Tahadhari: Wizi mpya maeneo ya shopping malls

Yaani kirahisi rahisi tuu from nowhere Kaka au Mshkaji naomba simu nimpigie mtu then unatoa simu unampa?hilo jicho la kikaksi nitakalomkata hata niangalia tena wala kuongea lolote lile tena.
 
Kwanini mwanamke utegemee mwanaume kusurvive? Eti Kwa vile watu hawahongi sasa hivi Basi mwanamke automatically uwe hoi kimaisha kiasi cha kufanya wizi ili upate usivyomudu. Nonsense! Una mikono na miguu plus Akili,halafu bado utegemee MTU kama vile unaumwa?
 
Hongera sana kwa kupata simu yako,ila umezidi upole ndugu yangu umeshindwa hata kumkata vibao viwli vitatu vyenye adabu??
 
Pole mkuu,una bahati sana kumpata na vilevile kutoitwa mwizi kwa kumpora simu. Hali ya maisha ni ngumu tusimwamini mtu yeyote tusiyemfahamu.
 
Juzi nimeenda Mlimani city kwa ajili ya kujipatia huduma katika maduka yaliopo pale, baada ya mihangaiko ya mda mrefu kutafuta ninachokitaka bila ya mafanikio, nikaamua kupata chakula katika mgahawa wa mary brown, wakati nasubiri chakula na kinywaji nilichoagiza, ghafla akatokea dada mmoja mrembo na alievaa nguo zinazoonekana za gharama kidogo alipofika alikuja kukaa meza karibu na yakwangu na kuanza kuchezea chezea simu, nikashangaa kwa nini hakuenda kutoa oda na amekuja straight kukaa!!!

mara akaniomba simu na hapa ninamnukuu "kaka samahani naomba kidogo uniazime simu nimpigie rafiki yangu ananitafuta na mm simu yangu imeisha chaji" kwa jinsi alivyo sikuwa na mashaka nae hata chembe, nikazama mfukoni na kutoa simu, kidogo akaanza kunyanyuka na kusogea kaunta akiwa na simu yangu kama anaenda kuagiza chakula akiwa bado anaongea kwa kutumia simu yangu niliompa wakati wote huo alikuwa anaongea na huku kila baada ya sekunde kadhaa ananiangalia mimi, na mimi kwa kumtoa wasi wasi nikaamua kuangalia upande mwengine ghafla kama niliepitiwa na mshangao kidogo sikumuona tena machoni mwangu,

nilichokifanya ni kukimbia mbio nikiwacha chakula mezani na kukimbilia nje kabisa ya eneo lile, nilienda kumkamata nje kabisa akijiandaa kupanda bodaboda. Nilikwapua simu yangu na kurudi ndani kuendelea na mambo yangu na sikutaka ugomvi. Tuchukue tahadhari sana wakuu.
Ni mdada mrefu kidogo mweupe, miaka kati ya 20 na 25, chini ya midomo ametoga na ana kito flani hivi cha silver, neno moja anaweka english, anavaa miwani rangi kama ya kahawia.

WEKA PICHA MKUU,
MAANA'KE SASA HIVI NAENDA MLIMANI SITI KUSAJILI LAINI YANGU YA ZANTEL-

LAZIMA NIKUTANE NA'E HUYO!

ANGALIZO:
MIMI SIO WA MCHEZO MCHEZO,
NA HUWA SIJARIBIWI KABISAAA!!!



 
Labda 'alijisahau' tu kuwa ni simu ya kuazima!:D:D:D:D

Maana kwa namna unavyoelezea naona ni kama wizi wa kijinga na wa hatari sana.
 
Hahahahahaha nmekaa APA nkavuta hisia jinsi ulivokimbia kuiokoa cm yako mikononi mwa mnyanganyi hahahahahahahaha
na mimi kwa kumtoa wasi wasi nikaamua kuangalia upande mwengine ghafla kama niliepitiwa na mshangao kidogo sikumuona tena machoni mwangu.

Nilichokifanya ni kukimbia mbio nikiwacha chakula mezani na kukimbilia nje kabisa ya eneo lile, nilienda kumkamata nje kabisa akijiandaa kupanda bodaboda. Nilikwapua simu yangu na kurudi ndani kuendelea na mambo yangu na sikutaka ugomvi. Tuchukue tahadhari sana wakuu. Ni mdada mrefu kidogo mweupe, miaka kati ya 20 na 25, chini ya midomo ametoga na ana kito flani hivi cha silver, jino moja anaweka english, anavaa miwani rangi kama ya kahawia.
 
Back
Top Bottom