Tahadhari: Wizi mpya maeneo ya shopping malls

Juzi nimeenda Mlimani city kwa ajili ya kujipatia huduma katika maduka yaliopo pale, baada ya mihangaiko ya mda mrefu kutafuta ninachokitaka bila ya mafanikio, nikaamua kupata chakula katika mgahawa wa mary brown, wakati nasubiri chakula na kinywaji nilichoagiza, ghafla akatokea dada mmoja mrembo na alievaa nguo zinazoonekana za gharama kidogo alipofika alikuja kukaa meza karibu na yakwangu na kuanza kuchezea chezea simu, nikashangaa kwa nini hakuenda kutoa oda na amekuja straight kukaa!!!

mara akaniomba simu na hapa ninamnukuu "kaka samahani naomba kidogo uniazime simu nimpigie rafiki yangu ananitafuta na mm simu yangu imeisha chaji" kwa jinsi alivyo sikuwa na mashaka nae hata chembe, nikazama mfukoni na kutoa simu, kidogo akaanza kunyanyuka na kusogea kaunta akiwa na simu yangu kama anaenda kuagiza chakula akiwa bado anaongea kwa kutumia simu yangu niliompa wakati wote huo alikuwa anaongea na huku kila baada ya sekunde kadhaa ananiangalia mimi, na mimi kwa kumtoa wasi wasi nikaamua kuangalia upande mwengine ghafla kama niliepitiwa na mshangao kidogo sikumuona tena machoni mwangu,

nilichokifanya ni kukimbia mbio nikiwacha chakula mezani na kukimbilia nje kabisa ya eneo lile, nilienda kumkamata nje kabisa akijiandaa kupanda bodaboda. Nilikwapua simu yangu na kurudi ndani kuendelea na mambo yangu na sikutaka ugomvi. Tuchukue tahadhari sana wakuu.
Ni mdada mrefu kidogo mweupe, miaka kati ya 20 na 25, chini ya midomo ametoga na ana kito flani hivi cha silver, neno moja anaweka english, anavaa miwani rangi kama ya kahawia.
Hio style ya wizi mbona ya siku nyingi?!
 
Duh pole... Watu kama hawa ndio wanafanya binadamu tushindwe kusaidiana... Hamna imani kabisa
 
Dah! Nimechoka mbaya kabisa. Yaani jamaa anasema urembo wa mdada ulimwacha hoi. Hii ndo Bongo darisalama. Warembo sasa hawaoleki kwani walishajijengea ngome kuwa watakula kwa mgongo wao tu. Sasa kaingia JPM, nakuambia kabana, kakaba kila kona. Milango yoote katia kufuli zake na anazo nyingi ka jina lake. Mwaka huu, pamoja na sura yako, utaisoma namba. Hakuna tena keep change.
 
Duuuuu! Ingekuwa ndo mm, nngemkata Calb mbaya sana. Au nngemtandika kofi ambalo lingepelekea shingo kuzunguka nyuzi360. Hakika angeacha kama sio kuritaya huo wizi.

Wizi sio mzuri kabisa.
 
Tena utakuta alificha kitochi akampa techno phantom ili mtoto amuone wa maana, matokeo yake kalizwa, unaweza kukuta hiko chakula alivyorudi yule mdada mhudumu anayefuta meza akamwambia nimekimwaga nimejua umeondoka.
 
Kwanza kwa kitendo cha kumkwapua sim akijiandaa kupanda bodaboda, ulihatarisha maisha yako.
Ingetokea akakuita mwizi aiseeee.....
Hapa tungekua tunaongea mengine.
 
Miss natafuta kinachonishangaza kwa jinsi alivyo mrembo hata kama atakuwa na vyeti feki akienda kuomba kazi ofisini kwa mwanaume yoyote rijali atapata tu. Kwa nini anaamua kufanya kazi ile?
Mkuu....
Bila shaka utakua unatokea huku ushirombo, maana naona lip down pin na english ili kuzingua ukajua ni mtoto wa masaki kamasio mikocheni...
 
Nyani Ngabu huenda anamjua kwani Ni mteja mzuri Sana wa pale jimmy jones na Mary Brown
Mhhhh.....
Kweli Dar kuna raha sana aiseeee....
Yaani migahawa yote imebatizwa kwa majina ya kingereza tu...
Huku ushirombo kuna migahawa kama kwa mama sofi, mama saidi nk...
 
Back
Top Bottom