi nilipigiwa.wanajua habari nyingi za kwako nahisi watumishi wa kampuni za simu au bank wasiowaaminifu.ila nilimstukia mapema.pole sana
 
Pole sana ndugu yangu pia nashukuru kwa kunijuza. Pia kuna mabinti wanaodai wakimbizi toka kambi fulani Dakar- Senegal wanaomba urafiki kupitia mtandao fulani wa kijamii. Ukikubali wanakuomba uwe trustee ktk kutoa pesa zilizoachwa na wazazi wao ktk benki fulani huko Ulaya. Kiwango cha chini ni dola milioni 3.5 za Usa.unatakiwa kugharamia mchakato mzima kuhamisha pesa kutoka benki ya kigeni kuingia ktk akaunt yako. Unatakiwa kutuma dola 2000 kama gharama. Mabinti kama tisa hivi wameomba msaada wakitokea Liberia, Sierra Leone, sudan na Ivory coast. Jamani huu si utapeli? Wanawatumia pastors kama njia ya mawasiliano.
 
Kilichokuponza ni kukimbilia bonus. Nijuavyo mimi mwenye kunufaika zaidi na mobile banking ni bank wenyewe na hao wa mtandao husika.
 
Back
Top Bottom