Tahadhari vibaka na sensa

Msendekwa

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
442
168
Naomba kuwashirikisha hili wana fikra pevu.
Waratibu wa sensa wanatuambia sensa itaanza usiku wa kuamkia Aug 26.
Nachelea vibaka na wezi wasije tumia mwanya huo, wanakuja kukugongea saa 9 usiku, wakijidai ni kina Ngoswe(makarani wa sensa),
kwa nia njema ukafungua, wakakupora mali na roho.
Nadhani watu wa sensa wanapaswa kutoa elimu na tahadhari zaidi kwa umma kuhusu hili suala.
 
Na ukizingatia govt inatoa onyo kuwa atakaekataa kuhesabiwa anatenda jinai,
wanaweza tumia mwanya huo kukutisha ufungue, kwamba ukigoma,
umetenda jinai,
kumba wakora.
Dhahama inakukuta!
 
Hicho kitu mie pia nimejiuliza .....hawa vibaka sina hakika kama watatuacha salama kwa mda huo!
 
hata kwa viboko usiku sitofungua geti, si tu kwa ajili ya usalama bali pia wala sitokatisha usingizi wangu na kuhatarisha maisha yangu na ya familia.......
 
Back
Top Bottom