Tahadhari: Wizi mpya maeneo ya shopping malls

Juzi nimeenda Mlimani city kwa ajili ya kujipatia huduma katika maduka yaliopo pale, baada ya mihangaiko ya mda mrefu kutafuta ninachokitaka bila ya mafanikio, nikaamua kupata chakula katika mgahawa wa mary brown, wakati nasubiri chakula na kinywaji nilichoagiza, ghafla akatokea dada mmoja mrembo na alievaa nguo zinazoonekana za gharama kidogo alipofika alikuja kukaa meza karibu na yakwangu na kuanza kuchezea chezea simu, nikashangaa kwa nini hakuenda kutoa oda na amekuja straight kukaa!!!

mara akaniomba simu na hapa ninamnukuu "kaka samahani naomba kidogo uniazime simu nimpigie rafiki yangu ananitafuta na mm simu yangu imeisha chaji" kwa jinsi alivyo sikuwa na mashaka nae hata chembe, nikazama mfukoni na kutoa simu, kidogo akaanza kunyanyuka na kusogea kaunta akiwa na simu yangu kama anaenda kuagiza chakula akiwa bado anaongea kwa kutumia simu yangu niliompa wakati wote huo alikuwa anaongea na huku kila baada ya sekunde kadhaa ananiangalia mimi, na mimi kwa kumtoa wasi wasi nikaamua kuangalia upande mwengine ghafla kama niliepitiwa na mshangao kidogo sikumuona tena machoni mwangu,

nilichokifanya ni kukimbia mbio nikiwacha chakula mezani na kukimbilia nje kabisa ya eneo lile, nilienda kumkamata nje kabisa akijiandaa kupanda bodaboda. Nilikwapua simu yangu na kurudi ndani kuendelea na mambo yangu na sikutaka ugomvi. Tuchukue tahadhari sana wakuu.
Ni mdada mrefu kidogo mweupe, miaka kati ya 20 na 25, chini ya midomo ametoga na ana kito flani hivi cha silver, neno moja anaweka english, anavaa miwani rangi kama ya kahawia.
Kaka nilikuwepo maeneo yale na Mimi ndio niliwaomba wahudumu wasitoe msosi wako maana jinsi ulivyotoka nduki' Ungekuta msosi umetolewa ,.najua pangechimbika bila ya kuchimbwa..
 
sio lulu huyu?
1475168427142.jpg

Unamaanisha huyu?
 
siku nyingine tembea na simu ya tochi akija mpe hiyo afu uone ataipokea????
 
Ni kweli mkuu luushu nakiri udhaifu huo tunao wanaume wengi na pengine hata wewe, wanatumia feminism kutuibia
Mungu mwenyewe ndo aliamua wawe wasaidizi wetu hao sasa utafanyaje???hakuna ujanja hapo ukishaombwa tena unampa smartphone hata kama una nokia ya torch umeiweka lime ya vod
 
Back
Top Bottom