Tahadhari:.Staili mpya ya wizi na uporaji kwenye Taxi Dar

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Jamani kuweni makini siku hizi hasa mitaa ya Posta na Kariakoo kumeibuka mtindo wa aina yake ya uporaji kwa abiria kwenye Taxi. Kinachofanyika hasa mida ya jioni kuna Taxi huwa zinasanya abiria watano kwa elfu 2 toka Posta na Kariakoo kumbe ndani ya wale abiria wanne pamoja na dereva lao moja wewe ukiongezeka kutimiza idadi ya watano gari inasepa lakini wanakupeleka chobingo na kukupora Simu, pochi, saa na hata viatu n.k

Kuweni makini na Taxi 'bubu' hizo za mujini
 
Thanks for alert.............ila waswazi bwana, hawaishi mbinu za kuibia watu
 
Maskini hawana cha kupoteza. Hii hali ngumu ya maisha cjui itatufikisha wapi. Vijana wanatafuta coping strategy
 
Maisha magumu,ajira hakuna,watu wanakaa vijiweni kinachoendelea nikubuni jinsi ya kusukuma siku,kama hivyo mzee!
 
yote hii nisababu wale wenzetu wa kile chama wanajilimbikizia mali wkt kuna sisi wenzao hatuna kitu,hatujui kesho itakwendaje!asa kwanini watu wasbuni wizi kila uchao????????
 
yote hii nisababu wale wenzetu wa kile chama ambao wameamua kwa maksudi kujilimbikizia mali wkt kuna sisi wenzao hatuna kitu,hatujui kesho itakwendaje!asa kwanini watu wasbuni wizi kila uchao????????
 
Back
Top Bottom